SIRI YA KUKUA KWA USHIRIKIANO
Mapema katika miaka ile ya kuanzia 1960 na kuendelea, Ndugu Andrew,mtu wa Uholanzi, aliingiza kwa siri mzigo wa Biblia katika gari lake la VolksWagen (Folks Vageni) na kuvuka mpaka wa Romania na kuwapita walinziwa kikomunisti. Alipanga katika hoteli moja na kuanza kuomba kwambaMungu amwongoze kwenda kwenye makundi ya Kikristo yanayofaa – yaaniwale ambao wangeweza kuzitumia vizuri sana zile nakala zake zaMaandiko.
Mwisho wa juma lile Andrew alitembea kwenda kwa karani wa hoteli ile nakumwuliza angeweza kulipata wapi kanisa.
Yule karani akamwangalia kwa njia isiyo ya kawaida kidogo na kujibu,”Hatunayo mengi ya hayo, unajua. Isitoshe, usingeweza kuielewa lughayetu”
“Je! Wewe hukujua?” akajibu Andrew, “ya kuwa Wakristo wanazungumzalugha ya ulimwengu mzima.”
“Ehee! Ni lugha gani hiyo?”
“Inaitwa Agape [Upendo]”
Yule karani alikuwa hajapata kuisikia kamwe, lakini Andrew alimhakikishiakwa kusema hivi, “Ni lugha nzuri kuliko zote ulimwenguni”
Andrew aliweza kuyapata makundi kadhaa ya kanisa katika eneo lile nakufanikiwa kupanga kuonana na mwenyekiti na katibu wa dhehebu fulani.Kwa bahati mbaya, ingawa Andrew na watu hao walijua lugha kadhaa zaUlaya, wakajikuta hawana lugha hata moja waliyoijua wote. Basi, wakakaapale wakikodoleana macho tu. Andrew alikuwa amesafiri maili nyingi zahatari na ule mzigo wake wathamani, lakini ikaonekana ya kwambahapakuwa na njia yoyote ya kujua iwapo watu wale walikuwa ni nduguWakristo wa kweli au makachero wa Serikali.
Hatimaye akaiona Biblia yaKiroma juu ya meza katika ofisiile. Andrew akaingiza mkonowake katika mfuko wake nakuichomoa Biblia ya Kiholanzi.Alifunua 1 Wakorintho 16:20, nakuishika Biblia akiwa amenyoshamkono wake akisonda kidolechake kwenye jina la Kitabu kilewaliweza kulitambua. Mara mojanyuso zao zikang’aa kwa meru.Upesi wakaipata sura ile ile nafungu lile lile katika Biblia zao za Kiromania, Kisha wakasoma manenohaya: “Ndugu wote hapa wanawasalimu. Salimianeni kwa busu takatifu.”
Watu wale wakatabasamu na kumwangalia Andrew. Kisha mmoja waoakapekua katika Biblia yake na kupata Mithali 25:25. Andrew akalipatafungu lile na kulisoma “kama vile maji baridi yalivyo kwa mtu mwenye kiu,ndivyo ilivyo habari njema itokayo katika nchi ya mbali “
Watu wale walitumia nusu saa wakiongea na kupeana habari – kwa kupitiatu katika maneno ya Maandiko. Walikuwa na furaha nyingi sana kwa urafiki
wao huo uliovuka mipaka yote ya utamaduni hata wakacheka mpakamachozi yalipowatoka.
Andrew alijua kwamba amewapata ndugu zake. Alipowaonyesha mzigowake wa Biblia, Waromania wale walitekwa nao wakamkumbatia tena natena.
Jioni ile katika ile hoteli, yule karani alikuja karibu na Andrew na kusemakwa mshangao, ‘Aisee, nilitafuta ‘agape’ katika kamusi. Hakuna lugha yajina lile. Hilo ni neno la Kigiriki limaanishalo upendo.
Andrew akajibu “sawasawa. Mimi nilikuwa nazungumza kwa kutumia nenohilo mchana kutwa”.
Je! Wewe umeigundua lugha hiyo nzuri? Katika mwongozo huu utajifunzajuu ya jinsi Mungu anavyoweza kutuleta sisi sote katika jamii yake kubwaya upendo.
