MKUSDA CHURCH
Unity in Worship

19. KUINGIA KATIKA MAISHA YA KIKRISTO

KUINGIA KATIKA MAISHA YA KIKRISTO
Hapa ni barua ya kusisimua sana toka kwa mmojawapo wa wawakilishi waShule yetu ya Biblia katika Afrik.
” Miaka mitano iliyopita nilipokea ombi tokakwa sauti ya Unabii ili nimtembeleemfungwa mmoja ambaye alikuwamwanafunzi wa Shule ya Biblia kwa Posta.Nilionyesha ombi lile kwa wakuu wa gerezalile ambao kwa hisani yao walinipa ruhusa.Kwa kuwa mwanafunzi yule alikuwa nahamu kubwa sana ya kujifunza Biblia, basi,nilimtembelea mara kwa mara.
“Karibu miezi sita baada ya kumtembeleamara ya kwanza, aliomba kubatizwa nakujiunga na kanisa. Wakuu wale walikubalikuandaa mahali ili ubatizo ule ufanyike ndaniya gereza lile. Wasimamizi wao pamoja nawafungwa wengine walikusanyika palekushuhudia ubatizo ule niliopata kuufanyaambao uliigusa mioyo yao.
“Muda mfupi baada ya tukio lile, ndugu yetu yule alifunguliwa tokakifungoni, ingawa bado alikuwa na muda mrefu wa kutosha kutumikiakifungo chake. Nilipouliza imekuwaje, niliambiwa kwamba maisha yakeyalikuwa yamebadilika kabisa, naye akawa shahidi aliyemshuhudiaMwokozi wake, na dini yake hata hakuweza tena kufikiriwa kama mfungwawala kutendewa kama mfungwa. Mtu yule akaungana na familia yake nasasa ni kiongozi katika mojawapo ya makanisa yenye watu wengi.”


1.Ubatizo Maana Yake Nini?
Mfungwa yule alipogeuka na kuwaMkristo na maisha yakeyalipobadilika kabisa, kwa niniilikuwa ni lazima kwake kubatizwa?Katika mazungumzo yake naNikodemo, Yesu anaonyeshaumuhimu na maana ya huo ubatizo:
“Hakuna mtu ye yote awezayekuuona ufalme wa Munguasipozaliwa kwa maji na kwaRoho” – Yohana 3:3,5.
Basi kulingana na Yesu ni lazima sisi tuzaliwe ” kwa maji na kwa Roho.”Katika maisha mapya kupitia katika badiliko la mawazo na moyo. Kwa kuwakuingia katika ufalme wa Mungu kunataka maisha mapya kabisa, si yalemaisha ya zamani yaliyotiwa viraka, ndiyo maana yanaitwa kuzaliwa upya.Ubatizo wa maji ni ishara ya nje inayoonyesha badiliko hilo la ndani.Mwakilishi wetu alimbatiza yule mfungwa kama ishara ya kutambua kujitoakwake kwa Kristo na ishara ya badiliko kamili ambalo Roho Mtakatifualikuwa ameanza kufanya katika tabia yake.


