MTU AKIFA, KUNA NINI BAADAYE?
Tunajikunyata mtoto mdogo anapouliza kwanza swali hili, “kufa maana yakenini? Tunaywea kuzungumza au hata kufikiri juu ya mtu fulani tumpendayeanapokaribia kufa. Mauti ni adui wa watu wote kila mahali.
Je! majibu ni yapi kwa maswali magumu yahusuyo kifo? Je! kuna maishabaada ya kufa? Je! tutawaona tena wapendwa wetu waliokufa?
1.Kukikabili Kifo Bila Hofu
Sisi sote kwa wakati fulani, labda baadaya kufa rafiki yetu au mpendwa wetu,tumejisikia kana kwamba tumbo liko tupu,yaani, kuwa na hisia ile ya upwekeinayopita ndani yetu tunapoangalia kwaharaka kuona mwisho wa uhai wa mtu.
Katika jambo hili la maana sana, lililojaahisia nyingi, ni wapi basi, tunakowezakujifunza habari za kile kinachotokeatunapokufa? Kwa bahati nzuri, sehemuya utume wa Kristo hapa duniani ilikuwani “kuwaweka huru wale ambao katikamaisha yao yote walikuwa katika hali ya utumwa kwa hofu ya mauti”(Waebrania 2:15). Na katika Biblia, Yesu anatoa ujumbe wenye faraja, kishaanajibu maswali yetu yote juu ya mauti na yale maisha ya baadaye kwa njiainayoeleweka wazi.
2.Jinsi Mungu Alivyotuumba
Kuelewa kutoka katika Biblia ukweli halisi juu ya kifo, hebu na tuanzemwanzo na kuona jinsi Mungu alivyotuumba.
“BWANA Mungu akamfanya mtu (Adamu, Kiebrania) kwa MAVUMBI YAARDHI (adamah, Kiebrania), akampulizia puani PUMZI YA UHAI, namtu yule akawa NAFSI HAI [roho, Kiebrania].” – (Mwanzo 2:7).
Wakati ule wa uumbaji, Mungu alimfinyanga Adamukutoka katika “mavumbi ya ardhi.” Alikuwa na ubongokichwani mwake ulio tayari kufikiri; damu katikamishipa yake iliyo tayari kuzunguka mwilini mwake.Ndipo Mungu alipompulizia puani “pumzi ya uhai,” naAdamu akawa “nafsi hai” [Kiebrania, “roho hai”].Zingatia kwa makini, Biblia haisemi Adamu alipokearoho; bali inasema tu kwamba “mtu akawa roho hai.”Mungu alipompulizia Adamu pumzi puani mwake,uhai ukaanza kuingia ndani yake kutoka kwa Mungu.Mwungano huo wa mwili na “pumzi ya uhai”ulimfanya Adamu kuwa “nafsi hai,” tunaweza kundikamlinganyo (equation) wa kibinadamu kama hivi:
“Mavumbi ya Ardhi” + “Pumzi ya Uhai” = ” Roho Hai”
Mwili Usio na Uhai + Pumzi toka kwa Mungu = NafsiHai.
Kila mmoja wetu anao mwili na akili inayofikiri. Kwa kadiri sisitunavyoendelea kuvuta pumzi, tutaendelea kuwa nafsi hai, yaani, roho hai.
3.Kunatokea Nini Mtu Akifa?
Mtu anapokufa kinyume cha hatua zile za uumbaji zilizoelezwa katikaMwanzo 2:7 hutokea
“Nayo MAVUMBI huirudia ardhi yalikotoka, nayoROHO [PUMZI YA UHAI] humrudia Mungu aliyeitoa.” – (Mhubiri 12:7).
Mara nyingi Biblia hutumia maneno ya Kiebrania yamaanishayo “pumzi”(breath) na “roho” (spirit) kwa kubadilishana. Watu wanapokufa, mwili waounageuka na kuwa “mavumbi” na “roho (“pumzi ya uhai”) humrudia Mungualiyeitoa. Lakini, je! kunatokea nini kwa ile roho hai (living soul)?
