MKUSDA CHURCH
Unity in Worship

9. MAKAO YAKO YA MBINGUNI

MAKAO YAKO YA MBINGUNI
Marko Polo aliporudi kwenye mji kusafiri miaka mingi katika nchi zamashariki, rafiki zake walidhani kwamba safari zake zile ndefu sanazilikuwa zimemfanya kuwa mwehu. Alikuwa na hadithi nyingi za kusimuliazilizokuwa hazisadikiki.
Marko alikuwaamesafiri hadikwenye mjiuliojaa fedha nadhahabu. Alikuwaameyaona mawemeusi yaliyokuwayakiungua moto,lakini hakunahata mmoja waoaliyekuwaamepata kuzisikiahabari za makaaya mawe. Aliionanguo iliyokataakuwaka motohata kamailitupwa katika ndimi za moto, lakini hakuna hata mmoja wao aliyekuwaamepata habari za asbestos. Aliongea juu ya nyoka wakubwa urefu waohatua kumi na mataya yao mapana ya kutosha kumeza mtu mzima, kokwaambazo ukubwa wake ulikuwa kama kichwa cha mtu na nyeupe kamamaziwa ndani yake [nazi], na kitu fulani kilichokuwa kikibubujika kutokaardhini ambacho kilizifanya taa ziwake kabisa. Lakini hakuna hata mmojaaliyekuwa amepata kuona, mamba, nazi, wala yale mafuta yasiyosafishwa.Walicheka tu kusikia visa kama vile. Miaka mingi baadaye, Marko alipolalakitandani pake akiwa anakufa, mcha Mungu mmoja aliyekuwa kando yakitanda chake akamsihi kuzikana zile hadithi zake ngumu za kusadadikikaalizokuwa amezisimulia. Lakini Marko alikataa, alisema: “Zote ni za kwelikwa kila kipengele. Kusema kweli, mimi sijasimulia nusu ya yaleniliyoyaona.”
Waandishi wa Biblia watuonyeshao sisi picha kidogo tu ya mbinguniambazo huonekana kana kwamba zinatoa mwangwi wa hisia aliyokuwanayo Marko Polo. Katika maono yao walipatazama mahali pale palipokuwapaking’aa mno, pa ajabu mno, hata waliweza kueleza sehemu ndogo tu yayale waliyoyaona. Nasi tunakabiliwa na changamoto ifananayo na ile yamarafiki wa Marko Polo. Hatuna budi kujaribu kuwaza habari za “mamba nanazi,” yaani, mambo ambayo sisi hatujapata kamwe kuyaona kwa kuwa zilepicha kidogo tu tunazozipata katika Biblia zinatuonyesha kwamba mbingunini zaidi ya kukaa juu ya mawingu na kupiga vinubi.


1.Je, Mbinguni Ni Mahali Halisi?
Yesu anatuandalia sisi mahali halisi kabisa hivi sasa katika mbingu iliyo yahalisi kabisa.
“Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi[Yesu]. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi kama sivyo,ningaliwaambia. Naenda KUWAANDALIA MAHALI. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, NITAKUJA TENA, niwakaribishe kwangu; ilinilipo mimi, nanyi muwepo.” – Yohana 14:1-3, KJV.
Yesu anakuja mara ya pili katikadunia yetu hii ili kutuchukuakwenda kwenye makaoyaliyoandaliwa kukidhi utashi wakila mtu katika mji wa mbinguni uliona utukufu upitao ndoto zetu zotezilizochanganyikiwa mno; yaani,Yerusalemu mpya.
Baada ya kuishi kwa miaka elfumoja, Kristo anakusudia kuyaletamakao yetu ya mbinguni hapakatika sayari hii itwayo Dunia.Yerusalemu Mpya utakaposhuka hapa chini, moto utaitakasa dunia yote.Sayari yetu hii itakayofanywa kuwa mpya itakuwa makao ya kudumu yawaliookolewa. Ufunuo 20:7-15. mengi zaidi kuhusu suala hili yamo katikaMwongozo 22).
Je, Yohana, aliyekiandika kitabu cha Ufunuo, anatoa picha gani nyingine?
“Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu zakwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana baharitena. Nami nikauona mji ule Mtakatifu, Yerusalemu Mpya ukishukakutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi – arusialiyekwisha kupambwa kwa mumewe. Nikasikia sauti kubwa kutokakatika kile kiti cha enzi, ikisema, ‘Tazama, maskani ya Mungu nipamoja na wanadamu, naye ataisha pamoja nao. Watakuwa watuwake, naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao na kuwa Munguwao” – (Ufunuo 21:1-3).
Baada ya nchi hii kubadilishwa kabisa kwa moto, je! ni akina nani watakaakatika ile nchi mpya?
“Heri wenye upole; maana hao watairithi nchi” – (Mathayo 5:5, Angaliapia Ufunuo 21:7).
Kristo anaahidi kwamba dunia hii ambayo zamani ilikuwa kamilifuitarejeshwa katika uzuri wake ule wa Edeni, na wapole “watairithi nchi.”


