KUHUSU MAMBO YAKO YA BAADAYE
Madaktari Patricia na David Mrazek walikuwa wamelemewa na huzunikubwa sana katika kazi yao. Kama mabingwa wa magonjwa ya watoto,waliwashughulikia watoto wengi waliokuwa wakiumwa. Lakini waligunduaukweli kwamba baadhi ya watoto walitoka katika hatari yao ya kufisha nakupata nguvu mpya, ambapo wengine waliangamizwa nayo. Kwa nini?Mathalani, kwa nini mtoto mmoja atumie madawa ya kulevya wakati yulemwingine anakwenda kusoma chuoni? Kwa nini baadhi ya watotowaliotendewa vibaya wanakua na kujitendea vibaya wenyewe, wakatiwengine wanakuwa wazazi wazuri?
Akina Mrazek hao walifanya utafiti wao mpana sana ili kupata majibu kwamaswali hayo. Katika uchunguzi wao tabia moja iliyozidi zote ilizidikujitokeza miongoni mwa watoto wale walionusurika kutoka katika kiwewechao na kuendelea kuwa na maisha “ulikuwa ni ule mtazamo wa maishauliojengwa juu ya mwelekeo wa kutazamia kuyaona mambo mazuri siku zambele na kuwa na matumaini.”
Kuwa na tumaini kulileta tofauti ile. Tumaini, kuliko kitu kinginecho chote,linatusaidia sisi kuyashinda mambo ya ajabu-ajabu yanapokuja kwa wingisana dhidi yetu.
Wanadamu wanalihitaji tumaini sana. Lakini, je! tunalipataje? Tumaini katikaulimwengu wetu huu ni vigumu kuliona – MPAKA tuliangalie kwa mtazamowa unabii wa biblia. Mwongozo huu wa GUNDUA unauchunguza unabii ulewa maana sana uliowatia tumaini lenye nguvu watu wengi wasio na idadi.
1.Unabii wa Biblia Unaoshangaza
Karibu miaka mia tano hivi kabla ya kuzaliwa kwake Kristo, Mungu aliupaulimwengu huu mtazamo wa haraka wa mambo ya mbele unaoshangazasana kupitia kwa nabii Danieli. Mungu alitoa muhtasari wa historia yaulimwengu huu miaka 2,500 kabla ya kutokea, kuanzia wakati ule waDanieli mpaka siku zetu hizi.
Unabii huo ulianzia katika ndoto ambayo Mungu alimpa Nebukadreza,Mfalme wa Babeli, yapata mika 2,500 hivi iliyopita. Ndoto ile ilimsumbuasana mfalme yule – lakini hakuweza kuikumbuka ndoto ile alipoamka kutokausingizini! Baada ya wenye hekima wote wa Babeli kushindwa kumsaidiamfalme yule kuikumbuka ndoto yake au kuifasiri, kijana mmoja Mwebrania,aliyekuwa kule uhamishoni, kwa jina Danieli, alijitokeza kwenye mandhariile, akidai kwamba Mungu wa Mbinguni alikuwa na uwezo wa kuzifunua sirizote.
Akiwa amesimama mbele ya mfalme yule, akanena kwa ujasiri, akasema
“Wewe, Ee, mfalme, ulitazama, na pale mbele yako ilisimama SANAMUKUBWA – sanamu kubwa sana, inayong’aa.
“Kichwa cha sanamu ile kilitengenezwa kwa dhahabu safi, kifua namikono yake ni ya fedha, tumbo lake na mapaja yake ni ya shabanyekundu, miguu yake ni ya chuma, na nyayo zake nusu za chuma nanusu za udongo wa mfinyanzi uliochomwa.
“Ulipokuwa ukiangalia, jiwe lilichongwa, lakini si kwa mikono yawanadamu. Likaipiga ile sanamu katika nyayo zake za chuma naudongo na kuivunja vipande vipande.
“Ndipo kile chuma, na ule udongo, na ile shaba nyekundu, na ilefedha, na ile dhahabu, vikavunjwa vipande vipande wakati ule ule na kuwa kama makapi juu ya sakafu yakupepetea wakati wa kiangazi.Upepo ukavipeperusha mbali bilakuacha kitu cho chote mahali pake.Lakini ULE MWAMBA ULIOIGONGASANAMU ILEukawa mlima mkubwa,UKAIJAZA DUNIA YOTE” – (Danieli2:31-35).
