MKUSDA CHURCH
Unity in Worship

18. SIRI YA MTINDO WA MAISHA ULETAO AFYA

SIRI YA MTINDO WA MAISHA ULETAO AFYA
Watafiti wanaoishi katika kipindi hiki tulicho nacho wamejitahidi sanakuithibitisha ile kweli iliyothibitishwa kwanza na Biblia kwa kutoa maelezohaya: Wanadamu ni viumbe kamili. Mara nyingi kile tunachokigawa katikasehemu za kimwili, kiakili, na kiroho ni sehemu za mtu zilizo na uwianounaoingiliana, wala hazitenganishiki. Kwa maneno mengine, kinachoidhuruakili, kinaudhuru mwili.Hali yetu ya kiroho ina shinikizo lake juu ya hali yetuya kimwili, na kinyume chake. Sisi ni watu kamili.
Kwa mfano watafiti wa kisayansi katika uchunguziwao uliodhibitiwa wamegundua kwamba kicheko kilekitokanacho na furaha na shangwe huleta mabadilikoyanayoweza kupimwa katika mfumo wa kinga mwilinimwa mtu. Unaweza kabisa kuusaidia mwili wakokupigana na ugonjwa kwa vizuri zaidi ukiwa na furaha!Uchunguzi huo huonyesha jinsi akili na mwilivinavyofanya kazi yao kwa pamoja kwa ushirikiano wakaribu sana.
Katika maelfu ya miaka iliyopita Neno la Mungulilidokeza kuwapo kwa uhusiano huo wenye nguvukati ya akili na mwili ambao ni hivi karibuni tuumekubaliwa na kuingizwa katika nadharia yakiganga:
“Moyo uliochangamka ni dawa nzuri, bali rohoiliyopondeka huikausha mifupa” – (Mithali 17:22)
Kulingana na mtume Yohana, Je, Ni kwa karibu jinsigani uhusiano huo uliopo kati ya akili na mwiliunaathiri usitawi wetu wa kiroho?
“Mpenzi wangu, nakutakia mafanikio mema ya kilaaina; nakutakia afya njema ya mwili kama ulivyonayo rohoni” – (3 Yohana 1:2).
Muumbaji wetu anataka sisi tupate ” kufurahia kuwa na afya njema ” Nenola Mungu linaweza kutumika kama chemchem yetu ya afya, pamoja nakuwa chemchem yetu ya uzima wa milele.
Kwa kuwa usitawi wetu kimwili na kiakili na kiroho unakwenda bega kwabega, Paulo anatoa kwetu ombi hili:
“Mlapo mnywapo au mtendapo neno lolote, fanyeni yote kwa utukufuwa Mungu” – (1 Wakorintho 10:31).
Injili inajumuisha mambo yote mawili, uponyaji wa mwili na uponyaji waroho. Mtindo wa maisha uletao afya unaweza kutusaidia sisi kuwa Wakristowenye uchangamfu mwingi.
Hapa zipo kanuni nane za kufuata endapo wewe kweli unataka kuishimaisha yenye afya na yenye manufaa mengi zaidi.


1.Hewa Safi
Hewa safi ya nje, ni ya lazima kwa afya nzuri. Wakati wa mchana na wakatiwa kulala usiku, kuingiza na kuitoa hewa kwa njia inayofaa katika nyumbazetu na mahali petu pa kazi hutuhakikishia kwamba damu yetu daimaitagawa oksijeni ya kutosha kila sehemu ya mwili wetu. Kuvuta pumzi nyingi wakati wa matembezi ya asubuhi ni njia kuu ya kuupatia mwili wakooksijeni.
Aina ya hewa tuivutayo ni dhahiri kwamba ni ya maana. Jihadhari usikaemahali penye moshi au mvuke mwingi, penye hewa mbaya au hewainayochukua vijimea vidogo sana (bacteria) kutoka mahali fulanipalipojificha.
Kuvuta tumbako huichafua sana hewa na ni mojawapo ya wauaji wakuu wasiku hizi. Utafiti wa sayansi umethibitisha kuwapo kwa uhusiano unaoletamadhara kati ya tumbako na kansa ya mapafu, ugonjwa wa kuvimbamapafu na kupumua kwa shida ( emphysema) na ugonjwa wa moyo.Mazoea ya mwili kuhusiana na hiyo sumu ya nikotini katika sigareti hufanyauvutaji huo wa sigara (tumbako) uwe mmojawapo wa mazoea magumukabisa kuachana hayo. Kuvuta tumbako kutaweza kuwaua watu milioni 12kwa mwaka kufukia mwaka wa 2020 endapo mwendo huu wa sasautaendelea.


