Waliikuta mifupa yake kandoya kibanda chake cha mudakatika kisiwa kisichokuwa nawatu katikati ya Atlantiki.Baharia yule asiyejulikanajina lake alitunza kitabu chamambo ya kila sikukilichoeleza kwakinagaubaga matesomabaya aliyopata kwa mieziminne. Alikuwaametelekezwa pwani yakisiwa cha Ascension na kundi la manowari za Kiholanzi chini ya kamandammoja katika mwaka wa 1725 kwa uhalifu wake fulani uliokuwa haujatajwa.Baada ya muda mfupi kupita, akawa akinywa damu ya kasa ili kuituliza kiuyake kali sana. Mateso ya mtu yule kimwili yalikuwa makali sana, lakinimaumivu makubwa zaidi yanaonekana wazi katika kitabu chake chamambo ya kila siku: yaani, ile hatia yake iliyomlemea kabisa.
Aliandika maneno yaliyomtesa sana kama haya: “Ni maumivu yaliyojeyanayowapata wanadamu wanaoziacha njia za haki, wakifurahia kuongezaidadi ya watu waliolaaniwa.” Kutengwa kabisa kwa baharia yule katikakisiwa kile cha upweke kulitokana na hisia yake ya kutengwa mbali naMungu. Hilo ndilo jambo ambalo mwishowe lilionekana kwake kuwahalivumiliki.
Wanadamu wamekuwa wakipambanana kutengwa huko mioyoni mwaotangu Adamu na Hawa walipo”jifichaBWANA Mungu asiwaone kati ya mitiya bustani” baada ya kula lile tundalililokatazwa (Mwanzo 3:8). Hisia mpya,ngeni, za kuona aibu, hatia, na hofuzikawalazimisha wale watu wawili,mume na mke, kumkimbia Mungualipokuja na kuwaita. Hisia zile, kwabahati mbaya, sasa zinafahamika sanakwetu.
Je, ni kitu gani kinachosababishautengo huo kati yetu na Mungu?
“Lakini maovu yenu yamewafarakisha ninyi na Mungu wenu; dhambizenu zimeuficha uso wake msiuone” – Isaya 59:2.
Ufa huo mkubwa unaowatenga wenye dhambi mbali na Mungu hautokanina Mungu. Mungu hakutimua mbio kumwacha Adamu na Hawa – wao ndiowaliomkimbia yeye.
1.Kukidhi Njaa Yetu Iliyojificha
Kabla dhambi haijaiharibu ile picha, Adamu na Hawa waliufurahia urafikiwao wa karibu sana na Muumbaji wao katika makazi yao yale katika ileBustani nzuri ya Edeni. Kwa bahati mbaya sana, waliukubali ule uongo waShetani kuhusu jinsi ambayo wao wangekuwa na hekima kama Mungu, wakakivunja kile kifungo cha imani kilichokuwapo kati yao na Muumbajiwao (Mwanzo 3).
Baada ya kufukuzwa katika ile Bustani ya Edeni, Adamu na Hawa walionamaisha yao yakizidi kuwa magumu sana kule nje. Kuzaa watoto na kuilimaardhi sasa kukawa ni kwa kutokwa na damu, jasho, na machozi. Uhusianowao wa karibu sana na Mungu ukavunjika, wakajikuta hawana kinga yoyote dhidi ya tamaa zao zisizotoshelezeka na shauku zao ziwaleteazomaumivu makali – yaani, huo upweke uletwao na dhambi.
Tangu Adamu na Hawa walipotenda tendo lao la uasi la kwanza, “wote”(jamii yote ya mwanadamu) wameanguka na kuwa na mwelekeo ule ulemmoja wa dhambi na kukabiliwa na kifo, yaani, hiyo ndiyo adhabu yamwisho ya dhambi.
“Kwa hiyo, kama vile dhambi ilivyoingia ulimwenguni kupitia kwa mtummoja, na mauti kwa njia ya dhambi hiyo, na hivyo MAUTIIKAWAFIKIA WATU WOTE, kwa sababu WOTE WAMEFANYA DHAMBI”-(Warumi 5:12).
