JE! NI MAPEMA KIASI GANI YESU ATARUDI?
Karibu wengi wetu tunao msukumo ambao kwa jumla ni wa kisilika wakutamani mambo yale yatakayotokea baadaye. Tunataka kujua ni kitu ganikilicho mbele ya upeo wa macho yetu. Lakini utabiri uliosahihi hutelezavibaya sana. Tunao wakati mgumu wa kutosha kuweza kujaribu kubashirihali ya hewa itakayokuwako kesho!
Lakini yuko Mmoja ambaye unabii wake umethibitika kwamba ni sahihi kwanamna ya kustaajabisha sana. Yesu Kristo, kupitia katika Neno lake,anaweza kutuchukua mpaka siku zile za usoni; yeye ni kiongozianayetegemewa. Katika somo hili tutaangalia kile alichosema yeye juu yakuja kwake mara ya pili. Kwa vyo vyote vile, ni nani, basi, ambayeangeweza kujua mengi sana juu ya mwisho wa dunia hii zaidi ya yulealiyeiumba pale mwanzo?
1.Ishara Zionyeshazo Kwamba Kristo Atarudi Katika Siku Zetu
Baada ya Yesu kuwaahidi wanafunzi wake kwamba angekuja tena katikaulimwengu huu kwa mara yake ya pili (Mathayo 23:39), je! ni swali ganiwalilomwuliza?
“Tuambie,’ wakasema,’mambo hayo yatatokea lini,tena, patakuwa na dalili ganiya kuja kwako, na yamwisho wa dunia?” -(Mathayo 24:3).
Yesu alijibu waziwazi napasipo shaka lo lote. Katikasura ya 24 ya Mathayo nasura ya 21 ya Luka yeyemwenyewe aliwapa “ishara”kadhaa, au ushahidi, ambao kwa huo sisi tunaweza kujua kuja kwakekunapokaribia. Unabii mwingine wa Biblia unasaidia kuijazia picha hiyo,unaonyesha kwa kinagaubaga hali ya dunia hii itakavyokuwa kabla tu yakurudi kwake Kristo.
Kama tutakavyoweza kuona, unabii huo unaendelea kutimia kabisa mbeleya macho yetu; unaonyesha kwamba kuja tena kwa Kristo kumekaribiasana.
Hebu na tuviangalie vibao kumi vya ishara za unabii wa Biblia vilivyo katikanjia ile kuu ya kwenda mbinguni, na kuyachunguza maswali ambayo msafiriwa siku hizi anaweza kuuliza anapovisoma vibao hivyo.
Kibao-cha-Ishara ya 1 – Dhiki! Hofu Kuu Mfadhaiko!
Zaidi ya miaka elfu moja na mia tisa iliyopita Yesu alitoa maelezo ya unabiiunaohusu maisha ya siku hizi yasikikayo kana kwamba yangeweza kuwayamechukuliwa kutoka katika habari za jioni hii:
“Tena, kutakuwa na ishara katika jua, na mwezi, na nyota; na katikanchi dhiki ya mataifa wakishangaa kwa uvumi wa bahari namsukosuko wake; watu wakivunjika mioyo kwa hofu, na kwakutazamia mambo yatayoupata ulimwengu. Kwa kuwa nguvu zambinguni zitatikisika. Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika wingu pamoja na nguvu na utukufu mwingi. Basi mambohayo yaanzapo kutokea changamkeni mkaviinue vichwa vyenu, kwakuwa ukombozi wenu umekaribia” – Luka 21:25-28.
Hakuna maelezo yaliyo sahihi zaidi juu yadunia yetu ya leo kama yalivyo manenohaya: ‘Watu watazimia kwa hofu,wakitazamia mambo yatakayoipata duniahii.” Silaha kali zilizolundikana zina uwezowa kuiteketeza sayari hii yote. Itakuwaje,basi, endapo gaidi mmoja atakipatakichwa kimoja cha nyuklia?
