MKUSDA CHURCH
Unity in Worship

22. JE! MUNGU ANA HAKI?

JE! MUNGU ANA HAKI?
Mvulana mmoja ndani kabisa ya mji anauawakwa risasi zilizofyatuliwa ovyo na majambaziwakati anafanya kazi yake ya shuleni akiwaameketi nyumbani kwao katika meza yafamilia yake.
Mama mmoja kijana katika viunga vya mjianagundua kwamba mtoto wakeamepatikana na Ukimwi kutokana na damualiyoongezewa mwilini mwake.
Misiba inazidi kuendelea tena na tena katikaulimwengu wetu huu. Nasi tunatamani sanakujua jibu kwa mambo hayo yote. Hivi Munguhuyo yuko wapi katika ulimwengu wetu huuuliojaa mateso na vifo visivyo na maana?Mtunga Zaburi anatuhakikishia sasa kwamba” dunia hii imejaa upendo wake usio na mwisho” (Zaburi 33:5).
Lakini, basi, kama hilo ni jambo la kweli, mbona hayakomeshi mateso hayopamoja na misiba? Sura ya 20 ya Ufunuo inatuonyesha sisi ni kwa ajili ganina lini Mungu atakapo komesha dhambi na mateso.
1.Miaka Ile Elfu Moja Yafunuliwa
Ufunuo 20 huelekeza mawazo yetu yote kwenye kipindi kile cha miaka1,000 ambacho kinakuja baada ya Kristo kuja mara ya pili. Matukio yaleyanayokizunguka kipindi hicho cha mika 1,000 ni lile tendo la mwisho katikapambano ambalo limekuwa likiendelea kati ya Kristo na Shetani tangudhambi ilipoingia katika ulimwengu huu.
Mfululizo wa matukio hayo yakuvutia macho ulianza kulembinguni wakati Lusifaalipomuonea wivu Kristo,akaanzisha vita kule dhidi yamalaika wale ambaohawakuanguka [dhambini]alifukuzwa kule, na kukimbiliakatika dunia yetu. Matukio hayoyaliendelea hapa duniani katika ileBustani ya Edeni, halafu kupitiakatika Karne zote na kushuka hadi yalipofikia kilele chake cha kwanzawakati ule Ibilisi alipowachochea wanadamu kumsulibisha Kristo. (Ukipendawaweza kukipitia tena kisa hicho cha kusikitisha katika Mwongozo 3.)Matukio hayo yatafikia kilele chake cha mwisho
kitakapokwisha kipindi kilecha miaka 1,000 wakati dunia yetu hii yenye dhambi itakapotakaswa nakuwekwa chini ya utawala wa Kristo. Ufunuo 20 unatuonyesha sisi kwambakipindi hicho cha miaka 1,000 kimetenganishwa na ufunuo wa aina mbili.
Je! Ni akina nani hao ambao Mungu anawafufua kutoka kwa wafu katikaufufuo wa kwanza unaotokea mwanzo wa ile miaka 1,000?
“Wameneemeka sana, heri yao wote wanaoshiriki ufufuo huu wakwanza. Kifo cha pili hakitakuwa na nguvu juu yao; watakuwa

makuhani wa Mungu na wa Kristo, na watatawala pamoja naye kwamiaka elfu moja”- (Ufunuo 20:6).
Wale walio “heri na watakatifu,” yaani, wale waliompokea Kristo kamaMwokozi wao wanatoka katika ule ufufuo wa kwanza wa wenye haki nahawana budi kutawala pamoja na Kristo katika kipindi cha miaka 1,000basi, ni lazima wafufuliwe mwanzo wa ile miaka 1,000.
Je hao ni akina nani wanaofufuliwa katika ufufuo wa pili utakaotokeamwisho wa kipindi cha miaka elfu moja?
Hao wafu Waliosalia hawakuwa hai mpaka ilipokwisha ile miaka elfumoja – (Ufunuo20:5).
Maneno haya “hao wafu waliosalia” yanaweza tu kuwataja waovu walewaliokufa kwa sababu wale wenye haki ambao ni heri na watakatifuwanaofufuliwa mwanzo wa ile miaka 1000.
Kwa hiyo, hicho kipindi cha miaka 1,000 kimetenganishwa na ufufuo waaina mbali : yaani, ufufuo wa wenye haki unatokea mwanzo wake, naufufuo wa waovu unaotokea mwisho wake.


