MKUSDA CHURCH
Unity in Worship

3. JE! MAISHA YANGU YANA MAANA KWA MUNGU?

1.Mungu Aliumba Dunia Kamilifu
Mungu ndiye Muumbaji, mwasisi na mbunifuwa kila kitu kuanzia nyota zinazotoa mlipukowa mwanga mkubwa kuliko jua na kutoweka(supernovas) hadi mabawa ya kipepeo.
“Kwa neno la BWANA mbingu zilifanyika najeshi lake lote kwa pumzi ya kinywachake…. maana yeye alisema, ikawa; nayeye aliamuru, ikasimama” – (Zaburi 33:6-9).
Mungu hana budi kusema tu, kisha vitu vyaasili hutii mapenzi yake.


2.Siku Sita Kuifanya Dunia Yetu
“Kwa siku zita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyotevilivyomo, akastarehe siku ya saba. Kwa hiyo, BWANA akaibarikia sikuya Sabato akaitakasa” – (Kutoka 20:11).
Muumbaji huyo wa milele, mwenye uweza wote angeweza kuiumba duniahii kwa dakika moja “kwa pumzi ya kinywa chake.” Lakini Mungu alichaguakuchukua siku sita kufanya kazi hiyo dakika sita, au hata nukta sitazingekuwa zinatosha. Sura ile ya kwanza katika Biblia, yaani, Mwanzo 1,inaeleza kile Mungu alichokiumba katika kila siku ya juma lile la Uumbaji.
Ni kazi gani bora ya kilele aliyoiumba Mungu katika siku ile ya sita?
“Mungu Akaumba Mtu Kwa Mfano Wake, kwa mfano wa Mungualimwumba; Mwanaume Na Mwanamke Aliwaumba” – (Mwanzo 1:27).
Juma La Uumbaji
Siku ya Kwanza: Nuru; mfuatano wa mchana na usiku
Siku ya Pili: Anga, hewa ya dunia hii
Siku ya Tatu: Nchi kavu na mimea
Siku ya Nne: Jua na mwezi vikaonekana
Siku ya Tano: Ndege na Samaki
Siku ya Sita: Wanyama wa nchi kavu na mwanadamu
Siku ya Saba: Sabato
Mungu aliamua kuwaumba watu wanaofanana naye ambao wangewezakufikiri na kujisikia na kupenda. Kila mtu ameumbwa kwa “mfano” waMungu.
Kufikia siku ile ya sita, dunia hii ilikuwa imejazwa na mimea na wanyama,ndipo Mungu akaileta kazi yake bora kuliko zote ya uumbaji. Kulingana naMwanzo 2:7, Mwenyezi aliuumba mwili wa Adamu kwa mavumbi ya ardhi.Basi Mungu alipompulizia “pumzi ya uhai”, puani mwake, mtu akawa”kiumbe hai” – yaani, akawa na uhai. Mungu alimwita Adamu, yule mtu wakwanza aliyeumbwa kwa mfano wake, neno hilo limaanishalo tu “mtu” namwanamke yule wa kwanza akamwita Hawa maana yake, “aliye hai” (2:20;3:20). Muumbaji huyo mweye upendo aliona ipo haja kwa binadamu kuwana mwenzi.

Wakiwa wametoka wenye afya mkononi mwakeMungu, Adamu na Hawa, wote wawili, waliakisi[walirudisha mwanga wa] sura yake. Munguangeweza kuwaumba wanadamu kama [kikaragosi]roboti wakizurura huku na huku katika ile bustani yaEdeni na kutosheka na kupaza sauti zao kumwabuduyeye. Lakini Mungu alitaka zaidi ya hilo; yaani, alitakakuwa na uhusiano wa kweli nao. Maroboti yanawezakutabasamu, kusema, na hata kuosha vyombo vyakulia chakula, ila hayawezi kupenda.
Mungualituumbasisi kwamfanowake,tukiwa nauwezo wa kufikiri na kuchagua,na kukumbuka, kufahamu nakupenda. Adamu na Hawawalikuwa watoto wa Mungu, nakwa namna isiyoelezeka walikuwa wanapendwa sana naye.


