JE! NAWEZA KULIPATA KANISA LA MUNGU LEO?
Mara kwa mara Mungu ametoa ujumbe wapekee kukidhi mahitaji ya vizazi tofauti mbalimbali: ujumbe wa kumsaidia Adamu naHawa baada ya dhambi kuiharibu dunia yao,ujumbe kwa ulimwengu uliokuwako kabla yagharika ile kuu ya maji, ujumbe kwa Israeliwakati Ashuru au Babeli ilipowatishia. Yesualikuja na ujumbe maalum kwa siku zetu.Sura ya 12 na 14 ya Ufunuo hutoamuhtasari wa ujumbe wa Mungu wa pekeekwa ajili yetu leo. Katika GUNDUAMwongozo huu na mwongozo uleunaofuata, tutauangalia ujumbe huo.
1.Kanisa Lilianzishwa Na Yesu
Maisha na mafundisho ya Yesu yalianzisha umoja wa imani na ushirika wakaribu sana katika kanisa lile la mitume walilolianzisha. Mitume walewalikuwa na uhusiano wa karibu kabisa na Kristo yule aliyefufuka. Pauloalitoa picha ya kifungo hicho cha karibu sana na kukilinganisha na uhusianowa ndoa:
“Naliwaposea Mume mmoja, yaani, Kristo, ili niwalete ninyi kwakemkiwa bikira safi.” – 2 Wakorintho 11:2.
Kulingana na maneno ya Paulo, kanisa la Kikrsto ni mwanamke safi, ni bibi-arusi wa Kristo, ishara inayofaa kabisa kwa kanisa lake Kristo alipendalo.Katika Agano la Kale mithali iyo hiyo inatumika kuielezea Israeli, yaani,wateule wa Mungu. Mungu aliwaambia Israeli: “wewe kama bibi-arusiulinipenda mimi” (Yeremia 2:2); “Mimi ni mume wenu” (Yeremia 3:14).
Kitabu cha Ufunuo pia kinazungumza juu ya kanisa kama mwanamke:
“Ishara kuu na ya ajabu ilionekana mbinguni: mwanamke aliyevikwajua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na taji ya nyota kumi nambili juu ya kichwa chake” – (Ufunuo 12:1).
Mwanamke huyo ame”vikwa jua”. Maneno hayoyanadokeza kanisa linalong’aa kama jua, kwasababu ya kuvikwa utukufu wa kuwako kwakeKristo. Yesu, “Nuru ya Ulimwengu” (Yohana 8:12),anaangaza kupitia kwa washiriki wa kanisa lake,nao kwa upande wao wanapaswa kuwa “nuru yaulimwengu” (Mathayo 5:14).
Mwanamke huyo ana”mwezi chini ya miguuyake.” Mwezi huo unawakilisha nuru ya Injiliiliyoakisiwa [iliyoangaza] katika dhabihu nataratibu za ibada ya watu wa Mungu katika Aganola Kale. Mwezi huo ukiwa “chini ya miguu yake”unadokeza kwamba nuru ya Injili iliyoakisiwaimepitwa na huduma anayofanya Kristo.
Mwanamke huyo anayo “taji ya nyota kumi na mbili juu ya kichwa chake.”Nyota zinawakilisha vizuri sana mitume wale kumi na wawili, watu waadilifuambao ushuhuda wao juu ya Yesu unang’aa sana mpaka siku hii ya leo.
Ni dhahiri, basi, kwamba maelezo yamhusuyo mwanamke huyoyanaonyesha kwamba Yohana katika mawazo yake analiona badilikolililotokea kutoka kwa watu wa Mungu, Israeli, katika Agano la Kale kwendakwenye kanisa lile la Kikrsto la Agano Jipya alilolianzisha Yesu. Jua, mwezi,na nyota huitilia mkazo huduma ya kupeleka nuru inayofanywa na kanisahilo la Kikristo kwa kuzitangaza hizo Habari Njema.