1.Kanisa Lilianzishwa Kwa Ajili Ya Ushirika
Yesu alilianzisha kanisa ili kukidhi hitaji la msingi la kibinadamu la malezi nakusaidiana. Sisi sote tunayo mahitaji yetu. Na hivyo ndivyo kanisalinavyohusika na mambo hayo yote. Hapo ni mahali tunapokuja ilikushirikiana na kusaidiana. Maandiko yanalidhihirisha kanisa lile lenyenguvu la Mitume ambalo liliwaita wanaume na wanawake kuja katikaushirika uliojaa furaha ambao ulikwenda juu ya njia yote hadi kwaMwenyezi:
“Tulichokiona na kukisikia ndicho tunachowatangazieni nyinyi pia, ilinanyi mpate kujiunga nasi katika umoja tulio nao na Baba na MwanaeYesu Kristo.
Tunawaandikia nyinyi mambo haya kusudi furaha yetuikamilike” – 1 Yohana 1:3,4.
Mioyo yenye mawazo sawa iliyofungwa pamoja kwa njia ya mawasiliano naYesu na mawasiliano ya wao kwa wao, huionja “furaha kwa kiwango chakechote! Wote wanaongea lugha moja, lugha ile ya upendo.
Wakristo wanakuwa sehemu ya familia iliyotandaa. Wanakuwa ndugu nadada katika Kristo kwa kuwa wote wanayo roho ya undugu. Kadiriunavyozidi kupanuka umoja huo wa imani, ndivyo kadiri vifungo vyenyenguvu zaidi vinavyokuwepo miongoni mwa Wakristo.
Washiriki wa makanisa yale yaliyoanzishwa na mitume wa Yesu walifungwapamoja wakiwa na itikadi zao zinazofanana, kwa upendo wao waliokuwanao kwa Mungu na kwa shauku yao ya kumtumikia na kuugawia ulimwenguhuu neema yake. Kifungo hicho cha ushirika wao wa karibu sana kilikuwakimojawapo ya sababu zilizowafanya watu wale wachache wasiokuwa nanguvu, ambao walikuwa wakiteswa, kuupindua ulimwengu wa wakati ule.
2.Kanisa Aliloanzisha Kristo
Je! Hivi Kristo analo kanisa, au wazo zima juu ya shirika la dini nimavumbuzi tu ya wanadamu? Yesu anajibu hivi:
“Juu ya MWAMBA huu nitalijenga kanisa langu, wala milango yakuzimu haitalishinda” – (Mathayo 16:18).
Yesu ndiye ule Mwamba wa kutia nanga zetu,Jiwe la pembeni la kanisa lake.
Je! Ni kusudi gani ambalo lilikuwa sehemu yamsingi wake?
“Mmejengwa juu ya msingi wa mitume namanabii, naye Kristo mwenyewe ni jiwe lapembeni” – Waefeso 2:20.
Je! Injili ile ilipohubiriwa, Bwana alifanikiwakufanya nini?
“Na Bwana akalizidisha kanisa kila siku
kwa wale waliokuwa wakiokolewa” – (Matendo 2:47, KJV).
Yesu alipoanzisha kanisa lile, aliahidi kwamba “milango ya kuzimuhaitalishinda”(Mathayo 16:18), na kanisa la Kikristo mpaka sasalinaendelea kuwapo. Limepata kuwa na maadui wenye nguvu nyingi kabisakuanzia na wafalme wale wa Dola ya Kiroma hadi kwa madikteta waKikomunisti lakini damu ya wafiadini imelifanya lizidi kuwa na nguvu nyingi.Mkristo mmoja alipochomwa moto kwenye mti wa kuchomea au alipotupwakwa simba, wengine kadhaa walijitokeza kuchukua nafasi yake. Watuwenye nadharia ya kushuku mambo ya Mmungu wamefanya kilawaliloweza kujaribu kutoa sababu zao na kulipotosha kanisa. Lakini ilekweli ya Kikristo inashindana nao kwa ufasaha sana kuliko hapo kwanzakatika kizazi hiki cha sayansi na kinachopenda mambo ya ulimwengu.
