MKUSDA CHURCH
Unity in Worship

4. MPANGO KWA AJILI YA MAISHA YAKO

Baada ya mchungaji kuzungumza juu ya somo hili, “Kwa nini miminamwamini Yesu,” mwanaume mmoja kijana, aliyevalia vizuri, alimtembeleakatika chumba chake cha kusomea na kusema naye kwa mshangao,”Hotuba yako usiku wa leo ilitoka katika Biblia yako. Hebu niambie, kamaYesu alipata kuishi hapa duniani, mbona historia haisemi habari zo zote juuyake?
“Hilo ni swali zuri,” mchungaji akajibu alipogeuka na kuchukua vitabukadhaa na kuviweka chini. “Lakini, kwa kweli, historia inasimulia habari zaYesu Kristo.”
“Hizo ningependa kujionea mwenyewe,” yule mwanaume kijana akajibu.”Vema, hapa ni barua ya 97 ya kitabu cha 10 cha barua za (Pliny) Ndogo,Balozi wa Roma katika nchi ya Bithinia, jimbo la Asia ndogo ya zamani.Plinio alimwandikia mfalme wa Dola ya Roma Trajani (Trajan), akimwambiahabari za matukio katika jimbo lake. Tazama, hapa anaomba ushauri juu yajinsi anavyopaswa kulishughulikia dhehebu jipya, yaani, Wakristo.Anasimulia habari inayohusu kuongezeka kwao haraka sana na jinsiwalivyoimba nyimbo za kumsifu Mungu zilizotungwa kwaajili ya kiongoziwao, yaani, Kristo. Pliny aliituma barua yake karibu na mwaka ule wa 110B.K. Barua hiyo iliyoandikwa na Pliny inatoa ushahidi wa kihistoria wa yulemwanadamu, Kristo, na juu ya kuenezwa kwa imani yake katika siku zile zamitume wake.”
Akiwa ameshangaa, mwanaume yule kijana alisema, “Hebu niambie zaidi!”
Mchungaji alipoendelea kukipekuakitabu kingine, aliongeza kusema hivi,”Mwanahistoria mwingine, aliyeishikipindi kile kile kimoja na Pliny, alikuwani Tacitus. Katika habari zake za miakazilizotengwa (Anals), kitabu cha 15,sura ya 44, anasimulia habari zauhasama aliokuwa nao Nero namateso yake dhidi ya Wakristo wakatimji wa Roma ulipochomwa moto.Tacitus anaeleza kwamba neno hilo”Mkristo” linatokana na jina la ‘Kristo.’Anataja kwamba Yesu Kristo, mwasisiwa dini ya Kikristo, alikuwa ameuawa na Pontio Pilato wakili wa Yudea,katika kipindi cha utawala wa mfalme wa Dola Tiberio. Maelezo haya yoteanayotupa Tacitus yanalandana kabisa na matukio, majina na mahalipalipotajwa katika Biblia.”
“Mchungaji, mimi sikujua kabisa mambo hayo kuwa yalikuwamo katikahistoria ya ulimwengu.!” mgeni yule akasema kwa mshangao.
Mchungaji yule akaongeza kusema hivi, “Nataka uzingatie kwamba karibuna mwaka wa 180 B.K. Celsus aliandika kitabu akiwashambulia Wakristo,akionyesha kwamba kufikia wakati ule Ukristo ulikuwa ni nguvu iliyopaswakutambuliwa.
“Kama wewe bado una mashaka, basi, kumbuka kwamba vitabu hivyovinne vya Injili ni historia iliyosawa na ile ya vitabu hivyo vya kidunia.”
Yule mwanaume kijana alipotambua kwamba historia zote mbili, yaani, iletakatifu na ile ya kidunia, zinakubaliana kwamba Yesu alipata kuishi hapa duniani kama mwanadamu, alikwenda zake akiwa ameamini kwamba YesuKristo alikuwa mtu halisi wa kihistoria.


1.Kristo Alikuwako Tangu Milele
Yesu hakuwa tu mtu mwema, alikuwa Mungu pia. Je, ni madai ganialiyoyatoa Yesu mwenyewe kuhusu Uungu wake?
“Kama mngalinijua mimi kweli kweli,mngalimjua na Baba. Tangu sasamnamjua, tena mmemwona…. Ye yotealiyeniona mimi amemwona Baba” -Yohana 14: 7-9.
Ukitaka kujua jibu kwa maswali haya,”Mungu ni nani? Anafananaje?”unapaswa kumtazama tu Yesu,aliyetangaza, akasema,
“Mimi na BabaTu umoja (Yohana 10:30.)
Mungu Baba na Yesu mwanawewamekuokoa pamoja tangu milele(Waebrania 1:8.) Haukuwako wakati wowote ule ambapo Kristo hakuwa umojana baba yake. Baba yake anatoaupendo na ulinzi wake ule ule kwa kila mtu kama aliouonyesha Yesu katikakipindi cha maisha yake ya kibinadamu hapo duniani.