2.Mwanga Wa Jua
“Faida za mwanga wa jua ni nyingi:
1.Dakika kumi na tano hadi 30 za kupatamwanga wa jua kila siku katika ile sehemu yamwanzo ya asubuhi au baadaye mchanaalasiri husaidia mwili kukusanya pamoja aukutengeneza Vitamini D yake wenyewe,kirutubisho muhimu/homoni ndani ya ngozi.Vitamini D huisaidia damu kutengeneza kalisi(calcium) na fosforasi, inayoijenga nakuitengeneza mifupa.
2.Mwanga wa jua unafanya kazi yake kamadawa ya kuvika viini vya maradhi na kuuavijimea vidogo sana (bacteria)
3.Jua linatoa nguvu ambayo kwa hiyo mimeainaweza kuigeuza kaboni dioksidi na maji kuwa kabohidreti [chakula chawanga]… Bila ya njia hiyo wanyama na wanadamu wangekufa kwa njaa
4.Jua pia linamsaidia mwanadamu kujirekebisha na kukabiliana na kazi yausiku na kupunguza unyong’onyevu (depression) unaotokana na siku zagiza wakati majira ya baridi kali yanapotokea.
Neno la tahadhari: Mwanga wa jua unaweza pia kuleta madhara kukaa kwamuda mrefu kwenye mwanga wa jua kunaweza kuiunguza ngozi, kunawezakuongeza hatari ya kupatwa na kansa ya ngozi kunaweza kuharakishakuzeeka, kunaweza kuyaharibu macho, na kusababisha mtoto wa jicho(cataracts). ” [Madondoo yote katika Mwongozo huu yamenukuliwa kutokakatika Look up and Live: A Guide to Health, Lesoni ya Watu Wazima, Roboya kwanza ya mwaka wa 1993, (Nampa, Idaho: Pacific Prexss PublishingAssociation). Mambo mengi katika Mwongozo huu ambayo hayajawekwakatika Alama za kunukuu yamefundishwa kutoka katika lesoni hiyo hiyo]


3.Kupumzika
Mwili huu ni lazima upumzike ili upate kujitengeneza upya wenyewe.Yatupasa kuwa na muda wa burudani na wa kupumzika ili kupunguzamsongo utokanao na kazi pamoja na majukumu ya kifamilia. Bila kuwa namuda wa kutosha kupumzika mara nyingi watu wanakuwa na wasiwasi,mfadhaiko na hasira kali. Msongo huo wa moyo unaweza kuleta ugonjwaambao utatulazimisha kuchukua pumziko letu ambalo miili yetu ilikuwainataka kwa muda wote. Hakuna kitu cha badala cha kuweka mahali pausingizi mzuri wa usiku.
Kuzichaji upya betri zetu za kiroho kwa kuweka utaratibu wa kila siku nimuhimu pia kwa afya yetu ya kimwili. Muda wa kila siku anaotumia Mkristokatika kutafakari, kusoma Biblia, na maombi utaweza kuuponya mwili pamoja na roho. Tunakuhitaji pia kupata pumziko ili kuuvunja mzunguko wakazi, yaani, kuwa na siku ya kupumzika kila juma, na likizo ya mwaka aunusu mwaka.


4.Mazoezi Ya Mwili
Mazoezi ya mwili ni ya muhimu sana kwa afyayetu:
1.Mazoezi ya mwili husaidia kulirekebishashinikizo la damu.
2.Mazoezi ya mwili huiruhusu damu nyingi zaidikuzifikia sehemu zote za mwili na kuifanyamikono na miguu ipate joto.
3.Mazoezi ya mwili yanaondoa mambo yotemawili. Yaani mkazo wa mwili na mfadhaiko wamoyo, na kukusiadia wewe kujisikia vizuri zaidikatika maisha yako. Mazoezi ya mwili kwakawaida ni tiba bora kabisa ya wasiwasi namsongo (stress).
4.Mazoezi ya mwili hutupatia nguvu ya umemekwa ajili ya ubongo wetu pamoja na seli za neva.Yanaongeza afya kwa kuuamsha mfumo wakinga mwilini (immune system). Mwili unapowekwa katika hali ya afya kwakufanya mazoezi yanayofaa. Ubongo unakuwa na uwezo wa kufikiri kwaubunifu na ufanisi zaidi.
5.Yanaweza kukusaidia kuiweka vizuri rangi ya uso wako na kukuwekakatika hali nzuri kabisa kimwili.
6.Mazoezi ya mwili hukufanya uwe na nguvu nyingi zaidi, hivyokuchelewesha kupatwa na uchovu kimwili na kimawazo
7.Yanausaidia ubongo wako kutengeneza dawa inayokupa wewe hali yakujisikia vizuri na kukuongezea uwezo wa kustahimili maumivu.


