NAFASI YA PILI YA KATIKA MAISHA
Baada ya kuishi karibu maisha yake yote kama mfuasi wa Budha, mtu wamakamo mmoja katika nchi ya Singapore aliyekuwa amegeuka na kuwaMkristo aliulizwa swali hili, “Bwana Limu, je, wewe unaona tofauti gani katiya kuwa mfuasi wa Budha na kuwa Mkristo?
“Hilo ni rahisi,” alijibu. “Tangu mimi nimempokea Yesu kama Mwokoziwangu, nina amani nyingi ajabu moyoni mwangu.”
Hilo ndilo linalotokea tunapoyaweka maisha yetu ndani ya Kristo.
“Wewe [Mungu] utamlinda katika amani kamilifu, yeye ambaye moyowake umekutegemea, kwa kuwa anakutumaini” – (Isaya 26:3).
Kuishi maisha ya Kikristo huleta amani kamilifu – hisia kamili ya kuwa nausalama na raha.
Wale walioligundua hili wameiona njia pekee ya kupata nafasi ya pili yakuishi – yaani, kumpata Yesu!
1.Maana Ya Kupotea
Yawezekana kwa mtu aliye haikimwili kuwa na kile watu wenginewanachokiita kustarehe, na badoakawa amekufa – yaani, amekufakiroho.
“NANYI MLIKUWA WAFUKATIKA MAKOSA NA DHAMBIZENU, ambazo mlizoziendeazamani kwa kuifuata kawaida yaulimwengu huu na kwakumfuata mfalme wa uwezo waanga roho YULE [MWOVU] ATENDAYE KAZI SASA katika wana wakuasi” – Waefeso 2:1,2.
Shetani anamwongoza mtu yule aliyekufa kiroho na kushuka naye kuelekeachini ya ngazi ya dhambi na kutotii. Lakini kweli ile ya ajabu ya injili inasemakwamba Mungu anawapenda watu kama hao. Anawapenda wakiwawamekufa katika dhambi zao, kisha anawapa ukombozi kamili na wa bure[bila gharama] kutoka katika hatari yao.
“Lakini Mungu ni mwenye huruma nyingi. Alitupenda kwa pendolisilopimika, hata, ingawa tulikuwa tumekufa kwa sababu ya dhambi,alitufanya hai pamoja na Kristo. Kwa neema ya Mungu ninyimmeokolewa. Kwa kuungana na Kristo Yesu, Mungu alitufufua pamojanaye, tukatawale pamoja naye mbinguni. Ndivyo alivyopendakuonyesha kwa watu wa nyakati za baadaye ukuu wa neema yakealiyotujalia kwa ukarimu katika kuungana kwetu na Kristo Yesu” -(Waefeso 2:2-7).
Mungu alitupenda sisi tulipokuwa hatuna cha kupendeka ndani yetu.Neema yake iliweka ndani yetu maisha mapya ndani ya Kristo. Hatuwezikujibadilia wenyewe, ila Mungu anaweza. Tunapokuja kwake kwa imani na unyenyekevu, anatupa nafasi ya pili ya kuishi kama zawadi inayotolewabure.
2.Ni Kutoka Katika Nini Tunahitaji Kuokolewa?
(1)Twahitaji kuokolewa kutoka katika dhambi.
“Wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu” -(Warumi 3:23).
Kusema bila kuficha: sisi hatuishi kulingana na kile tunachojua kuwa nihaki. Mzazi akisongwa sana na matatizo hasira yake inaweza kulipuka nakumwumiza kihisia mtoto wake. Mtu fulani anaweza kumkasirikia sanadereva mwingine na kuwa karibu sana kusababisha ajali. Mwanafunzianaweza kuchukia na kusema maneno mabaya kwa kunong’ona dhidi yamwanafunzi mwingine. Mfanya biashara anaweza kupanga “kusahau”chanzo fulani cha mapato yake wakati wa kutozwa kodi. “Wote wamefanyadhambi”, hiyo ndiyo hali ya wanadamu.
Biblia inaelezaje maana ya dhambi?
“Kila lisilo la haki ni dhambi” – (1Yohana 5:17).
Tunahitaji kuokolewa kutoka katika aina zote za tabia zetu mbaya pamojana misukumo ya ndani inayotushurutisha kufanya mambo fulani mabaya:kama vile, kusema uongo, hasira inayomfanya mtu atukane watu, tamaambaya za mwili, uchungu, kutaja machache tu.
“Kila atendaye dhambi afanya uasi kwakuwa dhambi ni uasi” (1 Yohana 3:4).