Yesu anatupa sisi msingi wa kuwa natumaini katika kizazi hiki chenye maafamakubwa. Hali iliyopo sasa ya hatariinayoikabili dunia hii nzima itakayoleta “dhiki na mfadhaiko” inautilia tunguvu ukweli usemao kwamba kuja kwake Kristo “kunakaribia.” Watu sikuhizi huomboleza mara kwa mara na kukata tamaa, wakisema, “Tazamailivyo dunia hii!” Lakini mwanafunzi wa unabii wa Biblia anaweza kusemaghafla kwa sauti iliyojaa matumaini, akisema, “Tazama, NI NANI HUYOajaye katika dunia yetu.”
Kibao-cha-Ishara ya 2: Maafa katika Dunia hii
Je! maafa haya ya asili yanaingiaje na kukubaliana na matukio ya siku zamwisho?
“Kutakuwa na MATETEMEKO makubwa ya nchi, na njaa na TAUNImahali mahali, na mambo ya kutisha na ishara kuu kutoka mbinguni…Nanyi kadhalika mwonapo mambo hayo yanaanza kutokea, tambueniya kwamba UFALME WA MUNGU U KARIBU” (Luka 21:11,31).
Hebu fikiria habari za njaa kwadakika moja. Picha za watotowanaokufa kwa njaa wenyematumbo yaliyovimba huendeleakutangazwa katika habari. Je!hilo sijambo la kushangaza sanakwamba dunia hii inayowezakuwatuma watu mwezini, HAIWEZIkuwalisha watu wake wote? Yesualijua kwamba njaa ingeendeleakuwako, kwamba tabia ya uchoyoya kibinadamu ingezidi kuwambaya zaidi na zaidi karibu na ule mwisho wa wakati.
Lakini, je! vipi kuhusu hayo matetemeko ya nchi? Kwa mujibu wa WorldAlmanac ya 1999, karne baada ya karne za kipindi hiki cha kikristopamekuwa na ongezeko la kustaajabisha la matetemeko makubwa ya nchi:karne ya kumi na nane palikuwa na matetemeko makubwa ya nchi 6; karneya kumi na tisa yalikuwa 7; karne ya20 yalikuwa zaidi ya 100. Kwa hiyoushahidi unazidi kuwa wa kuvutia zaidi na zaidi kadiri tunavyokaribiakuzifikia siku hizi zetu.
Takwimu hizo zinauthibitisha unabii ule alioutoa Yesu. Njaa na matetemekomakubwa ya nchi yanazidi kuongezeka taratibu – yakisema, “ufalme waMungu umekaribia!” Je! karne yetu hii ya ishirini na moja italetamatetemeko makubwa ya nchi mengi zaidi, au itakuwa ni kuja kwa yuleMfalme wa wafalme?
Kibao-cha-Ishara ya 3: Kujilimbikizia mali.
Hivi maana yake ni nini kwamba utajiri unateleza na kuingia katika mikonoya watu wachache kwa wingi zaidi na zaidi, huku watu wengi zaidi na zaidiwakizidi kuwa maskini?
“Mmejiwekea akiba katika siku za mwisho” – (Yakobo 5:3).
Licha ya ujuzi wetu wote wa uchumi, matajiri wanazidi kuwa matajiri, namaskini wanazidi kuwa maskini. Utajiri wa kuwa na mamilioni mengi ya dola [za Kimarekani] ni kibao-cha-ishara kingine kituonyeshachokwamba “kuja kwake Bwanakunakaribia” (fungu la 8).
Kibao-cha-Ishara ya 4 -Misukosuko ya Kiraia
Kwa nini hali hii ya kutoridhikana misukosuko miongoni mwawafanyakazi imeongezeka kwanamna inayojionyesha wazimno?
“Angalieni! Ujira wa wakulima waliovuna mashamba yenu ninyimliouzuia kwa hila unapiga kelele dhidi yenu na . VILIO VYAO VYAWALIOVUNA vimeingia masikioni mwa Bwana wa majeshi… Nanyivumilieni mthibitishe mioyo yenu kwa maana KUJA KWAKE BWANAKUNAKARIBIA” – (Yakobo 5:4,8).
