MKUSDA CHURCH
Unity in Worship

2. TWAWEZA KUIAMINI BIBLIA

Mabaharia waasi maarufuwalioizamisha meli yaKiingereza iliyoitwa Bountywaliishia kufanya makazi yaowakiwa pamoja na wanawake,wenyeji wa eneo lile katikakisiwa cha Pitcairn katika Bahariya Pasifiki ya Kusini. Kundi lilelilikuwa mabaharia tisa waKiingereza, wanaume wa Kitahitisita, wanawake wa Kitahiti kumi,na msichana wa miaka kumi namitano. Mmojawapo wamabaharia wale alivumbuanamna ya kutonesha [kugeuzakuwa mvuke] alkoholi, na baadaya muda mfupi ulevi ukaliharibu koloni lile lililokuwa katika kisiwa kile.Ugomvi kati ya wanaume na wanawake ukageuka na kuwa wa kutumianguvu.
Baada ya kupita muda fulani mmoja tu kati ya wanaume wale wa kwanzawaliofika mle kisiwani ndiye alibaki kuwa hai. Lakini mtu huyo, AlexanderSmith, alikuwa ameigundua Biblia katika mojawapo la makashayaliyochukuliwa kutoka katika ile meli. Alianza kuisoma na kuwafundishawengine juu ya kile ilichosema. Alipofanya hivyo maisha yake yeyemwenyewe yakabadilika na hatimaye maisha ya wote waliokuwa katikakisiwa kile.
Wakazi wa kisiwa kile walikuwa wametengwa na ulimwengu wa nje mpakailipowasili meli ya Kimarekani iliyoitwa Topaz katika mwaka wa 1808.Wafanyakazi katika meli hiyo wakakikuta kisiwa kile kikiwa na jumuiainayokua na kusitawi, bila ya kuwa na pombe kali (wiski), gereza, walauhalifu. Biblia ilikuwa imekigeuza kisiwa kile kutoka jehanamu ya dunianikwenda katika kielelezo cha vile Mungu atakavyo ulimwengu huu uwe. Nampaka leo hii kinaendelea kuwa katika hali hiyo.
Je, hivi Mungu bado anaendelea kusema na watu kupitia katika kurasa hizoza Biblia? Bila shaka anafanya hivyo. Ninapoandika haya, naliangaliakaratasi la majibu lililotumwa kwetu na mwanafunzi mmojawapo wa kozizetu za Biblia. Maelezo chini yake yanasema hivi “Mimi nimo gerezani, nikokatika orodha ya watu wanaostahili kunyongwa, nimehukumiwa kufa kwakutenda kosa la jinai. Kabla ya kuchukua kozi hii ya Biblia, nilikuwanimepotea lakini sasa ninacho kitu cha kutumainia tena nimeupata upendompya.”
Biblia inao uwezo unaoweza kuyabadilisha kabisa maisha ya watu. Kwakweli, watu wanapoanza kujifunza Biblia, maisha yao hubadilika kwanamna ya kuvutia sana.


1.Jinsi Mungu Anavyozungumza Nasi Kupitia Katika Biblia
Baada ya kumwumba Adamu na Hawa, yaani, yule mwanaume namwanamke wa kwanza wa duniani, Mungu alizungumza nao uso kwa uso.Lakini Mungu alipokuja kuwatembelea baada ya wao kutenda dhambi, je,wale watu wawili walifanya nini?

“Mwanaume yule na mkewewakasikia sauti ya BWANA Mungualipokuwa akitembea mle bustaniniwakati wa jua kupunga, naoWAKAJIFICHA ASIWAONE BWANAMUNGU katikati ya miti ya bustani.”(Mwanza 3:8).
Dhambi ilikata mawasiliano ya anakwa ana kati ya mwanadamu naMungu. Baada ya dhambi kuingiakatika ulimwengu huu, je, Mungualiwasilianaje na watu?
“Hakika Bwana Mwenyezi hafanyikitu, bila kuwafunulia watumishiwake manabii nia yake.” – Amosi 3:7.
Mungu hakutuacha sisi gizani kuhusu maisha haya tuliyo nayo na maanayake. Kupitia kwa manabii wake – yaani, watu wale aliowaita Mungu kuwawanenaji na waandishi wake – wamefunua majibu yake kwa maswali makuuyahusuyo maisha yetu.


