JE! MUNGU ANAO UJUMBE WA PEKEE KWA AJILIYA SIKU ZETU?
Ramon Umashankar alizaliwa katika tabaka ya juu ya Kihindu (Brahmin).Wakubwa wake kwa umri walimfundisha akiwa na umri ndogo ya kwambayeye alikuwa mungu, na ya kwamba ili kuufikia uungu wake ni lazimaafanye mazoezi ya yoga na kutafakari. Yeye kama kijana mbichi [tineja],Ramon alianza kushangaa kama kweli angempata Mungu kupitia kwasanamu zile mbali mbali zilizoabudiwa katika mahekalu ya Kihindu[Kibaniani].
Ramon akaanza kuichunguza Bibliana madai ya Kristo. Yeye alikuwaamemheshimu Yesu siku zote kwaunyenyekevu wake aliokuwa nao,lakini sasa Ramon akasikia kwambahuyo Yesu alidai kwamba alikuwandiye Mwana pekee wa Mungu.Tena aligundua kwamba Wakristowengi walionekana wanayo amaniambayo kutafakari kwa miaka mingi kulikuwa kumeshindwa kuifikia. Lakini,Ramon bado alikuwa amedhamiria kuipata kweli katika dini yake yaKibaniani.
Lakini baadaye aliiona filamu iliyoonyesha maisha yake Kristo. Kwa marayake ya kwanza alitambua kwamba Yesu alikuwa amepatikana na matesona hofu kama mwanadamu. Kabla ya hapo alikuwa amedhani kwambaYesu kwa njia fulani alikuwa ametumia uweza wake wa Uungu kuyakwepamaumivu yale yaliyotokana na kusulubiwa kwake. Lakini sasa, alishindwakueleza habari za msalaba ule. Alishangaaa na kujiuliza-uliza: Hivi ilikuwa-kuwaje huyo Yesu aliweza kuyapitia mateso makubwa kama yale – kwa ajiliya wanadamu wenye dhambi?
Ramon alipoendelea kutafakari juu ya kifo cha Kristo, alizidiwa nguvu kwakudhihrishwa kwa upendo kama ule. Aliamua kukitupilia mbali cheo chakekinachotamaniwa sana na watu wa Brahmini [tabaka la juu la Kibaniani] nakutoa maisha yake kwa Yesu, Mwokozi wake. Alipoyalinganisha mamboyote na ule upendo wa kujitoa mhanga wa Kristo, Ramon alisema hivi, “Kilakitu cho chote kingine kikasambaratika.”
Mbrahmini huyo kijana alikigundua kiini cha ile kweli ya Ukristo: yaani, YesuMwokozi wa ulimwengu.
1.Dini Ipi Inaokoa?
Yesu ndiye Njia – njia pekee – ya wokovu.
“Wokovu haupatikani katika mwingine awaye yote, kwa maana hapanajina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisikuokolewa kwalo.” – Matendo 4:12.
Biblia inafundisha wazi kwamba sisi tumepotea katika dhambi, na hivyotunakabiliwa na adhabu ya dhambi: yaani ile mauti (Warumi 6:23). Wotewametenda dhambi (Warumi 3:23), kwa hiyo wote wanakabiliwa na hiyomauti. Na Yesu ndiye yule mmoja – mmoja pekee awezaye kutuokoa sisikutoka katika laana ya dhambi.
“Kila mmoja amtazamaye Mwana na kumwamini yeye atapata uzimawa milele, nami nitamfufua siku ya mwisho” – (Yohana 6:40).
Kuna dini moja tu ya kweli:
“Bwana mmoja, IMANI MOJA, ubatizo mmoja” – (Waefeso 4:5).
2.Je! Mungu Anao Ujumbe Wa Pekee Kwa siku zetu?
Ndiyo! Ujumbe huo wa aina tatuunaonekana katika Ufunuo 14:6-16.kutangazwa kwa ujumbe huouliotolewa na malaika hao watatukunafikia kilele chake wakati ulewa kuja mara ya pili kwa Kristo(fungu la 14-16).
Ujumbe wa Malaika wa Kwanza.
“Kisha nikamwona malaikamwingine, akiruka juu ya angaakiwa na Habari Njema yamilele ya Mungu, aitangaze kwa watu waishio duniani, kwa mataifayote, makabila yote na watu wa lugha zote na rangi zote. Nayeakasema kwa sauti kubwa, “Mcheni Mungu na kumtukuza! Maana saaimefika ya kutoa hukumu yake. Mwabuduni yeye aliyeumba mbingu nanchi, bahari na chemchemi za maji” – (Ufunuo 14:6,7).