2.Kufufuliwa Wakati Wa Marejeo Ya Kristo
Ufufuo wa kwanza, yaani, ule wa wenye haki unatokea wakati wa kuja maraya pili kwa Kristo.
“Maana patatolewa amri, sauti yatarumbeta ya Mungu, naye Bwanamwenyewe atashuka kutoka mbinguni.Ndipo wale waliokufa wakiwawanamwamini Kristo watafufuliwa kwanza.Kisha sisi tulio hai wakati huotutakusanywa pamoja nao katika mawingukumlaki Bwana hewani. Na hivyo tutakuwadaima pamoja na Bwana” (1Wathesalonike4:16,17)
Yesu anapokuja katika dunia hii anawafufuawale “waliokufa katika Kristo” na kuwachukuakwenda nao mbinguni pamoja na wenye hakiwale walio hai. Kwa kuwa wale waovu badowanaendelea kung’a ng’ania dhambi, hawawezi kuendelea kuwa hai mbelezake Mungu, nao wanaangamizwa wakati ule wa kuja kwake Kristo (Luka17:26-30). (Unaweza kupenda kupitia tena Mwongozo 8 uhusuo matokeoyale yanayoambatana na kurudi kwa Yesu).


3.Shetani Afungwa Mnyororo Hapa Duniani Kwa Miaka Elfu Moja
Miaka hiyo elfu moja inapoanza, wenye haki wote watakuwa wamekwishakwenda zao mbinguni, na waovu watakuwa wamekufa wote. Je! hivikutatokea nini juu ya dunia hii katika hiki kipindi cha miaka 1,000?
“Kisha, nikamwona malaika mmoja anashuka kutoka mbinguni akiwana ufunguo wa kuzimu na mnyororo mkubwa mkononi mwake.Akalikamata lile joka – nyoka wa kale, yaani Ibilisi au Shetani -akalifunga kwa muda wa miaka elfu moja. Malaika akalitupa kuzimu,akaufunga mlango wa kuingilia huko na kuutia mhuri ili lisiweze tenakuyapotosha mataifa mpaka hapo miaka elfu moja itakapotimia. Lakinibaada ya miaka hiyo ni lazima lifunguliwe tena, lakini kwa muda mfupitu ” Ufunuo 20:1-3.
Wakati wa kuja kwake Yesu Shetani anafungwa, naye atabaki na minyororoyake katika kipindi kile cha miaka 1,000. Je! Ni wapi atakapofungwaShetani? Atafungwa “kuzimu” (Abyss), hili ni neno la Kigiriki limaanishalo”kilindi kirefu” au “shimo la kuzimu” katika Mwanzo 1:2 tafsiri ya Kigiriki yaAgano la Kale inatumia neno hili “vilindi” (Abyss) kuielezea dunia hiiilipokuwa katika hali yake isiyotengenezwa vizuri kabla ya siku zile za

uumbaji kuanza. Kwa hiyo dunia yetu hii ndiyoiitwayo kuzimu (Abyss), ni mahali ambapoMungu anamfunga Shetani kuwa amefungwa”na minyororo halisi? La, ni mfano, nimnyororo wa mazingira. Shetani angependasana kuendelea kuwadanganya wanadamukatika kipindi kile cha miaka 1,000. Lakini,basi, yeye hawezi kuwapata wenye hakiwowote wa kuwajaribu, kwa sababu wotewako kule mbinguni. Wala hawezi kuwapatawaovu wa kuwaongoza, kwa kuwa wotewamekufa, wamelala usingizi wa mauti katika mavumbi ya ardhi. Akiwahana uwezo wowote wa kuwadanganya au kuwajaribu, anatangatangakatika dunia hii tupu akilazimishwa kutafakari huzuni kubwa na misibaaliyoisababisha.