2.Matukio Yanayofuatana Ya Kushindwa Kwa Shetani
Kuingia kwa mwanamke huyo kunaweka jukwaa kwa matukio haya makuuyanayofuatana:
“Alikuwa mja mzito, naye akapaaza sauti kwa maumivu na uchunguwa kujifungua mtoto. Kisha, ishara nyingine ikatokea mbinguni: jokamkubwa jekundu na lenye pembe kumi na vichwa saba; na kila kichwakilikuwa na taji. Joka hilo liliburuta kwa mkia wake theluthi moja yanyota za anga na kuzitupa duniani. Nalo lilisimamaa mbele ya huyomama aliyekuwa karibu kujifungua mtoto, tayari kabisa kummezamtoto, mara tu atakapozaliwa. Kisha, mama huyo akajifungua mtotowa kiume ambaye atayatawala mataifa yote kwa fimbo ya chuma.Lakini mtoto akanyakuliwa na kupelekwa kwa Mungu na kwenye kitichake cha enzi” – Ufunuo 12:2-5.
Wakuu watatu wanashiriki katika mfululizo wa matukio haya:
Mwanamke, huyo tayari ametambulishwa kama kanisa lake Mungu.
Mtoto wa kiume aliyezaliwa na mwanamke huyo ana”nyakuliwa hata kwaMungu na kwenye kiti chake cha enzi,” na siku moja “atayatawala mataifayote.” Yesu ndiye mtoto peke yake aliyepata kuzaliwa katika ulimwengu huuambaye alinyakuliwa kwenda kwenye kiti cha enzi cha Mungu na ambayesiku moja atayatawala mataifa yote.
Joka anamwakilisha Ibilisi, au Shetani.
“Kisha kukazukaa vitambinguni: Mikaeli na malaikawake walipigana na hilo joka,nalo likawashambulia pamojana malaika wake. Lakini jokahilo na malaika wakewalishindwa, na hatimayehapakuwa tena na nafasimbinguni kwa ajili yao. Basi,joka hilo kuu likatupwa nje.Joka hilo ndiye yule nyoka wakale ambaye huudanganyaulimwengu wote. Naam,alitupwa duniani, na malaika wake wote pamoja naye.” – Ufunuo 12:7-9.
Picha hiyo inakuwa dhahiri mara tu tunapoifahamu mifano hiyo. Ibilisi namalaika zake “wa[lipo] poteza mahali pao mbinguni,” wali”tupwa duniani.”Yesu alipozaliwa katika dunia hii, Ibilisi alijaribu kumwua Yesu, mwana yulewa kiume, mara tu alipokwisha kuzaliwa. Alishindwa, kisha Yesu”akanyakuliwa” kwenda kwenye kiti cha enzi cha Mungu.
Ndipo Shetani akaondoka kwenda kuliangamiza kabisa kanisa la Kristoalilolianzisha Kristo. Mtume Yohana, aliyekiandika kitabu cha Ufunuo,aliliona kidogo tu pambano hilo kuu kati ya Kristo na Shetani likipiganwavikali sana juu ya dunia hii. Vita hiyo ilipofikia kilele chake wakati ule wakusulibiwa kwake Kristo, Yohana alisikia sauti ikipiga kelele kutokambinguni, ikisema:
“Kisha nikasikia sauti kubwa kutoka mbinguni ikisema: Sasa umefikiamkombozi na nguvu na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristowake! Maana yule aliyewashtaki ndugu zetu mbele ya Munguametupwa chini. Naam, ametupwa chini huyo anayewashtaki usiku namchana”- Ufunuo 12:10.
(Linganisha na Yohana 12:31 na Luka 10:18).
Yesu alipata ushindi dhidi ya Shetani pale msalabani. Wakati ule ndipoalipothibitisha uhakika wa mpango ule wa “wokovu” na kutoa “uwezo” wakuzipinga hila za Shetani. “Ufalme wa Mungu” ukaimarishwa, na “mamlaka”ya Mwokozi ya kuwa Kuhani wetu Mkuu na Mfalme wetu ikawaimethibitishwa.
“Sasa umekuja wokovu” ni tangazolinaloonyesha kwamba tendo lile la kilele lahistoria limefika. Kuzaliwa kwake Kristo,Mwokozi wa ulimwengu, kumekwishakutokea (fungu la 5). Licha ya majaribumakali ya Shetani, Yesu aliishi maishayasiyo na dhambi, alikufa na kufufukaakiwa mshindi dhidi ya dhambi na mauti(fungu la 10). Shetani ameshindwa milele(fungu la 7-9). Msalaba umetukuzwa katikauwezo wake wote.
Tangazo hili, “Sasa umekuja wokovu,”halimpendezi Yohana tu, bali malimwenguyote:
“Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, naninyi mkaao humo! Ole kwa nchi na bahari, kwa sababu Ibilisiameshuka kuja kwenu! Amejaa ghadhabu nyingi, kwa sababu anajuakwamba ana wakati mchache tu.” – (Ufunuo 12:12).