Ingawa Maandiko yanaonyesha picha ya kuvutia ya ujumbe huo wa ainatatu kwa njia ya mfano wa hao malaika watatu, watu wa Mungu ndiowajumbe hasa wautangazao kwa ulimwengu mzima. Hawahubiri injili mpya,bali “injili ya milele” kwa ulimwengu mzima- yaani, kwa kila taifa na kabilana lugha na jamaa. “Injili ya milele” ya Kristo ni ujumbe ule ule wa wokovuambao watu katika kipindi kile cha Agano la kale waliupokea ” kwa imani”(Waebrania 3:16-19; 4:2; 11:1-40); ni mafundisho yale yale aliyoyatangazaYesu mwenyewe; ni injili ile ile iliyounguruma katika karne zile zote zakipindi cha Kikristo.
Injili hiyo rahisi, iokoayo, ya Yesu Kristo ilikuwa karibu imetoweka kabisakatika Kanisa kwa zaidi ya miaka elfu moja katika kipindi cha zama za giza(Dark Ages), lakini matengenezo ya Kanisa (Reformation) yaliifufua, nawatu wa Mungu wanaihubiri ulimwenguni kote leo. Malaika wa kwanzaanatangaza ujumbe wa injili iyo hiyo, lakini inahubiri katika mwelekeo mpya-yaani, wa ulimwengu mzima – kwa ajili ya watu wanaoishi kabla tu ya kujaYesu mara ya pili.
Wale wanaoupokea ujumbe huu wanajikuta wanaitwa ku “mch[a] Mungu nakumtukuza [kuakisi tabia yake].” Wanauonyesha ulimwengu tabia ya Munguya upendo, sio tu kwa maneno yao, bali pia kwa maisha yao yenyeushuhuda wenye nguvu. Wanatoa ufunuo wa kusisimua wa kile Munguawezacho kufanya kupitia kwa watu waliojazwa na Roho wa Kristo.
Hivi ni lini utakapotangazwa huo ujumbe wamalaika hao watatu katika ulimwengu mzima?Wakati saa ya “hukumu yake [Mungu] imekuja.”Mwongozo 13 unaeleza kwamba Yesu alianzakazi ya hukumu inayotangulia kabla ya kujakwake katika mwaka ule ule, yaani, 1844, Yesualiwavutia watu ulimwenguni kote kuanzakuhubiri ujumbe huo wa Ufunuo 14.
Ujumbe huo unatuagiza sisi ku”msujudi[a] yeyealiyezifanya mbingu, [na] nchi” [Ufunuo 14:7].Mungu anatutaka sisi ku “ikumbuk[a] siku yaSabato [t]uitakase” kwa sababu “kwa siku sitaBwana alifanya mbingu na nchi” (Kutoka 20:8-11). Katika mwaka ule wa 1844 Darwinalipokuwa anaitoa nadharia yake ya evalusheni[kutokea vyenyewe tu vitu vyote], Mungu alikuwa anawaita watu wakekurudi na kumsujudia yeye kama Muumbaji wao. Wakati ule ule hasa, walewaliokuwa wakiuhubiri ujumbe huo wa malaika watatu waliigundua Sabato
ya siku ya saba ya neno la Mungu, nao wakaanza kuitunza kwakumheshimnu Muumba wa Mbingu na Nchi.
(2)Ujumbe wa malaika wa pili.
“Malaika wa pili akafuata, akasema, ‘Umeanguka! Umeanguka BabeliMkuu, uliowafanya mataifa yote kunywa mvinyo wa uasherati wakeunaowafanya kuwa vichaa.!! – ufunuo 14:8.
Malaika wa pili anaonya anasema,”Umeanguka Babeli Mkuu.” Ufunuo 17unaonyesha picha ya “Babeli” ya kiroho-yaani, Ukristo ulioasi – kamamwanamke kahaba (fungu la 5).Anasema akiwa tofauti na mwanamkesafi wa Ufunuo 12 anayeliwakilishakanisa la kweli la Kikristo. Mwanamkeanayewakilisha Babeli ni mwanamkealiyeanguka [aliyeasi] ambayealiwafanya “mataifa yote kunywa mvinyowa uasherati wake unaowafanya kuwavichaa.” Mvinyo wa mafundisho yauongo umeenea kote katika mfumopotofu wa Ukristo. Ujumbe huo wa malaika wa pili unawaita watu wa Mungukuyapinga mafundisho hayo ya uongo ya Ukristo huo ulioasi.
