YESU AJAPO KWA AJILI YAKO
Baada ya miaka mingi ya kutendewa vibaya, Armando Balladares alikuwaamekonda vibaya sana na kulemaa akiwa kama kinyago tu cha vilealivyokuwa mara ya kwanza. Alikuwa amevutiwa sana na imani yakeiliyomletea mateso. Muda mfupi baada ya watu wale wawili kuoana katikasherehe ya kuwafungisha ndoa yao iliyoendeshwa kiserikali katika uwanjawa gereza lile, Martha alilazimka kuhamia Miami.
Kutengana kwao kulileta uchungumwingi sana. Lakini Armandoalifanikiwa kutuma kwa siri ahadiyake kwenda kwa mpenzi wake.Juu ya kipande cha karatasikilichotupwa aliiandika ahadi yakehii:
“Nitakuja kwako. Singe hizo zilizokatika upeo wa mgongo wanguhazitakuwa na maana tena.”
Mfungwa huyo alidhamiria kwamba kwa njia fulani yeye na Marthawangetoa ahadi zao ndani ya kanisa mbele za Mungu. Siku mojamuungano wao ungekamilika. ” Wewe u pamoja nami daima” alimwambiamwanamke yule.
Ahadi aliyotoa Armando ilimfanya aendelee kuishi katika miakaaliyotendewa vibaya sana ambayo ingekuwa imeivunja mioyo ya wanaumewengi. Nayo ilimfanya Martha aendelee kuishi. Alifanya kazi bila kuchoka ilikuyaamsha mawazo ya umma yapate kutambua hali mbaya iliyomkabilimumewe. Yeye hakukata tamaa kamwe.
1.Ahadi
Kuna nyakati fulani sisi tunaweza kujaribiwa na kushangaa, je! hivi kwelisiku moja Kristo atashuka na kuja tena katika mbingu hizo za samawi zilizojuu yetu kwa muungano ule wa ajabu pamoja nasi? Mwisho huo wenye
furaha wa historia hii ndefu, yenye misiba mingi ya ulimwengu, unawezakuonekana kama ni mzuri mno kiasi cha kufikiriwa kuwa si wa kweli kwetusisi. Lakini kuna kitu kimoja ambacho kinaweza kulifanya tumaini letu kuwahai mioyoni mwetu. Na kitu hicho ni ahadi ya Yesu pekee aliyoitoa kwambayeye atakuja tena. Muda mfupi tu kabla hajajitenga mbali na wanafunziwake, Yesu alitoa ahadi hii:
“Yesu aliwaambia, Msifadhaike mioyoni mwenu. Mwaminini Mungu;niaminini na mimi pia. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi;kama isingekuwa hivyo, ningekwisha waambieni. Sasa nakwendakuwatayarishieni nafasi. Na nikienda na kuwatayarishieni nafasi,nitarudi na kuwachukueni kwangu, ili nanyi mwe pale nilipo mimi” -(Yohana 14:1-3).
Kabla Yesu hajapaa kwenda mbinguni, aliwaahidi wafuasi wake, akisema”NITAKUJA TENA!” Aliahidi kurudi tena kuja kuwachukua wale wotewanaomtegemea ili awape mahali maalum alipowaandalia. Maandikoyanasema juu ya kuja kwake mara ya pili karibu mara 2,500 hivi. Ukwelikwamba Kristo anakuja mara ya pili katika ulimwengu huu ni wa hakikakama ulivyo uhakika kwamba yeye aliwahi kuishi hapa dunaini miaka elfumbili iliyopita.
Zamani sana Mungu aliahidi kwambaMasihi angekuja, yaani Mkomboziambaye angechukua mwilini mwakeuovu wetu na kutoa msamaha wakekwa ajili ya dhambi za wanadamu.Ahadi ile ilionekana kana kwambailikuwa ni nzuri mno kiasi kwambaisingeweza kuwa ya kweli kwa wengikatika ulimwengu ule wa zamaniambao walikuwa wakiendelea kufanyakazi zao kwa bidii katika maisha yaoyote. Lakini kweli Yesu alikuja na kufajuu ya msalaba. Ahadi ilitimia kweli kwautukufu kuliko vile watu walivyowazakwamba uwezekano kama uleungekuwapo. Ahadi yake ya kuruditena pia itakuwa ni ya kweli. Sisitwaweza kumtegemea yeyeatupendaye, kurudi tena na kuwakusanya wale ambao kwa ajili yao amelipagharama kubwa mno isiyokadirika.