Mbingu yote ilisherehekea ushindi wa Kristo. Kristo aliyavunjilia mbalimadai ya aina yo yote ile aliyokuwa nayo Shetani zamani kuhusu kuwa namahali pake kule mbinguni, na yule Shetani aliyeshindwa akapoteza milelemadai yake aliyosema dunia hii ni yake.
3.Kanisa La Kikristo Katika Mapambano Dhidi Ya Shetani
Kabla Yesu hajapaa kwenda mbinguni alilianzisha kanisa la Kikristo(ambalo linafananishwa na mwanamke). Kifo chake pale msalabani kililipahilo kanisa la Kikristo uwezo wa kumshinda Shetani.”Nao [Kanisa la Kikristo] wakamshinda [Shetani] kwa damu ya Mwana-Kondoo na kwa neno la ushuhuda wao; hawakuyapenda sana maishayao kiasi cha kuogopa kufa.” – (Ufunuo 12:11).
Kristo anaweza kulipa kanisa lakeuwezo wake sasa, yaani, kulipa liletunda la ushindi wake. Yesualimshinda Shetani kabisa kwa njia yakanisa lake. Sifa tatu zinalitambulishakanisa hilo lenye kushinda katikakarne zilizokuwa zikiendelea kupitaza kipindi hiki cha Kikristo:
“Wakamshinda [Shetani] kwa damuya Mwana-Kondoo.” Yesualinyakuliwa hadi kwenye kiti cha enzicha Mungu ili apate kuifanya damu yake iwe na matokeo mema katikamaisha ya wafuasi wake. Yeye anaweza kuiondoa kumbukumbu ya dhambizetu, anaweza kutuokoa kwa njia ya damu yake iliyomwagika (1Yohana1:7), na kutupa uwezo wa kuishi maisha yenye afya ya Kikristo siku kwasiku.
“Hawakuyapenda sana maisha yao kiasi cha kuogopa kufa.” “Damu yaMwana-Kondoo” iliwafanya wawe tayari kufa kwa ajili ya kazi yake Kristo;hawa”kuogopa kufa.” Mungu alikuwa ameteseka sana,kwa hivyo Wakristowale wafia dini walikuwa tayari kuteswa na kuuawa. Hata watoto wadogowalijitoa mhanga hatimaye. Kisa kinasimuliwa cha mama mmoja Mkristoaliyetupwa kwa Simba katika uwanja wa michezo wa Kiroma kwa kuwaalitoa utii wake kwa Kristo, wala si kwa serikali. Binti yake mdogo,
badala ya kujikunyata kwa hofu kuu, alisikia ari ya kujitoa wakfu ikijaa ndaniyake. Wale simba walipomshambulia mama yake, alisimama na kupigakelele, “Mimi pia ni Mkristo.” Maafisa wa Kiroma wakamkamata na kumtupakwa nguvu kwa wanyama wale wenye njaa.
“Wakamshinda [Shetani]… kwa neno la ushuhuda wao.” Sio maneno, balineno la ushuhuda wao yaani, ushuhuda wa maisha yao, ushuhuda wao haikwa uweza wa Yesu na injili yake. Katika zile saa za giza nene kabisa lakipindi kile cha Kikristo, jeshi la Wakristo – kuanzia kwa mababa wale wakwanza wa kanisa hadi kwa wanamatengenezo wa kanisa la Kiprotestanti -waliyashinda mambo yote mabaya mno, ambayo Ibilisi aliweza kuwatupiakwa nguvu, kwa njia ya ushuhuda wao tu wenye nguvu wa maisha yao.
Ufunuo 12:11 huonyesha picha yakanisa linaloshinda ambalo limejaawashindi: mitume, wafia dini,wanamatengenezo ya kanisa, naWakristo wengineo waaminifu. Upole,uaminifu, ujasiri, na ushindi waoumenguruma kushuka katika karnenyingi na kuupindua ulimwengu.
Kwa kuwa Shetani alishindwakumwangamiza Yesu alipoishi hapa duniani, sasa anajitahidi sanakumwangamiza Kristo anayeishi ndani ya kanisa lake.