2.Ni Nani Aliyeiandika Biblia?
Manabii waliutoa ujumbe wa Mungu kwa kutumia sauti na kalamu zaokatika kipindi chao walichoishi, na walipokufa, maandiko yao yaliendeleakuwapo baada yao. Kisha ujumbe huo wa manabii ulikusanywa pamojachini ya uongozi wake Mungu, na kuwekwa katika kitabu tunachokiitaBiblia.
Lakini maandiko yao hayo yanaaminika kwa kiasi gani?
“Zaidi ya hayo, lakini kumbukeni kwamba hakuna mtu ye yoteawezaye kufafanua mwenyewe unabii ulio katika Maandiko Matakatifu.Maana hakuna ujumbe wa kiunabii unaotokana na matakwa yabinadamu bali watu walitoa unabii wakiongozwa na Roho Mtakatifu” (2Petro 1:20,21).
Waandishi wa Biblia waliandika si kwakufuata mapenzi au tamaa yao, bali kamawalivyoongozwa au kuvuviwa na Roho waMungu. Biblia ni kitabu cha Mungu!
Katika Biblia hiyo Mungu hutuambia habarizake Mwenyewe, tena hutufunulia makusudiyake aliyo nayo kwa ajili ya wanadamu.Inaonyesha mtazamo wa Mungu kwamambo yale yaliyopita, kisha inatufunuliamambo ya mbele, ikitueleza jinsi tatizo lauovu litakavyotatuliwa mwishoni na jinsiamani itakavyokuja katika dunia yetu.
Je, hivi Biblia yote ni ujumbe utokao kwaMungu?
“Maandiko yote, Matakatifu yameandikwa kwa uongozi wa Mungu, nayanafaa kuonya, kusahihisha makosa yao, na kuwaongoza, katikakufundishia ukweli, mtu wa Mungu awe mkamilifu na tayari kabisakufanya kila kazi njema, waishi maisha adilifu” – (2 Timotheo 3:16,17).
Biblia Takatifu huyabadilisha kabisa maisha ya wanadamu kwa sababuBiblia “yote” ina “pumzi ya Mungu,” ni hati iliyovuviwa, ni kitabu cha Mungu.Manabii walisimulia kile walichokiona na kukisikia kwa kutumia lugha yawanadamu, lakini ujumbe wao ulitoka moja kwa moja kwa Mungu. Kwahiyo, ukitaka kujua maisha haya yana maana gani, soma MaandikoMatakatifu. Kuisoma Biblia kutayabadilisha kabisa maisha yako. Kadiriunavyozidi kuisoma kwa maombi, ndivyo utakavyozidi kupata amanimoyoni mwako.

Roho Mtakatifu yule yule aliyewavuvia manabii kuandika, Biblia hiyo,atayafanya mafundisho ya Biblia, injili yake, ifae kuyabadilisha kabisamaisha yako ukimwalika Roho kuwapo wakati unapoisoma hiyo Biblia.