3.Uovu Waingia Katika Dunia Hii Kamilifu
Adamu na Hawa walikuwa na kila kitu cha kuwaletea furaha. Walifurahiakuwa na afya kamili kimwili na kiakili, wakiishi katika bustani ile nzuri katikadunia hii isiyo na dosari (Mwanzo 2:8; 1:28-31). Mungu aliwaahidi kuwapawatoto na kufurahia kuona kazi ya mikono yao (Mwanzo 1:28; 2:15).Walikuwa na uzoefu wa kirafiki wa ana kwa ana na Muumbaji wao.Hapakuwa na wasiwasi, hofu, au ugonjwa wo wote wa kuziathiri siku zaozilizowaletea furaha kamili.
Je, dunia hii ilibadilikaje kwa ghafula mno na kuwa mahali pa mateso namisiba? Sura ya pili na ya tatu ya Mwanzo inatusimulia kisa chote juu yajinsi dhambi ilivyoingia katika dunia yetu. Uzisome kwa nafasi yako. Hapa nimuhtasari mfupi wa mambo yaliyomo katika sura hizo.
Muda fulani baada ya Mungu kuiweka dunia hii kamilifu, yule Shetani akajakatika Bustani ile ya Edeni kumjaribu Adamu na Hawa ili wamwasiMuumbaji wao. Mungu alimwekea yule Shetani mipaka ya mvuto wakekwenye mti mmoja tu katika ile bustani, yaani, kwenye ule “mti wa ujuzi wamema na mabaya.” Kisha akawaonya wale watu wawili, mume na mke,kuwa mbali na mti ule na kutokula kabisa matunda yake, la sivyo,wangekufa.
Lakini siku moja Hawa akazurura kuelekeakaribu na mti ule uliokatazwa. Shetaniakamshambulia upesi kwa kumwuzia manenoya kumshawishi. Alidai kwamba Mungu alikuwaamesema uongo kwake na ya kwamba endapoyeye angekula matunda ya mti ule, asingekufa,ila angekuwa na hekima kama Mungumwenyewe, akijua mema na mabaya. Kwabahati mbaya sana Hawa, na hatimaye Adamu,ambao walikuwa wanayajua mema tu,wakamruhusu Shetani kuwarubuni, kishawakalionja lile tunda lililokatazwa – hivyokukivunja kifungo chao cha imani na utii kwaMungu.
Mungu alikuwa amefanya mpango kwamba Adamu na Hawa wa “tawale”dunia yetu hii kama mawakili wake wa kazi zile alizoziumba Mungu(Mwanzo 1:26). Lakini kwa kuwa walikosa uaminifu kwa Mungu nakumchagua Shetani kama kiongozi wao mpya, basi, wale watu wawili,mume na mke, wakaipoteza mamlaka yao. Leo hii Shetani anadai kwambadunia hii ni yake, tena anajitahidi sana kuwanasa watu wa dunia hii.

Mara nyingi sana tunajikuta tukifanya jambo fulani la uchoyo au hata kuwawakatili wakati tunalotaka kufanya hasa ni kinyume chake. Hivi kwa nini?Kwa sababu huyo adui asiyeonekana kwa macho yetu, yaani, huyoShetani, anafanya kazi yake ili kuwafanya watu washindwe kimaadili.
Unapoisoma sura ya tatu ya Mwanzo, utagundua kwamba dhambi ilimfanyaAdamu na Hawa kujificha kwa hofu ili Mungu asiwaone. Dhambi iliathiriuumbaji wote. Miiba ikajitokeza pamoja na maua. Ardhi ikaathirika kwaukame, na kazi ikawa ni mzigo ulemeao. Ugonjwa ukaanza kuwashambuliawatu hapa na pale bila kuwa na mpangilio. Wivu chuki, na uchoyovikazidisha taabu zao. La kutisha mno, pamoja na ile dhambi ikaja mauti.