Sisi sote tunaona njaa kubwa moyoni mwetukwa kile tulichokwisha kukipoteza, yaani,tunakuwa na shauku ya kupata usalama waaina fulani ambao ni Mungu tu awezayekutupa. Mara kwa mara sisi tunajitahidikuikidhi hiyo njaa kwa kuwa walevi wakununua vitu madukani, au kuwa na mbio zawendawazimu za kutaka kupandishwa cheokazini, au kwa kuizimisha tu hiyo njaa kwakutumia alkoholi [pombe], madawa yakulevya au kwa uzinzi.
Lakini hizo shauku zetu zote ni dalili ya upweke wa kutokuwa na Mungu.Wala hakuna tiba isipokuwa kwa kuuonja upendo wake katika maisha yetu.
“Utanijulisha njia ya uzima, mbele za uso wako ziko furaha tele. Nakatika mkono wako wa kuume. Mna neema milele” – (Zaburi 16:11).
Kuridhika kweli kweli huja tu kama ufa ule uliopo kati yetu na Munguumejengewa daraja, na sisi tunaweza kuvuka ng’ambo na kuingia mbelezake.
2.Kuziba Ufa Wa Dhambi Na Mauti
Wanadamu sio pekee yao tu wafanywao kuwa wakiwa kutokana na dhambihiyo. Moyo wa Mungu pia uliumia sana siku ile Adamu na Hawawalipomgeuzia migongo yao. Na bado yeye anaendelea kusikitika kuhusuile huzuni na misiba inayowapata wanadamu. Mungu anatamani sanakukidhi tamaa zetu zilizojificha na kutuponya majeraha yetu ya kimaadili.Hakuwa ametosheka kuangalia kwa huruma ng’ambo ya ufa uleuanaotutenga sisi mbali naye. Mungu akaazimu kujenga daraja kuvuka ufaule mkubwa wa dhambi na mauti.
“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoaMwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asiangamie, bali awe nauzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni iliauhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye” -(Yohana 3:16,17).
Mungu alimtoa Mwanawe, na Yesualitoa uhai wake kama kafara yadhambi, akalipa ile adhabu ya mautiyeye mwenyewe. Maisha yake, kifochake, na ufufuo wake vikafanyauwezekano uwepo wa kuwasamehena kuwaokoa wenye dhambi bila yakuihafifisha dhambi, kishaakayaonyesha yale malimwengutabia halisi ya Kristo na Shetani.Daraja lile lililojengwa kwa mwili wa Kristo ulivunjika na kutoka na damu nyingi linawavuta watu na kuwarudishanyuma kutoka katika mtego wa dhambi. Upendo unavuka ng’ambo ya ufahuo mkubwa, na kuwawezesha kuvuka ng’ambo na kuingia katika uzimawa milele wale wote wanaoiweka imani yao ndani ya Kristo kama Bwana naMwokozi wao.
3.Mambo Muhimu Saba Ya Kweli Upaswayo Kuyafahamu KumhusuYesu
Mambo hayo saba ya kweli si ya kweli kwa mtu mwingine awaye yotealiyepata kuishi hapa:
(1)Yesu Alitoka Mbinguni. Na Kuja Hapa Duniani Je, Yesu alidai kwambaalikuwako kwa muda gani?
“Kabla Ibrahimu hajazaliwa ulimwengu huu, na kusema: “Mimi Niko!” Miminimekuwako siku zote. Ingawa Yesu alizaliwa na mama wa kibinadamu.
Akina Dwight L. Moody, Billy Graham wa karne ile ya kumi na tisa, sikumoja walisema hivi juu ya kufanyika mwili kwa Yesu, “Kungekuwa nikujitolea mhanga kukubwa kwa upande wa Yesu kuja hapa nakubembelezwa katika kitanda kidogo cha fedha cha watoto, kulelewa namalaika, na kulishwa kwa kijiko cha dhahabu. Lakini yule Muumbaji wambingu na nchi alikuja hapa na kutwaa mwili wa kibinadamu, na kuzaliwana wazazi maskini katika zizi la ng’ombe katika mazingira yale mabayakabisa.”
Malaika yule alimwambia Yusufu manenohaya wakati ule wa kuzaliwa kwake Yesu:
“Naye [Mariamu] atazaa mwana, naweutamwita jina lake Yesu, maana YEYEATAWAOKOA WATU WAKE KUTOKAKATIKA DHAMBI ZAO” – (Mathayo 1:21).
Yesu, Muumbaji wa ulimwengu (Yohana1:1-3,14), kwa hiari yake alitaka kuja katikadhambi na mauti.
