Siku moja Jimi alimwuliza mtu mmoja anayekana kuwa kuna Munguendapo alipata kujaribu sana, hata kwa dakika chache tu, kupigana nawazo lisemalo kwamba huenda Mungu yuko.
“Sawa kabisa!” mkana Munguyule akajibu, akimwacha Jimina mshangao. “Miaka mingiiliyopita, mimi nilikuwa karibusana nigeuke na kuwa mtuanayemwamini Mungu.Nilipokiangalia kile kiumbekidogo sana – lakini – kikamilifukatika kitanda chake kidogo,nilipochungulia na kuvionavidole vile vidogo fahamu zakwanza za kutambua, nilipitakatika kipindi cha miezi kadhaaambayo katika hiyo miminilikuwa karibu kabisa niache kuwa mkana Mungu. Kule kumwangaliamtoto yule kulikuwa kumenishawishi karibu kabisa kuwa hapana budiMungu alikuwa yuko.”
1.Kila Kitu Kilichobuniwa Kina Mbunifu Wake
Muundo wa mwili wa kibinadamu unafanya iwepo haja ya kuwako mbunifuwake. Wanasayansi wanatuambia kwamba ubongo wetu hukusanya nakukumbuka picha elfu nyingi katika mawazo yetu, huyaunganisha matatizoyetu yote na kuyatatua, hufurahia kuona uzuri, huitambua nafasi ya mtu, nakutaka kukuza yaliyo bora ndani ya kila mtu. Chaji za umeme zitokazokatika ubongo huongoza shughuli zote za misuli ya miili yetu.
Kompyuta pia zinafanya kazi kwa njia ya mikondo ya umeme. Lakiniilichukua akili ya mwanadamu katika kuitengeneza hiyo kompyuta nakuiambia la kufanya.
Si ajabu, basi, kwamba mtunzi wa Zaburi alihitimisha kwa kusema kwambamwili wa mwanadamu unasimulia habari za Muumbaji huyo wa ajabu kwasauti kubwa iliyo wazi:
“Nakusifu maana nimefanywa kwa namna ya ajabu, matendo yako niya ajabu, wewe wanijua kabisa kabisa” – (Zaburi 139:14)
Hatuna haja ya kwenda mbali ili kuyaona hayo “matendo” ya Mungu. Umbola ubongo wetu wenye sehemu nyingi za ajabu na viungo vyetu vingine ni”matendo” ya Mungu, nayo husonda kidole chake kwa yule mbunifu stadikabisa.
Hakuna pampu yoyote iliyotengenezwa na mwanadamu inayowezakulinganishwa na moyo wa mwanadamu. Hakuna mtandao wo wote wakompyuta uwezao kuwa sawa na mfumo wetu wa mishipa ya fahamu.Hakuna mfumo wo wote wa Televisheni unaofanya kazi yake vizuri kamasauti, sikio, na jicho la mwanadamu. Hakuna kiyoyozi kikuu cho chote(central air conditioning) wala mfumo wa kuipasha joto nyumba uwezaokushindana na kazi inayofanywa na pua, mapafu, na ngozi yetu. Mfumowenye sehemu nyingi za ajabu wa mwili wa mwanadamu unadokezakwamba mtu fulani alihusika katika kuubuni, na Mtu huyo fulani ni Mungu.
Mwili wa mwanadamu ni mfumo kamili wa viungombali mbali – vyote vikiwa vinashirikiana, vyote vikiwavimeumbwa kikamifu. Mapafu na moyo, mishipa yafahamu na misuli, hiyo yote hufanya kazi za ajabumno kiasi cha kuwa vigumu kusadikika ambazohutegemezwa juu ya kazi nyingine zilizo za ajabu mnokiasi cha kutufanya sisi tushindwe kusadiki.
Endapo ungetakiwa kuzipa nambari sarafu kumikuanzia moja mpaka kumi, na kuziweka mfukonimwako, na kuzitikisa-tikisa huku na huku, kishakuzitoa mfukoni mwako na kuziweka tena mfukonimoja moja, je, kuna uwezekano gani kwambaungefanya hivyo kwa kufuata mfuatano wa nambarizake sawa sawa? Kwa sheria ya mahesabu unayobahati moja tu katika bilioni kumi ya kuzitoa kwampangilio wake kuanzia ya kwanza mpaka ile yakumi.
Sasa, basi, hebu fikiria ni bahati ngapi tumbo lachakula, ubongo, moyo, ini, arteri, vena, figo, masikio,macho, na meno vingekuwa nazo vikikua vyotepamoja na kuanza kufanya kazi yao kwa dakika ile ileya wakati mmoja.