Kwa ajili hiyo, sisi tunahitaji kuokolewakutoka katika dhambi – yaani, kutoka katikauvunjaji amri [kumi] za Mungu.
(2)Twahitaji kuokolewa kutoka katikauhusiano wetu na Mungu ambao ulivunjika.
“Lakini maovu yenu yamewafarikishaninyi na Mungu wenu; na dhambi zenuzimeuficha uso wake msiuone” – (Isaya59:2).
Dhambi ile isiyosamehewa inakata uhusiano wetu na Mungu. Kristo alikujakuturudishia tumaini letu kwa Mungu, ambalo Shetani alikuwaamelidhoofisha.
(3)Twahitaji kuokolewa kutoka katika mauti ya milele. – adhabu ya dhambi[kuvunja amri Kumi].
“Kwa hiyo kama mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwadhambi hiyo mauti, na kwa hivyo mauti ikawafikia watu wote, kwasababu wote wamefanya dhambi” – (Warumi 5:12).
(4)Twahitaji kuokolewa kutoka katika maisha yetu ya dhambi yasiyo nafuraha, yaliyo tupu.
Kwa mwenye dhambi, maisha ni kama mtaa uliofungwa mwisho wake.
(5)Twahitaji kuokolewa kutoka katika ulimwengu wenye dhambi.
Ni lazima tuokolewe kutoka katika ulimwengu uliojaa dhambi na athari zake-kama vile, umasikini, huzuni kubwa moyoni, upweke vita, magonjwa nakifo!
3.Ni Nani Awezaye Kutuokoa?
Yesu peke yake aweza kutuokoa sisi.
(1)Yesu aweza kutuokoa sisi kutoka dhambini.
“Naye atazaa mwana nawe utamwita jina lake Yesu, maana yeye ndiyeatakayewaokoa watu wake na dhambi zao” – (Mathayo 1:21).
Baniani [Mhindu] mmoja alimwambia rafiki yake Mkristo maneno haya,”Mimi napata mambo mengi katika dini hii ya Kihindu ambayo hayapatikanikatika Ukristo, lakini kuna kitu kimoja Ukristo ulicho nacho ambacho dini yaKibaniani haina – yaani, Mwokozi.” Ukristo ndiyo dini pekee katikaulimwengu huu inayowapa watu Mwokozi.
(2)Yesu anaweza kutuokoa kutoka katika uhusiano wetu na Mungu ambaoulivunjika.
“Mlitengwa mbali na Kristo… mlikuwa hamna tumaini, wala hamnaMungu duniani. Lakini sasa katika Kristo Yesu ninyi ambao zamanimlikuwa mbali, mmeletwa karibu kwa damu yake Kristo” – (Waefeso2:12,13).
Yesu ndiye Rafiki mkamilifu ambayetwaweza kufurahia kuwa na uhusianonaye. Yeye anapenda kijitokezendani yetu kile kilicho bora sana.”Kwa damu yake Kristo” maisha yetuya dhambi yaliyopita yanasamehewa,na siku-kwa-siku yeye anatupaukubali wake, nguvu za kushindadhambi, na maisha yake makamilifu.Tunajua kwamba atakuwa palekutuinua na kila wakatitunapoanguka. Kwa upande wetuupendo wetu kwake unazaa shaukuya kuishi kwa kufuata njia ileimpendezayo yeye.
(3)Yesu anaweza kutuokoa sisi kutoka katika ile mauti ya milele, adhabu yadhambi.
“Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti [ya milele]; bali karama yaMungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu” – (Warumi6:23).
Sisi tu wavunjaji wa sheria yake [amri za Kumi], tumehukumiwa kufa. Yesuanatuokoa sisi kutoka katika mauti ya milele, kisha anatupa uzima wake wamilele.
“Mungu auonyesha dhahiri upendo wake kwetu sisi; tulipokuwatungali wenye dhambi, Kristo alikufa kwa ajili yetu” – (Warumi 5:8).
Kwa sababu ya upendo wake usio na mwisho, Yesu “alikufa kwa ajili yetuna kupata mateso kamili ya dhambi zetu, Mungu sasa anawezakuwasamehe na kuwakubali wenye dhambi bila kuihafifisha hiyo dhambi.
(4)Yesu anaweza kutuokoa kutoka katika maisha ya dhambi, yasiyokuwana furaha.
“Hata imekuwa mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya – yakale yamepita, tazama! Yamekuwa mapya”- (2 Wakorintho 5:17,Philips).