Mojawapo ya changamoto kuu kuliko zote kwa kanisa ilikuja mara tu baadaya kukubalika kwake kama dini rasmi ya Dola ya Roma. Kanisa likapatautajiri mwingi – na hatimaye likaharibika. Likaonekana limekufa kiroho katikazile zama za giza. Lakini siku zote Bwana alihifadhi sehemu ya maana yawaumini waliokuwa wajasiri na waaminifu ambao katikanyakati zilezisizokuwa na matumaini na ngumu, waling’aa sana kama nyota wakati wausiku usiokuwa na mbalamwezi.
Paulo analinganisha uhusiano uliopo kati ya Kristo na Kanisa lake nauhusiano ule wa upendo, unaotunza, wa mume kwa mke wake (Waefeso5:23-25). Kanisa ni familia, kila mshiriki akifanya uhusiano wake nawashiriki wengine wa familia hiyo na kuchangia katika usitawi wao(Waefeso 2:19)
Paulo pia analionyesha kanisa kama mwili hai, Kristo mwenyewe akiwandiye kichwa chake (Wakolosai 1:18).
Tunapokuwa tumebatizwa, tunatoa ushuhuda wa imani yetu ndani ya Yesuna kuwa washiriki wa ule “mwili” yaani kanisa.
“Maana sisi, tukiwa Wayahudi au watu wa mataifa mengine, watumwaau watu huru, sote TUMEBATIZWA kwa Roho mmoja KATIKA MWILIHUO MMOJA; na sote tukanyweshwa Roho huo mmoja” – (1Wakorintho 12:13).
Kitabu cha ufunuo kinaonyesha picha ya Kristo aliyefufuka akitembeakatikati ya makanisa akionyesha ulinzi wake alionao juu yake (Ufunuo1:20,12,13). Kristo hajawaacha watu wake kamwe, wala hatawaachakamwe.
3.Kanisa Lenye Kusudi Maalum
Kuhudhuria kanisani ni kwa maana sana kwa Mkristo. Tunahitaji msaadawa wengine kuifanya imani yetu iwe hai na iendelee kukua.
Kanisa pia lina wajibu wa maana wa aina tatu:
1)Kanisa linalinda kweli.
Likiwa ni “nguzo na msingi wa kweli”(Timotheo 3:15), kanisa linatetea nakuilinda kweli ya Mungu mbele yaulimwengu.
Tunahitaji hekima ya pamoja ya wauminiwengine ili kutusaidia kukuza mawazo yetujuu ya kweli zile zilizo za muhimu zamaandiko.
2)Kanisa ni kielelezo cha jinsi neema yaMungu iwezavyo kuwatendea wenyedhambi. Mabadiliko aliyoyafanya Kristokatika maisha ya waumini humtangazaMungu atuitaye sisi “Katika nuru yake yaajabu” (I Petro 2:9).
3)Watu wa Mungu ni mashahidi wake kwaulimwengu huu wenye shida. Kabla tuhajarudi mbinguni, Yesu aliwaahidiwanafunzi wake, alisema.
“Lakini mtapokea nguvu Roho Mtakatifu akiisha kuwajilia juu yenu,nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na ktika Uyahudiwote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi” – (Matendo 1:8).
Ni heshima kubwa kwa kanisa kuupeleka huo ujumbe wa pendo kuu laMungu ulimwenguni kote.
4.Limeanzishwa Kwa Ajili Ya Kutiana Nguvu
Kanisa lile alilolianzisha Kristo lilikuwa na mfumo halisi. Mtu aliwezakuingizwa au kutoingizwa katika ushirika wake (Mathayo 18:15-18). Kanisala Mungu liliwachagua viongozi, tena lilikuwa na makao makuu yaulimwengu pamoja na sehemu za kukutania za kila mahali (Matendo8:14;14:23;15:2 1Timotheo 3: 1-13) Walipokwisha kubatizwa, wauminiwalijiunga na kundi lililokuwa limeanzishwa. (Matendo 2:41 na 47).
Kanisa lipo kwa ajili ya kutiana moyo.
“Hebu na tufikirie jinsi tuwezavyo kuhimizana katika upendo wa kazinzuri. Tusiache kukusanyika pamoja, kama wengine walivyozoeakufanya, bali TUTIANE moyo sisi kwa sisi – na kuzidi kufanya hivyokadiri mwonavyo. Siku ile (ya kuja kwake Kristo) kuwa inakaribia. “-Waebrania 10:24,25.