“Kama mimi niishivyo, atangaza Bwana Mungu,…. Kila ROHO ILIYOHAI (LIVING SOUL) ni mali yangu;… ROHO YULE ATENDAYE DHAMBINDIYE ATAKAYEKUFA.” – Ezekieli 18:3-4.
Roho inakufa! Kwa sasa haina uwezo wa kuishi milele – inawezakuangamizwa. Mlinganyo ule ulioupata kutokana na Mwanzo 2:7, Mungualipotuumba sisi, unajipindua wakati ule wa kufa.
“Mavumbi ya Ardhi” – “Pumzi ya Uhai” = “Roho Iliyokufa”
“Mwili usio na uhai – Pumzi toka kwa Mungu = Nafsi Iliyokufa.
Mauti ni kukoma kabisa kwa uhai. Mwili unavunjika-vunjika na kugeukakuwa mavumbi, na ile pumzi, au roho, humrudia Mungu. Sisi ni roho haitunapoendelea kuishi, lakini tunapokufa tunakuwa maiti tu, yaani, rohoiliyokufa, nafsi iliyokufa. Kwa hiyo wafu hawana fahamu zo zote. Munguanapoiondoa kwetu pumzi yake ya uhai aliyotupa, roho yetu hufa. Lakinikama tutakavyoona baadaye katika somo hili, tukiwa na Kristo tumaini liko.
4.Mfu, Anajua Kiasi Gani?
Baada ya kufa ubongo unaharibika; hauwezi kujua, wala kukumbuka kitucho chote. Hisia zote za moyo za kibinadamu hukoma kabisa mtuanapokufa.
“Upendo wao, chuki yao na wivu wao, vimetoweka siku nyingi sana…”-(Mhubiri 9:6).
Wafu hawana fahamu zo zote, hivyo hawana habari na kitu cho chotekinachotokea hapa. Hawana mawasiliano yo yote na wale walio hai:
“Kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa, lakini WAFUHAWAJUI CHO CHOTE.” – (Mhubiri 9:5).
Kifo ni kama usingizi usio na ndoto-kwa kweli, Biblia inakiita kifokuwa ni “usingizi” mara 54. Yesualifundisha kwamba kifo ni kamausingizi., alisema hivi kwawanafunzi wake:
Yesu alipomaliza kusema manenohayo, akawaambia,
“Rafiki yetuLazaro amelala, lakini miminitakwenda kumwamsha”.Wanafunzi wake wakamwaabia, “Bwana, ikiwa amelala, basi atapona”.Wao walidhani kwamba alikuwa amesema juu ya kulala usingizi,kumbe alikuwa amesema juu ya kifo cha Lazaro. Basi, Yesuakawaambia waziwazi, Lazaro amekufa;- (Yohana 11:11-14).
Lazaro alikuwa amekufa yapata siku nne kabla Yesu hajafika pale. LakiniYesu alipokwenda kwenye kaburi lake, alithibitisha kwamba kwa Mungu nirahisi kuwafufua wafu kama ilivyo rahisi kwetu kumwamsha mwenzetualiyelala usingizi.
Ni faraja kubwa kwetu kujua kwamba wapendwa wetu waliokufa wame “lalausingizi,” yaani, wanapumzika salama salimini ndani ya Yesu. Shimo lilerefu la mauti, ambalo sisi wenyewe tutalipitia siku moja, ni kama kulalausingizi mtulivu wa amani.
5.Je! Mungu Anawasahau Wanaolala Usingizi Wa Mauti?
Usingizi huo wa mauti sio mwisho wa kisa hiki. Pale kaburini, Yesualimwambia Martha, dada yake Lazaro, maneno haya:
“MIMI NDIMI HUOUFUFUO, na uzima. YEYE ANIAMINIYE MIMI ATAKUWA ANAISHI, HATAKAMA ATAKUFA.” – (Yohana 11:25).