Hatuwezi kujiokoa wenyewe kutoka katika dhambi au kuigeuza tabia yetukwa kujitegemea wenyewe kama vile Simba asivyoweza kuamua awemwana-kondoo (Warumi 7:18). Dhambi ina nguvu nyingi kuliko nia yetu yakufanya yale tuyatakayo. Lakini Kristo anaweza kukufanya wewe uwe”imara kwa uweza wake, kwa kazi ya Roho wake katika utu [wako] wandani” (Waefeso 3:16). Anafanya kazi yake ili kuondoa tabia zetu ziletazouharibifu na mahali pake kuweka tabia hizi nzuri: upendo, amani, furaha,upole, uwezo wa kujitawala (Wagalatia 5:22,23). Kristo anaishi maisha yakekupitia ndani yetu, kisha tunapokea uponyaji wa kiroho, tunarejeshwa katikamaisha mapya, na kuwezeshwa kuishi maisha hayo mapya.
Harold Hughes alikuwa amepoteza tumaini lake kabisa la kuwezakubadilika kwa wakati uwao wote ule. Alikuwa amejitahidi sana kuachakunywa pombe mara nyingi sana. Alijua fika kwamba vita yake dhidi yachupa ya pombe ilikuwa imewaletea maisha ya jehanamu mke wake nabinti zake wawili kwa miaka kumi kamili. Basi asubuhi moja yenye baridi kaliakaingia katika bafu lake na kuuelekeza mtutu wa bunduki yake kinywani mwake. Kabla hajafyatua risasi, aliamuakwamba ingekuwa heri kwake kumwelezaMungu mambo yake yalivyokuwa. Salayake ile ikageuka na kumfanya alielewakwikwi kwa muda mrefu akimsihiamsaidie.
Mungu akamjibu. Harold Hughes akajitoakabisa kwa Kristo na kupata nguvu zakiroho kumwezesha kulishikilia lile tumainilake la kubadilika. Aliacha kabisa kunywapombe, akawa mume na baba mwenyemapenzi na wa kutegemewa, kishaakasonga mbele na kujipatia kiti katika Seneti [sehemu ya Bunge] laMarekani. Harold Hughes aligundua uwezo mkubwa kabisaunaoyabadilisha maisha ya watu katika dunia hii – yaani, Yesu!
(5)Yesu anaweza kutuokoa kutoka katika dunia hii ya dhambi.
Miongozo minne ya GUNDUA ifuatayo itaeleza jinsi jambo hilo linavyowezakufanyika.
4.Tunaokolewa Kwa Kuchukua Hatua Rahisi Tatu
Hatua ya 1. mwombe Kristo aingie na kuishughulikia dhambi katika maishayako.
Je, sisi tunayo sehemu gani ya kufanya ili kuondokana na maisha yetuhaya ya dhambi?
TUBUNI, basi na kumgeukia Mungu, ili dhambi zenu zipate kufutwakabisa”
-(Matendo 2:38).
Ni kitu gani kinachomwongoza mtu kutubu?
“WEMA WA MUNGU WAKUVUTA WEWE UPATE KUTUBU” – (Warumi2:4).
“HUZUNI YENU ILIWAONGOZA HATA MKATUBU” – (2 Wakorintho 7:9).
Toba ni kuhuzunika tu kwa ajili ya maisha yetu ya dhambi yaliyopita, kishakugeuka na kwenda mbali na dhambi zetu, tukizikomesha tabia zetu mbayaza zamani, pamoja na mazoea yetu, na mtazamo wetu. Hivyo si huzuni kwasababu sisi tunaogopa tu ile adhabu, bali ni mwitikio wetu kwa ule “wemawa Mungu” uliomfanya Yesu kufa badala yetu kwa ajili ya dhambi zetu.Tunaikataa dhambi kwa sababu inamwumiza Mungu.
Tunapoyaonja maisha mapya ndani ya Kristo, tungeyasahihisha makosayetu tuliyofanya zamani kwa kadiri iwezekanavyo (Ezekieli 33:14-16).
Je, sehemu ya Mungu ni ipi katika kutuondolea maisha yetu yenye dhambiya zamani?
Mambo yote mawili, toba na msamaha, ni vipawa vitokavyo kwa Mungu.
“Mungu amemtukuza kwa kumweka mkono wake wa kulia, awe mkuuna Mwokozi ili apate KUWAPA TOBA na MSAMAHA WA DHAMBI” -(Matendo 5:31).