Baada ya kutabiri dhidi ya kujilimbikizia mali nyingi zisizo na idadi katikasiku hizi zetu, Yakobo aliona misukosuko ya watu ikitokana na wafanyakaziwasioridhika. Migogoro iliyopo kati ya wale”walio nacho” na wale “wasionacho” inazidi kuongezeka. Hiyo ni ishara nyingine inayoonyesha kwamba”kuja kwake Bwana kunakaribia.”
Kibao-cha-Ishara ya 5: Mmomonyoko wa Maadili
Mbona uzi wa maadili ya jamii unaonekana kana kwamba unakatikavipande vipande?
“Lakini ufahamu neno hili; ya kuwa siku za mwisho kutakuwako naNYAKATI ZA HATARI. Watu watakuwa wakijipenda wenyewe, wenyekupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana,wasiowatii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, wasio wapendawa kwao, wasiotaka suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali,wasiopenda mema, wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendaoanasa kuliko kumpenda Mungu – wenye mfano wa utauwa, lakiniwakikana nguvu zake hao nao ujiepushe nao…. LAKINI WATUWABAYA NA WADANGANYAJI WATAENDELEA, NA KUZIDI KUWAWAOVU, wakidanganya na kudanganyika” – (2 Timotheo 3:1-5,13).
Je! kuna mtu ye yote ambaye angewezakufikiria na kutoa maelezo yaliyo sahihizaidi ya hayo kuihusu hii dunia yetu?Hebu elekeza kamera yako upande wowote katika hizi siku tulizo nazo, naweutapiga picha inayoonyesha ufedhuliutokanao na ile tamaa ya kupenda anasaza ulimwengu huu. Utainasa picha yakushtua inayoonyesha ukatili wakuwatenda vibaya watoto wadogo,pamoja na maudhi yanayoletwa kwa makusudi mazima. Utapata matukiomengi yasiyo na idadi ya vijana wasioweza kudhibitika kabisa, pamoja nawatoto walio katika ule umri wa miaka ya mwanzo ya ujana wao, yaani,kuanzia miaka kumi na mitatu na kuendelea juu kidogo, ambao wanawauawatu ovyo ovyo na kuwafanya watu vilema. Mambo hayo yote yanajengachumba kidogo kirefu ambacho kinaonyesha picha zinazotangaza kwasauti kuu kwamba kuja kwake Yesu kumekaribia sana.
Kibao-cha-Ishara ya 6: Kuenea kwa Dini za Siri (Kiinimacho)
Hivi kwa nini tunauona mlipuko wa kupendezwa sana na dini za siri (occult)miongoni mwa watu?
“Kwa maana watatokea wakristo wa uongo, na manabii wa uongo, naowatatoa ishara kubwa na maajabu [miujiza] wapate kuwapoteza kamayamkini hata walio wateule” -(Mathayo 24:24).
Vifungu hivi vya maneno vinatabiri kwamba wakati huu wa mwishoitaonekana miujiza ya kila namna, pamoja na ishara, yaani maonyesho yabandia ya uwezo usio wa kawaida kwa wanadamu. Wanawake wachawi na wanaume wachawi wafanyao uchawi wa Kiafrika wataonekana katikamaonyesho mbalimbali wakizungumza. Waumini wa Kizazi Kipya (NewAge) wako kila mahali, wanauza vijiwe vya uchawi vinavyong’aa kama kioona maajabu hayo ya uongo hujitokeza ghafla kwa wingi. Hayo yotehuyafanya mambo yawe wazi zaidi kama Yesu alivyotabiri kwamba sisitunaishi katika kipindi cha “kuja kwake Mwana wa Adamu” (fungu la 27.)
Kibao-cha-Ishara ya 7 – Dunia Iliyozinduka
Huko kuzinduka kunakohusu mambo ya dunia hii kunamaanisha nini kwaAfrika, Mashariki ya Kati, Ulaya Mashariki, na kwa matatifa yale yaMashariki ya Mbali?