2.Kwa Nini Mimi Nibatizwe?
Wokovu wetu unayazunguka matendo makuu matatu ya Kristo.
“Kristo ALIKUFA kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo Maandiko,… ALIZIKWA, … ALIFUFUKA siku ya tatu, kama yanenavyo Maandiko”-(1 Wakorintho 15:3,4).
Kristo alifanya wokovu huo uwezekane kwa njia ya kifo chake, kuzikwakwake, na kufufuka kwake.
“Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo YesuTULIBATIZWA KATIKA MAUTI YAKE? Basi TULIZIKWA PAMOJA NAYEKWA NJIA YA UBATIZO katika mauti yake, kusudi KAMA KRISTOALIVYOFUFUKA KATIKA WAFU kwa njia ya utukufu wa Baba, VIVYOHIVYO NA SISI TUPATE KUISHI MAISHA MAPYA.” – Warumi 6:3,4.
Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, alizikwa, kisha alifufuka katika kaburiili kutupa sisi maisha mapya ya haki. Kwa kubatizwa sisi tunashiriki kabisakatika kifo, kuzikwa, na kufufuka kwake Yesu. Ubatizo una- maanishakwamba sisi tumeifia dhambi pamoja na Kristo, kisha tunafufuka na ” Kuishimaisha mapya” ndani ya Kristo. Kifo chake Kristo ufufuo wake huwa ni Kifochetu na ufufuo wetu. Mungu anaweza kutufanya sisi kuwa hai katikamambo yale ya Roho kana kwamba sisi tulikuwa tumefufuliwa katika wafu.Tendo la kimwili la ubatizo kwa picha huwakilisha hatua za kuongoka.
Kwanza, tunaingizwa ndani ya maji, yaani,tunazamishwa majini kabisa, sawasawa tu nawatu ambao wamekufa wanavyoshushwakaburini na kufunikwa na udongo. Hii nikusema kwamba sisi tunapenda kufa pamojana Kristo na kuyazika maisha yetu yale yazamani. Ubatizo ni mazishi (maziko), nikuyaaga rasmi maisha yale ambayoyalitawaliwa sana na dhambi. Halafu,tunanyanyuliwa juu kutoka ndani ya maji nayule anayebatiza, sawasawa tu na mtuanayefufuliwa kutoka kaburini. Hii ni kusemakwamba sisi ni ” [vi]umbe vipya” tumejitoa kabisa kuishi hayo maishamapya anayotupa Mungu.
Ni kuzamishwa ndani ya maji peke yake kunakoweza kuonyesha kielezosahihi cha maana halisi ya ubatizo – yaani, kifo, kuzikwa na kuzaliwa upya.”Ubatizo” kwa njia ya kunyunyiza maji kidogo kichwani hauonyeshi kwautoshelevu mfano huo wa kuzaliwa upya.


Je! Kufa pamoja na Kristo maana yake ni nini hasa?
“Tukijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulubishwa pamojanaye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena” – (Warumi6:6)
Ubatizo unawakilisha kwa nje kile anachopaswa mtu kufanya ndani yake:yaani, kusalimisha kila kitu kwa Kristo. Tukizuia kitu chochote kwa Mungu,huenda tutaendelea kuwa ” Watumwa wa dhambi” Tunapojisalimishakabisa kwa Kristo, tamaa zetu za dhambi zinafanywa kuwa bila nguvuyoyote na badiliko kamili linaanza kutokea.
Je! Ni nani ahusikaye na mabadiliko yanayotokea?
Nimesulubiwa pamoja na Kristo wala mimi si hai tena, lakini KRISTOANAISHI NDANI YANGU. Na maisha haya ninayoishi katika mwili huu,NAISHI KWA KUMWAMINI MWANA WA MUNGU, aliyenipenda nakujitoa nafsi yake kwa ajili yangu” – (Wagalatia 2:20).
Ninapojifananisha na kusulibiwa kwake Kristo kwa njia hiyo ya ubatizonakaribisha uwezo wenye nguvu nyingi katika maisha yangu – yaani, “Kristo anaishi ndani yangu”. Ili upate kuyaweka maisha yako mikononi mwaKristo kabisa kwanza huna budi kumtazama Kristo akifa pale msalabani.Usiiangalie ile dhambi inayokutishia wewe, usiingalie kumbukumbu yako yazamani na kuomboleza mtazame Yesu. Kukitazama kifo chake Kristokilichojaa neema na ujasiri pale Kalvari, unaweza kuonyesha mshikamano wako ulio nao pamoja naye, kwa maneno haya: ” Kwa nguvu ya msalabanadai kwamba mimi ni mfu kwa zile tabia zangu za zamani, na Mungu.Naamua kusimama pamoja na Kristo. Kuanzia sasa na kuendelea miminita”ishi kwa kumwamwini aliyenipenda na kujitoa nafsi yake kwa ajiliyangu”
Tunapoichota ile nguvu itokanayo na kifo na ufufuo wake Kristo, tunazionasifa za tabia yake zikijitokeza zaidi na zaidi na kuchukua mahali pa tabiazetu zile za zamani:
“Mtu awaye yote akiwa NDANI YA KRISTO, amekuwa KIUMBE KIPYA:ya Kale yametoweka, MAPYA yamekuja!” – (2 Wakorintho 5:17).