(2)Yesu Aliishi Maisha Yasiyo na Dhambi
“Yesu, Mwana wa Mungu,… amejaribiwakwa kila njia sawasawa na sisi – lakini bila kufanya dhambi”(Waebrania 4:14,15).
Mungu alifanya mengi kuliko kule kusema nasi ili kututaka tutoke katikamaisha ya dhambi na kuingia katika maisha yale yanayoridhisha. Kwakuishi kwake hapa kama mwanadamu, Yesu aliyafanya maisha yake yaleyasiyo na dhambi kuwa ya kuvutia sana kuliko hubiri lo lote lile ambavyolingeweza kufanya.
Shetani, adui yake Kristo alipanga mipango yake mibaya katika kipindichote cha maisha ya Yesu aliyoishi hapa duniani ili kumshawishi atendedhambi.l kule nyikani Shetani alianzisha mashambulio yake makali mnodhidi ya unyofu wake (Mathayo 4:1-11). Kule Gethsemane kabla yakusulibiwa kwake, shinikizo la majaribu lilifikia kiwango chake kikubwakama kile, Yesu alitoa jasho la damu (Luka 22:44).
Lakini Kristo alisimama imara dhidi ya kila kitu alichomtupia Shetani – “lakinibila kufanya dhambi.” Kwa kuwa Yesu aliyapitia matatizo yote yawanadamu na majaribu yao, anaelewa jitihada zetu tunazofanya. Yeyeanaweza “kutuhurumia katika udhaifu wetu” (Waebrania 4:15).
Kwa nini ilikuwa ni lazima kwa Yesu kuishi maisha yasiyo na dhambi?
“Mungu alimfanya Yesu, aliyekuwa hana dhambi, kuwa dhambi kwaajili yetu; na badala ya maisha yetu ya dhambi, Yesu anatupa sisimaisha yake yasiyo na dhambi, ili tuweze kuwa bila dhmbi ndani yake”(2 Wakorintho 5:21, limefafanuliwa).
Yesu aliyashinda majaribu na kuishi maisha yasiyo na dhambi ili atupe sisihayo kwa kubadilishana na maisha yetu ya dhambi ya zamani.
(3)Yesu Alikufa Kuiondoa Dhambi
e, ni watu wangapi waliofanya dhambi?
“Kwa sababu WOTE wamefanya dhambina kupungukiwa na utukufu wa Mungu.” -Warumi 3:23.
Je, adhabu ya dhambi ni nin?
“Kwa maana Mshahara wa dhambi niMAUTI; bali karama ya Mungu ni uzimawa milele katika Kristo Yesu Bwanawetu” – (Warumi 6:23).
Kwa nini Yesu alikufa?
“Tazama, Mwana-Kondoo wa Mungu,AICHUKUAYE DHAMBI ya ulimwengu!”(Yohana 1:29).
Sisi sote tumefanya dhambi, tenatunakabiliwa na mauti ya milele, lakini
Yesu alikufa badala yetu. Akafanywa kuwa “dhambi kwa ajili yetu.” Yeyealilipa hiyo adhabu ya mauti kwa niaba yetu. Kifo chake ni zawadi (karama),na hiyo “KARAMA [ZAWADI] ya Mungu ni UZIMA WA MILELE katika KristoYesu Bwana wetu” (Warumi 6:23).
Yesu aliyatoa maisha yake makamilifu, ya haki, kama zawadi yake yaupendo kwetu. Upendo kama ule unapita karibu ufahamu wote wawanadamu. Na kwa sababu ya kifo chake sisi” tu[na] AMANI kwa Mungu”(Warumi 5:1).
(4)Yesu Alifufuka Kutoka kwa Wafu
Kifo cha Yesu pale msalabani hakikuwa mwisho wa kisa chake cha ajabu.Naam, yeye asingeendelea kuwa mfu wakati huo huo kuwa Mwokozi wetu.
“Na kama Kristo hakufufuka, basi, imani yenu ni bure; mngalimokatika dhambi zenu. Na hapo wao nao waliolala katika Kristowamepotea” – (1 Wakorintho 15:17,18).
Muhammad na Budha wameupa ulimwengu huu baadhi ya zile kweli kuu zakifalsafa. Wameyaongoza maisha ya mamilioni ya watu, lakini hawanauwezo wa Mungu wa kuwapa uzima kwa maana wao bado wanaendeleakubaki katika makaburi yao.