“‘MATAIFA NA WAJIHIMIZE;… haya utieni mundu, maana mavunoyameiva… kwani uovu wao ni mwingi sana!’ Makutano makubwa,makutano makubwa, wamo katika bonde la kukata maneno [kuamuamwisho wa kila mtu]” – (Yoeli 3:12-14).
Leo hii katika nchi za Asia na Afrika, UlayaMashariki, Muungano wa Zamani waKisovieti, na nchi za Mashariki ya Kati,huenda sisi tunashuhudia kuona mwamkomkubwa sana wa tatifa moja moja katikahistoria yote iliyopata kuandikwa, “kwamaana siku ya BWANA I KARIBU.”
Kibao-cha-Ishara ya 8 – Mipango ya Amanina Maandalizi ya Vita
Tunaishi katika ulimwengu huu wa ajabu.Kila mmoja anaafiki kwamba tungeipatianafasi amani; lakini basi, zile chuki zilizokandamizwa kwa kipindi cha karnefulani zilizopita, zinalipuka na kuwa vita ya wazi. Nabii Mika na Yoeliwalitabiri kwamba wakati ule ule mataifa yatakapokuwa yanasema juu yashauku yao ya kuwa na amani (Mika 4:1-3) watalazimika kujiandaa kwa vitakutokana na shauku yao waliyo nayo dhidi ya majirani zao (Yoeli 3:9-13).
Zamani sana Biblia ilionyesha picha hii ya mgogoro wetu wa sasa wa kuwana amani au vita, kisha ikatangaza kwamba amani ya kudumu itatawalakatika dunia hii wakati ule tu Yesu atakapokuja.
Kibao-cha-Ishara ya 9 – Maendeleao ya kisasa
Mbona usafiri na mawasiliano vimeuleta ulimwengu huu kuwa karibu mnobaada ya karne nyingi za historia ya wanadamu?
“HATA WAKATI WA MWISHO, wengi wataenda mbio huko na hukomaarifa yataongezeka” – (Danieli 12:4).
Hapo Danieli anadokeza kwamba maarifa ya kuuelewa unabii wakeyataongezeka “katika” (KJV), au “hata wakati wa mwisho.” Lakini utabirihuo pia unaonekana kana kwamba unasonda kidole chake kwenye kizazichetu hiki kilichoyaweka maarifa katika kompyuta. Maarifa ya kila namnayameongezeka kwa kasi kubwa inayolandana na umeme katika miaka hiimichache iliyopita. Pamekuwako na mabadiliko mengi sana katika kipindicha miaka hamsini iliyopita kuliko katika kipindi kile cha miaka elfu mbilikabla yake.
“WENGI WATAENDA HUKU NA KULE kuongeza maarifa.” Kabla ya mwakaule wa 1850, watu walisafiri kwa magari yaliyovutwa na farasi, ikiwa karibusawa kabisa na vile ilivyokuwa tangu mwanzo wa wakati. Hivi sasatunasafiri kasi kuliko sauti na kuizunguka dunia hii kwa ndege za konkodi(concorde) hata kwa roketi za safari fupi katika anga za juu.
Ongezeko la safari na gharika ya uvumbuzi ya hivi karibuni hutoa ushahidimwingine zaidi kuonyesha kwamba sisi tunaishi “katika siku za mwisho.”
Kibao- cha- Ishara ya 10 – Injili Ulimwenguni Kote
Yesu alitabiri kwamba, muda mfupi tukabla ya kuja kwake, injili ingefikakatika ulimwengu wote:
“Tena habari njema ya ufalmeitahubiriwa katika ulimwengu wote,kuwa ushuhuda kwa mataifa yote,hapo ndipo ule mwisho utapokuja” -(Mathayo 24:14).