Endapo wewe ulikuwa hufanyi mazoezi, basi anza taratibu (polepole) nakuongeza nguvu yake hatua kwa hatua upatapo uwezo wa kustahimili.Laweza kuwa ni jambo la busara kumwona mganga wako kabla ya kuanzamazoezi hayo. Lengo lako na liwe kujishughulisha na kila aina ya mazoezihayo ya mwili ambayo yanaweza kulinganishwa na kutembea maili mojakwa dakika kumi na tano mara nne au zaidi kw ajuma.


5.Maji
Kwa vile maji ni ya lazima kwa kila seli mwilini,basi, ingetupasa kunywa maji mengi.
1.Kwa uzito, mwili wetu karibu asilimia sabinini maji…
2.Mwili wetu unahitaji takribani visaga (quarts)viwili na nusu vya maji kila siku ili uwezekufanya kazi zake zote. Baadhi ya kazi hizo nipamoja na mzunguko wa damu mwilini,kuondoa uchafu mwilini, kusafirishavirutubisho vya chakula mwilini, nakukiyeyusha chakula mwilini
3.Mtu wa kawaida anazo seli za ubongo katiya billioni 15 na 40 hivi. Kila moja ya hizo inamaji asilimia 70 hadi 85. Maji ya kutoshakuweza kuzigawa seli hizo hukufanya uwe naakili iliyochangamka, halafu husaidia kuzuiamfadhaiko (depression) na hasira kali.
4.Si maji yale tu unayokunywa ambayo ni ya muhimu. Kuoga maji ya baridikidogo au vuguvuvugu kila siku au kwa kutumia bafu ya manyunyu(shower) huboresha mzunguko wa damu mwilini, hivyo kuupa mwili naubongo wako nguvu. Bafu ya manyunyu au kuoga kwa njia ya kawaidahuweza pia kutuliza mishipa ya fahamu iliyochachamaa, ambayo inawezakuleta ugonjwa kwa kudhoofisha mfumo wa kinga mwilini. Kuoga piakunaondoa uchafu kutoka juu ya ngozi, pia kunaweza kupunguzahoma.