Wale wanaokufa “katika Kristo” wanalala usingizi makaburini mwao lakiniwao bado wanalo tumaini zuri la kupata maisha yale ya baadaye. Yeyeanayeuhesabu kila unywele juu ya vichwa vyetu na kutushika katika kiganjacha mkono wake hatatusahau sisi. Tunaweza kufa na kurudi mavumbini,lakini kumbukumbu ya utu wetu bado i wazi katika mawazo ya Mungu. NaYesu atakapokuja, atawaamsha wenye haki waliokufa kutoka katika usingiziwao, kama vile alivyofanya kwa Lazaro.
“Ndugu, twataka mjue ukweli kuhusu waleambao wamekwisha fariki dunia, ili msipatwena huzuni kama watu wengine wasio namatumaini. Maana patatolewa amri, sauti yamalaika mkuu, sauti ya tarumbeta ya Mungu,naye Bwana mwenyewe atashuka kutokambinguni. Ndipo wale waliokufa wakiwawanamwamini Kristo watafufuliwa kwanza.Kisha sisi tulio hai wakati huo tutakusanywapamoja nao katika mawingu kumlaki Bwanahewani. Na hivyo tutakuwa daima pamoja naBwana. Basi, farijianeni kwa maneno haya” – (1Wathesalonike 4:13, 16-18).
Siku ile ya ufufuo lile shimo refu la mautilitaonekana kana kwamba ni pumziko letu la muda mfupi sana. Wafuhawana habari na muda unaopita. Wale waliompokea Kristo kama Mwokoziwao, wataamshwa kutoka usingizini kwa sauti yake ya ajabu ikishuka kujahapa duniani.
Tumaini hilo la ufufuo linaye mwenzake; yaani, tumaini la kuwa na makaoyale ya mbinguni ambako Mungu “atafuta kila chozi katika macho yao.”Mauti haitakuwapo tena, wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu”(Ufunuo 21:4). Wale wanaompenda Mungu hawana haja ya kuogopa mauti.Ng’ambo yake kuna umilele wa maisha yale matimilifu pamoja na Mungu.Yesu anazo “funguo za mauti” (Ufunuo 1:18). Bila Kristo, mauti ingekuwa ninjia ya moja kwa moja inayoishia katika hali ya usahaulifu kabisa, lakinitukiwa pamoja na Kristo, basi, kuna tumaini linalong’aa, lenye furaha.
6.Je! Tuna Miili Isiyokufa Sasa?
Mungu alipomwumba Adamu naHawa, waliumbwa wakiwa na miiliinayokufa, yaani, walikabiliwa nakifo. Laiti kama wangaliendeleakuwa watii kwa mapenzi yakeMungu, wasingeweza kufakamwe. Lakini
walipotenda dhambi, walipotezahaki yao ya uzima. Kwa uasi waoule wakakabiliwa na mauti.Dhambi yao iliwaambukiza wanadamu wote, na kwa kuwa wote wamefanyadhambi, basi, sisi sote tuna miili inayokufa, yaani, tunakabiliwa na mauti(Warumi 5:12). Wala hakuna dokezo hata moja katika Biblia lisemalokwamba roho ya mwanadamu inaweza kuishi peke yake kama kitu kilichona fahamu.
Kamwe Biblia haijaeleza hata mara moja kwamba roho kama ilivyo sasa inahali hiyo ya kutokufa kamwe – yaani, kwamba haiwezi kufa. Maneno yaKiebrania na Kigiriki ya neno hili “roho” (soul), na “roho” (spirit), na “pumzi”(breath) hutokea mara 1,700 katika Biblia. Lakini hakuna hata mara mojaambapo roho ya binadamu (soul), roho (spirit), au pumzi (breath) inatajwakuwa haiwezi kufa. Kwa wakati huu wa sasa ni Mungu peke yake ambayeana hali hiyo ya kutokufa kamwe.
“Mungu…. PEKE YAKE HAPATIKANI NA MAUTI.” – I Timotheo 6:15,16.
Maandiko yanaeleza wazi kwamba katika maisha haya wanadamu wanahali ya kufa: yaani, wanakabiliwa na kifo. Lakini Yesu ajapo, mwili wetuutafanyiwa mabadiliko makubwa.