4.Wenye Haki Wanawahukumu Waovu

Kipindi kile cha miaka elfu moja ni kipindi cha hukumu pia. Lakini kumbukakwamba hukumu hiyo ina hatua kuu nne:
(1)Hukumu ya wenye haki kabla ya kuja kwa Kristo mara ya pili.
(2)Thawabu ya wenye haki wakati ule wa kuja mara ya pili kwa Kristo.
(3)Hukumu ya waovu katika kipindi kile cha miaka elfu moja.
(4)Thawabu ya Shetani na waovu mwishoni mwa kipindi kile. (ukipendawaweza kuupitia tena Mwongozo 13 ambao unashughulika na hatua ya 1na ya 2 ya hukumu hiyo, yaani, upelelezi na thawabu ya wenye haki.)
Tumekwisha kuona ya kwamba wenye haki waliokufa ambao wamekwishakufufuliwa, pamoja na wenye haki wale walio hai wananyakuliwa kwendambinguni wakati ule wa kuja kwake Kriso mara ya pili. Wao wako nyumbanikwao kule mbinguni katika kipindi kile cha miaka 1,000. Je, watakuwawakifanya nini huko?
“Je! hamjui kwamba watu wa Mungu watauhukumu ulimwengu? Ikiwabasi, ulimwengu utahukumiwa nanyi kwa nini hamstahili kuhukumuhata katika mambo madogo? hamjui kwamba, licha ya kuhukumumambo ya kawaida ya kila siku, tutawahukumu hata malaika?” – (1Wakorintho 6:2-3).


“Kisha nikaona viti vya enzi na watu walioketi juu yake; watu haowalipewa mamlaka ya hukumu. Niliona pia roho za wale waliokuwawamenyongwa kwa sababu ya kumshuhudia Yesu na kwa sababu yaneno la Mungu. hawa hawakumwabudu yule mnyama na sanamuyake, wala hawakupigwa alama yake juu ya paji ya nyuso zao, au juuya mikono yao. Walipata tena uhai, wakawatawala pamoja na Kristokwa miaka elfu moja “- (Ufunuo 20:4).
Katika kipindi kile cha miaka 1,000,wenye haki watazichunguza kesi zawanadamu wale waovu pamoja namalaika wale walioanguka, akiwamona kiongozi wao Shetani. Ni jambolifaalo jinsi gani kwa wafia dini,washindi, na wale walio na makovu yavita walioifuata injili kuwezakuichunguza na kuielewa ile hukumuya Mungu aliyotoa dhidi ya waovu.
Kwa neema yake nyingi Munguamewapa wanadamu waliokombolewa nafasi ya kutathminialivyowashughulikia waovu. Tunaweza kuwa na maswali mengi kama haya:”mbona shangazi yangu hayupo hapa? Alionekana kana kwamba alikuwamtu mzuri” Tutakapozipitia kumbukumbu zile na kuwahukumu wale wafu “kulingana na matendo yao kama yalivyoandikwa katika vitabu vile” (fungu la12), tutajionea wenyewe ya kwamba katika kushughulika kwake kote kulena wanadamu, Mungu amekuwa wa haki wala hana upendeleo kwa kilamtu. Tutaona jinsi Roho Mtakatifu alivyowapa wanadamu nafasi baada ya
nafasi ili wapate kujitoa kabisa kwa Mungu, na haki ya kila hukumuitaonekana wazi.


5.Shetani Afunguliwa Mwisho Wa Ile Miaka Elfu Moja
Mwisho wa ile miaka 1,000 Biblia inatangaza hivi:
“Nikaona mji Mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka kwaMungu mbinguni. Ulikuwa umetayarishwa vizuri kama bibi harusialiyepambwa tayari kukutana na mumewe” – (Ufunuo 21:2).
Mji huu wa ajabu umekuwa makao yetu kwa miaka elfu moja. Sasa Mji huuMtakatifu – ndani yake ukiwa na Kristo na watu wote aliowakomboa -unashuka kutoka mbinguni kuja katika dunia mpya.


Je! Shetani anafanya nini mwisho wa mika hiyo 1,000?
“Wakati miaka elfu moja itakapotimia, Shetani atafunguliwa kutokagerezani mwake. Basi, atatoka nje, ataanza kuyapotosha mataifa yoteyaliotawanyika kila mahali duniani, yaani Gogu na magogu. Shetaniatawakusanya pamoja kwa ajili ya vita; nao watakuwa wengi kamamchanga wa pwani. Walipita katika nchi yote, wakaizunguka kambi yawatakatifu na mji wa Mungu aupendao. Lakini moto ulishuka kutokambinguni, ukawaangamiza” – (Ufunuo 20: 7-9).
Waovu wanafufuliwa katika ufufuo wa pilimwisho wa ile miaka1,000 (fungu la 5).Wenye haki wanaposhuka duniani wakiwandani ya huo mji Mtakatifu, na waovuwanapofufuliwa, Shetani ata”funguliw[a] kwamuda mchache” (fungu la 3). Yeye anao tenawale waovu ili kuwaongoza na shabaha yakeni wale wenye haki. Bila kupoteza hatadakika moja, anaanza mara moja,kuwapanga waovu katika jeshi kubwa sana.Shetani anatoa amri ya kusonga mbele dhidiya mji huo. Waovu wanapojipanga mahalipao kuuzunguka Yerusalemu Mpya (fungu la9), mara moja wanaingiwa na hofu kuu yakupotea – yaani kupotea milele.