2.Kristo, Kiini Cha Historia Na Unabii
Kwa kuwa kisa cha maisha ya Kristo niutimizo wa unabii, kisa cha maisha yakekiliandikwa kabla yeye hajazaliwa unabii waAgano la kale huonyesha kwa kifupikinachoeleweka wazi maisha yake, kifochake na ufufuo wake kabla hayajatokea.Agano Jipya ni kisa cha maisha yakekilichoelezwa kama utimilizo wake. Wakiishikuanzia miaka mia tano hadi elfu moja namia tano kabla ya kuzaliwa kwake Kristo,manabii wale wa Agano la Kale waliotoautabiri mwingi wa pekee kuhusu maisha yakeMasihi, na tangu mwanzo kabisa wa kaziyake hapo duniani,
Watu walipoyalinganisha maisha yake naunabii wa Agano la Kale walifikia
hitimisho gani?
“Tumemuona yeye aliyeandikwa maisha katika torati na ambayehabari zake manabii pia waliziandika Yesu Nazareth Mwana waYusufu”_ (Yohana 1:45).
Mwokozi wetu aliwaelekeza watu kwenye unabii uliotimizwa ili kuthibitishakwamba yeye ndiye:
“Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza yoteyaliyosemwa juu yake katika Maandiko yote [ya Agano la Kale]kumhusu yeye mwenyewe” – (Luka 24:25-27).
Unabii uliotimizwa unatoa ushahidi unaosadikisha kwamba Yesu ndiye yuleMasihi aliyeahidiwa.


3.Maisha Ya Kristo Ni Utimilizo Wa Unabii
Hebu na tuviangalie vifungu hivi vichache vya unabii huo toka katika Aganola Kale – na kutimizwa kwake katika kumbukumbu za Agano Jipya.
Mahali Pake Alipozaliwa
Unabii wa Agano la Kale:
“Bali wewe BETHELEHEMU Efrata,…. kutokakwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli,ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele”(Mika 5:2).

Kutimizwa kwake katika Agano Jipya:
“Yesu alizaliwa BETHELEHEMU ya Yudea” – (Mathayo 2:1).
Kuzaliwa Kwake Na Bikira
Unabii wa Agano la Kale:
“BIKIRAatachukua mimba, atazaa mwana,naye atamwita jina lake Imanueli[Mungu pamoja nasi]”. – Isaya7:14.
Kutimizwa kwake katika AganoJipya:
“Yusufu, mwana wa Daudi,usihofu kumchukua Mariamunyumbani kwako kama mkeo,maana MIMBA YAKE NI KWAUWEZA WA ROHO MTAKATIFU.Naye atazaa mwana, nawe utampajina lake Yesu [BWANA huokoa]” – (Mathayo 1:20-23).
UKOO WAKE WATOKA KATIKA KABILA LA YUDA,… mpakaatakapokuja yeye anayeimiliki” – (Mwanzo 49:10).
Kutimizwa kwake katika Agano Jipya:
“Maana ni dhahiri kwamba BWANA WETU ALITOKA KATIKA YUDA” -(Waebrania 7:14).
Kukataliwa Kwake
Unabii wa Agano la Kale:
“Alidharauliwa na KUKATALIWA na watu” – (Isaya 53:3).
Kutimizwa kwake katika Agano Jipya:
“Alikuja kwa wale waliokuwa wake, lakini WALIO WAKEHAWAKUMPOKEA” – (Yohana 1:11).
Kusalitiwa Kwake Na Ujira AliolipwaMsaliti Wake
Unabii wa Agano la Kale:
“MSIRI WANGU niliyemtumaini,aliyekula chakula changu, ameniinuliakisigino chake” – (Zaburi 41:9).
“Nikawaambia, “Mkiona vema, nipeniujira wangu; kama sivyo, msinipe. Basiwakanipimia VIPANDE THELATHINIVYA FEDHA” – (Zakaria 11:12).
Kutimizwa kwake katika Agano Jipya:
“Wakati huo mmoja wa wale kumi nawawili, jina lake Yuda Iskariote -aliwaendea wakuu wa makuhani na kuwauliza, ‘Ni nini mtakachonipanikimsaliti kwenu? Wakamhesabia VIPANDE THELATHINI VYA FEDHA”-(Mathayo 26:14,15).
Kifo Chake Msalabani
Unabii wa Agano la Kale:
“WAMENIZUA MIKONO na miguu yangu” – (Zaburi 22:16).
Kutimizwa kwake katika Agano Jipya:
“Walipofika mahali paitwapo FUVU la kichwa, WAKAMSULIBISHApale” – (Luka 23:33. Angalia pia Yohana 20:25).
Kutoka Kwake Kaburini
Unabii wa Agano la Kale:
“Maana hatukuachia kuzimu nafsiyangu, wala hutamtoa Mtakatifuwako aone uharibifu” – Zaburi16:10.
Kutimizwa kwake katika AganoJipya:
“Yeye mwenyewe akitanguliakuyaona haya, alitaja habari zakufufuka kwake Kristo, yakwamba roho yake HAKUACHWAKUZIMU, wala mwili wake haukuona uharibifu. Mungu amemfufua huyu Yesu, na sisis sote tu mashahidi wake” – (Matendo 2:31,32).
Ushahidi huo una nguvu kuonyesha kwamba Yesu hakutimiza utabirimchache tu. Maandiko yahusuyo maisha yake kwa kweli yaliandikwa kablayake kwa njia ipitayo uwezo wa kibinadamu. Kweli, Yesu ni Mwana waMungu.
Baada ya kuuangalia ushahidi huo, tunahitaji kufanya uamuzi wetu kwa njiaya maombi kuhusu nani atakayekuwa Bwana katika maisha yetu. Kamawewe bado hujafanya hivyo, je! utayaweka maisha yako mikononi mwakeYesu?