6.Lishe Ifaayo
Wakati ule wa uumbaji Mungu alimwagizaAdamu na Hawa kula chakula cha kokwa,nafaka na matunda (Mwanzo 1:29). Baada yaAdamu na Hawa kutenda dhambi, ziliongezwamboga za majani katika lishe yao
(Mwanzo 3:18). Baada ya ile gharika, Muumbajialiongeza nyama ya wanyama “safi” katika lisheyao (Mwanzo 7:2-3, 9:1-6)
Nyama ya wanyama ina mafuta ya majimaji(saturated fat) na mafuta mazito kolestero[cholesterol], ambayo yote huongeza hatari yakupatwa na shinikizo la damu, kupooza(stroke), ugonjwa wa moyo, kansa, unene usiowa kawaida, kisukari na magonjwa mengineyo.Leo matabibu wengi wanawashauri walewanaokula nyama kula mnofu ule tu usiokuwana mafuta, uliopikwa vizuri, pamoja na kula samaki na kufanya hivyo kwanadra sana.
Kwa vile watu wanaokula chakula cha mimea wana afya bora zaidi, tenawanaishi kwa muda mrefu zaidi, wataalamu wengi wa lishe na afyawanatusihi sana sisi ili tupate kufikiria kukirudia chakula kile cha awaliwalichopewa wanadamu cha kokwa, nafaka na matunda pamoja na mbogaza majani zilizoongezwa.
Ukitaka kuanza kula vyakula vya mimea, hakikisha kwamba unaelewakwanza namna ya kuandaa lishe bora bila kutumia nyama. Ule kiasi chachakula kinachomtosha mtu kula kwa siku (migawo [serving] mitano au sitahivi) ya aina mbalimbali za matunda, pamoja na kokwa [karanga n.k.]nafaka, maharage, kunde, mbaazi na mboga za majani. Mboga za majaniza kijani na za njano, pamoja na machungwa ni za muhimu sana. Tumiaunga wa nafaka isiyokobolewa na mchele mwekundu (brown rice) badalaya ule mweupe. Ulaji wako wa wanga na sukari za mchanganyikoungekuwa katika migawo (servings) sita au zaidi kwa siku moja. Badilishamatumizi yako ya mafuta ya wanyama (samli, siagi, mafuta ya nguruwe,shahamu izungukayo figo, n.k.) kwa kutumia mafuta ya mimea. Lishe hiyojuu inatosha bila kutumia nyama kama wewe unatumia vitu vinavyotokanana maziwa.
Wale wanaochagua kula nyama kama sehemu ya chakula chao,wangepaswa kuzila nyama zile tu ambazo Biblia inasema ni “safi”au zilezinazofaa kuliwa na wanadamu. Mungu alipowaruhusu wanadamu kulanyama baada ya gharika (Mwanzo 7:2-3) (Mambo ya walaei 14:47),alibainisha nyama za wanyama gani zilikuwa safi, na zipi zilikuwa najisi nazilikuwa hazifai kuliwa.
Soma katika Mambo ya Walawi 11 na Kumbukumbu la Torati 14 orodha yandege, wanyama, na samaki ambao Mungu alisema hawafai kuliwa. Kwamujibu wa sura hizo, wanyama safi ni lazima kwato zao zigawanyike na piawacheue. Samaki safi ni lazima wawe na magamba na mapezi, vyote viwili.Ndege wanaokula uchafu ni marufuku kuliwa.
Miongoni mwa wanyama najisi, kwa namna ya pekee nguruwe wanatajwakwa kulaaniwa (Kumbukumbu la Torati 14:8) Asilimia ya juu ya miili yawanadamu inayofanyiwa uchunguzi na waganga imejaa minyoo isiyokufaya trikina (trichinae). Minyoo hiyo midogo sana inahamishiwa kwawanadamu wale wanaokula nguruwe walioambukizwa minyoo hiyo. Utafitiwa kisanyansi wa siku hizi unazidi kufunua sababu zinazoonyesha kwa niniMungu alitangaza nyama za wanyama fulani kuwa ni najisi. Sababu mojahuenda ikawa ni yale matokeo yanayoleta uharibifu mkubwa kutokana namafuta ya wanyama ya majimaji katika mfumo wa mwili wa kibinadamu wakuyeyusha chakula.


7.Epuka Vitu Vinavyoleta Madhara
Je, ni maonyo gani ambayo Biblia inatoa kuhusu vinywaji vyenye alcoholndani yake?
“Mvinyo hudhihaki na kileo huleta ugomvi;Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima” -Mithali 20:1
Wala wezi wala watamanio, wala WALEVI,wala watukanaji hawataurithi ufalme waMungu” – (1 Wakorontho 6:10).
Alkoholi huathiri mifumo ya mwili ifuatayo:
1.Mfumo wa kinga mwilini – Alkoholi inapunguzauwezo wa chembechembe nyeupe wa kupiganana ugonjwa, hivyo kuzidisha hatari ya kupatwana nimonia (pneumonia), kifua kikuu, homa yamanjano, na kansa za aina kadhaa.
2.Mfumo wa tezi (endocrinesystem) zinazotoamajimaji mwilini – Vinywaji viwili tu au vitatu kwasiku huzidisha hatari ya kuharibika mimba, kuzaa watoto waliokufa, nawatoto waliozaliwa kabla ya wakati wake.
3.Mfumo wa mzunguko wa damu mwilini Matumizi ya alkoholi huzidishahatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo, hupunguza sukari katika damu, nakuzidisha kiwango cha mafuta katika damu na kuongeza mapigo ya moyo,hivyo kuzidisha shinikizo la damu.
4.Mfumo wa kuyeyusha chakula – Alkoholi inaleta kuwasha tumboni, nakwa njia hiyo kusababisha kutoka damu katika tumbo hilo… Mazoea yakutumia alkoholi huzidisha hatari kwa ini kuw ana mafuta mengi, homa yamanjano, na ugonjwa wa ini (cirrhosis).
Alkoholi inahusika na asilimia kubwa ya watu wanaojiua wenyewe, vifovinavyosababishwa na magari, kuwatendea vibaya watoto, na ukatili uliomonyumbani.


