JE! WENGI WANAWEZA KUKOSEA?
Katika Mwongozo 16 tuligundua kwamba kulionja pumziko la Sabato ni tibamuhimu kwa maisha ya siku hizi yaliyojaa msongo mwingi. Kwa kuwaMungu anaelewa kila haja tuliyonayo , aliiweka kila siku ya saba kwa ajili yapumziko letu la kimwili na burudiko letu la kiroho. Baada ya kuiumba duniayetu kwa siku sita, yeye “akapumzika” katika siku ile ya saba, “akaibariki”na “kuifanya takatifu” (mwanzo 2:1-3).
Mungu alipowapa watu wake Amri kumi,yaani, wana wa Israeli, aliiweka amri yakuitunza Sabato ya siku ya saba katikatiya sheria yake (Amri kumi) (Kutoka20:8-11). Kulingana na amri hiyo,Sabato ni ukumbusho wa uweza waMungu wa Uumbaji, ni siku ya kutulia nakutafakari juu ya uzuri na maajabu yakazi zake alizoziumba, ni siku yakustarehe na kumkaribisha sanaMuumbaji wetu, siku ya kuchunguza kwa kina zaidi uhusiano wetu na yeye.
Katika kipindi kile cha maisha ya kibinadamu ya Yesu aliyoishi hapaduniani, yeye pia aliitunza Sabato (Luka 4:16) na kuiidhinisha kama sikuinayowaletea Wakristo manufaa (Marko 2:27,28.) Mafungu kadhaa katikakitabu cha Matendo yanaonyesha wazi kwamba wanafunzi wake Kristowaliabudu katika siku ya Sabato baada ya ufufuo wake (Matendo 13:14,16:13, 17:2, 18: 1-4, 11).
1.Suala Lenye Utata
Hiyo inatufikisha sisi kwenye somo ambalo wengi huliona kuwa lina utatakwao. Kwa kipindi fulani ulimwengu wa Kikristo umekuwa ukizitunza sikumbili tofauti. Kwa upande mmoja, Wakristo wengi sana kwa unyofu wamoyo wanaitunza Jumapili, siku ya kwanza ya juma, ambayo waowanaamini kwamba ndiyo ukumbusho wa ufufuo wake Kristo. Kwa upandeule mwingine, kundi kubwa la Wakristo, nao vilevile wakiwa ni wanyofu wamoyo, wanaamini kwamba Biblia inaipa heshima siku ya saba peke yakekama ndiyo Sabato na ya kwamba hakuna mahali popote inapothibitishautakatifu wa Jumapili.
Je! inaleta tofauti yeyote juu ya siku gani tunayoitunza kama Sabato? Sisikama watu walio wanyoofu wa moyo na wenye ari tunaotaka kuijua kweli, nilazima tujiulize wenyewe swali hili. “Je! Ni jambo gani ambalo ni maana kwaYesu? Hivi Yesu anataka mimi nifanye nini?
Katika kufikiria uamuzi wa jambo hilo, mambo kadhaa ya maana hayanabudi kuwekwa wazi, je ni nani aliyeibadili Sabato kutoka Jumamosi siku yasaba ya juma, kwenda Jumapili siku ya kwanzia ya juma? Je! Hivi Bibliainatoa idhini kwa badiliko kama hilo?Kama jibu ni ndiyo, Je, Mungu, Kristo,au labda wale mitume ndio waliofanya badiliko hilo?
Tutaendelea mbele kwa kuangalia uwezekano wo wote uliopo
2.Je! Ni Mungu Aliyebadili Siku?
Je! Kuna tamko lolote toka kwa Mungu ambalo linaibadilisha Sabato kutokasiku ya saba kwenda siku ya kwanza ya juma?
Wakristo wengi sana wanazikubali Amrikumi kama mwongozo halali ambao kwahuo sisi tunpaswa kuishi. Huu ni ujumbe wapekee ambao Mungu mwenyewe amepatakuandika kwa ajili ya wanadamu. Ni zamuhimu sana, aliziandika juu ya mbao zamawe kwa kidole chake mwenyewe(Kutoka 31:18).
Katika ile amri ya nne Mungu anatuagizasisi anasema:
“Ikumbeke siku ya Sabato uitakase. Sikusita fanya kazi na kutenda mambo yakoyote, lakini SIKU YA SABA NI SABATOYA BWANA, MUNGU WAKO. Siku hiyousifanye kazi yoyote, … maana kwa sikusiku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari na vyotevilivyomo, lakini AKAPUMZKA siku ya saba. Kwa hiyo BWANAAKAIBARIKI siku ya Sabato AKAITAKASA” – Kutoka 20:8-11.