4.Maisha Yaliyopangwa Na Mungu
Yesu aliishi maisha yaliyopangwa na Mungu, ambayo yameelezwa kwamaelezo machache mamia ya miaka kabla ya kuzaliwa kwake. Siku zoteakiwa anautambua ukweli huo, alikuwa mwepesi kutambua maongozi yaMungu. Kristo alisema:
“Sifanyi neno lo lote kwa nafsi yangu, ila nanena yale tualiyonifundisha Baba… kwa sababu nafanya siku zote yaleyampendezayo” – (Yohana 8:28,29).
Mungu alipanga maisha ya kibinadamu ya Yesu kabla ya kuzaliwa kwake,tena Mungu anao mpango kwa kila mwanadamu pia. Anajua jinsi kilammoja wetu anavyoweza kutimiza haja zake zenye kina sana na kujipatiamaisha tele.
Ray siku zote hakuwa na hakika kabisa iwapoalitaka kuufuata mpango wa Mungu. Lakinialipokabiliwa na uamuzi mkubwa kuhusu wapialipaswa kwenda kusoma chuoni, basi, kwamara yake ya kwanza katika maisha yakealiamua kutafuta uongozi wa Mungu katikasuala lile. Aliomba kwa siku kadhaa nakujitahidi kusikiliza jibu la aina fulani. Baada yamuda fulani kupita alionekana amepata sababuzilizo wazi sana kwa nini angepaswa kuchaguachuo B: Chuo Kikuu kisicho na gharama kubwasana, lakini kikubwa na ambacho hakiendeshwina mtu fulani mahsusi. Mara tu baada yakuanza kusoma pale alifahamiana na Wakristofulani wa ajabu waliokuwa wamejiunga nachama fulani cha kumtetea Kristo katika eneolile la kile chuo kikuu. Uzoefu wote aliokuwa nao pamoja nao katika kipindicha miaka miwili iliyofuata uliyabadilisha maisha yake kabisa.
Ray anapoangalia nyuma leo, anaona kwamba kila wakati alipokuwaamekabiliwa na uamuzi mkubwa na kutafuta uongozi wa Mungu, “Mungualinifunulia uwanja mpya wa maisha yangu.”


Je, unawezaje kuujua mpango wa Mungu kwa maisha yako? Mungu anatoauongozi wake kwa njia kadhaa:
1.Biblia
Kulingana na mtunga Zaburi, je! ni kitabu gani kinachoyaongoza maishayetu?
“Neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu” -(Zaburi 119:105).
Neno la Mungu huifanya upya mioyo yetu na kutupatia maarifa (Warumi12:2, Zaburi 199:99). Wakati maalum uliopangwa kwa kujifunza Maandikona kuomba ndiyo njia bora kuliko zote ya kuyaratibu mambo yenyekipaumbele.
2.Maongozi Ya Mungu Katika Mambo Yanayotupata
Mungu anatuongoza pia kwa mambo yaongozwayo na Mungu mwenyewe.Zaburi 23 huonyesha yeye kama mchungaji mwema. Mchungaji anawaongoza kondoo wake katika mabonde yenye majani mabichi sana na
kupitia katika makorongo yenye miamba. Anao uwezo wa kuwasaidia waleanaowapa maagizo yake ili wanufaike na kujifunza kutokana na kila jambo linalowapata katika maisha yao. Tunaye mchungaji anayeambatana nasi nakukaa karibu sana kando yetu.