Kwa njia hiyo ubatizo sisi tunaonyesha tamaa yetu tuliyonayo ya kushikanamikono na Yesu na kuishi hayo maisha mapya yaliyo bora tukiwa ndani yaKristo” Yesu anafanya ndani yetu kile ambacho sisi tusingeweza kamwekujifanyia wenyewe. Tunapanda kutoka ndani ya maji tukiwa ” [vi]umbe[vi]pya” anatupa uwezo wa kuishi hayo “maisha mapya”.


3.Hivi Kwa Nini Yesu Alibatizwa?
Wakati ule wa Pentekoste, Petro aliwaambia wale waliotaka kuwekwa hurumbali na dhambi kwamba wanapaswa kutubu na kubatizwa ili Kristo awezekuwasamehe “dhambi zenu” (Matendo 2:38) Kwa kuwa Yesu hakutendakamwe dhambi hata moja, basi kwa nini alijiachia mwenyewe kubatizwa?
“Wakati huo YESU AKAJA kutokaGalilaya MPAKA YORDAN ILI ABATIZWEna Yohana … KUITIMIZA HAKI YOTE” -Mathayo 3:13,15.


Yesu alikuwa hana dhambi. Hakuwa nahaja ya kutubu dhambi yoyote. Alibatizwakutokana na sababu nyingine: “Kutimizahaki yote” kwa kubatizwa kwake, Yesualitoa kielelezo chenye nguvu kwa ajili yetusisi wanadamu dhaifu na wenye dhambi.Kristo kamwe hawaombi wafuasi wakekwenda mahali kokote ambako yeyehajapata kufika. Kwa hiyo wauminiwanapozamishwa ndani ya maji ya ubatizo,wanafuata nyayo za bwana wao.
Kwa vile Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, anaweza kutupa sisi hakiyake.
Mungu alimfanya yeye asiyekuwa na dhambi kuwa dhambi kwa ajiliyetu, ili ndani yake sisi tupate kuwa haki ya Mungu” 2 Wakorintho5:21.
Tukiwa tumebadilishwa kabisa kutoka katika hali yetu ya kuwa wenyedhambi na kuwa watakatifu machoni pake Mungu, tunakuwa ndani ya ile”haki” na kwa njia hiyo tunaishi maisha mapya ndani ya Kristo.


4.Kwa Nini Nizamishwe Ndani Ya Maji?
Kristo alizamishwa ndani ya maji wakati wa ubatizo wake. Hakunyunyiziwamaji kidogo kichwani. Yohana alimbatiza ndani ya mto wa Yordani “kwasababu huko kulikuwa na MAJI TELE” (Yohana 3:23) Yesu alipobatizwaalikwenda na kuingia ndani ya maji, kisha “mara tu Yesu alipokwishakubatizwa [alipokwisha kuzamishwa , Kigiriki] AKAPANDA KUTOKA NDANIYA MAJI” (Mathayo 3:16)
Tunapoielewa maana halisi ya ubatizo, hatuna shida sana kuutambuamfumo sahihi wa ubatizo. Neno lenyewe hasa la “ubatizo”linatokana naneno la Kigiriki baptizo ” ambalo linamaanisha kuchovya au kuzamisha,kuweka chini ya).