Mungu alipowapa watu wake zile Amri kumi, pia alieleza wazi kwambamaagizo yale yaliyotoka kinywani mwake asiwepo mwanadamu yeyote wakuyafanyia marekebisho yeyote ili kuyafanya yawe bora zaidi au kuondoamaneno yake yeyote anapofanya uhariri wake.
“MSIONGEZE neno lolote katika yale niwaamuruyo, walaMSIPUNGUZE neno lolote, bali zishikeni amri (kumi) za BWANA,Mungu wenu ninazowapa ninyi” – (Kumbukumbu la Torati 4:2).
Mungu mwenyewe anatoa ahadi kwamba hawezi kuzibadili amri zake[kumi]:
“MIMI SITALIVUNJA agano langu, wala SITABADILI NENO LILILOTOKAMIDOMONI (MWANGU) – (Zaburi 89:34).
Biblia inaeleza waziwazi kwamba Mungu hakubadili Sabato kutoka siku yasaba kwenda ile ya kwanza ya juma.
3.Je! Yesu Aliibadili Sabato?
Kulingana na maneno ya Yesu, Amri kumi haziwezi kubadilika kamwe:
“Msidhani ya kuwa nimekujakutangua sheria na mafundishoya manabii. Sikuja kutangua balikukamilisha. Kweli nawaambieni,mpaka hapo mbingu na duniazitakapopita, hakuna hata nuktamoja au sehemu ndogo kabisa yasheria itakayoondoka mpaka yoteyametimia” – (Mathayo 5:17-18).
Katika Mwongozo 16 tuligundua kwamba desturi ya Yesu ilikuwa ni kwendakuabudu katika sinagogi siku ya Sabato (Luka 4:16). Pia tuligunduakwamba Yesu alitaka wanafunzi wake waendelee kuionja raha ya kuitunzaile Sabato ya kweli (Mathayo 24:20)
Ni dhahiri, basi, kwamba kutokana na mafundisho ya Yesu na kielelezochake sisi bado tunayo haja ya hilo pumziko la Sabato, yaani, kustarehe nakuutumia wakati wetu pamoja na Mungu.
4.Je! Wale Mitume Waliibadili Sabato?
Yakobo, kiongozi wa kwanza wa kanisa lile la mwanzo, aliandika manenohaya kuhusu zile Amri kumi:
“Anayevunja amri mojawapo ya sheria, atakuwa na hatia ya kuivunjasheria yote. Maana yule yule aliyesema: “USIZINI, “alisema pia””USIUE.” Kwa hiyo, hata ikiwa hukuzini, lakini umeua, weweumeivunja sheria” – (Yakobo 2:10, 11).
Luka, tabibu na mwinjilisti katika kanisa lilela kwanza, anatoa taarifa hii.
“Siku ya Sabato tukatoka nje ya mji,tukaenda kando ya mto, ambapotulidhani kuwa mahali pa kusali. Tuliketi,tukiongea na wanawake waliokusanyikamahali hapo” – (Matendo 16:13).
Kitabu cha Matendo cha Agano Jipyakinataja mara 84 ilipotunzwa. Sabato hiyona wafuasi wa Kristo, zote hizo zilikuwazikitunzwa zaidi ya miaka 14 baada ya ufufuo wa Yesu: Sabato 2 paleAntiokia (Matendo 13:14,42,44); 1 pale Filipi (Matendo 16:13), 3 paleThesalonike (Matendo 17:2,3), Sabato 78 pale Korintho (Matendo 18:4,11).
Yohana, wa mwisho kufa miongoni mwa wale mitume kumi na wawili,aliitunza Sabato. Aliandika hivi:
“Siku ya Bwana nilikuwa katika Roho” – (Ufunuo 1:10).
Kulingana na maneno ya Yesu, siku ya Bwana ni Sabato:
“Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato” – (Mathayo 12:8).