4.Shetani Huyo Ni Nani Ambaye Aliiambukiza Dunia Yetu Dhambi?
“Yeye alikuwa MWUAJI TANGU MWANZO; wala hakusimama katikakweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, yaliyoyake mwenyewe, kwa sababu yeye ni mwongo na BABA WA UONGO”-(Yohana 8:44).
Kulingana na Yesu, Shetani ndiye mwanzilishi wa dhambi katika dunia hii,yeye ni “baba” wa dhambi na hivyo ni baba wa mauaji na uongo
Thomas Carlyle, mwanafalsafa mashuhuri wa Kiingereza, siku mojaalimchukua Ralph Waldo Emerson na kumtembeza kupitia katika baadhi yamitaa michafu sana iliyoishia mashariki mwa mji wa London. Walitembeapamoja, wakiangalia kimya kimya na kuona umaskini na uovuuliowazunguka pande zote, hatimaye Carlyle akauliza, “Je! unaamini juu yaShetani sasa?”


5.Je! Mungu Alimwumba Shetani?
La! Mungu mwema asingeweza kumwumba Shetani. Na, hata hivyo, Bibliainasema kwamba Shetani, pamoja na malaika wale aliowadanganya,walipoteza mahali pao mbinguni na kuja katika dunia yetu.
“Kulikuwa na VITA MBINGUNI.Mikaeli na malaika zakewakapigana na yule joka, nayeJOKA NA MALAIKA ZAKEakapigana nao. Naohawakushinda wala mahali paohapakuonekana mbinguni. Yulejoka mkubwa akatupwa chinikwa nguvu – nyoka yule wazamani, aitwaye Ibilisi auShetani, audanganyayeulimwengu wote. Akatupwa kwa nguvu mpaka duniani, na malaikazake wakatupwa pamoja naye” (Ufunuo 12:7-9).
Huyo Shetani aliingiaje kwanza kule mbinguni?
“Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye. Naamnalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu;……ULIKUWA MKAMILIFU KATIKA NJIA ZAKO tangu siku ileULIPOUMBWA HATA UOVU ULIPOONEKANA NDANI YAKO” (Ezekieli28:14,15).
Mungu hakumwumba Shetani, alimwumba Lusifa, malaika mkamilifu,mmojawapo wa malaika wakuu wa mbinguni, aliyesimama karibu na kiticha enzi cha Mungu. Lakini baadaye alitenda dhambi -“uovu ulionekanandani” yake. Akiwa amefukuzwa mbinguni, naye akijifanya ni rafiki waAdamu na Hawa, aligeuka na kuwa adui, mwenye madhara makubwa mno,kwa wanadamu.


6.Kwa Nini Lusifa, Alitenda Dhambi?
“Jinsi ULIVYOANGUKA KUTOKA MBINGUNI, Ewe nyota ya alfajiri(Lusifa), mwana wa asubuhi!…….. Nawe ulisema moyoni mwako,

“Nitapanda mpaka mbinguni; nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota zaMungu………. NITAFANANA NA YEYE ALIYE JUU”- (Isaya 14:12-14).
Kiumbe yule aliyegeuka na kuwa Shetani, zamanialiitwa Lusifa, maana yake “nyota ya alfajiri” au”yule anayeng’aa.” Ndani ya moyo wa malaikahuyo, kiburi na kutaka makuu, mambo hayo,yakaanza kuchukua mahali pa kumwabuduMungu. Mbegu ya kiburi ikakua mpaka ikawatamaa isiyotulizika ya kutaka kuchukua mahali paMungu.
Bila shaka Lusifa alikuwa amejitahidi sanakuwashawishi viumbe wale wengine wa mbingu.Ni rahisi kuingiwa na mawazo na kumwonaShetani akibishana na Mungu kwamba alikuwaakizuia kitu fulani ili wao wasikipate, na yakwamba sheria ya Mungu [Amri Kumi] ilikuwainawabana vibaya mno, na ya kwamba Mungualikuwa ni mtawala asiyejali. Akamsingizia yulemmoja ambaye tabia yake inaonyesha upendo ninini.
Vita hiyo ilisuluhishwaje kule mbinguni?
“Moyo wako ukiinuka kwa sababu ya uzuri wako,……….. nimekutupachini” (Ezekieli 28:17).
Kiburi kilimgeuza yule mkuu wa malaika na kumfanya Ibilisi au Shetani. Naili kuhifadhi amani na umoja ulioko kule mbinguni, yeye pamoja na theluthimoja ya malaika wa mbinguni waliojiunga naye katika maasi yale.Wakapaswa kufukuzwa kule (Ufunuo 12:4, 7-9).