Sanamu hiyo, kwa kuitupia jicho maramoja, yaweza kuonekana kanakwamba haina kazi sana kuwezakutupatia sisi tumaini katika nyakatihizi tunazoishi, lakini wewe endelea tukusoma habari zake.
2.Unabii Watafsiriwa
Baada ya kumsimulia Nebukadrezaaliyekuwa amevutiwa sana na kilealichokuwa amekiona hasa katikamaono yake, nabii Danieli alitoaufafanuzi wake:
“Hii ndiyo ile ndoto, na sasa tutaifasiri kwa mfalme” – (Danieli 2:36).
KICHWA CHA DHAHABU: Je, ni mamlaka ganiya dunia ambayo Danieli alimwambia yulemfalme kuwa ilionyeshwa kwa mfano wa kichwacha dhahabu?
“Wewe, Ee mfalme, u mfalme wa wafalme.Mungu wa mbinguni amekupa wewe ufalmena uwe, na nguvu, na utukufu…. WEWE UKICHWA KILE CHA DHAHABU” – mafungu ya37,38).
Danieli alikuwa anampasha habari hizi mtawala yule wa dola kubwa kulikozote ulimwenguni: “Nebukadreza, Mungu anakuambia wewe kwamba dolayako, Babeli, imewakilishwa na kichwa hicho cha dhahabu cha hiyosanamu.”
KIFUA NA MIKONO YA FEDHA. Kwa mtazamowa kibinadamu Babeli ilionekana kama dolaambayo ingeweza kudumu milele. Lakini, je,unabii unasema kitu gani kitatokea baada yake?
“Baada yako, utainuka ufalme ulio mdogokuliko wako” fungu la 39.
Kwa kutimiza utabiri huo wa Mungu, ufalme ule wa Nebukadreza ulivunjikavipande vipande na kuwa magofu wakati yule Koreshi, Jemedari waKiajemi,
alipoiangusha dola ile ya Babeli mwaka ule wa 539 K.K. kwa hiyo, kifua namikono ya fedha huwakilisha Uamedi na Uajemi, dola nyingine yenyenguvu nyingi.
TUMBO NA MAPAJA YA SHABA NYEKUNDU:Sehemu hii ya sanamu ile kubwa ya madinihuwakilisha nini?
“Halafu, ufalme wa tatu, ufalme wa shabanyekundu, utatawala juu ya ulimwengu nzima.”-(fungu la 39).
Tumbo na mapaja ya shaba nyekundu ni mfano waufalme wa Uyunani (Ugiriki). Iskanda mkuu(Alexander the Great) aliwashinda Waamedi na Waajemi, na kuingizaUyunani kuwa dola kuu ya tatu ya ulimwengu . ilitawala kuanzia mwaka wa331 hadi mwaka 168 K.K.
MIGUU YA CHUMA:
“Hatimaye, patakuwa na ufalme wa nne [alisema yule nabii], wenye nguvu kama chuma – kwa maana chuma huvunjavitu vyote na kukishinda kila kitu – na kamachuma kisetavyo vitu hivi vyote, ndivyoutakavyovunja-vunja na kuseta zile nyinginezote.” -(fungu la 40).
Baada ya kifo chake Iskanda, dola yake ilidhoofikana kugawanyika katika makundi yanayoshindanampaka hatimaye katika mwaka ule wa 168 K.K,”Dola ya Chuma” ya Roma ikaishinda Uyunani katikavita ya Pydna.
Kaisari Augusto alitawala katika ile Dola ya Roma wakati alipozaliwa Yesumnamo miaka elfu mbili iliyopita (Luka 2:1). Kristo na mitume wake waliishikatika kipindi kile kilichowakilishwa na miguu ya chuma. Giboni,mwanahistoria wa karne ile ya kumi na nane, bila shaka mawazoni mwakealikuwa na unabii wa Danieli, alipoandika maneno haya: “Zile sanamu zadhahabu, au fedha, au shaba, ambazo zingetumika kuyawakilisha mataifana wafalme wao, zilivunjwa na kurithiwa na ufalme ule wa chuma waRoma” – Edward Gibbon, The History of the Decline and Fall of the RomanEmpire (John D. Morris and Company), gombo la 4, uk. 89.
Hebu kwa dakika moja tafakari juu ya utabiri huo kwa mtazamo wakibinadamu. Je, kwa vipi Danieli, aliyeishi katika kipindi kile cha Babeli,angekuwa na wazo lo lote kuhusu dola ngapi zingefuatana moja baada yanyingine mamia ya miaka katika siku zile za mbele. Sisi tunakuwa na wakatimgumu kukisia soko la biashara litakuwaje juma lijalo! Na, hata hivyo,Babeli, Umedi-Uajemi, Uyunani, na Roma zilifuatana kabisa moja baada yanyingine, kama vile ilivyotabiriwa – kama watoto wa shule watiifu ambaowamesimama katika mstari.