Babeli unawakilisha mseto wa mifumo mingi ya Ukristo ulioasi. Ni wa hatarimno kwa sababu unaipotosha picha ya Mungu na kuifanya kama vikaragosi[sanamu za kuchekesha]: yaani, unamfanya Mungu kuwa ni mlipiza kisasina mwenye madai mengi, unamfanya Mungu kama babu yetu mwenyeupendo ambaye ni mwema mno kuweza kumsumbua mtu awaye yote juuya dhambi zake. Kanisa lenye afya litatoa picha yenye uwiano mzuri wa sifazote za Mungu, kisha litaonyesha jinsi haki na rehema yakeinavyofungamana na kweli isemayo kwamba Mungu ni upendo.
Mungu anawaita watu wake anasema “tokeni” Babeli (Ufunuo 18:4),anataka wayakatae mafundisho yale yasiyotoka katika Biblia, kishawayafuate mafundisho ya Kristo.
(3)Ujumbe wa malaika wa tatu
“Na malaika wa tatu aliwafuata hao wawili akisema kwa sauti kubwa,Yeyote anayemwabudu yule mnyama na sanamu yake na kukubalikutiwa alama yake juu ya paji la uso wake au juu ya mkono wake, yeyemwenyewe atakunywa divai ya ghadhabu ya Mungu ambayoimemininwa katika kikombe cha ghadhabu yake bila kuchanganywana maji. Mtu huyo atateseka ndani ya moto na kiberiti mbele yamalaika watakatifu na mbele ya Mwanakondoo. Moshi wa motounaowatesa hupanda juu milele na milele. Watu hao waliomwabuduhuyo mnyama na sanamu yake na kutiwa alama ya jina lake,hawatakuwa na nafuu yoyote usiku na mchana. Hivyo lazimawatakatifu, yaani watu wanaotii amri ya Mungu na kumwamini Yesu,wawe na uvumilivu” – (Ufunuo 14:9-12).
Ujumbe wa malaika wa tatu unaugawa ulimwengu wote katika makundimawili. Upande mmoja wanasimama Wakristo waasi [ yaani, wasiofuatamafundisho ya Biblia] ambao hu “msujudu huyo mnyama na sanamu yake,na kuipokea alama yake katika kipaji cha uso wake au katika mkono wake.”Upande ule mwingine wanasimama wale wanaoikataa mamlaka yamnyama, yaani. Wale “watakatifu wanaozitii amri [kumi] za Mungu nakuendelea kuwa waaminifu kwa Yesu.”
Zingatia tofauti iliyopo kati ya makundi hayo mawili yanayopingana. Walewanaoipokea alama ya mnyama ni waabudu wanaoyalegeza masharti yaimani ambao wanafuata mawazo yaliyotungwa na wanadamu yaonekanayokama yanafaa pamoja na kuzifuata desturi zao. “Watakatifu wanatabia hizizinazowatambulisha: “uvumilivu” utii kwa “Amri za Mungu” kisha”wanaendelea kuwa waaminifu kwa Yesu.”
Baada ya ujumbe huo wa aina tatu kutangazwa ulimwenguni kote, Yesuatakuja ku “vun[a] wale waliookolewa:
“Kisha, nikatazama, na kumbepalikuwapo wingu jeupe hapo.Na juu ya wingu hilo alikuwakoaliye kama Mwana wa Mtu.Alikuwa amevaa taji ya dhahabukichwani, na kushika mundumkononi mwake. Kisha malaikamwingine akatoka hekaluni, nakwa sauti kubwa akamwambiayule aliyekuwa amekaa juu yawingu, “Tafadhali, tumia munduwako ukavune mavuno, maana wakati wa mavuno umefika; mavunoya dunia yameivaa”. Basi, yule aliyekuwa amekaa juu ya winguakautupa mundu wake duniani, na mavuno ya dunia yakavunwa” -(Ufunuo 14:14-16).
3.Kanisa La Kristo La Siku Za Mwisho
Je! umevutiwa sana na Mkristo mwenye nguvu, aliye imara, na kushangaakuiona bidii aliyo nayo katika kumwabudu Mungu, uvumilivu wake, na imaniyake, na kutamani sana kuwa na uzoefu wa kiroho unaofanana na huo?Mungu alitoa ujumbe wake wa pekee kwa ajili ya siku zetu katika Ufunuo 14kwa sababu unaweza kuleta uzoefu wa maisha kama huo.
Kama tulivyojadili katika Mwongozo 25, Ufunuo 14:17 unawatambulishaWakristo wa siku hizi za mwisho kuwa ni “wanaozitii amri [kumi] za Munguna kuwa na ushuhuda wa Yesu.” Ufunuo 14:12 unaeleza habari za kundihilo kuwa ni la “watakatifu kwa Yesu.”