Nasi tunapotubu, Mwokozi huyo mwenye upendo anatusamehe dhambizetu, anatusafisha dhambi zetu, na kuzitupa katika vilindi vya bahari.
“TUKIZIUNGAMA dhambi zetu, YEYE NI MWAMINIFU na wa haki, NAYEATATUSAMEHE dhambi zetu na KUTUSAFISHA na udhalimu wote” – (1Yohana 1:9. Angalia pia Mika 7:18,19).
Hakuna dhambi ambayo ni ya kutisha sana asiyoweza kuisamehe Mwokoziwetu aliyekufa kwa sababu ya hizo dhambi zetu juu ya msalaba ule waKalvari. Mtu yule anayemtumainia Yesu anahitaji tu kumwomba yeye iliampe msamaha wake. Kufa kwake Kristo kwa ajili yetu hakuwezi kutupatiasisi msamaha mpaka tuombe kusamehewa. Ni ukweli ulio na busara ndaniyake ya kwamba dhambi zetu zilichangia katika kuipigilia ile misumari nakutoboa viganja na nyayo zake Kristo. Na, hata hivyo, Yesu anayo shauku nyingi sana kuliko vile tuwezavyo kuwaza ili tupate kukipokea kipawa chakecha msamaha na upatanisho.
Habari zilimfikia kijana mmojamwanaume aliyekuwa ametorokanyumbani kwao kwamba mama yakealikuwa akifa. Habari zile zikamjazamajuto mengi kuhusu uhusiano waouliokuwa umevunjika. Akaharakishakwenda nyumbani, akaingia harakakatika chumba kile na kujitupa juu yakitanda cha mama yake. Machozi yakiwayanabubujika akamsihi amsamehe.
Akamvuta karibu na kunong’ona,”Mwanangu, ningekuwa nimekusamehezamani sana endapo ungekuwa tu umeniomba mimi.”
“Kama wewe umetanga mbali na Mungu – au bado hujamjua – tafadhalifikiria jinsi Baba yako, akupendaye, aliye mbinguni alivyo na shauku kubwakukukaribisha nyumbani kwake. Zaidi ya kitu kinginecho chote yeyeanataka wewe upokee msamaha wake anaokupa. Yesu anakupenda wewe.Alikufa kwa ajili yako. Siku zote yu tayari kukusamehe wewe. Basi itikiamwaliko wake wa neema unaokutaka utubu. Ungama dhambi zako. Amininaye anafanya hivyo. Mtumainie yeye! Tegemea ahadi zake.
Hatua ya 2. pokea maisha mapya toka kwa Yesu.
Sehemu yako katika kupokea maisha mapya toka kwa Yesu ni kuaminikwamba Yesu amekuokoa kweli kweli. Kubali bila swali ukweli kwambayeye amekusamehe na kukusafisha, ameyaondoa maisha yako ya dhambiya zamani, na kukupa wewe maisha mapya kabisa yaliobadilika.
“Bali wote… waliompokea, aliwapa uwezo wa kufanyika watoto waMungu” – (Yohana 1:12).
Wewe kama mtoto wa Mungu, unayo “haki” ya kupokea hayo maishamapya kutoka kwa Yesu. Kama tulivyokwisha kusema, wewe huwezikuipata hiyo kwa kujitegemea mwenyewe – ni zawadi toka kwa baba yakoaliye mbinguni! Yesu anatoa ahadi kama hiyo iliyo ya kweli ili kutuondoleawasi wasi na mashaka yetu.
Je, sehemu ya Mungu ni ipi katika kutupa sisi maisha hayo mapya?
“Yesu akamwambia, Amini, amini nakuambia, hakuna mtu awezayekuuona ufalme wa Mungu asipozaliwa mara ya pili” – (Yohana 3:3).
Kulingana na Yesu, mwenye dhambi aaminiye na kutubu, anazaliwa kabisana kuwa na maisha mapya. Ni mwujiza ambao ni Mungu peke yakeawezaye kuufanya. Yeye anaahidi hivi:
“Nami nitawapa ninyi MOYO MPYA, nami nitatia ROHO MPYA ndaniyenu; nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani yenu, nami nitawapamoyo wa nyama”- (Ezekieli 36:26).
Yesu anaubadilisha moyo wetu – yaani, hisia zetu pamoja na tabia zetu -kisha anakaa “ndani yetu” (Wakolosai 1:27). Maisha hayo mapya si wazomoja tu lililo zuri la kiroho; ni ukweli ulio mkakamavu na imara, ni ufufuokutoka katika kifo cha kiroho kwenda katika maisha hayo mapya kabisa nauzima.