Katika kipindi chote cha kufungwa kwake, Armando aliendelea kutuma kwaMartha kwa siri mashairi, ujumbe, na picha alizochora. Naye [Martha]alifanikiwa kuyachapisha baadhi ya maandiko yale. Ufasaha wake [yalemaandiko] uliyavuta mawazo ya ulimwengu. Serikali zikaanza kumbanaCastro ili awaachilie wafungwa wale waliofungwa kwa sababu ya kuzifuatadhamiri zao. Rais wa Ufaransa akaingilia kati na hatimaye katika mwezi waOktoba mwaka wa 1982 Armando alipakiwa katika ndege iliyokuwa ikiendaParis. Ilikuwa ni vigumu sana kwake kuamini kwamba alikuwa huru-hatawakati ndege ile ilipotua. Lakini basi, baada ya miongo miwili [miaka ishirini]ya mateso na shauku yake ya kungoja, Armando alikimbia na kukumbatiwana mikono ya Martha.
Miezi michache baadaye katika kanisa la Miami la Mtakatifu Kierani walewawili wakasimama na kurudia kutoa kiapo chao cha ndoa. Hatimayemuungano wao ukawa umekamilika. Ahadi ikawa imetimizwa: “Nitakujakwako.”
Je, waweza kufikiria ni muungano wa ajabu jinsi gani utakaokuwakohatimaye tutakapoweza kumwona Kristo uso kwa uso? Kuja kwake katikautukufu wake kutazimeza huzuni zetu zote pamoja na kuvunjika mioyokwetu kote, kutayafutilia mbali maumivu yetu yote tuliyoyaficha mioyonimwetu. Kurudi tena kwa Yesu kutakidhi shauku zetu zenye kina sana namatarajio yetu ya kusisimua sana. Kisha tutaingia katika umilele wamuungano wa karibu sana na mtu yule wa ajabu sana katika Malimwenguyote. Yesu yu aja upesi! Je, wewe unayo shauku ya kukutana naye?
2.Yesu Atakujaje?
(1)Je! Yesu atakuja kwa siri?
“Tazama, [Yesu] nimekwishakuwaonya mbele. Basiwakiwaambia, “yuko jangwani,’msitoke; ‘yumo nyumbani,’msisadiki. KWA MAANA KAMA VILEUMEME utokavyo mashariki naKUONEKANA hata
magaharibi, HIVYO NDIVYOKUTAKVYOKUWA KUJA KWAKEMWANA WA ADAMU” – (Mathayo24:25-27).
Umeme unamulika ghafla nakuonekana wazi wazi kabisa mpakambali sana, hivyo ndivyo ambavyo kujakwake Yesu hakutakuwa kwa siri yaaina fulani au kuwa tukio la kihisia tu.
(2)Je, Yesu atakuja tena kama mtu halisi?
“Walipokuwa wakikaza macho mbinguni, yeye alipokuwa akiendazake, tazama watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguonyeupe, wakasema, enyi watu wa Galilaya mbona mmesimama hapamkitazama mbinguni? HUYO YESU, aliyechukuliwa kutoka kwenuKWENDA JUU MBINGUNI, ATAKUJA JINSI IYO HIYO mlivyomwonaakienda zake mbinguni” – (Matendo 1:10-11).
Siku ya kuondoka kwake kutoka katika dunia yetu hii, malaika walewaliwathibitishia wanafunzi wale kwamba “Yesu yule yule” aliyechukuliwakwenda mbinguni – si mtu mwingine awaye yote – angerudi tena kamaMfalme wa wafalme. Yesu yule aliyewaponya wagonjwa na kuyafunguamacho ya vipofu. Yesu yule yule aliyezungumza kwa upole na mwanamkeyule aliyekamatwa akizini. Yesu yule yule aliyeyafuta machozi yamwombolezaji yule na kuwapokea watoto na kuwakalisha katika paja lake.Yesu yule yule aliyekufa juu ya msalaba ule wa Kalwari akapumzikakaburini, na kufufuka kutoka kwa wafu siku ile ya tatu.
(3)Je, Yesu atakuja ili sisi tuweze kumwona?