Kwa kuwa Yesu alifufuka kutokakaburini siku ile ya tatu baada yakifo chake, je, ni ahadi ganiawezayo kuitoa kwetu?
“Na kwa sababu mimi ni hai,ninyi nanyi mtakuwa hai” Yohana14:19.
Yesu yu hai! Kwa kuwa yeye anaouwezo juu ya mauti, anawezakutuokoa toka mautini na kutupauzima ule ambao ni tele, tena ni wa milele. Ataishi ndani ya mioyo yetukama tukimkaribisha. Kristo yule aliyefufuka yupo ili kukidhi mahitaji yetuleo.
“Na tazama mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wadahari” – (Mathayo28:20).
Wanaume na Wanawake ulimwenguni kote wanabadilishana visa vyao juuya jinsi Kristo alivyowaokoa kutoka katika mazoea yao mabaya sana nahisia nzito sana za moyoni mwao ziwatiazo kiwewe.
Mmojawapo miongoni mwa wanafunzi wetu wa zamani aliandika manenohaya ya shukrani katika mojawapo ya karatasi zake za majibu: “Miminilikuwa mlevi sugu. Siku moja nilipokuwa nimelewa, niliiona kadi mferejiniikitangaza kozi yenu ya Biblia. Niliiokota, nikaijaza kupata ujuzi wangu wakwanza wa Kristo. Muda mfupi baada ya kuchukua kozi hiyo ya Biblia, nilitoa moyo wangu kwa Mungu na kuipoteza hamu niliyokuwa nayo kwawiski. 2
Yesu alipoyatawala maisha ya mtu huyo, nguvu mpya ilimpa uwezo wakuyashinda mazoea yake yale mabaya. Kwa vile Kristo ni Mwokozialiyefufuka, anaweza kuwaokoa wote watakaomjia yeye kuomba msaadawake.
(5)Yesu alipaa Mbinguni
Kabla Yesu hajarudi kwa Baba yakebaada ya ufufuo wake (Matendo 1:9),alitoa ahadi hii kwa wafuasi wake:
“Msifadhaike mioyo mwenu.Mwaminini Mungu; niaminini namimi pia nyumbani mwa Baba yangumna makao mengi;… Ninakwendakule KUWAANDALIA NINYI MAHALI.Nami.. nitakuja tena na kuwachukuampate kuwa pamoja nami…. palenilipo mimi” – (Yohana 14:1-3).
(6)Yesu Anahudumu Kama KuhaniMkuu
Daima Yesu anajitahidi sanakutuandalia sisi mahali kule mbinguni.
“Ilimpasa kufananishwa na nduguzake kwa kila njia, ili apate kuwa KUHANI Mkuu mwenye rehema,mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili apate kufanya upatanisho kwadhambi za watu wake. Na kwa kuwa mwenyewe aliteswa alipojaribiwa,aweza kuwasaidia wale wanojaribiwa” (Waebrania 2:17-18).
Yesu alikuja katika dunia yetu ili “kufanya upatanisho kwa dhambi za watuwake,” na kutuokoa sisi kutoka katika janga la kuwa watumwa wa dhambi.Alikufa kutuokoa sisi ili hatimaye apate kukifutilia mbali chanzo cha dhambi,maumivu na mauti kwa kumwangamiza Shetani.
Yesu kama Kuhani wetu Mkuu alifananishwa na ndugu zake kwa kila njia.”Na sasa anaonekana daima mbele zake Baba kwa ajili yetu kamampatanishi wetu. Yesu yule yule aliyewabariki watoto, aliyemrudishiaheshima yake mwanamke yule aliyekamatwa akizini, na kumsamehe mwiziyule aliyekuwa anakufa pale msalabani, hivi sasa anaendelea kufanya kaziyake kule mbinguni akituhudumia katika mahitaji yetu, ili “kuwasaidia walewanaojaribiwa.”
(7)Yesu Atarudi Tena
Kabla hajarudi mbinguni, Yesu alitoa ahadi gani?
“Nikienda na kuwaandalia mahali, NITAKUJA TENA na kuwachukuakuwa pamaoja nami ili ninyi pia muweze kuwa pale nilipo mimi(Yohana 14:3).