Wakati wa ziara yake moja John Wesley kule Amerika katika mwaka wa1737, baraza la wazee wa mahakama ya kanisa wapatao wanaume 34walimhukumu yeye kwa shtaka la ajabu la “kukataa kumbatiza mtoto waBwana Parker, isipokuwa kwa njia ya kumzamisha ndani ya maji.” Ni dhahirikwamba baba huyo wa Kimethodisti aliwabatiza waongofu wake kwakuwazamisha ndani ya maji.
Mwanamatengenezo ya kanisa John Calvinalieleza hivi: “Ni jambo la hakika ya kwambakuzamisha majini ilikuwa ndiyo desturi yaKanisa lile la kale” – Institute of the ChristianReligion, Kitabu cha 4, Sura ya 15, Sehemu ya19.
Historia ya kanisa lile la kwanza inadhahirishakwamba ubatizo ulimaanisha kuzamishwandani ya maji.
Mkuu wa makasisi Stanley, wa Kanisa laAnglikana, aliandika maneno haya: “Kwa karnekumi na tatu za mwanzo, desturi ya ubatizoiliyoenea sana mahali pote ilikuwa ni ile tuisomayo katika Agano Jipya, naambayo ndiyo
maana halisi ya neno “batiza” – kwamba wale waliobatizwa walitumbukizwa,yaani walifunikwa kabisa na maji, walizamishwa ndani ya maji” – ChristianInstitutions, Uk. 21
Mashimo ya kubatizia ndani ya maji yanaonekana katika makanisa mengiyaliyojengwa kati ya karne ya nne na karne ya kumi na nne kule Ulaya naAsia, makanisa kama vile kanisa Kuu la Pisa, Italiana la Mtakatifu Yohana,kanisa kubwa kuliko yote mjini Roma.
Kanisa Katoliki halikuukubali ubatizo wa kunyunyizia maji kichwani kuwa niwa halali kama ule wa kuzamishwa majini mpaka lilipokaa Baraza laRavena mapema katika karne ile ya kumi na tano. Katika masuala yaleyanayohusu desturi za kanisa, hatutakiwi kufuata kile anachofundishamwanadamu, bali kile ambacho Kristo na mitume wake wanafundisha.
Wakristo wengi waliowanyofu wa moyo wanayapenda sana yale mapokeoyahusuyo ubatizo wa watoto wachanga, na kule kuwatoa watoto wetu kwaMungu kuanzia mwanzo kabisa wa maisha yao ni jambo linalopendezahakika. Walakini, Biblia inaeleza wazi ya kwamba ni lazima mtu afundishweile njia ya wokovu kabla ya ubatizo wake (Mathayo 28:19,20) kwamba nilazima mtu amwamini Yesu kabla ya kubatizwa (Matendo 8:35-38) na yakwamba ni lazima mtu atubu dhambi zake na kusamehewa kabla yakubatizwa (Matendo 2:38) Mtoto mchanga hana uwezo kabisa wa kuamini,kutubu au kuungama dhambi zake, mambo ambayo ni lazima yatanguliekabla ya ubatizo.


5.Kwa Nini Ni Muhimu Kubatizwa?
Kulingana na Yesu, ubatizo ni wa lazima kwa wale wanaotaka kuingiambinguni.
“Hakuna mtu ye yote awezaye kuingia katika ufalme wa Munguasipozaliwa kwa maji na kwa Roho”- Yohana 3:5.
Yesu anatoa walakini mmoja tu. Yule mwizi pale msalabani ali”zaliwa kwaRoho” ingawa kwake ilikuwa haiwezekani kabisa hata kuondoka tu palemsalabani na kwenda kuzamishwa ndani ya maji kama ishara ya badilikolake la moyo. Naye Yesu alimwahidi kwamba angekuwa pamoja naye[Kristo] katika ufalme wake (Luka 23:42,43) Kwa yule mwizi, kuzaliwa kwamaji na kwa Roho” kuliwakilishwa na damu ya Yesu iliyomwagika palekumtakasa dhambi zake. Agostino (Augustine) alichunguza na kusema”Kuna tukio moja la toba ya mtu mmoja aliyekuwa akifa kitandani pakeambalo limewekwa katika kumbukumbu, yaani lile la mwizi yule aliyetubu, iliasiwepo mtu hata mmoja wa kukata tamaa, naye alikuwa ni yule mmoja tuili asiwepo hata mmoja anayethubutu kufanya hivyo”

Yesu mwenyewe alitoa onyo hili zito:
Aaminiye na kubatizwa ataokoka,asiyeamini [na kwa sababu hiyohabatizwi]atahukumiwa ” – Marko16:16
Alipokuja badala yetu pale KalwariYesu alionyesha mbele yawanadamu wote upendo wakealionao kwetu sisi. Tunahitaji kuitikiakwa kufanya ungamo letu bila hayambele ya watu kuhusu kujitoa kwetukwa Kristo kwa njia ya ubatizo. Je! Hivi wewe umeanza maisha hayomapya ndani ya Kristo? Je! Umebatizwa ? Kama sivyo kwa nini weweusijiandae kwa ubatizo katika siku za karibuni?