7.Nani Anawajibika Kwa Dhambi?
Kwa nini Mungu hakuwaumba viumbe wasio na uwezo wa kutendadhambi? Kama angefanya vile, basi, pasingekuwako na tatizo lo lote lauovu katika dunia yetu. Lakini Mungu alitaka kuwa na watu ambaowangekuwa na uhusiano unaoleta maana. Kwa hiyo “Mungu akaumba mtukwa mfano wake” (Mwanzo 1:27). Hii maana yake ni kwamba sisi tukohuru, tena tunawajibika. Tunaweza kuamua kumpenda Mungu aukumgeuzia migongo yetu.
Mungu aliwapa malaika wale pamoja na wanadamu wa kila kizazi, tabia yakiroho na uwezo wa kufanya tabia ya kiroho na uwezo wa kufanya uchaguzihalisi.
“Chagueni wenyewe hivi leo mtakayemtumikia.” Yoshua 24:15.
Mungu anatoa changamoto kwa viumbe wake aliowaumba kwa mfanowake ili wachague kutenda mema kwa sababu uwezo wao wa kufikiriunawaambia kwamba “Njia ya Mungu ni bora kuliko zote.” Kisha kugeukiambali na makosa kwa sababu uwezo wao wa kufikiri unawaonya dhidi yamatokeo ya uasi na dhambi.
Ni viumbe wale tu walio na uwezo wa kufikirina kuchagua wawezao kuwa na upendo wakweli. Mungu alitamani sana kuwaumbawatu ambao wangeweza kuijua nakuithamini tabia yake, kuitikia kwakuonyesha upendo wao kwake, na kujazwana upendo wake, kwa ajili ya wengine.Mungu alitaka sana kuwashirikisha upendowake hata akawa tayari kujiingiza katikahatari kubwa mno ya kuwaumba malaika nawanadamu wenye uwezo wa kuchagua.Alijua kwamba uwezekano uliokuwapokwamba siku moja mmojawapo wa viumbe wake aliowaumba angewezakuchagua asimtumikie yeye. Shetani alikuwa kiumbe wa kwanza katika malimwengu kufanya uchaguzi wa kutisha. Misiba iliyoletwa na dhambiilianzishwa naye (Yohana 8:44, 1 Yohana 3:8).


8.Msalaba Unafanya Uwezekano Uwepo Wa Kuangamizwa KwaDhambi
Kwa nini Mungu hakumwangamiza Lusifa kabla ya ugonjwa wake wadhambi kuweza kuenea? Lusifa alikuwa amepinga kwa kusema kwambaserikali ya Mungu ilikuwa haina haki. Alikuwa amesema uongo kumhusuMungu. Kama Mungu angekuwa amemwangamiza Lusifa wakati ule ule,basi, malaika wale wangekuwa wameanza kumtumikia yeye [Mungu] kwahofu badala ya kumtumikia kwa upendo. Hilo, kwanza kabisa lingekuwalimelivunjilia mbali kusudi la Mungu la kuwaumba viumbe wenye uwezo wakuchagua.
Mtu ye yote angewezaje kujua kama njia ya Mungu ilikuwa kweli bora kulikozote? Mungu alimpa Shetani nafasi ya kuonyesha mfumo wake mbadala.Hii ndiyo maana alipewa fursa [nafasi] ya kumjaribu Adamu na Hawa.
Sayari hii imegeuka na kuwa uwanja wa majaribio ambamo hulinganishwatabia ya Shetani na aina ya ufalme wake na tabia ya Mungu na aina yaSerikali yake. Nani mwenye haki? Ni nani tuwezaye kumtegemeamwishowe? Lusifa alikuwa mdanganyifu mno, hata imechukua muda kwaviumbe wa malimwengu kuweza kusadiki kabisa jinsi ilivyo hasa ile njiambadala iletayo maafa aliyoichagua Shetani. Lakini hatimaye kila mtuatatambua kwamba “mshahara wa dhambi ni mauti” na ya kwamba”karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu”(Warumi 6:23).
Kila kiumbe katika malimwengu hayo wakati ule kitakubali kwamba:-
“Ni makuu, na ya ajabu, matendo yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi. Niza haki, na za kweli, njia zako, Ee mfalme wa mataifa…. mataifa yotewatakuja na kusujudu mbele zako, kwa kuwa matendo yako ya hakiyamekwisha kufunuliwa” – (Ufunuo 15:3,4).
Baada ya kila mtu kuielewa tabia yakufisha ya dhambi na hali ya uharibifuinayoletwa na falsafa ya Shetani, ndipoMungu anaweza kumwangamiza Shetanipamoja na dhambi. Atalazimika piakuwaangamiza wale ambao kwa ukaidiwao wanapinga neema yake nakuing’ang’ania ile njia mbadala aliyoiwekaShetani.
Mungu anahangaika vile vile kulitatuatatizo hilo la dhambi na mateso kama sisitunavyotaka yeye afanye hivyo. Lakinianangojea mpaka hapo atakapoweza kufanya hivyo kwa msingi utakaoletamatokeo ya kudumu, na mpaka hapo anapoweza kuuhifadhi uhuru wetu wakuchagua na kuuzuia uovu usipate kutokea tena.
Mungu ameahidi kuiangamiza dhambi milele kwa njia ya kuzitakasa mbinguna dunia hii kwa moto. “kama ilivyo ahadi yake” tunaweza ku”tazamiambingu mpya na nchi mpya, makao ya wenye haki” (2Petro 3:10,13).Dhambi haitaenea kamwe katika malimwengu kwa mara ya pili. Matokeomabaya sana ya dhambi yataonekana wazi kabisa kiasi kwamba uasi dhidiya Mungu utaonekana kuwa ni wa kuchukiza milele zote.
Je, ni nani anayefanya uwezekano uwepo wa kumwangamiza Shetanipamoja na dhambi?
“Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye[Kristo] vivyo hivyo alishiriki katika ubinadmu wao, ili kwa njia yamauti apate kumharibu yeye aliye na nguvu za mauti – yaani Ibilisi -awaache huru wale ambao katika maisha yao yote walikuwawameshikiliwa katika hali ya utumwa kwa hofu yao ya mauti” -(Waebrania 2:14,15).