Hivi maelezo ya busara kabisa ni yapi kuhusu ubunifu huo wa mwili wamwanadamu?
“Kisha Mungu akasema, ‘Natumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa surayetu,’…………..
Hivyo Mungu Akamwuumba Mtu Kwa Mfano Wake,……mwanamume na mwanamke aliwaumba” – (Mwanzo 1:26,27).
Mwanaume na mwanamke wa kwanza wasingeweza kuwa wametokeawenyewe tu. Biblia inathibisha kwamba Mungu alitubuni sisi kwa mfanowake. Alituwaza katika mawazo yake na kutuumba.
2.Kila Kitu Kilichoumbwa Kina Muumbaji Wake
Lakini ushahidi wa kuwako kwake Mungu haufungamani tu na ubunifu wamiili yetu; pia umetandaa huko mbinguni. Acha taa za mjini, angalia juukatika mbingu ya usiku. Wingu lile jeupe kama maziwa lenye nyota,tunaloliita Mkanda wa Nuru (Milky Way) ambalo kwa kweli ni kundi lamabilioni ya majua (galaxy) yanayotoa mwanga mkali wa moto sawa na ulewa jua letu ambao unaweza kuonekana hapa duniani kwa kupitia katikadarubini kubwa zilizopo hapa duniani kama ile darubini iitwayo “HubbleTelescope” iliyo katika anga za juu.
Si ajabu, basi, kwamba mtunga Zaburi alihitimisha kwa kusema kwambanyota zinamtangaza Muumbaji Mtukufu:
“Mbingu zatangaza utukufu wa Mungu, anga ladhihirisha kazi yamikono yake” (Zaburi 19:1-3).
Je, hivi sisi twaweza kutoa hitimisho gani la busara kwa kuangaliampangilio huo unaotatanisha sana na ukubwa wa malimwengu yote?
“Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi” (Mwanzo 1:1).
“Yeye [Mungu] alikuwako kabla ya vitu vyote; vyote hudumu mahalipale kwa uwezo wake” (Wakolosai 1:17).
Viumbe vyote humshuhudia yule Mungu Mbunifu Mkuu na Muumbaji asiyena Mwisho. Katika maneno haya rahisi, “Hapo mwanzo Mungu,” tunalipatajibu la siri ile ya uhai. Yuko Mungu aliyeumba kila kitu.
Wanasayansi wakuu wengi siku hizi wanamwamini Mungu. Dk. ArthurCompton, mwanafizikia mshindi wa tuzo ya Nobel, akitoa maoni yake juu yafungu hilo la Maandiko, siku moja alisema hivi:
“Kwangu binafsi, imani huanza ninapotambua kwamba yule aliye na akili isiyo na kifani ndiye aliyeyaweka hayomalimwengu na kumwumba mwanadamu.Kwangu mimi si vigumu kuwa na imani hii,kwa maana ni dhahiri kwamba po pote palepalipo na mpango yupo Mungu mwenyeakili. Malimwengu yaendayo kwa utaratibu,na kujifunua kwetu hushuhudia ukweli wausemi huu adimu mno uliopata kunenwa -‘Hapo mwanzo Mungu'”
Biblia haijaribu kumthibitisha Munguinatangaza kuwako kwake. Dk. ArthurConklin, mwana biolojia, siku mojaaliandika hivi: “uwezekano kwa uhaikutokea kwa ajali ni sawa na uwezekanokwa kamusi kamili kutokea kutokana namlipuko katika kiwanda cha kuchapishavitabu”.
Twajua kwamba wanadamu hawawezikutengeneza kitu cho chote bila kutumiakitu kingine. Twaweza kujenga vitu,kuvumbua vitu, kuunganisha vitu, lakini kamwe hatujapata kufanya kitu chochote bila kuwa na kitu kingine cha kuanzia, awe ni chura mdogo kabisa uala kawaida kabisa. Vitu vituzungukavyo pande zote hupiga kelele vikisemaMungu ndiye aliyevibuni, Mungu ndiye aliyeviumba, Mungu ndiyeanayevitegemeza. Jibu pekee linaloaminika kuhusu chimbuko lamalimwengu hayo, dunia hii, na wanadamu – ni Mungu.