Kwa miongo mingi [makumi mengi yamiaka] karibu nusu ya dunia hii ilikuwaimefungiwa nyuma ya pazia la chuma, ilifungiwa mbali na ile Habari Njema.Lakini baadaye, karibu kwa usiku mmoja Ulaya Mashariki iliteleza kutokakatika kubanwa na chuma cha Ukomunisti. Ukuta wa (Berlin) ukaangukachini na kuvunjika vipande vipande, na ile dola yenye nguvu nyingi yaKisovieti ikasambaratika. Ghafla karibu nusu ya sayari hii ilikuwa ikinyooshamikono yake ili kuipokea injili.
Injili hii inakwenda katika “ulimwengu wote” kwa namna isivyopatakufanyika katika siku zile za nyuma. Kwa njia ya Satelaiti ujumbe waKikristo kwa wakati uo huo unaendelea kutangazwa karibu kwa kila taifa.Tunaishi katika kipindi kile kile hasa ambacho Yesu alisema habari zakealipotangaza hivi: “Injili hii itahubiriwa katika ulimwengu wote.”
2.Ni Mapema Kiasi Gani Yesu Atakuja?
Baada ya kuyaelezea yale matukio yaliyokusudiwa kuonyesha kipindi kilekinachotangulia muda mfupi tu kabla ya kuja kwake mara ya pili, Yesuanahitimisha maneno yake kwa kusema hivi,
“Amini nawaambia, kizazi hiki hakikahakitapita, hata hayo yote yatakapotimia ” -(Mathayo 24:34).
Hitimisho hilo ni dhahiri – yaani, kizazi hichokilichodokezwa kwa hivi vibao-vya-ishara zaunabii ndicho kitakachojaliwa kumwona Yesuakirudi duniani mara ya pili. Muda hautakuwamrefu hadi hapo atakapoifagilia mbali dhambina mateso, na kuusimika ufalme wake ule wamilele. Yesu anatutahadharisha sisi, anasema,”Hakuna aijuaye.. siku ile au saa ile” (fungu la36.)
Tena, Yesu anaendelea kusema hivi:
“Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekenitayari, kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja” -(Mathayo 24:44).
3.Yesu, Tumaini Pekee La Dunia Hii
Kristo ndiye tumaini bora la mwisho kwa dunia yetu hii kwa kuwa ni yeyepeke yake awezaye kukishughulikia hasa kitu kile kile kinacholivunjilia mbalihilo tumaini – yaani, ile dhambi. Yesu alikufa pale kalwari kufanyauwezekano uwepo wa kuyashinda maovu na kuwapatia ukombozi walewote wanaoitikia na kuupokea wokovu wake.
“Atendaye dhambi [avunjaye Amri Kumi] ni wa Ibilisi, kwa kuwa Ibilisiamekuwa akitenda dhambi [akizivunja Amri Kumi – Yn. 8:44) tangumwanzo. Sababu ya kuja kwa Mwana wa Mungu ilikuwa ni kuzivunjiliambali kazi za Ibilisi” – (1 Yohana 3:8).
Mwokozi wetu alitayarisha njia ya kututoa kutoka katika dunia yetu hiiinayovunjika-vunjika kwa kutoa kafara mwili wake na damu yake. Na Yesuyule yule, ambaye siku moja atayaponya magonjwa ya dunia hii kwakuiteketeza dhambi, hivi sasa anakupa wewe haki yake inayoifutilia mbalihatia ya dhambi katika maisha yako. Huna haja ya kungoja mpaka siku yakuja kwake mara ya pili ili upate kuwekwa huru mbali na hatia yako nambali na wasiwasi wako pamoja na ile tabia yako ileayo uharibifu. Yesu yutayari sana kukupa wewe amani yake katika dakika hii hii.
Mwanamke mmoja kijana alipokuwaakiendelea kuhudhuria katika mikutano yadini aliguswa moyo wake kiajabu na injiliiliyohubiriwa pale. Aliposikia ikifunuliwahabari ya kuja upesi kwa Mwokozi, kila kitukikaingia vizuri mahali pake. Habari ileilileta maana kwake. Yeye katika nia yakealikuwa akitafuta upendo, furaha, na amanikutoka kila mahali palikuwa pabaya. Yesuakawa jibu lake.