3.Umoja wa Biblia
Kwa kweli Biblia ni maktaba ya vitabu 66. vitabu 39 vya Agano la Kaleviliandikwa kuanzia karibu na mwaka wa 1450 K.K hadi 400 K.K, Vitabu 27vya Agano Jipya viliandikwa kati ya mwaka wa 50 B.K na mwaka wa 100B.K.
Nabii Musa alianza kuandika vitabu vitano vya kwanza wakati fulani kablaya mwaka wa 1400 K.K. Mtume Yohana alikiandika kitabu cha mwisho chaBiblia, yaani, kitabu cha Ufunuo, karibu na mwaka wa 95 B.K. Katika kipindicha miaka 1,500 kati ya kuandikwa kitabu cha kwanza na cha mwisho chaBiblia, walau watu wengine wapatao 38 waliovuviwa walitoa mchango wao.Wengine walikuwa wafanya biashara, wengine wachungaji wa kondoo,wengine wavuvi, wengine askari, matabibu, wahubiri, wafalme – wanadamutoka katika tabaka zote za maisha. Mara nyingi waliishi katika utamaduni nafalsafa vilivyohitilafiana.
Lakini hapa ndipo yalipo maajabu ya maajabu yote: Vitabu hivyo 66 vyaBiblia pamoja na sura zake 1,189 zenye idadi ya mafungu 31,173vikiwekwa pamoja, tunaona umoja na mwafaka katika ujumbe vinaoutoa.
Hebu na tuseme kwamba mtu mmojaanagonga mlangoni pako, halafuanapokaribishwa ndani, anawekakipande cha marumaru chenye umbo laajabu juu ya sakafu ya chumba chakocha kuongea, halafu anaondoka bilakusema neno lo lote. Wageni wenginewanamfuata, mmoja baada yamwingine, mpaka takribani watu 40wanaweka kila mmoja kipande chake cha marumaru mahali pake.
Wa mwisho anapokwenda zake, kwa mshangao wewe unaona jengo zurilimesimama mbele yako. Ndipo wewe unajifunza kwamba sehemu kubwaya “mafundi hao wanachonga mawe” hawajawahi kuonana kamwe, wakiwawamekuja, kama walivyofanya, kutoka Amerika ya Kusini, China, Urusi,Afrika na sehemu nyingine za ulimwengu.
Je, wewe ungeamua nini? Ya kwamba mtu fulani alipanga umbo hilolililojengwa kwa mawe ya kuchonga naye alimtumia kila mtu vipimo sahihikutokana na kipande chake kile kimoja cha marumaru.
Biblia nzima inatoa ujumbe mmoja unaoshikamana – sawasawa tu na lilejengo la mawe yaliyochongwa ya marumaru. Mtu fulani mmoja mwenyeakili alipanga yote hayo, yaani, ni akili za Mungu. Umoja wa kushangaza waMaandiko Matakatifu unatoa ushahidi wake kwamba ingawa ni wanadamuwalioyaandika mawazo yale, yalikuwa yamevuviwa naMungu.


4.Waweza Kuiamini Biblia
1.Kuhifadhiwa kwa Biblia ni jambo la ajabu sana. Maandiko yote ya awaliya Biblia yalinukuliwa kwa mkono – muda mrefu kabla ya kuwako
mitambo ya kuchapisha vitabu. Waandishi wale walitayarisha nakala zamaandiko ya mkono ya asilia na kuzitawanya. Maelfu ya nakala kama hizoza maandiko ya mkono au sehemu zake bado ziko mpaka sasa.
Maandiko ya mkono ya Kiebrania yanayorudi nyuma hadi ule mwaka wa150 mpaka 200 kabla ya Kristo yalipatikana karibu na Bahari ya Chumvimnamo mwaka 1947. Ni jambo la kushangaza sana kwamba magombohayo mawili yenye umri wa miaka elfu mbili yanazo kweli zile ziletunazozikuta katika Agano la Kale la Biblia zinazochapishwa siku hizi. Huuni ushahidi wenye nguvu unaoonyesha jinsi Neno la Mungu linavyoaminika.