“Joka lilipotambua kwamba limetupwa chini duniani, likaanzakumwinda yule mama aliyekuwa amejifungua mtoto wa kiume. Lakinimama huyo akapewa mabawa mawili ya tai apate kuruka mbali sanana hilo joka, mpaka mahali pake jangwani ambapo angehifadhiwasalama kwa muda wa miaka mitatu na nusu. Basi, joka likatapika majimengi kama mto, yakamfuata huyo mama nyuma ili yamchukue.Lakini nchi ikamsaidia huyo mama: ikajifunua kama mdomo nakuyamezaaa maji hayo yaliyotoka kinywani mwa hilo joka – (Ufunuo12:13-16).
Kama vile ilivyotabiriwa, katikazama zile za giza za kipindi kilecha Kikristo, Shetani alitoa “mto”wa mateso ili kufanya kanisali”chukuliwe na mkondo ule wamto.” Shetani anataka kuufutiliambali mvuto wa Kristo kwakulifutilia mbali kanisa lake, tenaanatumia kila hila ambayo akiliyake nyingi iliyojaa uovu inawezakubuni. Kimsingi Jokaanamwakilisha Shetani. Lakini kumbuka kwamba Shetani anazitumiataasisi za wanadamu katika utendaji wake kama joka ili kuwashambuliawatu wa Mungu. Alimtumia mfalme wa Kiroma Herode katika jaribio lake lakumwua mtoto Kristo mara tu alipokwisha kuzaliwa. Alifanya kazi yakekupitia kwa viongozi wa dini wenye husuda na wenye kuwania madarakawaliomnyemelea na kumsumbua Mwokozi, na hatimaye kumwua juu ya ulemsalaba. Lakini ule ulionekana kama ni ushindi mkubwa usio na kifani waKristo.
Akiwa amekasirika vibaya sana dhidi ya kushindwa kwake pale msalabani,Shetani akaielekeza ghadhabu yake dhidi ya Kanisa lile alilolianzisha Yesu.Katika miongo [miaka kumi-kumi] iliyofuata baada ya kusulibiwa kwakeKristo, maelfu waliuawa katika ule uwanja wa duara uliojengwa mjini Roma(Colosseum), maeneo tupu ya pembe mraba yaliyokuwa mijini, magerezayale ya chini ya ardhi, na katika maficho ya jangwani.
Mwanzoni wale wenye mamlaka [serikali] ya kidunia walianzisha hayomateso. Lakini baada ya kufa wale mitume badiliko lilitokea taratibu ndaniya kanisa lile. Katika kipindi kile cha karne ya pili, ya tatu, na ya nne, wengindani ya kanisa lile walianza kuzibadili kidogo zile kweli zilizokuwazimefundishwa na Kristo pamoja na mitume wake. Viongozi fulani, walioasihata wakaanza kuwatesa Wakristo wale waliosisitiza kuwa na usafi waitikadi [imani] za Agano Jipya.
Wataalam wa Biblia wanakadiria kwamba takriban milioni 50 ya walewaliokuwa waaminifu waliuawa. Katika jitihada yake ya kulizamisha nakuliangamiza kanisa, Ibilisi alitoa “mto” wa mateso ili kulifanya “lichukuliwe[lile kanisa] na mkondo ule wa mto.” “Lakini nchi ikamsaidia yulemwanamke kwa… kuumeza ule mto” wa mateso na mafundisho ya uongo.
Katika kipindi cha mateso ya Zama za Kati [1100-1500], kanisa la kwelililijiondoa kutoka katika uongozi ule ulioasi na kujificha “Nyikani, mahalialipoandaliwa na Mungu, ili wamlishe muda wa siku 1,260” (fungu la 6).Utabiri huo ulitimizwa katika kipindi cha miaka 1260 ya mateso kuanziamwaka wa 538 hadi mwaka wa 1798 B.K. (siku moja mara nyingi
husimama badala ya mwaka mmoja katika unabii wa mifano wa Biblia,angalia Ezekieli 4:6).
Katika kipindi cha karne za giza Wakristo waaminifu walioiamini Bibliawalipata kimbilio lao po pote walipoweza kupapata kwa mfano, katikamabonde ya Wawaldensia wa Italia magharibi na Ufaransa mashariki, nakatika kanisa la Kikeltiki [Waskoti Waairishi, Waweishi] la visiwa vyaUingereza.
4.Kanisa La Mungu Katika Siku Hizi Zetu
Jambo hilo linatufikisha katika siku hizi zetu – yaani, kwenye kanisa la kwelila Kristo tangu mwaka wa 1798. Kama ambavyo ingeweza kutarajiwa, yulejoka bado amewakasirikia watu wa Mungu. Vita kuu isiyoonekana kwamacho inaendelea. Kwa kweli, Shetani anafanya shambulio lake kubwakabisa dhidi ya kanisa hilo muda mfupi tu kabla ya kuja kwake Yesu.