Uchunguzi wa ushahidi wa maandiko unaoonyesha wazi kwamba walemitume hawakufanya jaribio lolote la kuibadili siku ya Mungu ya mapumzikokutoka siku ya saba kwenda ile siku ya kwanza ya juma. Agano jipya,linaitaja siku hiyo ya kwanza ya juma mara nane tu. Katika mifano hiyo yotehakuna ambapo siku ya kwanza ya juma inatajwa kuwa ni takatifu, walahata kudokezwa kuwa tunapaswa kuitenga kama siku ya ibada. Uchunguziuliofanywa kwa makini sana wa hayo mafungu manane yanayoitaja siku yakwanza ya juma huonyesha matukio haya yaliyotokea Jumapili:
(1)Wanawake walikwenda kaburini siku ile ya kwanza ya juma (Mathayo28:1).
(2)”Hata Sabato ilipokwisha” wanawake wakaanza tena kufanya shughulizao za kidunia katika siku ile ya kwanza ya juma (Marko 16:1,2).
(3)Yesu alimtokea kwanza Mariamu Magdalena mapema siku ile kwanzaya juma (Marko 16:9).
(4)Wafuasi wa Yesu walianza tena kufanya shughuli zao katika ile siku yakwanza juma (Luka 24:1).
(5)Mariamu alikwenda kwenye kaburi lile la Yesu na kulikuta kaburi likotupu katika ile siku ya kwanza (Yohana 20:1).
(6)Wanafunzi wale walikusanyika mahali pamoja “kwa hofu ya Wayahudi”(si kwa ajili ya kuendesha ibada ) Katika ile siku ya kwanza ya juma(Yohana 20:19).
(7)Paulo aliwaomba washiriki wa kanisa kufanya mahesabu ya fedha zaowalizopata katika ile siku ya kwanza ya juma, na “kuweka kando kiasi fulanicha fedha” kwa ajili ya maskini kule Yerusalemu (I Wakorintho 16:1,2).Kifungu hicho hakitaji mkutano wowote wa dini ambao ulifanyika.
(8)Katika Matendo 20:7 Luka anaongea habari za hotuba (mahubiri) yaPaulo aliyoitoa katika ile siku ya kwanza ya juma wakati wa mkutano ule wakuagana ambao haukutazamiwa kufanyika. Kusema kweli, Paulo alihubirikila siku, na mitume wale walimega mkate kila siku (Matendo 2:46).
Hakuna hata moja kati ya mafungu hayo linalodokeza ya kwamba walemitume waliazimu kuacha kuitunza Sabato ya siku ya saba. Mitume walehawakulitaja badiliko lolote la Sabato kutoka siku ya saba kwenda ile ya
kwanza ya juma. Hakuna ushahidi wowote ulio wazi katika Agano Jipyaunaoonyesha badiliko hilo la Sabato kutoka Jumamosi, siku ya saba yajuma, kwenda Jumapili, siku ya kwanza ya juma. Badiliko hilo lilikuja baadaya siku zile za Yesu na mitume wake, kwa hiyo, yatupasa sisi kuigeukiahistoria ili kuona ni lini na kwa jinsi gani badiliko hilo lilitokea.
5.Jumapili Ilitoka Wapi?
Mitume wale wanatuonya sisi waziwazi kwamba Wakristo fulaniwangetangatanga na kwenda mbali na mafundisho ya Ukristo ule wa AganoJipya: “Iweni macho ” (Matendo 20:29-31). Na ndivyo ilivyotokea hasa.Wanahistoria wanaoaminika wanaandika waziwazi kuonyesha jinsi Wakristo.
walivyoanza kupotea na kuuacha usafi ambaokanisa lile la mitume lilikuwa nao. Mapokeo namafundisho ambayo hayakuungwa mkonokamwe na Paulo, Petro na waasisi walewengine wa kanisa lile la Kristo, yakaanzakuingia taratibu ndani ya kanisa.
Badiliko lililofanyika kutoka katika utunzaji waSabato kwenda kwenye utunzaji wa Jumapilililitokea baada ya kukamilika kuandikwa kwaMaandiko ya Agano jipya na baada ya kufamitume wale wote. Historia inaandika katikakumbukumbu zake ya kwamba hatimayeWakritsto wakahama kutoka katika kufanyaibada yao na kupumzika siku ya saba kwendakatika siku ile ya kwanza ya juma. Lakini, kwa kweli, waumini hawakuachakuitunza Sabato ile ya siku ya saba mwishoni mwa juma fulani lililowekwana ghafla kuanza kuitunza Jumapili kama siku ya Bwana. Mfano mmojauliothibitishwa ambao ulitokea mapema sana wa utunzaji wa Jumapili naWakristo ulitokea katika nchi ya Italia, katikati ya karne ile ya pili baada yapale Wakristo wengi walizitunza siku zote mbili, ambapo wengine badowaliendelea kuitunza Sabato peke yake.