Mitume waliandika kwanza sehemukubwa ya Agano Jipya kama nyarakawalizozituma kwa makanisa ya Kikristoyaliyoanzishwa baada ya kifo na ufufuowake Kristo. Zaidi ya maandiko yamkono 4,500 ya Agano Jipya lote ausehemu yake yanapatikana katikanyumba za Makumbusho na maktabaza Ulaya na Amerika. Baadhi yakeyanakwenda nyuma hadi karne ile yapili. Kuyalinganisha maandiko hayo yamkono ya awali na biblia ya siku hizi,twaweza kuona kwa urahisi kwambakwa kawaida Agano Jipya limeendeleapia kubaki bila mabadiliko yo yotetangu lilipoandikwa kwa mara ya kwanza.
Siku hizi Biblia au sehemu zake zimetafsiriwa katika lugha zaidi ya 2,060 na(dialects). Ni kitabu kinachouzwa sana ulimwengu: zaidi ya Biblia milioni150 na sehemu za Biblia huuzwa kila mwaka.
2.Usahihi wa Biblia kihistoria ni wakushangaza sana. Uvumbuzi mwingi waelimu ya mambo ya kale (akiolojia)umethibitisha kwa namna ya kuvutia sanausahihi wa Biblia. Wanahistoriawamevigundua vibao vya udongo wamfinyanzi pamoja na majengo yakumbukumbu ya mawe ambayoyameonyesha majina, mahali, na matukioyaliyojulikana kuhusu siku za nyumakutokana na Biblia tu.
Kwa mfano, kulingana na Mwanzo 11:31,Ibrahimu na familia yake “wakatoka wotekatika Uru… waende katika nchi yaKanaani.” Kwa kuwa ni Biblia peke yakeiliyosema juu ya Uru, mabingwa fulani waBiblia walisema kwamba mji kama huo ulikuwa haujapata kuwako kamwe.Ndipo wachimbaji wa mambo ya kale wakagundua mnara wa hekalu katikanchi ya Iraki Kusini ukiwa na kwenye msingi wake iliyoandikwa katikamaandishi ya kikabari yaliyokuwa na jina la Uru. Ugunduzi wa baadayeulionyesha kwamba Uru ulikuwa ni mji mkuu ambao ulikuwa unasitawiwenye ustaarabu wa hali ya juu uliokuwa umefikiwa. Sura ya mji ule ilikuwaimesahaulika ni Biblia peke yake iliyolihifadhi jina lake – mpaka pale koleoya mwanaakiolojia mmoja ilipouthibitisha ukweli wa kuwako kwake. Na huoUru ni mmoja tu miongoni mwa mifano mingi ya akiolojia inavyothibitishausahihi wa Biblia.
3.Kutimia kwa usahihi kabisa kwa utabiri wa Biblia hukuonyesha wewekwamba unaweza kuitegemea Biblia. Maandiko hayo yana utabiri mwingiwa kushangaza sana wa matukio ya siku za usomi ambayo hivi sasayanaendelea kutimia mbele ya macho yetu. Tutauchunguza baadhi yaunabii huo wa kusisimua katika masomo ya mbele.


5.Jinsi Ya Kuielewa Biblia
Unapolichunguza Neno la Mungu, weka kanuni hizi mawazoni mwako:
1.Jifunze Biblia ukiwa na moyo wamaombi. Ukiyaendea MaandikoMatakatifu kwa moyo na mawazoyaliyofunguliwa kwa maombi,yatageuka na kuwa mawasiliano katiyako na Yesu (Yohana 16:13-14).
2.Soma Biblia kila siku. KujifunzaBiblia kila siku ni ufunguo wa kupata nguvu katika maisha yetu, ni kukutana na mawazo ya Mungu (Warumi1:16).
3.Unapoisoma, iache Biblia ijieleze yenyewe. Uliza: mwandishi huyu waBiblia alikusudia kusema nini? Kwa kuzingatia kile limaanishacho funguhilo, twaweza kuitumia kwa akili katika maisha yetu ya leo hii.
4.Soma Biblia kwa kufuata somo. Linganisha andiko na andiko. Yesualitumia mbinu hii kuthibitisha kwamba yeye alikuwa ndiye Masihi:
“Akaanza kutoka Musa na Manabii wote, akawaeleza katika maandiko yotemambo yaliyomhusu yeye mwenyewe.”
5.Jifunze Biblia ili kupokea uwezo wa kuishi kwa ajili ya Kristo. Neno laMungu limeelezwa katika Waebrania 4:12 kama upanga mkali ukataokuwili. Ni zaidi ya maneno tu yaliyo juu ya ukurasa, ni silaha iliyo haimikononi mwetu ya kupigia na kuyaondolea mbali majaribu yaleyanayotushawishi kutenda dhambi.
6.Sikiliza Mungu anapozungumza nawe kupitia katika Neno lake. Endapomtu anataka kuujua ukweli wa Bilbia juu ya somo fulani, basi, ni lazima awetayari kufuata yale inayofundisha (Yohana 7:17), sio yale anayofikiri mtufulani, au yale yanayokaziwa na fundisho lolote la kanisa lake.