Je, Mungu anayadhibiti mambo yale ya baadaye? Je, tunaweza kuwa natumaini kwa kutegemea msingi wa mpango wake ule mkuu? Jibu lake ni”Ndiyo!” ivumayo kote.
NYAYO NA VIDOLEVILIVYOCHANGANYIKA CHUMANA UDONGO:
Je! kuna dola ya tano yaulimwengu mzima ambayoingefuata baada ya Roma?
“Na kama vile ulivyoziona nyayona vidole vyake kuwa vilikuwanusu udongo na nusu chuma, hivyo HUO UTAKUWA NI UFALMEULIOGAWANYIKA; hata hivyo, utakuwa na nguvu kiasi fulani zachuma ndani yake, kama vile ulivyoona kile chuma kimechanganyikana udongo wa mfinyanzi. Na chuma na nusu udongo, kadhalika ufalmeule utakuwa nusu yake una nguvu na nusu yake umevunjika” – (Danieli2:41,42).
Nabii huyo alitabiri, sio juu ya dola ya tano ya ulimwengu mzima, bali juu yamgawanyiko wa ufalme ule wa chuma wa Roma. Roma ingevunjika katikafalme kumi, kama ilivyowakilishwa na nyayo na vidole vya ile sanamu.
Je, jambo hilo lilitokea kweli? Hakika lilitokea. Katika kipindi cha karne ile yanne na ya tano ya kipindi kile cha Kikristo washambuliaji wa kishenzi(wasiostaarabika) kutoka kaskazini walimiminika kushuka chini kuja katikaDola ya Kiroma iliyokuwa inazidi kupungua nguvu zake, wakaipiga kipigobaada ya kipigo. Hatimaye kumi miongoni mwa makabila yale yakajipatiasehemu kubwa ya Roma ya Magharibi, na mataifa kumi tofautiyanayojitawala yenyewe yakajiimarisha katika mipaka ile ya Ulaya. Hivyovidole vile leo vinayawakilisha mataifa ya siku hizi ya Ulaya.
Vidole Kumi – Makabila Makuu Kumi Katika Dola Ya Roma Ya Magharibi
Anglo – Saxons Uingereza
Franks Ufaransa
Alemanni Ujerumani
Lombards Italia
Ostrogoths Wagothi wa Mashariki waliangamizwa baadaye
Visigoths Wagothi wa Magharibi au Hispania
Burugundians Uswis – Switzerland
Vandals Wavandali – Afrika Kaskazini,
waliangamizwa baadaye
Suevi Ureno
Heruli Waharuli – walitoweka baada ya karne chache tu
4.Mtazamo katika Wakati Ujao
Sehemu moja tu ya unabii wa Danieli bado haijatimizwa. Jiwe lile, je!linamaanisha nini ambalo linaipiga ile sanamu nyayoni, na kuisaga tikitiki,kasha ligeuka na kuwa mlima mkubwa unaoijaza dunia nzima?
“KATIKA SIKU ZA WAFALME HAO [mataifa ya siku hizi ya Ulaya(Magharibi)]. MUNGU WA MBINGUNI ATAUSIMAMISHA UFALMEambao hautaangamizwa kamwe, wala watu wengine hawataachiwa.Utazivunja falme hizo zote vipande vipande na kuzikomesha, lakiniWENYEWE UTADUMU MILELE NA MILELE” – (Danieli 2:44).
“Wafalme hao” huwahusu tu wafalme wale waliowakilishwa na nyayo navidole vya sanamu ile – yaani, watawala wa Ulaya (Magharibi) ya leo,huzionyesha siku zetu. Jiwe lile lililochongwa bila kutumia mikono yakibinadamu litaipiga hiyo sanamu na kuivunja vipande vipande, kishalitaijaza dunia nzima (mafungu ya 34, 35, 45). Yesu atashuka hivi karibunikutoka mbinguni kuja ku “usimamisha ufalme,” huo, yaani, ufalme wakeuliojaa furaha na amani. Hapo ndipo Kristo, Mwamba wa Kale na mfalmewa wafalme, atakapoitwaa dunia hii milele hata milele!