“Tazama yuaja na mawingu, na KILA JICHO LITAMWONA” – (Ufunuo1:7).
(Sehemu ya Kwanza).
Wote walio hai wakati Yesu anakuja tena, yaani, wenye haki na waovu,watashuhudia kuyaona marejeo yake.
Ni wangapi ambao Yesu mwenyewealisema watakuona kurudi kwake tena?
“Ndipo itakapoonekana ishara ya Mwana wa Adamu mbinguni, ndipoMATAIFA YOTE YA ULIMWENGU yatakapoomboleza nao,WATAMWONA Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni,pamoja na nguvu na utukufu mwingi” – (Mathayo 24:30).
Kila mtu aliye hai katika dunia yetu hii atamwona Yesu akirudi tena.
(4)Ni nani atakayefuatana na Yesu atakapokuja?
“Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wotepamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu ule wake” -(Mathayo 25:31).
Fikiria jinsi itakvyokuwa Yesuatakaporudi tena katika fahariyake yote akiwaamezungukwa pande zote na”malaika wote.”
(5)Je, tunaweza kutabiriwakati halisi wa kurudi kwakeYesu?
“Walakini habari ya siku ilena saa ile hakuna aijuaye,hata malaika walio mbinguni, wala Mwana ila Baba peke yake…. Kwasababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saamsiyodhani Mwana wa Adamu yuaja” – (Mathayo 24:36,44).
Kila mmoja atakuona kuja kutukufu kwa Yesu, lakini wengine hawatakuwatayari kwa kuja kwake huko. Je, wewe binafsi u tayari kwa kuja kwakeYesu?
3.Yesu Atafanya Nini Atakapokuja Tena?
(1)Yesu atawakusanya pamoja wote waliookolewa (wateule).
“Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda,nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huuwa mbingu mpaka mwisho huu” – (Mathayo 24:31).
Kama wewe umemruhusu Yesu akutayarishe moyoni mwako na katikamaisha yako, basi utampokea kwa furaha kama Mwokozi. Wako.
(2)Yesu atawaamsha watakatifu waliokufa.
“Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja namwaliko, na kwa sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu, nao
WALIOKUFA KATIKA KRISTO WATAFUFULIWA KWANZA” – (1Wathesalonike 4:16).
Yesu anashuka kutoka mbinguni kwa sauti kuu. Sauti yake yenye nguvunyingi inasikika ulimwenguni kote. Inayapasua makaburi katika kila eneo lamakaburi na kuwafufua mamilioni ya watu waliompokea Yesu katika vizazivyote. Hiyo itakuwa ni siku ya kusisimua sana jinsi gani!
(3)Yesu atawabadilisha wenye haki wote wakati atakapokuja – si wafuwenye haki peke yao, bali pia wenye haki walio hai.
“Kisha sisi tulio hai, tuliosalia TUTANYAKULIWA PAMOJA NAO katikamawingu ili tumlaki Bwana hewani; Na hivyo tutakuwa pamoja naBwana milele” – (fungu la 17).
Ili kutuandaa sisi kwa maisha yale ya milele, Kristo anabadilisha miili yetuhii inayokufa kuwa miili mizuri isiyokufa.
“Angalieni nawaambia ninyi siri; hatutalalasote, lakini sote tutabadilika, kwa dakikamoja, kufumba na kufumbua, wakati waparapanda ya mwisho; Maana parapandaitalia, na wafu watafufuliwa, wasiwe nauharibifu, nasi tutabadilika. Maana shartihuu uharibikao uvae kutokuharibika, naohuu wa kufa uvae kutokufa” – (1Wakorintho 15:51-53).
Yesu ajapo “sote tutabadilika.” Hebu fikiriasasa: hakuna ugonjwa wa baridi yabisi,kupooza, wala kansa. Fungeni hospitali, nafungeni nyumba za matanga. Kristo amekuja!
(4)Yesu atawachukua wenye haki wote kwenda nao mbinguni.
Yesu mwenyewe alitoa ahadi hii, “Nitakuja tena na kuwachukua mpatekuwa pamoja nami” nyumbami mwa Baba yangu (angalia Yohana 14:1-3).Petro anazungumza juu ya urithi wa waliokombolewa “uliotunzwa mbingunikwa ajili yao” (1 Petro 1:4). Tuanaweza kutazamia mbele kuwezakuyavumbua maajabu ya mji ule wa Mungu, yaani, Yerusalemu Mpya, nakumfahamu Baba yetu aliye mbinguni.