Pale msalabani malaika pamoja na wale wa dunia zisizoanguka dhambiniwalimwona Shetani kama alivyo hasa – laghai, mwongo, mwuaji. Pale ndipoalipoidhihirisha tabia yake halisi kwa kuwalazimisha wanadamu kumwuaMwana wa Mungu asiye na hatia. Wakazi wa malimwengu yote walijioneawenyewe jinsi dhambi isivyo na maana kabisa na ilivyo katili kama vile ilivyohasa. Msalaba uliyafichua kabisa makusudi ya Shetani, na Munguatakapomwangamiza Shetani pamoja na wale wanaoendelea kutendadhambi, wote watakiri kwamba Mungu ni mwenye haki.
Kifo cha Yesu pale msalabani kilifunua wazimbele ya viumbe wote walioumbwa kusudihalisi alilonalo Shetani (Yohana 12:31,32). Piamsalaba ule ulimfunua Kristo alivyo hasa -yaani, yeye ndiye Mwokozi wa ulimwengu.Pale Golgotha nguvu ya upendo ilijitokezawazi kabisa dhidi ya kupenda mamlaka.Msalaba ule ulithibitisha bila shaka lolotekwamba ni ule upendo unaojitoa kafaraambao unamsukuma Mungu katikakushughulika kwake kote na Shetani, dhambi,pamoja na wanaume na wanawake wenyedhambi.
Pale msalabani Kristo alionyesha upendo waMungu usio na masharti kwa njia iliyokuwa nauwezo wa kuushawishi moyo na kumshinda kabisa Shetani. Vita ilikuwa juuya nani atakayeitawala dunia hii, Kristo au Shetani? Tena, msalaba uleuliamua hoja hiyo kwa wakati wote. Ni lazima awe Kristo juu ya wote!
Je, umeugundua uhusiano wako na Mwokozi aliyekufa ili kuudhihirishaupendo wake usio na kifani, ambao haubadiliki? Unajisikiaje kuhusiana nahuyo mmoja aliyekuja katika dunia yetu kama mwanadamu, na kufa badalayako ili kukuokoa wewe mbali na matokeo ya dhambi? Je, utainamishachini kichwa chako hivi sasa na kumshukuru Yesu, na halafu kumwombaaingie ndani na kuyatawala maisha yako?…………………

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top
MKUSDA CHURCH