6.Mandhari Ya Hukumu Ya Mwisho
Hapo, kwa mara ya kwanza, wanadamu wote wanakutana pamoja ana kwaana. Yesu anawaongoza wana wa Mungu waliokombolewa ambao wamondani ya mji huo. Shetani anaongoza akiwa mbele ya hilo kundi kubwasana lililosongamana la waovu ambao wako nje ya kuta hizo. Katika wakatihuu wa hatari sana, Mungu anatekeleza hatua ya mwisho ya hukumu nawaovu wanapokea siku yao katika mahakama hiyo.
“Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yule aketiye juuyake. Dunia na mbingu vikatoweka mbele ya macho yake, nahavikuonekana tena. Kisha nikawaona watu wakubwa na wadogo,wamesimama mbele ya kiti cha enzi, na vitabu vikafunguliwa. Halafukitabu kingine, yaani kitabu cha uhai, kikafunguluwa pia. Wafuwakahukumiwa kadri ya matendo yao, kama ilivyoandikwa ndani yavitabu hivyo” – (Ufunuo 20:11,12).
Waovu wanaposimama mbele ya hicho kiti cha enzi cha hukumu, maishayao yote yanaonyeshwa mbele yao. Kutoka katika zile kumbukumbuzilizoko kule mbinguni, Yesu, Jaji mwenye haki, anakifunua rasmi kisachake kamili kuhusu jinsi alivyowashughulikia wanaume, wanawake, namalaika walioanguka.
Malimwengu yote yanaangalia kwa hamu kubwa. Akisimama mbele ya kiticha enzi cha Mungu, Yesu anamwonyesha kila mmoja picha kamili ya kaziyake ya ukombozi. Anawaonyesha kwamba yeye alikuja kuwatafuta nakuwaokoa wale waliopotea. Aliingia katika dunia yetu akiwa na mwili wakibinadamu, aliishi maisha yasiyo na dhambi katikati ya mapambano namajaribu, alitoa kafara yake ya mwisho pale msalabani, na kuhudumu kama

Kuhani wetu kule mbinguni. Mwisho,Yesu anapopiga hatua kuja mbelekwa huzuni na kutamka hukumu dhidiya wale walioendelea kwa ukaidikuikataa neema yake, kila kiumbekatika malimwengu hayo atakirikwamba tendo hilo la mwisho lahukumu ya Mungu ni la haki, tena nila lazima.
“Sisi sote tutasimama mbele ya kiticha hukumu cha Mungu. Imeandikwa: ‘Kama niishivyo,’ asema Bwana,kila goti litapigwa mbele zangu; na kila ulimi utamkiri Mungu!” -(Warumi 14:10-11).
“Kristo Yesu akawa mtii hata mauti – naam, mauti ya msalaba!. Ili kwajina la Yesu kila goti lipigwe, mbinguni na duniani.. kila ulimi ukiri yakuwa Yesu Kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba” – (Wafilipi2:5-11).
Tangu dhambi ilipoanza, Ibilisi amekuwa akiielezea vibaya tabia ya Mungu,akimshtaki kwamba hatendi haki. Lakini sasa maswali yote yamejibiwa,utata wote umeondolewa. Sasa kila kiumbe aliye katika hayo malimwenguanakiri kwamba Yesu, Mwana-Kondoo wa Mungu, anastahili kupewaupendo wetu na kuabudiwa.
Mpango wote na kusudi la Mungu sasa vimefunuliwa kikamilifu, na tabia yaMungu inasimama ikiwa imethibitishwa kuwa ni ya haki.
Si wale tu waliokombolewa, bali pia wale malaika waovu pamoja na Shetanimwenyewe watakiri kwamba njia ya Shetani imekuwa na makosa na yakwamba njia za Mungu ni za haki na za kweli. Wote wanaona wazi kwambauovu na uchoyo vimeleta huzuni tu na kutokuridhika, na kwamba mambohayo hayafai kuendelea.