(5)Yesu atayaondoa kabisa maovu na maumivu kwa kipindi chotekitakachofuata.
Waovu – yaani, wale ambao kwa shingo ngumu wameendelea kuikataarehema yote anayowapa Yesu – wanajihukumu kabisa wenyewe.Wanapokodoa macho yao kutazama uso wa Yesu anapokuja kwao kutokamawinguni, fahamu zao zinazinduka ghafula na kutambua dhambi zao,tena wanaona ni vigumu kabisa kuvumilia maumivu ya dhambi zao;wanapiga makelele na kuiomba milima na miamba, wakisema,”Tuangukieni, tusitirini mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi,na hasira ya Mwana -Kondoo!” (Ufunuo 6:16). Wanaona ni heri kufa kulikokusimama mbele za macho ya Yesu yaliyokazwa ambayo yanawaona wote.
Wanajua fika kwamba sauti inayounguruma sasa kutoka mbinguni iliwasihisana zamani kwa upole ili wapate kuikubali neema ya Mungu. Walewalioamua kupotea wenyewe katika mbio za kiwendawazimu ili kutafutafedha au anasa au cheo sasa wanatambua kwamba wamekidharau kitu kilecha pekee chenye manufaa ya kweli katika maisha yao.
Ni uvumbuzi unaowamaliza kabisa. Kwa vyovyote vile, hakuna hata mmojawao ambaye alikuwa na haja ya kupotea. Mungu mwenyewe hakufurahiikufa kwake mtu mwovu” (Ezekieli 33:11). Yeye “hapendi mtu ye yoteapotee, bali wote wafikilie toba” (2 Petro 3:9). Yesu anatusihi sana sisi,anasema, “njoni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa namizigo, nami nitwapumzisha” (Mathayo 11:28). Lakini basi, kwa namnaisiyosadikika, wengine wanautupilia kando mwaliko huo uliojaa neema.
4.Je! U Tayari Kwa Kuja Kwake Yesu?
Ilimgharimu sana Yesu kutuhakikishia sisi yale maisha mazuri sana ya sikuza mbele “nyumbani mwa Baba ya[ke].” Ilimgharimu uhai wake!
KADHALIKA KRISTO NAYE AKIISHA KUTOLEWA SADAKA MARAMOJA azichukue dhambi za watu wengi; Pasipo dhambi kwa haowamtazamiao kwa wokovu” – (Waebrania 9:28).
Mwokozi yule aliyekufa juu ya msalaba ilikuzichukua dhambi zako, atatokea “mara yapili” naye atawaletea wokovu walewanaomngojea.” Kristo alijitoa sadaka yeyemwenyewe ili kutupatia sisi wokovu, yaani,kila mmoja wetu. Lakini pasipo kuja kwakemara ya pili, msalaba ule usingefaulukutokana na kazi yake aliyoifanya. Kristoanataka kutupatia sisi makao salamapamoja naye milele zote. Ili jambo hili lipatekutimizwa, yatupasa sisi kumruhusu yeye iliatawale ndani ya mioyo yetu kama Mwokozina Bwana wetu kuanzia hivi sasa.
Alfajiri moja ya tarehe 16, Agosti, 1945mvulana mdogo alikimbia kupitia katikakiwanja cha Shantung katika China yakaskazini, akipiga makelele na kusemakwamba ameiona ndege angani. Wafungwawote wenye miili yenye nguvu wakakimbiana kutoka nje na kutazama juu. Wanaumehao pamoja na wanawake walikuwa wameteseka sana kwa miaka mingi yakukaa upweke, umaskini, na wasiwasi, wakiwa wamefungwa na Wajapanikama raia wa mataifa yale ya kiadui. Kwa wengi wao kitu kimoja tu kilikuwakimewafanya kuwa hai kiroho: tumaini kwamba siku moja vita ile ingekoma.