2.Je, Tutakuwa Na Miili Halisi Mbinguni?
Yesu alipowatokea wanafunzi wake akiwa na mwili wake uliofufuka nakutukuzwa, je, aliuelezaje mwili ule?
“Tazameni mikono yangu na miguuyangu, ya kuwa ni mimi mwenyewe.Nishikeni, mwone; kwa kuwa rohohaina mwili na mifupa, kamamnavyoniona mimi kuwa nayo” -(Luka 24:39).
Yesu alikuwa na mwili halisi; alimtakaTomaso amguse (Yohana 20:27). Wakatiule Yesu alitembea na kuingia katikanyumba halisi, na kuzungumza na watuhalisi, na kula chakula halisi (Luka24:43).
Kule mbinguni hakukaliwi na roho, balina watu halisi wanaoyafurahia maishaya kiroho, na ambao wana “mwili.. wa utukufu.”
Nasi kwa hamu kubwa tunamngojea Mwokozi wetu kutoka kule, yaani,Bwana Yesu Kristo, ambaye, kwa uweza wake unaomfanya kuvidhibitivitu vyote chini yake, ataibadilisha miili yetu hii minyonge ili ipatekufanana na mwili wake wa utukufu” – (Wafilipi 3:20,21).

Tunaweza kuwa na hakika kwamba miili yetu ya mbinguni itakuwa imara naya kweli kweli kama ulivyokuwa mwili wa Kristo aliyefufukwa.
Je, tutaweza kuwatambua watu wa familia yetu pamoja na marafiki zetukule mbinguni?
“Tuanachoona sasa ni kama tu sura hafifu katika kioo, lakini hapobaadaye tutaona uso kwa uso. Sasa ninajua kiasi fulani tu, lakini hapobaadaye nitajua yote kikamilifu, kama vile Mungu anavyonijua mimi -(1 Wakorintho 13:12).
Kule mbinguni tutajua sana.” Tutaelewana na kuthaminiana kwa kina kulikotulivyopata kufanya katika dunia ya sasa.
Wanafunzi wa Yesu walimtambua akiwa katika mwili wake wa mbinguni, nidhahiri kutokana na sura yake walipokuwa wamezoea kuiona (Luka 24:36-43). Mariamu alimjua pale kaburini kutokana na sauti yake aliyokuwaamezoea kuisikia wakati alipomwita kwa jina lake (Yohana 20:14-16). Emauwalimtambua kutoka na ishara zake fulani za mikono walizokuwawamezoea kuziona. Walipoangalia jinsi mgeni wao alivyokibariki kilechakula, walimtambua kuwa ni Bwana kwa tabia yake (Luka 24:13-35).
Waliokombolewa wanayo hakika ya kuwa na maisha ya kusisimua sanakwa kuungana uso-kwa-uso tena kule mbinguni. Fikiria furaha utakayokuwanayo ukiitambua tabasamu ya aina yake ya mume au mke wako, au sautiinayokuita ambayo kwako inafahamika ya mtoto wako uliyemlaza kaburinizamani sana, ishara za mikono zinazoonyesha upendo kwako za rafiki yakofulani mpendwa wako. Tutakuwa na umilele utakaoimarisha vifungo vyamaisha yetu kwa kina zaidi na kukuza urafiki wa karibu sana pamoja nawatu wale wanaotuvutia sana katika ulimwengu.