7.Dhambi Yaufikia Mwisho Wake

Ingawa Shetani na kundi lile kubwa sana lililosongamana la watu walewaovu wanakiri kwamba njia ya Mungu haijabadilika, tabia zao bado zinadhambi. Na baada ya hukumu ile kutamkwa wale waovu:
“Wakatembea kijeshi kupitia katika mapana ya nchi, wakaizingirakambi ya watu wa Mungu, mji ule aupendao. Lakini moto ukashukakutoka mbinguni na kuwateketeza kabisa. Na yule Ibilisi, aliyekuwa,anawapotosha katupwa ndani ya ziwa linalowaka moto wa kiberiti….Kisha kifo na kuzimu vikatupwa ndani ya ziwa la moto. Ziwa hili lamoto ndicho kifo cha pili. Mtu ye yote ambaye jina lake halikupatikanalimeandikwa katika kitabu kile cha uhai, alitupwa katika ziwa la moto” -(Ufunuo 20:9-15).
Katika hukumu ya mwisho moto wa milelewa Mungu utateketeza dhambi pamoja nawale ambao kwa ukaidi waowanaing’ang’ania. Shetani na wotewaliopotea wanaangamia katika hicho “kifocha pili,” yaani, wanapatikana na kifo chamilele ambacho katika hichohawataamshwa kamwe. Mwenendo waowa uasi umewaacha waovu hao wakiwahawafai kuingia katika furaha ya kweli,kisha wanateketezwa pamoja na Ibilisi namalaika zake. Moto ule utokao mbinguniunaitakasa dunia kabisa kutokana nauharibifu wa dhambi; hatimaye Munguanakuwa na ulimwengu safi, usioweza tena kutiwa makovu ya uovu.Pambano hilo la kishujaa kati ya wema na uovu, kati ya Kristo na Shetani,sasa limekoma, na Kristo anatawala. Pazia linayafunika matokeo yadhambi ya zamani yaliyofuatia, kasha linafunuliwa ili kuuonyeshaulimwengu mpya wenye utukufu usiokuwa na kikomo.

8.Dunia Inatakaswa Na Yafanywa Upya
Kutoka katika majivu yale ya maangamizi makuu ya mwisho, Munguataiumba dunia mpya:
“Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu zakwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita… Nami nikauona mji ulemtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu..”Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye fanyamaskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungumwenyewe atakuwa pamoja nao. Naye atafuta kila chozi katika machoyao, wala mauti haitakuwapo tena, wala maombolezo, wala kilio, walamaumivu, hayatakuwapo tena kwa kuwa mambo ya kwanzayamekwisha kupita… Tazama, nayafanya yote kuwa mapya” – (Ufunuo21:1-5).
Itakapokuwa imerudishwa katika uzuri wakewa awali, dunia hii itakuwa makao yawaliokombolewa milele hata milele. Ikiishakukombolewa mbali na choyo, magonjwa, namaumivu, tutayachunguza na malimwenguyote na tutakuwa na uhusiano wa ajabu nakuukuza, na umilele wa kuketi miguuni pakeYesu na kusikiliza, kujifunza, na kupenda.(Kwa maelezo kamili ya dunia mpya,ukipenda waweza kusoma tena Mwongozo 9.)
Je! wewe unapanga kuwa wapi siku hiyo? Je!umeamua kuwa pamoja na Kristo ndani ya mji ule na kuokolewa milele? Auutakuwa nje ya ule mji bila Kristo na kupotea milele?


Kama wewe umeyakabidhi maisha yako mikononi mwake Yesu, basi, hunahaja ya kuionja ile hofu isiyoneneka ya wale walio nje ya mji ambaowanatambua kwamba wamepotea milele. Haidhuru maisha yakuletee kitugani, kama wewe unayaweka maisha yako mikononi mwake Yesu hivi sasa,basi, unaweza kuwa ndani ya mji ule pamoja na Kristo na pamoja na walewaliokombolewa. Endapo wewe hujafanya hivyo, basi mpe Yesu moyowako sasa, naye atakuzungushia upendo wake na msamaha. Hii ni nafasiyako ya pekee. Hii ndiyo siku yako ya wokovu kwako.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top
MKUSDA CHURCH