8.Kuutumainia Uweza Wa Mungu
Mtu anayesumbuliwa mara kwa mara na hofu au hatia ataona vigumukwake kupata manufaa kamili kutokana na mazoea hayo ya afya tuliyotokakuyaeleza muda mfupi tu uliopita. Lakini mtu yule mwenye imani isiyo nashaka kwa Mungu atapata chimbuko hili la mwisho litakalomletea halinjema katika maisha yake.
“Ee nafsi yangu umhimidi BWANA, wala usizisahau fadhili zake zote -yeye anayekusamehe dhambi zako zote na KUKUPONYA MAGONJWAYAKO YOTE, ANAYEUKOMBOA UHAI WAKO na kaburi” – Zaburi 103:2-4.
David Larson, mshauri wa Taasisiya Taifa ya Afya ya Akiliki kuleMarekani, alifanya utafiti wakempana juu ya uhusiano wa mojakwa moja uliopo kati ya dini naafya.Uchunguzi wake ulionyeshawazi kwamba upo uhusiano wamoja kwa moja kati ya Mkristoaliyejitoa na afya. Alishangaa kujuakwamba, wale wanaohudhuriakanisani wanaishi kwa muda mrefukuliko wale wasiohudhuria. Wale wanaokwenda kanisani wana upungufuwa kupatwa na mshtuko wa moyo, Mishipa ya arteri kuwa migumu,shinikizo la damu, na magonjwa mengine. Wale wanaomwamini Munguhuishi maisha yenye manufaa zaidi kwa sababu hawapatwi kirahisi namfadhaiko, hawageuki na kuwa walevi sugu, kufungwa kama wahalifuwanaorudia mle tena na tena, na kunaswa katika ndoa isiyo na furaha.Kuutamainia uweza wa Mungu ndio msingi wa ustawi wa kweli na maishaya afya yenye furaha.
Waadventista, Wasabato wapatao 50,000 hivi walichunguzwa, hasa kuleCalifornia kwa kipindi cha zaidi ya miaka 30. Matokeo yalionyesha kwambaWaadventista wanaume wanaishi miaka 8.9 na wanawake miaka 7.5 kuliko
watu wengine wote kwa jumla. Uchunguzi huo wa Waadventista kuleUholanzi, Norway na Polandi huonyesha matokeo yanayofanana na hayo.

Watafiti wanaona kwamba sababu ya kipindi kirefu cha kuishi kwaWaadventista inatokana na kuzifuata kwao baadhi au kanuni zote nane zaafya zilizoelezwa katika mwongozo huu. Wale wanaozifuata kanuni hizi siotu kwamba wana maisha marefu zaidi, bali pia wana maisha yaliyo borasana.
Tukiutumia mtazamo wa Biblia katika maisha yetu tutakuwa tofauti katikaaina zote za njia za utendaji wetu na kutoa ushahidi unaovutia kuonyeshakwamba katika ulimwengu mzima Ukristo ni dini inayoweza kuwekwa katikavitendo. Inawabadilisha watu – yaani, fikra zao na matendo yao na kujengamtindo mpya wa maisha.
Kutokana na uhusiano wa karibu sana uliopo kati ya akili, mwili na maishayetu ya kiroho, Wakristo wale wanaoishi kwa Neno la Mungu watatakakuzifuata kanuni hizo za mtindo wa maisha uletao afya wanapojiandaa kwaajili ya marejeo yake Yesu (1 Yohana 3: 1-3). Sio tu kwamba Kristo anatakasisi tuwe tayari kukutana naye atakaporudi, pia anataka kuyaboreshamaisha yetu ya sasa. Tunaweza kushirikiana naye kwa kuzifuata hizokanuni za afya za Mungu.
Yesu anaahidi kutuokoa sisi mbali na kila tabia iletayo uharibifu mwilini kwa” kadri ya nguvu [yake] itendayo kazi ndani yetu” (Waefeso 3:20). Endapowewe unajitahidi kuishinda tabia fulani inayokuathiri mwili wako kama vilekutumia tumbaku au kunywa vileo, basi, maazimio yako hayo mazuri sanaya kutaka kuacha tabia hiyo mara nyingi yanageuka na kuwa kwako kamakamba za mchanga. Lakini kwa kuuchota uwezo wa Mungu unaotenda kazindani yako Mungu aweze kukupa wewe nguvu za kukuwezesha kushinda.Neno la Mungu linaahidi hivi: ” Naweza kufanya mambo yote kwa njia yakeKristo anitiaye nguvu” (Wafilipi 4:13)

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top
MKUSDA CHURCH