3.Tutafanya Nini Kule Mbinguni?
Tutakuwa na shughuli nyingi za kutupatia changamoto kule mbinguni. Vipikama wewe utaibuni mwenyewe nyumba yako unayoiwazia?
“Tazama, mimi naumba mbingu mpya na nchi mpya… Naminitafurahia Yerusalemu, na kuwaonea shangwe watu wangu…Watajenga nyumba, na kukaa ndani yake; watapanda mashamba yamizabibu, na kula matunda yake… Wateule wangu wataifurahia kazi yamikono yao muda wa siku nyingi” – (Isaya 65:17-22).
Tayari Yesu anaandaa nyumba zetu binafsi katika ule Mji Mtakatifu, yaani,Yerusalemu Mpya (Yohana 14:1-3; Ufunuo 21). Mafungu hayo yanadokezakwamba sisi pia tutabuni nakuzijenga nyumba nyingine – huenda zikawa nizile nyumba zetu nzuri za mashambani, ambazo tutaziwekea mandharinzuri sana ya mimea hai mbalimbali. Tena, basi, ni nani ajuaye ni mbinugani za hali ya juu zinazotungojea kuzitumia katika ule ustaarabu wa juuzaidi wa Mungu? Uvumbuzi mpya wa sasa wa kisayansi, pamoja na safarindefu zenye matukio mengi katika anga za juu zitaonekana kama mchezowa kitoto tu tutakapoanza kufanya uvumbuzi wetu “nyumbani mwa Baba”yetu.
Je, unapenda uzuri wa maporomoko ya maji yanayounguruma, mashambaya malisho matulivu, misitu mingi iletayo mvua, na maua mazuriyanayochanua?
“Maana BWANA ameufariji Sayuni;… amefanya jangwa lake kuwakama bustani ya Edeni, na nyika zake kama bustani ya BWANA; furahana kicheko zitaonekana ndani yake, kushukuru, na sauti ya kuimba” -(Isaya 51:3).
Mungu ataigeuza nchi hii itakuwa kama Bustani ya Edeni ya zamani.Hakuna tena kumwagika ovyo ovyo kwa mafuta, wala mchanganyiko waukungu na moshi, wala ukame; maziwa yatakuwa safi kama kioo, mitiitakuwa na fahari yake, na mitelemko ya milima itakuwa bila waa lolote.
Sio tu uzuri wa dunia hii, bali pia uwezo wetu wa kuzingatia mamboutaongezeka sana. Utaonekana kama siku ya kwanza ya kutoka nje baada ya ugonjwa wa muda mrefu sana. Nazile “dakika ishirini za kuyaona mamboya kweli” za awali zitaendelea nakuingia katika ule umilele wa kimiujiza.
Je, unafurahia kuyaona mambo mapya? kujifunza? Kubuni vitu? “Kule, watuwaishio milele watatafakari kwa furahaisiyokoma maajabu ya ubunifu wauumbaji, siri ya upendo ukomboao…Kila uwezo wa kutenda kazi utakuzwa,kila uwezo wa kukumbuka au kujifunzautaongezeka. Kujipatia
maarifa hakutaichosha akili aukuzimaliza nguvu za mwili. Kuleshughuli kubwa mno zitawezakufanywa, hamu ya kuifikia hali borakiroho itafikiwa, tamaa ya kufanyamambo makuu mno itatimizwa; na badovilele vipya vya kuvipita vitainuka, maajabu mapya ya kuyastaajabia, kwelimpya za kuzifahamu, vitu vipya vitakavyohitaji kutumia nguvu za akili, rohona mwili. Hazina zote za ulimwengu zitawekwa peupe ili zipatekuchunguzwa na wale waliokombolewa wa Mungu.” – Ellen G. White, TheGreat Controversy (Nampa, Idaho; Pacific Pres Publishing Asociation,1950), ukurasa 677.