“Sikilizeni, nawaambieni siri sisi hatutakufa sote, ila sote tutageuzwa,wakati wa mbiu ya mwisho, kwa nukta moja, kufumba na kufumbua.Maana tarumbeta ya mwisho itakapolia, wafu watafufuliwa katika haliya kutokuweza kufa tena, na sisi tutageuzwa. Maana ni lazima kilakuharibikacho kijivalie hali ya kutoharibika, mwili uwezao kufa ujivaliehali ya kutokufa”- (1Wakorintho 15:51-53).
Sisi, kama wanadamu, hatuna miili isiyokufa sasa. Lakini ahadi inayotolewakwa Mkristo ni kwamba sisi tutakuwa na miili isiyoweza kufa kamwe wakatiYesu atakapokuja tena kwa mara yake ya pili. Uhakika wa ahadi ya uzimawa milele ulionyeshwa wazi Yesu alipolipasua kaburi lake na:
“Lakini imefunuliwa kwetu sasa kwa kuja kwake Mwokozi wetu, YesuKristo. Yeye amekomesha nguvu za kifo, na kwa njia ya Habari Njemaakadhihirisha uhai usio na kifo” – 2Timotheo 1:10.
Mtazamo wa Mungu kuhusu mwisho wa wanadamu uko wazi: yaani, mautiya milele kwa wale wanaomkataa Kristo na kuzing’ang’ania dhambi zao, auhali ya kutokufa kamwe kama zawadi kwa wale waliompokea Yesu kamaBwana na Mwokozi wao wakati ule atakapokuja.
7.Kukikabili Kifo Cha Mpendwa Wetu
Hofu zile ambazo kwa kawaida sisitunapambana nazo tunapokabiliana nakifo zinakuwa kali sana wakati uleanapokufa mpendwa wetu. Upwekepamoja na ile hisia ya kupotelewa,mambo hayo yanaweza kutulemea sana.Suluhisho pekee kwa utungu huouliosababishwa na kutengana nampendwa wetu ni ile faraja tu atupayoKristo. Kumbuka kwamba huyo mpendwawako amelala usingizi, na wapendwawako wanaopumzika katika Kristowatafufuliwa katika ule “ufufuo wa uzimaYesu atakapokuja.”
Mungu anapanga maajabu yake ya kuwaunganisha tena walewaliotengana. Watoto wadogo watarejeshwa kwa wazazi wao waliojaafuraha kubwa. Waume na wake zao watakumbatiana. Utengano wa kikatiliuliotokea katika maisha haya utakwisha. “Mauti imemezwa kwa ushindi”- (1Wakorintho 15:54).
Wengine wanajisikia vibaya sana kutengwa na mpendwa wao kiasi kwambawanajaribu kufanya mawasiliano na wapendwa wao waliokufa kupitia kwamjumbe wa mizimu (spiritualist medium) au kwa mtu yule anayeunganishamawasiliano kama hayo wa Kizazi Kipya (New Age Channeler). LakiniBiblia kwa njia ya pekee inatuonya sisi dhidi ya kujaribu kupunguzamaumivu yetu yanayotokana na kufiwa kwa njia hiyo:
“Baadhi watawaambieni “Nendeni mkatake shauri kwa mizimu namizuka iliayo kama ndege; kwani ni kawaida watu kutaka shauri kwamiungu yao; na kutaka shauri kwa wafu kwa ajili ya walio hai” – (Isaya8:19).
Ndiyo, Hivi kwa nini? Biblia inaeleza waziwazi kwamba wafu hawanafahamu yo yote. Suluhisho la kweli kwa huo uchungu uliosababishwa nakutengwa na mpendwa wetu ni ile faraja ambayo ni Kristo tu awezayekutupa. Kutumia muda wetu kuwasiliana na Kristo ni njia bora kabisa kiafyaya kukua kupitia katika hatua hizo za kuhuzunisha.
Kumbuka siku zote kwamba, kule kuzipata fahamu tena kwa wale walalaokatika Kristo kutawajia wakati ule zitakapopigwa kelele za kuja mara ya pilikwa Kristo ambazo zitawaamsha wafu!