Siku iliyofuata wakati mwinjilisti yule namwenzake walipokwenda kumwona,aliwasimulia habari yake yote ya maishayake machungu na yaliyojaa uhalifu.Alikuwa amezama mpaka chini sana kamamlevi sugu, tena alikuwa akipata riziki yakekwa kufanya umalaya. Baada ya kuelezamatatizo yake, alisema hivi huku akilia,”Ulikuwa unanisema mimi hasa jana usiku.”
Lakini ile sauti iliyougusa moyo wake ilikuwa ni sauti ya Mungu. Nayealikuwa akisema kwa upole. Aliamua kutoa yote. Alimkaribisha Kristokuingia moyoni mwake kama Bwana na Mwokozi wake, na kulishikilia sanalile tumaini la kuja kwake upesi.
Katika majuma yale yaliyofuata, akaanza kugundua kwamba zile hofu zakena kutokujisikia salama kwake ambako siku zote alkuwa amejitahidi sanakukuzima kwa kunywa vileo, sasa kulikuwa kumempa nafuu kiasi cha yeyeakaanza kumwokoa na kumweka mbali na ile misukumo mibaya iliyokuwaikimlazimisha kufanya mambo yale mabaya na kuyaharibu maisha yake.
Alikuwa amefanya mambo mengi sana ambayo hakuweza kujivunia. Lakinineema yake Kristo na msamaha wake vilikuwa na nguvu nyingi sana kulikoile aibu yake. Uzoefu wa maisha aliokuwa nao yule mwizi pale msalabaniulikuwa wa maana sana kwake yule mwanamke. Katika dakika zake zile zamwisho, akitapatapa na kutaka kufa, alimgeukia yule Mteswaji Asiye naHatia alikuwa kando yake na kumwomba, akasema, “Ee Yesu, unikumbukemimi utakapokuja katika ufalme wako” (Luka 23:42). Yesu yule yule aliyetoamsamaha wake kwa wingi kwa yule mwizi aliyekuwa akifa, hivi sasaanakupa wewe wokovu, msamaha kamili, na amani moyoni mwako. Hebuleo hii gundua hayo wewe mwenyewe.
Wewe pia unaweza kuomba pamoja na yule mwizi aliyekuwa akifa, nakusema:
“Ee Yesu, unikumbuke mimi utakapokuja katika ufalme wako.” Naye Yesuatakujibu hivi, “Nitakuja tena, nawe utakuwa pamoja nami katika Paradiso”
Asante sana. Walioitupa sabato ya Mungu wataenda mbinguni nao?
Kimsingi, maandiko yanabainisha kuwa mamlaka ya mwisho ya kuamua nani anaingia mbinguni yako mikononi mwa Mungu pekee. Biblia inasema katika 1 Samweli 16:7 kuwa wanadamu hutazama nje, bali Mungu hutazama moyo.
Hapa kuna mambo makuu yanayozingatiwa katika mjadala huu:
1. Mtazamo wa Amri za Mungu
Wale wanaoamini kuwa Sabato ni amri ya milele mara nyingi hurejea fungu la Kutoka 20:8-11, linalosema, “Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.” Hoja hapa ni kwamba amri kumi ni kioo cha tabia ya Mungu, na kuvunja amri moja ni sawa na kuvunja zote (Yakobo 2:10). Kwa mtazamo huu, kuitupa Sabato kwa makusudi baada ya kuijua kweli kunaonekana kama uasi dhidi ya mamlaka ya Mungu.
2. Mtazamo wa Neema na Imani
fundisho la mwanadamu haokolewi kwa kushika sheria, bali kwa neema kupitia imani katika Yesu Kristo (Waefeso 2:8-9). Kwa mtazamo huu:
Wokovu ni zawadi ya bure.
Matendo (ikiwemo kushika Sabato) ni matokeo ya wokovu, siyo sharti la kuupata.
Wanaamini kuwa Kristo ndiye “pumziko” letu la kweli, na kumpokea yeye ndiko kunakompa mtu haki ya kuingia mbinguni.