Kwa kifupi, hayo ndiyo mambo yafanywayona kundi la Kanisa lenye afya. Washirikiwake wanajengana katika imani, wanatianamoyo wao kwa wao. Mungu alilianzishaKanisa lake ili kuwatia nguvu watu waMungu na pia kutoa huduma kwa ulimwenguhuu. Twaweza kufanya mambo mengi sanatukiwa pamoja kuliko tuwezavyo kufanyamambo mengi sana tukiwa pamoja kulikotuwezavyo kufanya kama mtu mmoja mmojahapa na pale. Chukua mfano mmoja tu.Kanisa la Waadventista Wasabato. Sisi tunaendesha kazi ya uganga katikaeneo kubwa sana ulimwenguni kote – kuanzia yale magari ya afya yaliyondani kabisa ya mji mkuu kwenda kwenye kliniki zilizo katika visiwavilivyojijenga mbali katika bahari ya Pasifiki ya Kusini. Taasisi zetu za elimuzimewaletea makumi ya maelfu ya vijana maarifa ya maisha bora ndani yaKristo – kuanzia Chuo kikuu cha Loma Linda, kinachoongoza katika kazi yakupandikiza mioyo, kwenda kwenye shule ndogo kabisa za mishenizilizotawanyiika ndani ya nchi zote za Afrika. Sisi tunashughulika na njaa namaafa kupitia ADRA. Makanisa yaliyo katika maeneo mbali mbaliyanawavika nguo na kuwalisha maskini na wasio na kwao katika maelfu yavituo vya huduma kwa jamii. Nayo makundi ya waumini wa Kiadventistawanahubiri ujumbe wa wokovu katika nchi zaidi ya 200. Ni lile kundi laWakristo waliojitoa wakfu tu lililoundwa ambalo lingeweza kuleta matokeohayo kwa ulimwengu mzima.
Kristo na mitume walilifananisha Kanisa na mwili, na kuonyesha kwambasehemu zote za mwili zinahitajika (1Wakorintho 12:21-28). Sehemu zote zamwili hazifanani kabisa, lakini zote ni za muhimu na zote hazina budikufanya kazi pamoja kwa ushirikiano.Jicho lililojitenga na mwili haliwezikuona.
Mkono uliokatwa hauna faida yeyote. Si kitu kama sisi tu jicho, mkono, aukidole tu, hatuwezi kutenda kazi yetu kwa ajili ya Kristo kwa ufanisi kamakila mmoja wetu anajitegemea mwenyewe kabisa. Kuwa mshiriki wakanisa, kuungika na viungo vingine vya mwili hututua nguvu sisi kamawakristo.
5.Furaha Ya Kuabudu
Ndani kabisa ya mioyo yetu imo shauku ya kumwabudu Mungu, na hajahiyo yaweza kufifia au kutoweka tusipoiiruhusu kufanya kazi yake. Je!Mtunga Zaburi alijisikiaje alipofikiria kwenda mahali pale pa ibada?
“NALIFURAHI pamoja na wale walioniambia, “Na twende nyumbanimwa BWANA” – (Zaburi 122:1).
Je! Muziki una sehemu gani katika ibada ya watuwote?
“Mwabuduni BWANA kwa furaha, “Njoni mbelezake kwa nyimbo za furaha” – (Zaburi 100:2).
Biblia inatuambia kwamba kutoa sadaka nisehemu murua ya ibada ya Mungu.
“Leteni sadaka mkaziingie nyufa zake.Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu” -(Zaburi 96:8-9).
Maombi nayo pia ni sehemu ya maana ya ibadaya watu wote.
“Njoni tusujudu katika ibada tupige magotimbele za BWANA MUUMBAJI wetu’ – Zaburi 95:6
Kujifunza Biblia na kuhubiri ni kitovu cha ibada ya Agano Jipya. Kuanzia nalile hubiri la Petro katika ile siku ya Pentekoste, ambalo linapatikana katikaMatendo 2, na kuanzia katika nyakati zile za wanamatengenezo ya kanisawale wakiporotestanti hadi katika hizi siku zetu, kila uamsho mkuu wa kidiniumejengwa juu ya mahubiri yatokanayo katika Biblia. Hivi kwa nini?