Tarehe 7 Machi, 321 B.KKonstantino Mkuu alitoa amri yakwanza ya Kiserikali ya Jumapili,akawalazimisha wote, isipokuwawakulima, katika Dola ya Kiromakupumzika Jumapili. Hivyo pamojana sheria nyingine zipatazo tano zakiserikali zilizoamriwa naKonstantino kuihusu Jumapili,ziliweka mfano wa sheria zote zaJumapili kuanzia wakati ule mpakaleo. Katika ile karne ya nne Baraza la Laodikia liliwakataza Wakristowasiache kufanya kazi siku ya Sabato, huku likiwashurutisha kuiheshimuJumapili kwa kuacha kufanya kazi endapo uwezekano ulikuwapo wakufanya hivyo.
Historia inaonyesha kwamba ibada ya Jumapili na utunzaji wake ni desturiiliyowekwa na wanadamu. Biblia haitoi kibali chochote ili kuifutilia mbaliSabato ya siku saba ya amri ile ya nne. Nabii Danieli alitabiri kwambakatika kipindi kile cha Kikristo mamlaka fulani yenye hila ingejaribu kuibadilisheria ya Mungu (Amri Kumi) (Danieli 7:25)
6.Ni Nani, Aliyefanya Badiliko?
Je! Ni nani aliyeihamisha rasmi Sabato kutoka siku ya saba kwenda siku yakwanza ya juma? Kanisa Katoliki linadai kwamba limefanya badiliko hilo.Katika jitihada ya kutaka kuiokoa Dola ya Roma iliyokuwa inavunjika,viongozi wa kanisa waliokuwa na kusudi zuri wakafanya maridhiano nakujaribu kubadili siku ya ibada kutoka Jumamosi kwenda Jumapili.
Katekisimo ya kanisa Katoliki la Romainasomeka hivi:
“Swali: Ipi ndiyo siku ya Sabato?
“Jibu: Jumamosi ndiyo siku ya Sabato.
“Swali: Kwa nini sisi tunaitunza Jumapilibadala ya Jumamosi?
“Jibu: Tunaitunza Jumapili badala yaJumamosi kwa sababu kanisa Katoliki…. Liliihamisha ibada toka Jumamosikwenda Jumapili”.
-Peter Geirmannn, The Convert’s Catechism of Catholic Doctrine (toleo la1957). Uk. 50.
Kwa majivuno kanisa Katoliki linatangaza kwamba viongozi wa kanisaambao ni wanadamu tu ndio waliofanya badiliko hilo.
“Siku ile takatifu, yaani, Sabato, ilibadilishwa kutoka Jumamosi kwendaJumapili… si kutokana na maagizo yo yote yaliyoonekana katika Maandikobali kutokana na hisia ya kanisa kwamba linao uwezo wake lenyewe…watu wale wanaofikiri kwamba Maandiko ndiyo yangekuwa mamlaka pekeyake, kwa mantiki hiyo, ingewapasa kuwa Waadventista Wasabato , naowangeitakasa Jumamosi.” – Cardinal Maida, Askofu Mkuu wa Detroit, SaintCatherine Catholic Church Sentine, Algonac, Michigan, Mei 21, 1995.
7.Je! Makanisa Ya Kiprotestanti Yanasemaje?
Hati rasmi zinazotoa muhtasari wa itikadi za madhehebu kadhaa yaKiprotestanti zinakiri kwamba Biblia haitoi kibali cho chote cha kuitunzaJumapili.
Martin Luther, mwasisi wa kanisa la Kilutheri, aliandika katika ungamo laAugusiburgi (Augusburg Confession), sharti la imani la 28, aya ya 9,maneno haya: “Wao [Wakatoliki wa Roma] wanadai kwamba Sabatoilibadilishwa na kuwa Jumapili, siku ya Bwana, kinyume na ile sheria yaAmri kumi,.. wala hakuna mfano wanaojivunia sana kama huo wa kuibadilisiku ya Sabato. Ni mkuu, wasema wao, uwezo na mamlaka ya Kanisa, kwakuwa liliiondoa mojawapo ya zile Amri kumi.”