“Ndipo yule Joka [Ibilisi] akamkasirikia sana yule mwanamke [Kanisala Mungu], akaenda zake afanye vita dhidi ya wazao wake waliosalia -wale wanaozitii amri za Mungu na kuwa na ushuhuda wa Yesu.” -(Ufunuo 12:17).
Unabii huu unalenga katika siku zetu hizi. Shetani amekasirika sana;anafanya vita dhidi ya wazao wa mwanamke waliosalia” – yaani, dhidi yawatu wa Mungu wa siku hizi. Angalia alama zao zinazowatambulisha:
(1)Waumini hao wa siku za mwisho wanao”ushuhuda wa Yesu.” Kwa uaminifuwakiyang’ang’ania mafundisho safi ya Neno laMungu, wanamshuhudia Yesu kwa njia yamaisha yao yenye nguvu nyingi ya Kikristo.
(2)Wakristo hao wa siku za mwisho ni watuwa unabii. Kuupokea ule “ushuhuda wa YesuKristo” kulimwezesha Yohana kukiandikakitabu kile cha Ufunuo (Ufunuo 1:1-3). Kundihilo la mwisho la waumini linapokea karamaile ile: yaani, ushuhuda wa moja kwa mojatoka kwa Mungu kupitia kwa mjumbe wakibinadamu. Karama yao ya unabii inalenga juu ya ufunuo wa Mungukuhusu utume wao na mwisho wao.
(3)Wakristo hao wa siku hizi za mwisho wanatambulikana pia kama “walewanaozitii Amri [kumi] za Mungu.” Hawatetei tu ukamilifu wa hizo AmriKumi, bali wanazitii pia. Upendo wa Mugu ulio mioyoni mwao unawaleteautii unaotolewa kwa moyo wa furaha (Warumi 5:5; 13:8-10).
Wakristo hao wa siku hizi za mwisho wanakifuata kielelezo cha Kristo nacha kanisa lile la kwanza kwa kuzitii amri [kumi] za Mungu. Jambo hilolinamkasirisha vibaya sana yule Joka – yaani, yule Ibilisi. Naye anapiganavita dhidi ya “wazao” wa mwanamke “waliosalia” kwa sababu wanatoaushuhuda kwamba upendo wao kwa Mungu unawafanya wafuasi wake haokuwa watii. Kama vile Kristo alivyoagiza, aliposema:
“Mkinipenda, mtazishika amri zangu” – Yohana 14:15.
Maisha ya Wakristo hao wa siku hizi za mwisho yanaonyesha kwambauwezekano upo wa kumpenda Mungu kwa mioyo yetu yote na kuwapendawenzetu kama sisi tunavyojipenda wenyewe. Kulingana na maneno yaYesu, sifa hizo za tabia, yaani, upendo kwa Mungu na upendo kwa watu,hufanya muhtasari wa Amri kumi za Mungu (Mathayo 22:35-40).
Ya nne katika hizo amri inatutaka sisi kuitunza Jumamosi, siku ya saba yajuma, kama Sabato. Kwa kuwa upendo wao kwa Yesu umezitia ndani yamioyo yao amri zote kumi [Ebr. 8:10; Kut. 20:3-17; Yak. 2:10-12], basi,Wakristo hao wa siku hizi za mwisho ni Wasabato.
Sabato ndicho kiini cha ujumbe wa mwisho wa Mungu kwa watu wakekatika kitabu cha Ufunuo, sura ya 12 na 14:6-15. Nguvu zote za mbingunizinajipanga nyuma ya Wakristo hao wa siku hizi za mwisho walioelezwakatika sura hizo. Mwokozi wao aliye hai ndiye rafiki yao daima, na Roho
Mtakatifu anafanya kazi yake “kuwafanya imara kwa nguvu katika utu waowa ndani.” Ahadi yake ni ya hakika. WATAmshinda Shetani “kwa damu yaMwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao” (Ufunuo 12:11).
Je! unataka kuwa mmoja wa Wakristo hao wa siku hizi za mwisho ambao”wanazitii amri [kumi] za Mungu” tena wa”na ushuhuda wa Yesu”? Kwa niniusikate shauri sasa hivi?