Hebu na tufanye muhtasari wa sifa za tabia ya Wakristo wa siku za mwisho.
1.Wana”kuwa na ushuhuda wa Yesu.” Hata Shetani anapoionyesha hasirayake dhidi yao, wao “wanaendelea kuwa waaminifu kwa Yesu.” Imani yaohaitokani na nafsi yao wenyewe ni kipawa toka kwa Mungu (Waefeso 2:8).Kanisa la Mungu la siku hizi za mwisho linamwona Kristo katika tabia yakehalisi na kwa neema kwa njia ya imani wanakuwa minara hai yaukumbusho inayoshuhudia uweza wa Kristo anayekaa ndani yao.
- Wanayo “imaniā¦. Ya Yesu” ( Ufunuo 14:12, KJV). Imani aliyokuwa nayoYesu, yaani, imani aliyoifundisha, imani aliyoiweka katika maisha yake,sasa inaijaza mioyo yao. Hawanayo tu kweli, wanai”tunza” kweli – yaani,wanaifuata. Kwao dini ni maisha, imani yao inafungamana na matendo yao,tena imani hiyo inafungamana na utii wao. Katika maisha yao ya njewanaionyesha “imani ya Yesu.” Wamekwisha kugundua ya kwambamafundisho makuu ya Biblia, yakitumiwa katika maisha yao ya kila siku,yanawapa maisha ya Kikristo yenye nguvu. Wamegundua kwamba kwelihizo kuu za Biblia zinaamsha upendo na kicho chao kwa Kristo, mamboambayo hukidhi haja na shauku zote za moyo wa kibinadamu.
3.”Wanazitii amri [kumi] zaMungu” – Amri zile Kumi, yaani,sheria ya maadili ya Mungu. Juuya mambo hayo yote menginewanataka kutii kila alipendaloMungu, kutii kila amri yake.Wanauonyesha upendo wao kwaMungu na upendo wao kwa watuwengine kwa kuzifuata amri zote[kumi] za Mungu, pamoja na ileya nne inayotuamurukumwabudu Muumbaji wetu kwakuiheshimu Jumamosi, yaani,Sabato ya siku ya saba.
4.Wanautangaza ujumbe wa “injili ya milele” ulimwenguni kote (Ufunuo14:6). Injili hutangaza kwamba Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, halafualifufuka kutoka kaburini ili sisi tupate kuwa na kanisa la Kristo la siku hiziza mwisho limekuwa likiwaita watu kila mahali kutoka katika machafuko yakidini na kujenga uhusiano pamoja wa ile kweli ya Biblia peke yake.
5.Wanasukumwa na hisia ya kuharakisha mambo kwa sababu “saa yamavuno imekuja, kwa kuwa mavuno ya nchi yamekomaa” (Ufunuo 14:15),na mamilioni bado hawajamwona Kristo.
6.Wanajitoa kabisa kutekeleza utume waliopewa na Mungu. Kwa sababu”Babeli Mkuu” umeanguka, wao wanaendelea kuwasihi wale wanaoishikatika machafuko hayo ya kidini, wakiwaambia “Tokeni kwake, enyi watuwangu” (Ufunuo 18:4). Wanatamani kuwaeleza wengine juu ya uhusianowa ajabu walio nao pamoja na Kristo, na furaha waliyo nayo wao kwa wao.
Yote hayo na zaidi yanaiunganisha mioyo ya mamilioni ya Wakristo wa sikuhizi za mwisho walioitwa na ujumbe huo wa malaika hao watatu ili watoke.Maisha yao yenye furaha yanawafanya kujiunga na mtume Yohanakutangaza kote mwaliko huu:
“Tulichokiona na kukisikia ndicho tunachowatangazieni nyinyi pia, ilinanyi mpate kujiunga nasi katika umoja tulio nao na Baba na MwanaeYesu Kristo. Tunawaandikia nyinyi mambo haya kusudi furaha yetuikamilike” – (1 Yohana 1:3,4).
Kwa njia ya Roho wake na kwa njia ya kanisa lake, Yesu anakualika wewepia ili uje kwake na kusalimisha kila kitu kwake yeye:
“Roho na bibi-arusi [kanisa] wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme,’Njoo!’ ye yote mwenye kiu na aje; na ye yote atakaye, na atwae zawadihii inayotolewa bure ya maji ya uzima.”. – Ufunuo 22:17.