Wanatheolojia wa Kimethodisti Amosi Binney na Danieli Steele walitoamaoni yao haya:
“Ni kweli, hakuna amani dhahiri ya ubatizo wa watoto wachanga….walahakuna yo yote ya kuitakasa siku ya kwanza ya juma.” TheologicalCompend (New York: Methodist Book Concern, 1902), Kurasa 180,181.
Dk. N. Summerbell, mwanahistoria wa wanafunzi wa Kristo (Disciples ofChrist) au Kanisa la Kikristo (Christian Church), aliandika, alisema:
“Kanisa la Roma lilikuwa limeasi kabisa…..Liliigeuza Amri ya Nne kwakuiondoa Sabato ile ya Neno la Mungu, na kuiweka Jumapili kama sikutakatifu” A True History of the Christian and the Christian Church, kurasa za417,418.
8.Suala Lenyewe hasa ni lipi?
Jambo hilo linatuleta ana kwa ana kupambana na maswali haya: kwa niniWakristo wengi sana huitunza Jumapili bila kuwa na idhini ya Biblia? Lamaana zaidi ni hili, Je! Niitunze siku gani? Je! Niwafuate wale wasemao,”Sidhani kwamba inaleta tofauti yoyote kuhusu siku gani ninayoitunza mraditu mimi naitunza moja katika zile saba”? Au, Je! Niihesabu kuwa ni yamaana ile siku ambayo Yesu, Muumbaji wetu, aliianzisha alipoiumba Duniayetu hii, tena ni siku ile aliyoiteua Mungu na kuiweka katika zile Amri kumi:yaani, kwamba “siku ya saba ni Sabato”?
Hapa tunashughulika zaidi yautunzaji wa nje tu, bali juu ya siku ipiyaonekana kibiblia kuwa ni sahihi.Hoja muhimu inayohusu hapa ni ileya utii kwa Yesu. Muumbaji wetualiitenga Sabato kama siku”Takatifu,” kama ndio wakatiuliowekwa kwa ajili yetu na familiazetu kumkaribia yeye zaidi ili tupatekupewa nguvu na burudiko. Nitamtiinani? Je! Nimtii Kristo, mwana waMungu, au mapokeo ya wanadamukatika suala hili la siku ninayoitakasa? Uchaguzi uko wazi: mafundisho yawanadamu au amri za Mungu. Neno la wanadamu au Neno la Mungu. Sikumbadala iliyowekwa na wanadamu au amri ya Mungu.
Nabii Danieli anatoa onyo kwa wale ambao wange”jaribu kubadili majirayaliyowekwa pamoja na sheria” (Danieli 7:25,NIV) [“azimu kubadili majirana sheria” (Daniel 7:25, NKJV)]. Mungu anawaita watu wake warudi nakumtii yeye. Anawaita ili wapate kuitunza Sabato kama ishara ya Utii naupendo wao kwake yeye.
Yesu alisema, “Mkinipenda, mtakishika kile niwaamurucho” (Yohana 14:15).Tena yeye anaahidi kuwapa furaha kamili wale wampendao hata kuwezakuzitii amri zake (Yohana 15:9-11). Tunaye Mwokozi wa ajabu. Anayoshauku nyingi kwa ajili yetu ili sisi tupate kuuonja upendo wake kwa utimilifu
wake wote. Moyo ule ulio na utii wa hiari unafungua mlango wazi ilikuupokea upendo huo.
Katika ile bustani ya Gethsemane Kristo alijinyenyekeza kikamilifu chini yamapenzi ya Baba yake – licha ya kukabiliwa na msalaba na dhambi zaulimwengu mzima zilizokuwa zikiyaangamiza maisha yake. AlipomliliaMungu, na kusema, “Uniondolee kikombe hiki,” alikuwa amejinyenyekezakatika maombi yake, kisha akaongeza kusema hivi “Walakini, si kamanitakavyo mimi, bali utakavyo wewe” (Marko 14:36).
Kristo anatamani sana kwamba sisi tupate kuuonja utimilifu ule uletwao namaisha yaliyosalimishwa kweli kweli. Pia anataka sisi tuionje furaha yapumziko la Sabato. Anataka sisi tumtumainie yeye kiasi cha kutosha kumtiikatika mambo yote ya maisha yetu. Endapo wewe utaitika anapokuita nakuzitii amri zake zote [kumi], basi, wewe utaweza kuionja ahadi ya Yesuisemayo kwamba furaha yake itakuwa “ndani yenu” na “furaha yenu” ita”timizw[a]” (Yohana 15:11).
great