4.Je! Uovu Utaitishia Mbingu Tena?
“Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, walayeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katikakitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo” – (Ufunuo 21:27).
Mungu ataiondoa kabisa dhambi pamoja na athari zake za kutisha; mambohayo hayataonekana tena. Yesu atakapoonekana, “tutafanana naye” (1Yohana 3: 2). Badala ya kuipiga misukumo iliyo ndani yetu ya kuua, kuiba,kusema uongo, au kubaka, sisi tutaendelea kuwa na zile tabia nzuri zambinguni.
“Naye [Mungu] atafuta kila chozi katika macho yao, wala mautihaitakauwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivuhayatakuwepo, kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita”-Ufunuo 21:4.
Hata yule adui yetu wa mwisho, yaani, mauti, atatoweka kabisa. Katika nchiile ya mbinguni yenye ujana wa mielele wale waliokombolewa wanayo “miiliisiyokufa” (1 Wakorintho 15:53); hakuna mwenyeji ye yote wa nchi ileatakayeteseka kutokana na uharibifu uletwao na uzee.
Sio tu kwamba hiyo mbingu inateketeza athari za dhambi, bali pia inafanyamageuzi ya athari hizo. Hebu fikiria itakavyokuwa kwa wale ambaowamepambana na ulemavu mbali mbali katika maisha yao yote:
“Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa, na masikio ya viziwi
yatazibulia. Ndipo mtu aliye kilema ataruka-ruka kama kulungu, naulimi wake aliye bubu utaimba” – (Isaya 35:5,6).


5.Je, Furaha Kuu Kuliko Zote Mbinguni Ni Ipi?
Hebu fikiria kwamba wewe unamwona Bwana wa malimwengu uso-kwa-uso.
“Tazama maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanyamaisha yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Na Mungumwenyewe atakuwa pamoja nao, naye atakuwa Mungu wao” – (Ufunuo21:3).
Mungu mwenyezi anaahidi kwamba atakuwa mwenzi na mkufunzi wetu. Nifuraha iliyoje hiyo kukaa miguuni pake! Hebu fikiria kile ambacho mwanamuziki angeweza kutoa ili kuwezakutumia dakika chache pamoja naBeethoven au Mozart. Fikiria jinsimtaalamu wa fizikia ambavyo angewezakuithamini sana nafasi ya kuweza kukaachini pamoja na Albert Einstein, auingekuwa na maana kubwa kwa kiasigani kwa mchoraji kuweza kuongea naMichelangelo au Rembrandt.
Hebu fikiria tu jinsi wale waliokombolewawatakavyopata upendeleo mkubwa mnousio wa aina zote, sayansi yote, nasanaa yote. Watapatana kwa karibu sanana akili na moyo usio na kifani katikamalimwengu yote. Na uhusiano huoutafurika na kugeuka kuwa ibada.
“‘Na itakuwa mwezi mpya hata mwezi mpya, na Sabato hata Sabato,wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, ‘asema BWANA” -(Isaya 66:23).
Katikati ya mji wa mbinguni kinasimama kiti kikuu cha enzi, cheupe, chaMungu. Akiwa amezungukwa na duara ya upinde wa mvua wa zumaridi,uso wake unang’aa kama jua ambalo mng’aro wake unayatia macho kiwi.Chini ya miguu yake bahari ya kioo inakwenda pande zote. Katika sehemuile ya juu inayong’aa kama kioo utukufu wa Mungu unaakisiwa [nuru yakeinarudishwa], waliokombelewa wanakusanyika pale ili kutoa sifa zao kwashangwe kuu.
“Na hao waliokombolewa na BWANA watarudi,watafika Sayuniwakiimba; na furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao, naowatapatwa na kicheko na furaha, huzuni na kuugua zitakimbia” -(Isaya 35:10).
Hapa yupo mtu yule ambaye wema wake haukosi pigo hata moja. Uaminifuwake na subira yake na upendo wake huendelea tu milele zote. Nalihimidiwe jina lake takatifu!