3.Mungu Huingia Katika Mahusiano Na Watu Binafsi
Mungu yule aliyezibuni mbingu hizo na nyota, aliyeyaumba malimwenguhayo, anatafuta kuwa na uhusiano nasi binafsi. Alikuwa na uhusiano wakebinafsi na Musa: “Bwana akasema na Musa….kama vile mtu asemavyo narafiki yake” (Kutoka 33:11). Mungu Mwenyewe anataka kuingia katikauhusiano nawe na kuwa Rafiki yako. Yesu aliwaahidi wale wanaomfuata,akisema “Ninyi mmekuwa rafiki zangu” (Yohana 15:14).
Sisi sote tumeshughulika sana na wazo hilo la Mungu, kwa kuwawanadamu kwa asili wanapenda dini. Hakuna mnyama yeyote ajengayemadhabahu kwa ajili ya ibada. Lakini kila mahali unapowakuta wanaume nawanawake, unawakuta wakiabudu. Ndani ya kila moyo wa mwanadamukuna ufahamu kuwa Mungu yuko, tamaa ya kuwa rafiki wa Mungu.Tunapoitikia hiyo tamaa yetu na kumpata Mungu, hatuwi na mashaka tenajuu ya kuwako kwake na hitaji letu.
Katika miaka ile ya 1990 mamilioni ya wanaomkana Mungu katika nchi yaUrusi waliachana na imani yao hiyo ya kumkana Mungu, kishawakamgeukia Mungu. Profesa wa Chuo Kikuu cha St. Petersburg alitoakauli yake inayofanana na maoni yaliyotolewa na wakana Mungu wengikatika Umoja wa Kisovieti iliyopita:
“Nimetafuta maana ya maisha katika utafiti wangu wa kisayansi, lakinisikuona kitu chochote cha kutegemea. Wanasayansi wanaonizunguka mimiwanazo hisia hizo hizo za ukiwa. Nilipoangalia ukubwa wa malimwengukatika somo langu la elimu ya nyota, kisha nikaangalia ukiwa uliomomoyoni mwangu, niliona kwamba ni lazima pawe na maana fulani. Kishanilipoipokea Biblia uliyonipa na kuanza kuisoma, ukiwa katika maishayangu ukajazwa. Nimeiona Biblia kuwa ndiyo chimbuko la pekee lamatumaini kwa nafsi yangu. Nimempokea Yesu kama Mwokozi wangu,nami nimepata amani ya kweli pamoja na kuridhika katika maisha yangu”.
Mkristo anamwamini Mungu kwa sababu yeye amekutana naye nakugundua kwamba anayatosheleza mahitaji makubwa sana ya moyo wake.Mungu ambaye Wakristo wamemuona kuwa yuko, anatupatia mtazamompya, maana mpya, makusudi mapya na furaha mpya.
Mungu hatuahidi sisi kwamba tutakuwa na maisha yasiyo na taabu, walamapambano, ila yeye anatuhakikishia kwamba atatuongoza na kutusaidiakama tutakuwa na uhusiano binafsi naye. Na mamilioni ya Wakristo wanaweza kutoa ushuhuda wao kwamba ingekuwa heri kwao kuacha kilakitu kuliko kuyarudia maisha yale yasiyokuwa na Mungu.
Hii ndiyo ajabu kuu kuliko zote kwamba yule Mungu Mwenyezi aliyeyabuni,aliyeyaumba na kuyategemeza malimwengu hayo anataka kufanyauhusiano na kila mwanaume na mwanamke, kila mvulana na msichana.Daudi alishangaa sana kuhusu jambo hilo alipoandika maneno haya:
“Nikiangalia mbingu, kazi yavidole vyako, mwezi na nyotaulizozimika huko, mtu ni nini eeMungu hata umfikiriemwanadamu ni nini hata umjali?”-(Zaburi 8:3,4).
Muumbaji wetu ana “mjali” kilammoja wetu. Yeye binafsianakupenda sana wewe kanakwamba wewe ulikuwa ni kiumbechake cha pekee alichokiumba.
Basi tunaweza kumwamini Mungu:
(1)Kwa sababu ya ubunifu wake wenye sehemu nyingi katika kila kitualichokiumba ambacho kinatuzunguka sisi.
(2)Kwa sababu shauku ile iliyomo ndani yetu juu ya Mungu inatufanyatusiwe na raha mpaka tupatapo pumziko letu ndani yake tena.
(3)Kwa sababu tunapomtafuta na kumpata, Mungu hutosheleza kila hajatuliyo nayo pamoja na shauku yetu – kikamilifu!
4.Ni Mungu Wa Aina Gani?
Ni jambo la busara tu kwamba Mungu aliye na nafsi yake apende kujifunuamwenyewe kwa viumbe wake kama vile baba atakavyo watoto wakewamjue. Na katika Biblia Mungu anatuambia yeye ni nani, tenaanafananaje.