Yesu anaporudi tena, atatuokoa kutoka katika dhambi, magonjwa, misiba,na mauti, mambo ambayo yanaishambulia sayari hii. Naye atatukaribishakatika dunia mpya iliyojaa furaha ya milele na uzima wa milele.
4.Upendo Usiokoma
Hadithi hii inasimuliwa kuhusu ndoa iliyopangwa katika nchi ya Taiwani katiya U Long na mwanamke kijana aliyeitwa “Ua la Dhahabu.” U Long
alipolifunua shela la bibi arusi wake baada ya sherehe ile, alishtuka nakuchukizwa. Uso wake ulikuwa na makovu ya ndui.
Baada ya pale, U Long alikuwa akishughulika na mke wake kwa nadrasana kadiri ilivyowezekana.l alijaribu kadri alivyoweza kumfurahisha;alifanya kazi za nyumbani kwa bidii sana, akitumainia kwamba mume wakehatimaye angeweza kumkubali. Lakini yeye aliendelea kuwa baridi nakutojali kuonyeshwa kule kote kwa upendo wake [mkewe].
Baada ya miaka kumi na miwili ya ndoa yao ile ya kinafiki, U Long alianzakupoteza uwezo wake wa kuona katika macho yake yote mawili. Daktari akamwambia kwamba angekuwa kipofu kabisa kama asingepandikizwakioo cha macho. Lakini upasuaji ule ulikuwa wa gharama kubwa, tenapalikuwa na orodha ndefu ya watu waliokuwa wakingojea upasuaji huo.
Ua la Dhahabu akaanza kufanya kazi kwa masaa marefu jioni akitengenezakofia za mikeka ili kujipatia fedha za ziada. Siku moja U Long aliambiwakwamba kioo cha jicho la mtu mmoja kilikuwa kimepatikana baada yakutokea ajali. Aliharakisha kwenda hospitalini kufanyiwa upasuaji ule.
Baada ya kupona, yeye kwa shingo upande aliamua kumwona mke wake iliaweze kumshukuru kwa kuzipata fedha zile. Alipokigeuza kichwa chamkewe kilichoinama chini ili mkewe apate kumtazama, U Long alihema kwamshangao. Mkewe akamkazia macho yake akiwa na macho yasiyoona,yaliyo tupu, kioo cha macho yale kikiwa kimeondolewa. Akiwa amezidiwana jazba, akaanguka miguuni pa mkewe na kulia kwa kwikwi. Hapo ndipoyeye kwa mara yake ya kwanza alipolitaja jina la mkewe kwa kunong’ona,akasema: Ua la Dhahabu.
Yesu anatamani sana kuwa na uhusianona wale ambao kwa muda mrefu sanawamekuwa hawamjali. Anatamanikwamba hatimaye sisi tuwezekunong’ona kwa kulitaja jina lake kuwayeye ndiye Mwokozi wetu. Alijitoa kwahiari yake sio tu kwa kutoa kafara yamacho yake, bali mwili wake mzima iliapate kutuonyesha upendo wakeusiokwisha. Upendo wake una nguvunyingi sana kiasi kwamba Kristo “alikuja ulimwenguni awaokoe wenyedhambi” (1 Timotheo 1:15).
Kafara ile kuu aliyotoa Kristo ilijenga daraja linalopita juu ya kutokujalikwetu, linalofunika mfarakano wetu. Je! hivi wewe umegundua mwenyewekwamba yeye anataka kukuvuta juu ya ufa huo mkubwa na kukukumbatiamikononi mwake? Je! utaitikia na kuomba ukisema, “Yesu, nakupendawewe. Asante kwa kafara yako ya ajabu mno. Ingia moyoni mwangu nakuniokoa sasa – uniokoe kabisa, uniokoe kikamilifu, uniokoe milele”?
YESU
ALIKUJA
kama Mungu katika mwili wa kibinadamu.
ALIISHI
maisha yasiyo na dhmbi kwa niaba yetu.
ALIKUFA
kwa ajili ya dhambi zetu.
ALIFUFUKA
kutuokoa katika mauti.
ALIPAA
kwenda kutuandalia makao yetu kule mbinguni.
ANAHUDUMU
kila siku kama Kuhani wetu Mkuu.
ANAKUJA UPESI
kutuchukua sisi ili tuwe naye milele.