6.Huna budi kuwa Kule!
Yesu anatamani sana kukutana nasi uso kwa uso wakati ule. Ndiyo maanayeye alipenda kukuokoa wewe kutoka katika dhambi kwa gharama kubwakama ile. Wewe binafsi ni lazima unufaike kwa kuipokea zawadi hiyo. Nilazima wewe ujitoe kabisa kwake Kristo awe Bwana na Mwokozi wako.Unahitaji msamaha wake unaotolewa kwako kutoka katika ule msalaba,kwa sababu:
“Ndani yake kamwehakitaingia cho chotekilicho kinyonge, walayeye afanyaye machukizoya uongo, bali walewalioandikwa katika kitabucha uzima cha Mwana-Kondoo” – (Ufunuo 21:27).
Yesu anatuokoa kutokakatika dhambi [uvunjaji waAmri Kumi], sio pamoja nadhambi [uvunjaji wa Amri Kumi]. Yatupasa kuja kwake kwa uwezo wake uliondani yetu na kutengwa mbali na uchafu na uovu. Yesu ni neno letu kuu lakuingilia katika ufalme wake unaokuja upesi.
Na ufalme ule unaweza kuanza sasa hivi ndani ya moyo wako. Kristoanapotuokoa sisi kutoka katika dhambi, anaiweka mbingu ndogo ndani yamoyo wetu. Anaweza kutusaidia sisi katika kushughulikia wasiwasi, hasira,tamaa ya mwili, hofu, na hatia inayotusumbua. Tumaini la kwenda mbingunisi njia ya kuyakwepa matatizo yanayotukabili katika maisha yetu; linasaidiakuileta mbingu kwa wingi zaidi hapa duniani. Kura iliyopigwa hivi karibuni ilionyesha kwamba “wale wanaoamini kwamba maisha yatakuwako baadaya kifo walikuwa na maisha yenye furaha na kuwa na imani na watu kulikowale wasiosadiki hivyo.”
Hakuna kitu cho chote kitakachokuwa na mvuto unaosisimua sana katikamaisha yako ya wakati huu wa sasa kama kuwa na uhusiano wa imani naYesu Kristo. Hebu sikiliza jinsi Petro anavyoeleza matokeo ya imani iliyohai:
“Naye mwampenda, ijapokuwa hamkumwona; ambaye ijapokuwahamwoni sasa mnamwamini; na kufurahi sana, kwa furahaisiyoneneka yenye utukufu, katika kumpokea mwisho wa imani yenu,yaani wokovu wa roho zenu” – (1 Petro 1:8,9).
Yote hayo utapata – pamoja na mbingu pia. Je! wewe umekwisha kugunduaaina ile ya maisha tele ambayo Kristo anataka wewe uwe nayo? Tafadhaliusigeuke na kwenda zako kwa kuukataa mwaliko wake huu wa neema.
“Na Roho na Bibi-arusi, wasema, ‘Njoo!’ Naye asikiaye na aseme,’Njoo!’ Naye mwenye kiu, na aje; na ye yote atakaye, na ayatwae majiya uzima bure” – (Ufunuo 22:17).
Yesu yu pamoja nawe hivi sasa, anazungumza na moyo wako unaposomamistari hii. Anakualika wewe, anasema, “Njoo!” “Njoo!” “Njoo!” Asingewezakuwa na shauku kubwa zaidi ya hiyo, asingesisitiza zaidi ya hivyoalivyokwisha kufanya. Kama wewe bado hujafanya hivyo, basi, hii ndiyodakika yako ya kukichunguza kipawa chake hicho.
Kwa nini wewe usimwambie ya kwamba unakubali kukipokea kipawa chakehicho cha neema yake na ya kwamba wewe unataka kuishi milele pamojanaye? Mwambie kwamba wewe unampenda. Umshukuru kwa yotealiyokutendea na kwa yale ambayo unapanga kwa ajili yako. Kama kunakitu cho chote kati yako na Mungu, basi, mwombe akufanye upendekuachana nacho. Leo hii, unapoisikia sauti yake, wakati moyo wako badounavutwa kwake, jitoe kwake wewe mwenyewe bila kuacha kitu. Inamishakichwa chako dakika hii na kusema, “Yesu, Bwana wangu, naja kwako.Nakupa wewe vyote nilivyo navyo. Mimi nataka kuwa wako milele hatamilele.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top
MKUSDA CHURCH