Mshtuko kama wa umeme vile ukaenea katika lile kundi la wafungwa 1500waliokuwa wangali hai walipotambua kwamba ndege ile ilikuwa inakuja kwaajili yao. Mlio wa ndege ile ulivyozidi kuwa mkubwa zaidi na zaidi, mtu fulanimmoja akapiga kelele, akasema” Tazama, ile ni BENDERA YAKIMAREKANI imechorwa pembeni kwa rangi!” Nao wakiwa wamepigwa nabumbuazi kwa kutokuamini kwao, sauti zikapiga makelele, “Tazama,WANATUPUNGIA mikono! Wanajua sisi ni akina nani. Wanakujakutuchukua.”
Kwa wakati huo ulikuwa ni zaidi ya vile walivyoweza kumudu kuuzuia watuwale waliovaa nguo zenye viraka, waliokuwa wamechoka sana, na wenyeshauku ya kurudi nyumbani kwao ambao walikuwa wameendelea kuwa hai.Vurumai ikazagaa pote. Watu walikuwa wakikimbia katika miduara,wakipiga makelele yao kwa nguvu zao zote, wakipunga hewani mikono yaona kulia.
Ghafla kundi lile likaanza kuhema kwamshangao na kukodoa macho kimya kimya.Sehemu ya chini ya ndege ikafungukaghafla na watu wakaanza kuelea anganiwakishuka chini kwa miavuli. Waokoaji waowalikuwa hawaji tu siku fulani moja yabaadaye; walikuwa wanakuja leo, SASAHIVI ili kuwa miongoni mwao!
Kundi lile likasonga mbele kuelekea kwenyelango la uwanja ule. Hakuna aliyesimamana kuwaza juu ya zile bunduki za rashashazile zilizokuwa zimeelekezwa chini kwaokutoka kwenye minara ile. Baada ya miakamingi ya kukata tamaa na upweke,wakalivunja lile lango na kutimua mbiokuelekea mahali kule walikokuwa wakituawale askari wa miavuli.
Punde si punde gharika ya wanadamu ikarudi na kuingia kwa wingi ndaniya kambi ile – wakiwabeba wale askari mabegani mwao. Mkuu wa kambiakasalimu amri bila kupigana. Vita vilikuwa vimekwisha kweli. Uhuruulikuwa umekuja. Ulimwengu uligeuka na kuwa mpya kabisa tena.
Upesi Mungu WETU, yaani, Mwokozi WETU, atashuka kutoka mawingunikuja kutuokoa sisi. Kisa hiki cha kuogofya sana cha muda mrefu sana chaukatili wa mwanadamu kwa mwanadamu mwenzake hatimaye kitakomakabisa. Patakuwa na shangwe kuu siku ile, makelele ya furaha hatimayetutakapojua kwamba: “Anakuja karibu sana nasi; naweza kuwaona malaikawakizipiga zile tarumbeta zao.” Sauti inazidi kuwa kubwa zaidi, wingu lilelenye utukufu linazidi kung’aa zaidi na zaidi, mpaka sisi tunashindwakustahimili kuliangalia. Lakini basi, sisi hatuwezi kuacha kuliangaliatunapotambua kwamba: “Yeye ananiona mimi! Anajua mimi ni nani.” Tukiwatumejaa furaha isiyoelezeka tutajua, tutasema: “huyu ndiye Mungu wangu.Anakuja kwa ajili yangu, sio siku fulani ya baadaye, bali leo, sasa hivi.”
Je, wewe uko tayari kumpokea huyo mfalme (mtawala) katika utukufu wakewote kama siyo, basi, tafadhali mwalike Yesu wewe mwenyewe ili aingiendani ya maisha yako sasa hivi. Kama vile kuja kwa Yesu katika dunia yetuhii kutakavyoyatatua matatizo ya ulimwengu huu, ndivyo kuja kwake ndaniya moyo wako kutakavyokusaidia wewe kushughulika na matatizo yako yasasa ya kila siku. Mtatuaji mkuu wa matatizo anaweza kukuokoa wewekutokana na hatia na mzigo wako wa dhambi na kukupa wewe uzima wamilele.
Kuja kwa Yesu katika maisha ya mtu kunaweza kuyabadilisha milele kwanamna ya kuvutia sana kama kuja kwa Yesu kutakavyoibadilisha kabisa.Unaweza kumtegemea Yesu. Atakutayarisha wewe kwa ajili ya kuja kwakena kukupa ahadi ya ajabu ya maisha yale ya milele yenye furaha.