Hatua ya 3. Uishi kwa ajili ya Kristo kila siku.
Maisha ya Kikristo yanamaanisha kugeuka kila siku kutoka katika kujipendawenyewe na kuingia katika kifungo na Yesu atupendaye. Tunakua katikamaisha hayo mapya kwa kuuimarisha uhusiano wetu na Yesu. Hii inamaana kwamba wakati wetu bora tuutumie pamoja naye, tukijengamawasiliano ya kweli na yaliyo wazi. Mungu ametupa sisi misaada mitanokwa ajili ya kukua kwetu kiroho: Kujifunza Biblia, maombi, kutafakari, kuwana ushirika pamoja na Wakristo wengine, na kubadilishana uzoefu wetu wamaisha na wengine.
Kuishi ndani ya Kristo hakuna maana kwamba hatuwezi kamwe kufanyamakosa. Lakini tunapojikwaa na kutenda dhambi, tunadai msamaha wake Kristo, kisha tunasonga mbele. Tuanaelekea upande fulani, tena tunajuakwamba Kristo, anaendelea kuishi ndani ya mioyo yetu.
Jinsi Tupokeavyo Maisha Mapya Toka Kwa Kristo
1.Tunamwamini yeye na kumpokea kama Mwokozi na Bwana wetu.
2.Tunajenga uhusiano wetu pamoja nao. (kuwa na muda fulani kila siku wamaombi na kusoma Biblia ni jambo la muhimu sana.)
3.Kristo hufanya kazi yake kwa njia ya Roho wake Mtakatifu ili kuziondoatabia zetu mbaya na kuziweka tabia zake nzuri mahali pake.
5.Furaha Ya Kupewa Nafasi Hiyo Ya Pili
Harold Hughes alipewa vyeo vingi katika kazi yake maarufu kama senetawa Marekani, lakini kimoja cha maana sana kwake kilikuja muda mfupi tubaada ya kujitoa kwake kwa Kristo.
Jioni moja Harold alikuwaakijifunza Biblia yake akiwa pekeyake katika sebule yakealipoguswa na kiwiko kwenyekiwiko chake. Akaangalia juu.Walikuwa ni wale binti zakewadogo wawili, wakiwawamesimama kimya katikamagauni yao ya kulalia usiku.Akawakazia macho kwa dakikamoja hivi; walikuwa wamebadilikasana, naye alikuwa amekosamengi wakati ule alipokuwa akipambana vita dhidi ya chupa ya pombeiliyokuwa ikimletea uharibifu.
Hapo ndipo Carol, mdogo zaidi, aliposema, “baba, tumekuja kukubusu nakukutakia usiku mwema.”
Macho ya yule baba yakaingiwa na kiwi muda mrefu mno ulikuwa umepitatangu watoto wale walipokuja kwake na kukumbatiwa naye. Sasa yalemacho yao mazuri na maangavu hayakuwa na hofu yo yote. Hatimayebaba yao alikuwa amekuja nyumbani.
Yesu anawapa watu wake nafasi ya pili kweli. Anawachukua wale waliowabaya kupindukia na kuwapa mianzo mipya.
Mwokozi anatamani sana kwamba kila mmoja wetu hatimaye arudinyumbani. Je, umeukubali huo mwaliko wa upendo wa Kristo anaotoakwako? Kupokea msamaha na utakaso wa Mungu ni jambo rahisi na lamaana sana kama kuinyosha mikono yako na kumkumbatia mtoto ndogo.
Iwapo wewe bado hujamtumainia Kristo kama Mwokozi wako binafsi, basi,unaweza kufanya hivyo sasa hivi kwa kutoa ombi kama hili:
“Baba, nasikitika kwa ajili ya maisha yangu ya dhambi ya zamani. Asantekwa kumtuma Mwanao katika dunia hii kuja kufa badala yangu mimi. Yesu,tafadahli nisamehe dhambi zangu na kuingia katika maisha yangu nakuniokoa. Nataka nipewe nafasi ya pili ya kuishi maisha yangu – natakakuzaliwa mara ya pili. Naam, zaidi sana, nataka kujenga uhusiano wangusiku-kwa-siku pamoja nawe. Asante kwa kunifanyia mwujiza huo ndaniyangu. Katika jina la Yesu, Amina.”
Fanya ugunduzi huu wa ajabu: sisi tunapokuja kwake, Yesu hufanya kaziyake ya kutuokoa.