Kila kitu katika utabiri wa Danieli 2 kimetimia isipokuwa lile tendo la mwishoyaani, kupigwa kwa sanamu hiyo na lile jiwe. Kulingana na ratiba yaMungu, hivi sasa tunakikaribia kilele kile kikuu, yaani, kurudi kwake Kristokatika dunia yetu. Yesu Kristo, Mwana wa Mungu yu karibu sanakulikomesha hilo pambano la umwagaji wa damu la muda mrefu katikahistoria ya kibinadamu na kusimamisha ufalme wake wa milele wa upendona neema.
5.Ndoto Ya Mfalme Na Wewe
Unabii huu hudhihirisha mkonowa Mungu uongozi katikakuinuka na kuanguka kwamataifa. Mungu anajuayaliyopita, na huo unabii waBiblia huonyesha wazikwamba yeye anajua mamboya baadaye pia.
Kama Mungu anaongozanyendo za mataifa kwa usahihimkamilifu kama huo, basi, nihakika kwamba anaweza kuyaongoza maisha ya kila mtu mmoja mmoja.Yesu alituhakikishia sisi kwamba: “Hata nywele za vichwa vyenuzimehesabiwa zote. Msiogope basi” (Mathayo 10:30-31). Zawadi ya Munguya imani inaweza kuwa dawa ya kupunguza wasi wasi na hofu zetu zote.Tumaini analoliamsha ndani yetu linaweza kuwa nanga ya roho zetu(Waebrania 6:19).
Erasmo, mtaalam wa Biblia wa karne ya kumi na sita, alisimulia habari zatukio moja lililotokea wakati wa safari yake baharini, ambayo ilichukuamaisha yake yote. Chombo alichokuwa anasafiria kilipwelea wakati wadhoruba. Mawimbi yenye nguvu yakakipiga, kikaanza kupasuka, hata
mabaharia walianza kuingiwa na hofu kuu. Abiria walikuwa karibukupagawa.
Wengi sana walipiga makele wakiomba msaada toka kwa mtakatifu waomlezi, waliimba nyimbo za kumsifu Mungu, au walimsihi sana Mungu kwasauti kuu katika sala zao.
Walakini, Erasmo alimgundua abiriammoja aliyekuwa tofauti. “Miongonimwetu sisi sote, “aliandika Erasmo,”yule aliyebaki akiwa ametulia karibukabisa alikuwa ni mwanamke mmojakijana aliyekuwa amempakata mtotowake mchanga aliyekuwa akiendeleakumnyonyesha. Yeye peke yake ndiyehakupiga makelele, hakulia, walakujaribu kupatana na mbingu.Hakufanya kitu kingine cho chote, balialiomba kimya kimya moyoni mwake huku akiendelea kumshikilia sanamtoto wake yule mchanga kwenye paja lake.”
Saa ile, Erasmo alitambua, ilikuwa ni kuendelea na maisha yake ya sala yakila siku. Alionekana kana kwamba amejikabidhi mwenyewe kwa Mungu.
Meli ile ilipoanza kuzama, mama yule kijana aliweka juu ya ubao, nakupewa mhimili wa kutumia kama kasia kisha akaachiwa apate kukabilianana yale mawimbi. Akalazimika kumshika mtoto wake kwa mkono mmoja nakujaribu kupiga kasia kwa mkono ule mwingine. Ni wachache mnowaliodhani kwamba atanusurika katika mawimbi yale yaliyokuwayameumuka.
Lakini imani yake na ule utulivu wake ulimweka katika hali nzuri. Yulemwanamke na mtoto wake walikuwa wa kwanza kufika pwani.
Tumaini kwa Mungu aliye mwaminifu linaweza kuleta tofauti kubwa sana -hata dunia yetu hii inapoonekana kana kwamba inapasuka pande zotekutuzunguka. Sisi hatuko kule nje kupiga kasia kwa kujitegemea wenyewe.Mkono mkubwa zaidi unatuongoza na kutushika.
Ukija kwa Kristo kwa kujitoa kwakekabisa, atakupa imani ambayoitakupitisha salama katika kiladhoruba. Gundua amani hii ipitayoufahamu wote ambayo Yesuanakuahidi kukupa:
“Amani nawachieni, amani yangunawapa….. Msifadhaike mioyonimwenu, wala msiwe na woga” -(Yohana 14:27.
Je! unayo amani hiyo? Kama unayo,basi, mshukuru Yesu, Mwokozi wako.Kama hunayo, kwa nini usimkaribishekatika maisha yako leo hii?