6.Ubatizo Ni Mwanzo Tu
Ubatizo unawakilisha kujitoa kwetu ili tupate kuishi mtindo wa maisha yaKikristo. Lakini kule kujisalimisha kwetu wakati wa ubatizo hakujiendeshikwenyewe kama mashine katika kipindi chote cha maisha yetu.
Mtoto anapozaliwa, kufanyasherehe ni sawa. Baada yasiku ya kuzaliwa kupita namsisimko kupungua, yule mtotomchanga anahitaji kulishwa kilasiku, kuogeshwa kila siku, nakuwa makini kila siku kuangaliaafya yake.
Ni sawasawa na ubatizo. Pauloalisema hivi kuhusu uzoefuwake wa maisha “Ninakufa kilasiku” (1 Wakorontho 15:31)Kwa kubadilika kila siku nakuachana na ubinafsi wetu,tunakuwa wepesi kuvutwa na zaidi kwa Kristo.
Taratibu ya ibada ya ubatizo, kama sherehe ya kufungisha ndoa,ilikusudiwa kuwa uthibitisho rasmi uonyeshao kwamba uhusiano wa ajabuambao unakuwa umekwisha kuanza. Ili kuweza kukua daima tunahitajikujitoa sisi wenyewe kila siku kwa Kristo kupokea kila siku maisha hayomapya kwa njia ya maombi na kujifunza Biblia.
7.Sababu Ya Kushangilia
Ubatizo ni sababu iletayo kushangilia sana kwa sababu walewanaomwamini Kristo wanayo ahadi ya uzima wa milele. Yeyote aaminyena kubatizwa ataokoka (Marko 16:16) Tunapokwisha kubatizwa tunaingiakatika njia ile iendayo juu ambayo inatupeleka kwenye ile furaha ya milele.
Ubatizo pia unasherehekea furaha yetu tuliyo nayo sasa pamoja na Kristo.Anaahidi kuwapa zawadi ya thamani kubwa mno ya Roho Mtakatifu walewaliobatizwa (Matendo 2:38) Pamoja na huyo Roho huja lile “tunda laRoho” – yaani upendo ambao unayajaza maisha yao na “uvumilivu,utuwema, fadhili, uaminifu, upole na kujitawala nafsi” (Wagalatia 5:22,23)
Kuwa na Yesu anayeishi ndani yetu kwa njia ya Roho Mtakatifu hutupa sisihisia kubwa sana ya kuwa na hakika. Kwa maana ” Roho Mwenyewehushuhudia … ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu” (Warumi 8:15,16)
Uhusiano huo imara pamoja na Mungu unatuletea manufaa mengi, lakinihautoi dhamana kwetu ya kutupatia maisha yasiyokuwa na matatizoyoyote.
Kwa kweli, adui yetu mara nyingi anajitahidi sana kuwatupia shida nyingisana wale waliokwisha kujitoa sasa kwa Kristo. Walakini tunapokuwa
mikononi mwake Mungu tunaweza kujua kwamba atatumia kila jambolinalotupata sisi, liwe jema au baya, ili kutufundisha na kutusaidia kukua

(angalia Warumi 8:28)
Mwanamke mmoja kijana alikata shauri kutoa maisha yake kwa Kristo nakubatizwa licha ya vitisho vya kumpa talaka toka kwa mume wake. Yeyehakutaka sehemu yoyote ya imani yake ile mpya lakini mwanamke yuleakamng’ang’ania Yesu na kujitahidi kuwa mwenye upendo kulikoalivyokuwa kabla yake. Kwa kipindi fulani yule mume alifanya mambo kuwamagumu mle nyumbani. Lakini hatimaye alishawishiwa kwenda upande wamkewe kutokana na hoja aliyoshindwa kuijibu: yaani, maisha ya mkeweyaliyobadilika kabisa. Mtu huyo akasalimisha maisha yake kwa Kristo, nayeakabatizwa pia.
Kule kung’ang’ania kwetu kusimama karibu na Kristo “kwa heri na kwashari” [katika hali iwayo yote ile] kutatufanya kuwa vyombo vyenye nguvunyingi mikononi mwake. Tunaweza kumkabidhi maisha yetu bila mashartiyoyote kwa sababu yeye kimsingi tayari amekwisha kujitoa kwetu alipolipafidia kwa ajili ya dhambi zetu pale msalabani. Ni heshima kubwa iliyojetuliyopewa sisi kuweza kumpa upendo na utii wetu mbele ya watu! Endapowewe bado hujafanya hivyo, kwa nini usisalimishe maisha yako kwa Kristosasa hivi. Mwombe yeye akupe maisha mapya ndani yako kwa njia yaRoho wake Mtakatifu halafu batizwa na kuingia ndani ya Kristo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top
MKUSDA CHURCH