6.Biblia Yaweza Kubadilisha Maisha Yako
“Kuyafafanua maneno yako [Mungu] kwatia nuru, kunampa ufahamumjinga” – (Zaburi 119:130).
Kujifunza Biblia kutauimarisha “ufahamu” wako, kutakupa nguvu yakuyashinda mazoea yale yaletayo madhara, na kukuwezesha kukuakimwili, kiakili, kimaadili na kiroho.
Biblia inazungumza na moyo. Inashughulika na mambo yale yanayowapatawanadamu katika maisha yao – yaani, upendo, ndoa, uzazi na kifo.Inaliponya jeraha lenye kina kirefu sana katika tabia ya mwanadamu,pamoja na dhambi na taabu inayotokana nayo.
Neno la Mungu si kitabu cha jamiimoja, kizazi kimoja, taifa moja, auutamaduni mmoja. Japokuwaliliandikwa katika nchi ya Masharikiyakati, linawavutia pia wanaume nawanawake wa Magharibi. Linaingiakatika nyumba za wanyonge na katikamajumba makubwa ya matajiri.Watoto wanazipenda hadithi zakezinazosisimua. Mashujaa wakewanawavutia sana vijana. Wagonjwa,wanaoishi katika hali ya upweke, na wazee wanagundua ndani yake farajana tumaini la kuwa na maisha bora.
Kwa kuwa Mungu anafanya kazi yake kupitia katika Biblia, basi, inao uwezomkubwa. Inaivunjavunja hata mioyo iliyofanywa migumu dhidi ya hisia zoteza kibinadamu, inailainisha na kuijaza na upendo. Tumeona Bibliaikimbadilisha haramia wa zamani na mvuta bangi na kumfanya mhubirialiye motomoto. Tumeona Biblia ikimbadilisha mwongo na mdanganyaji nakumfanya kuwa mwalimu mwaminifu na mwenye kuheshimika. Tumeonakitabu hicho kikiwanyakua watu wakiwa karibu na kujiua wenyewe nakuwapa tumaini la kuanza maisha upya. Biblia inaamsha upendo miongonimwa maadui. Inawafanya wenye majivuno kuwa wanyenyekevu, nawachoyo kuwa wakarimu. Biblia inatutia nguvu tunapokuwa dhaifu,inatuchangamsha tunapokuwa katika hali ya kukata tamaa, inatufarijitunapokuwa na huzuni, inatuongoza tunapochoka sana. Inatuonyesha jinsiya kuishi kwa ujasiri na jinsi ya kufa bila hofu.
Kitabu hicho cha Mungu, yaani, Biblia kinaweza kuyabadilisha maishayako! Utagundua hivyo kwa dhahiri zaidi na zaidi, kadiri unavyoendeleakujifunza miongozo hii ya GUNDUA.

Kwa nini Biblia hiyo iliandikwa kwa ajili yetu? Yesu anatoa jibu:
“Lakini hizi[kweli za Biblia] zimeandikwa; ili mpate kuamini ya kwamba Yesundiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini muwe na uzima kwajina lake” – (Yohana 20:31).
Sababu kuu kuliko zote kwa nini sisi tunapaswa kuyafahamu MaandikoMatakatifu ni kwamba yamejaa picha zinazomfunua Yesu Kristo nakutuhakikishia sisi uzima wa milele. Kwa kumtazama Kristo katika Biblianzima, tunabadilika na kufanana naye zaidi. Basi, kwa nini wewe usianzesasa kugundua uwezo huo wa Neno la Mungu uwezao kukufanya wewekufanana zaidi na Yesu?

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top
MKUSDA CHURCH