3.Mawasiliano Toka Kwa Mungu Ya Moja Kwa Moja hadi Moyoni
Mungu anatuongoza pia kwa njia ya kuzungumza nasi kupitia katikadhamiri zetu. Roho wake anaweza kuyatia nuru “macho ya mioyo yenu”(Waefeso
1:18). Kadiri tunavyozidi kufanya mazoezi ya kuwasiliana na Mungu ndivyokadiri anavyoweza kutuongoza sisi. Anaziumba upya hisia zetu za ndani nauwezo wetu wa kufikiri na kuamua ili tupate kuiona wazi hatua inayaofuataambayo tunahitaji kuichukua.


5.Maongozi Hayo Ni Lazima (Yapatane)?
Naam, yawezekana kudhani kwamba wewe unaishi maishayanayoongozwa na Mungu wakati wewe unafuata tu mielekeo yako na hisiazako mwenye (Mithali 16:25). Hisia zetu ni lazima zipatane na mafundishoya Biblia. Si salama kuamua kwamba ni Mungu anayetuongoza isipokuwakama maongozi yote matatu yanapatana.
Hebu na tumchukue Jake, kwa mfano. Alikuwa na mke wake mzuri sana nawatoto wawili, lakini alifanya uzinzi na mwanamke mwingine. Aliwaambiahivi rafiki zake: P “Mimi nimeliombea jambo hilo, nami najua kwamba hayoni mapenzi ya Mungu.”
Hisia za moyoni za Jake na “maono yake ya ndani” kwa dhahiri yalimpelekakatika njia ile mbaya iliyokwenda chini. Yeye aliwaza kwamba yale yalikuwani “maongozi ya Mungu”yaliyompelekea kukutana na mwanamke yulemwingine, wala hakurudi nyuma kuziangalia amri za Biblia dhidi ya uzinzi.Na Biblia hiyo, ambayo ni “sheria na ushuhuda,” ndicho kitabu chamwongozo chenye mamlaka, ndiye mwamuzi wa mwisho anayeamua njiasahihi ya kufuata katika utendaji wetu (Isaya 8:20). Kamwe tusiruhusumaoni yo yote au jambo lo lote linaloonekana wazi kuwa ni maongozi yaMungu kutupeleka mbali na kanuni ya Biblia.


6.Kujikabidhi kwa Mpango Wa Mungu
Shetani alipokuja kumjaribu Yesu kule nyikani, alitoa shauri hili, “Kamawewe ukiachilia mbali kujitoa kwako mhanga kunakokuletea maumivu
makali, ambako Baba yako amekupangia wewe, mimi nitakupa dunia hiiyote iwe mikononi mwako – pamoja na sifa, mali, na maisha ya rahamustarehe.” Shetani akanukuu hata Maandiko katika jitihada yake yakumfanya Yesu apotee. Lakini kila wakati Yesu alipambana naye nakumsukuma nyuma kwa maneno haya, “Imeandikwa” (Mathayo 4:1-11).
Fundisho moja lenye nguvu tuwezalokujifunza kutokana na maisha yake Yesuni utii wake kwa mapenzi ya Baba yake.Hata katikati ya maumivu makali yakutisha ya Gethsemane, yeye akalia,kasema, “Baba yangu, ikiwezekana,kikombe hiki kiniepuke. Walakini si kamanitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe”(Mathayo 26:39). Baada ya ile miakamitatu ya kazi yake, akiishi siku kwa sikukupatana na mpango wa Baba yake,Kristo alipokuwa akifa maneno yakeyalikuwa ni haya: “Imekwisha” (Yohana19:30). Yesu alikuwa akisema manenohaya hasa, “maisha yangu yaliyopangwana Mungu sasa yamekamilika nakutimilika.”
Unapoanza kuisikia Sauti ya Mungu ikisema nawe kulingana na Neno lake,kupitia katika mambo yale yakupatayo yanayoongozwa na Mungu, nakupitia katika mawazo ya moja kwa moja, unaweza kujifunza kuyakubalimaongozi yake hayo kwa moyo wako wote. Wewe pia waweza kuigunduafuraha ya maisha yaliyopangwa na kuongozwa na Mungu.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top
MKUSDA CHURCH