Ni mfano gani alioutumia Mungu katika kuwaumba wanaume nawanawake?
“Hivyo Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungualimwumba” (Mwanzo 1:27).
Kwa kuwa sisi tumeumbwa kwa mfano wa Mungu, basi, uwezo wetu wakufikiri na kujisikia, kukumbuka na kutumaini, kutafakari na kuchambuamambo – chimbuko lake lote latoka kwake. Je, tabia kuu ya Mungu ni ipi?
“Mungu ni upendo” (1 Yohana 4:8).
Mungu hufanya uhusiano wake na wanadamu kutokana na moyo wake waupendo. Hakuna kitu cho chote alichofanya au atakachopata kufanyaambacho hakijasababishwa na upendo wake usio na ubinafsi, ujitoaomhanga.
5.Jinsi Yesu Anavyotufunulia Alivyo Mungu
Katika Biblia Mungu anarudia tena na tena kueleza habari zake Mwenyewekwamba Yeye ni Baba.
“Je! Sisi sote si watoto wa baba mmoja”?
“Je, sisi sote hatukuumbwa na Mungu yule yule?” Malaki 2:10.
Baadhi ya mababa tuwaonao leo si cho chote, bali hawapendezi. Kunamababa wasiojali, mababa wanaotukana matusi. Mungu si kama hao. Yeyeanajali, ni Baba anayeguswa sana na mambo yetu. Ni Baba apendayekucheza na mwanawe au binti yake, ni Baba anayewafurahisha sanawatoto wake kwa kuwasimulia hadithi kabla hawajaenda kulala usiku.
Baba yetu huyo mwenye upendo alitaka kufanya zaidi ya kule kujifunuaMwenyewe kwa njia ya maneno ya Maandiko. Alijua kwamba yule mtu tunayeishi naye ni mtu halisi kuliko yule tunayesikia tu habari zake autunayesoma habari zake. Kwa hiyo yeye akaja katika dunia yetu kama mtuhalisi – yaani, yule mtu Yesu.
“Kristo mfano wa Munguasiyeonekana” – (Wakolosai 1:15).
Basi kama wewe umemwona Yesu,utakuwa umemwona Mungu.Alijishusha hadhi yake na kuwa sawasawa na sisi akawa kama sisi – ili apatekutufundisha jinsi ya kuishi na kuwa nafuraha, ili kwamba sisi tupate kuonajinsi Mungu alivyo hasa. Yesu ni Mungualiyeonekana kwa macho. Yeyemwenyewe alisema, “Aliyeniona mimiamemwona Baba” (Yohana 14:9).
Usomapo kisa cha Yesu katika vitabuvinne vya Injili, yaani, vitabu vinne vyakwanza vya Agano Jipya, utagunduapicha ya kuvutia sana ya Baba yetualiye mbinguni. Wavuvi wale wakawaida tu walizitupa nyavu zao ilikumfuata Yesu, na watoto wadogowakasongamana kwenda kwakekupokea baraka zake. Aliweza,kumfariji mwenye dhambi aliyeharibika kabisa na kuzivunja nguvu zamnafiki sugu aliyejihesabia haki yeye mwenyewe. Aliponya kila maradhikuanzia upofu hadi ukoma. Katika matendo yake yote Yesu alidhihirishakwamba Mungu ni upendo! Alikidhi haja ya mwanadamu kwa namnaambayo hakuna mtu ye yote aliyepata kufanya hivyo kabla yake au tanguwakati wake!
Ufunuo wa Yesu wa mwisho ambao unaonyesha utukufu wa jinsi Mungualivyo ulitokea pale msalabani.
“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoaMwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzimawa milele” – (Yohana 3:16).
Yesu alikufa sio tu kutupatia maisha yenye furaha sasa, bali kutupa uzimawa milele pia. Kwa vipindi virefu watu walishangaa, na kutumaini, na kuota
ndoto juu ya Mungu. Waliiona kazi ya mikono yake mbinguni na katika uzuriwa viumbe vya asili. Kisha pale msalabani, Yesu alikivunjilia mbali kimyacha vizazi vingi, na watu wakajikuta wanautazama ana kwa ana uso waMungu, wakimwona yeye kama alivyo hasa – yeye ni upendo, wa milele,tena ni upendo udumuo milele!
Wewe waweza kumgundua Mungu sasa hivi Yesu anapomfunua kwako.Ugunduzi huo utakufanya utoe uthibitisho wako binafsi, ukisema: “Baba,nakupenda!”