4.Mavuno Ya Aina Mbili
Ujumbe wa malaika hao watatu unafikia mwisho wake Yesu anaporudiduniani kuwavuna waliookolewa wa vizazi vyote (Ufunuo 14:14-16). Yesu
anawakusanya wote waliookolewa na kuwachukua kwenda nao kulekwenye “makao mengi” mbinguni (Yohana 14:1-3, KJV). Anafutilia mbalidhambi, magonjwa, huzuni na mauti. Watakatifu wanaanza kuishi maishamapya mazuri sana pamoja naye milele hata milele (Ufunuo 21:1-4).
Yesu atawa”vuna piawaovu wakati wa kujakwake”.
“Kisha, malaikamwingine akatoka katikahekalu mbinguni akiwana mundu wenye makali.Kisha malaika mwinginemsimamizi wa moto,akatoka madhabahuni,akamwambia kwa sautikubwa yule malaikamwenye mundu wenyemakali, “Nawe tia huo mundu wako mkali ukakate vichala vyamizabibu ya dunia, maana zabibu zake zimeiva!” Basi, malaika huyoakautupa mundu wake duniani, akakata zabibu za dunia, akazitiandani ya chombo kikubwa cha kukamulia zabibu chombo chaghadhabu ya Mungu. Zabibu zikakamuliwa ndani ya hilo shinikizolililoko nje ya maji, na damu ikatoka katika shinikizo hilo mtiririkowenye kina kufikia hatamu za farasi na urefu upatao kilometa mia tatu”-(Ufunuo 14:17-20).
Huo utakuwa ni wakati wa kuhuzunisha sana wa maangamizi ya mileletukio la kuhuzunisha mno kwake Kristo, kwa sababu atalazimikakuwaangamiza wale wanaokataa kuokolewa. Yesu “huvumilia kwa ajiliyenu, hapendi mtu ye yote aangamie, bali kila mmoja aifikilie toba” (2 Petro3:9).
Yesu anapokuja kuvuna mavuno ya nchi, je! wewe utakuwa katika mavunoyapi? Je! utasimama miongoni mwa nafaka iliyokomaa pamoja nawaliokombolewa wa vizazi vyote (Ufunuo 14:13-16)? Au utakuwa mingonimwa zile zabibu zilizoiva sana za ghadhabu pamoja na wale waliopotea?(mafungu 17-20).
Jambo hilo limewekwa wazi.Upande mmoja, Yesu anasimamamikono yake iliyotobolewa kwamisumari ikiwa imenyoshwa kwako,akikusihi wewe ili upate kusimamapamoja na “watakatifu wanaozitiiamri [kumi] za Mungu na kuwa naimani ya Yesu” (fungu la 12).Upande ule mwingine ni sauti zawanadamu tu, zinazokusihi sanazikikuambia kwamba utii wako kwamafundisho yote ya Biblia na kwazile amri zote [kumi] za Mungu hauna maana.
Siku moja kundi lililokuwa katika ukumbi wa hukumu wa Pilato lilikabiliwa najambo ambalo linafanana ajabu na hilo. Upande mmoja alikuwako Yesu,mwenye hali ya uungu-ubinadamu, yaani, Mungu-mwanadamu. Upande ulemwingine alikuwako Baraba, mtu asiye na uwezo wo wote, yaani,asiyeweza kujisaidia mwenyewe, wala waliokuwa katika kundi lile ambaowalilishuhudia tukio la kuhuzunisha sana. Lakini, basi, yale maneno yaPilato yenye amri yalipovuma katika kundi la watu wenye tabia mbalimbali,yakisema, “Ni yupi kati ya hawa wawili mnayetaka niwafungulie?” sautinyingi za watu wale zikaunguruma kwa hasira, “Baraba!”
“Basi,” akauliza Pilato nimtendeje Yesu aitwaye Kristo?”
Kwa sauti moja lile kundi likapiga makelele, “Na asulubiwe!”
Na hivyo ndivyo Yesu, asiye na hatia yo yote, alivyosulibiwa; na Baraba,mwenye hatia, akaenda zake akiwa huru. (Angalia Mathayo 27:20-26).
Je! wewe unamchagua nani leo hii, Baraba au Yesu? Je, unachaguakufuata mawazo na mafundisho yaliyotungwa na wanadamu ambayoyanagongana na amri [kumi] za Mungu, tena yanagongana na injili yamilele ya Yesu? Au wewe unataka ku”zitii amri [kumi] za Mungu nakuendelea kuwa [m]waminifu kwa Yesu?” kumbuka, Yesu ndiye anayeahidikumtuma Roho wake Mtakatifu kutatua matatizo yako yote, kuiponya kilahuzuni kubwa uliyo nayo moyoni mwako, na kuitosheleza kila shauku uliyonayo.