8.Kukikabili Kifo Bila Hofu
Kifo kinatunyang’anya sisi karibu kila kitu. Lakini kitu kimoja ambachohakiwezi kutuondolea ni Kristo, na Kristo anaweza kukirudisha kila kitumahali pake tena. Mauti haitatawala daima katika dunia hii. Ibilisi, waovu,mauti na kaburi vitaangamizwa kabisa katika lile “ziwa la moto” ambalo ni”mauti ya pili” (Ufunuo 20:14).
1.Hapa yapo mapendekezo manne rahisi juu ya kukikabili hicho kifo bilahofu: Uishi maisha ya kuwa na matumaini kwa kumtegemea Kristo, ndipoutakuwa tayari kufa dakika yo yote.
2.Kwa uweza wa Roho Mtakatifu, uwe mtiifu kwa amri zake Kristo, naweutakuwa umejiandaa kwa yale maisha ya pili, ambayo ukiwa nayohutaweza kufa kamwe.
3.Ifikirie mauti kama usingizi wa muda mfupi ambao kutoka katika huosauti ya Yesu itakuamsha atakapokuja mara ya pili.
4.Itunze ile ahadi atupayo Yesu ya kutupa sisi makao yetu kule mbingunikuishi pamoja naye milele hata milele.
Kweli ya Biblia humweka mtu huru mbali na ile hofu ya mauti kwa sababuinamfunua Yesu, ambaye hata mauti haikuweza kumshinda. Yesuanapoingia katika maisha yetu, anaigharikisha mioyo yetu na amani:
“Amani nawaachieni; amani yangu nawapa… Msifadhaike mioyonimwenu , wala msiwe na woga.” – (Yohana 14:27).
Yesu pia anafanya uwezekano uwepo kwetu wa kukabiliana na msibaunaotokana na kumpoteza mpendwa wetu. Yesu alitembea katika lile”bonde la uvuli wa mauti;” anaujua usiku mnene tunaoupitia.
“Basi, kwa vile watoto hao, kama awaitavyo, ni watu wenye mwili nadamu, Yesu mwenyewe akawa kama wao na kushiriki ubinadamu wao.Alifanya hivyo ili, kwa njia ya kifo chake, amwangamize Ibilisi ambayeana mamlaka juu ya kifo, na hivyo awaokoe wale waliokuwa watumwamaisha yao yote kwa sababu ya hofu yao ya kifo” – (Waebrania2:14,15).
Dk. James Simpson, tabibu mkuualiyetengeneza ile dawa ya nusu kaputi [yausingizi wakati wa upasuaji], alipatikana nahasara ya kutisha mtoto wake mkubwa kulikowote alipokufa. Alihuzunika vibaya sana kamamzazi mwingine ye yote awezavyo kufanya.Lakini baadaye akaiona njia iliyomleteamatumaini. Juu ya kaburi la mtoto wake yulempendwa aliweka jiwe la kuonyesha alama najuu yake aliandika kwa kukata maneno hayaambayo Yesu alisema kuhusu ufufuo wake:”Na tazama, mimi ni hai.”
Hayo ndiyo yote. Msiba wa mtu mmoja wakati mwingine unawezakuonekana kana kwamba unaifutilia mbali ile mbingu; hata hivyo, Yesu yuhai! Mioyo yetu huenda ikawa ina huzuni nyingi sana; hata hivyo, Yesu yuhai!
Ndani ya Kristo tunalo tumaini la kuishi baada ya kifo chetu. Yeye ndiye”huo ufufuo, na uzima” (Yohana 11:25), naye anatoa ahadi hii kwetu, “kwakuwa mimi ni hai ninyi pia mtakuwa hai” (Yohana 14:19). Kristo ndiyetumaini letu la pekee la kuwa hai kwetu baada ya kifo chetu. Na Kristoatakapokuja tena atatupa sisi uzima wa milele. Kamwe hatutaishi tena chiniya uvuli wa mauti, maana tunao uzima wa milele. Je! wewe umeligunduatumaini hili kuu ambalo tunaweza kulihifadhi moyoni mwetu katika zilenyakati zetu za giza nene kabisa? Kama wewe hujapata kumpokea Yesukama Bwana na Mwokozi wako, je! utafanya hivyo sasa?