Kwasababu “Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu. Lina ukali kuliko upangauwao wote ukatao kuwili” – (Waebrania 4;12-13).
6.Je Kitu Gani Ni Chema Kuhusu Kanisa?
Wengine hupinga na kusema kwamaba kanisa limejaa watu ambao siwakamilifu. Lile alilolisema Henry Ward Beecher ni la kweli:
“Kanisa sio nyumba ya sanaa ya maonyehso ya Wakristo maarufu, bali nishule kwa ajili ya kuwaelimisha hao wasio wakamilifu.
Kwa kuwa hakuna hata mmoja miongoni mwetu aliye mkamilifu, basi kanisahalitakuwa kamilifu pia.
Katika mmojawapo wa mifano yake Yesu alitukumbusha sisi kwambamagugu huota pamoja na ngano (Mathayo 13:24-30). Tunapozisomanyaraka za Paulo za Agano Jipya, tunagundua kwamba kanisa lile lamitume lilikuwa na matatizo makubwa sana. Na kanisa la leo mara nyingilina upungufu mkubwa. Lakini,. Tafadhali, kumbuka kwamba hakunawashriki wenye makosa wawezao kuliharibu au kulivuruga lile Jiwe kuu laPembeni la kanisa – yaani, Yesu Kristo mwenyewe. Basi, ndani yamakanisa yasiyo makamilifu yatupasa kukaza macho yetu juu ya Mwokoziwetu anayetuhudumia na kulipa jambo hilo umuhimu wa kwanza. Licha yamakosa yake, kanisa ni mali yake, basi, ninyi kazeni macho yenu juu yaKristo.
“Nanyi waume, wapendeni wake zenu kama Kristo alivyolipendakanisa, akajitoa mwenyewe sadaka kwa ajili yake. Alifanya hivyo ilikwa neno lake, aliweke wakfu kwa Mungu, baada yakulifanya safi kwakulioshakatika maji, kusudi ajipatie kanisa lililo takattifu na safikabisa, kanisa lisilo na doa, kasoro au cho chote cha namna hiyo”(Waefeso 5:25 – 27).
Kanisa ni la maana sana kwa Yesu hata akajitoa nafsi yake kwa ajili yakealipokufa kwa ajili ya kila mmoja wetu na kanisa kwa jumla. Kwa hiyo,ushirika wa kanisa kwako wewe ungepaswa kuwa wa maana. Je ! hiviwewe ni mshiriki wa mwili wa Kristo?
7.Kulipata Kanisa Hilo
Je! Ni imani ngapi za kweli alizonazo Yesu uliwenguni humu?
“Kuna mwili (kanisa) mmoja , na roho mmoja…. Bwana mmoja, ImaniMoja, Ubatizo mmoja” – (Waefeso 4:4,5).
Kwa vile Kristo anayo “imani moja” tu, je! Twawezaje sisi kujua ni imani ipihiyo? Yesu anatupatia sisi ufunguo wake huu:
Kiswahili 20
https://languages.bibleschools.com/kiswahili/swahili20.htm 6/6
“Mtu anayependa kufanya yale anayotaka Mungu, atajua kamamafundisho yangu yametoka kwa Mungu, au mimi najisemea tumwenyewe” – Yohana 7:17.
(Angalia pia Yohana 8:31,32).
Tunapojitoa wenyewe kufanya mapenziya Mungu, atatusaidia sisi kujua endapomafunzo hayo yanatoka kwa Mungu, auni mapokeo tu ya wanadamu.Tunapolitafuta hilo kanisa jambo kuu nikuchunguza jinsi linavyoliheshimu nakulitii Neno la Mungu. Ushirika wa kweliumejengwa juu ya maandiko, sio juu yakiongozi mmoja mwenye uwezo wa ajabuau taasisi moja kuu.
Endelea kufanya ugunduzi wako mwingikatika miongozo hii, tembea katika nuruanayokufunulia Mungu kutoka katika Biblia, naye atayafunua mapenzi yakekwako. Mkristo anayekua ni mtu anayeufungua moyo wake na akili yake ilikuipokea ile kweli kama Mungu anavyoifunua kutoka katika Neno lake.