MKUSDA CHURCH
Unity in Worship

17. SIRI YA UKUAJI KWA KUSHUHUDIA

SIRI YA UKUAJI KWA KUSHUHUDIA
Larry alikuwa akifurahia maongozi yale mazuri, chai ya kijapani, walimkavu, nyumbani kwa Bwana Komari wakati wageni wengine walipoanzakuzitoa Biblia zao. Wote wakamtazama na kumngojea. “Tafadhali tupesomo letu sasa?” Bwana Komari aliomba.
Larry alikuwa karibu amepaliwa na chai yake. Alikuwa amedhani kwambamkutano ule wa dhifa (Karamu) ulikuwa wa kujifurahisha tu. Na sasahakuweza kufikiri juu ya kitu chochote cha kusema.
Kwa kweli Larry alikuwa amefundishamadarasa mengi ya Biblia katika shule yaKikrsito ya Lugha ya Kiingereza katika nchiya Japan alikokuwa akifanya kazi. Lakiniyalikuwa yameandaliwa vizuri. Aliwezakutoa maelezo juu ya Biblia kwa wepesi.Lakini kuweza kuzungumza habari zaMungu papo hapo bila kujiandaa vizuri…hilo lilikuwa ni jambo tofauti.
Larry alikuwa amezisikia hadithi zote zaBiblia tangu utoto wake. Lakini hazikuwa namaana sana kwake kwa msingi wa kibinafsi.Alikuwa anafanya mambo aliyojua kwambayalikuwa mabaya machoni pake Mungu.Angewezaje basi, kuwaambia wengine habari za Mungu ambaye yeyemwenyewe alikuwa hamjui kwa kweli?
Basi, akiwa ameketi pale kwenye kochi lile, amezungukwa na watuwaliokuwa wakimngojea, mchezo wake wa viigizo bubu ulikuwa karibukuporomoka. Katika saa ile ya hofu yake, fungu likapita kasi mawazonimwake lililosema kwamba roho Mtakatifu aweza kutupa sisi maneno yakusema tunapoletwa mbele ya watu kutoa ushuhuda wetu (Luka 12:12).Alitoa sala yake ya kufa na kupona kuomba msaada, kishaakaking’ang’ania kisa kile kinachojulikana sana ambacho aliweza kukifikiria:yaani, kisa cha mwana mpotevu.
Alipoeleza jinsi Mungu anavyowapenda sana hata wale ambaowanatangatanga mbali naye, Larry akajikuta anaongea moja kwa moja tokamoyoni mwake. Maneno yake yalikuwa yakiwaingia wale watu. Kwa maraya kwanza katika maisha yake Larry alitambua jinsi Mungu alivyompendasana.
Usiku ule Larry alipiga magoti kando ya Kitanda chake na kutoa maishayake kwa Mungu ambaye hatimaye alikuwa ni wa kweli kwake. Kushuhudiajuu ya upendo wa Mungu kulifanya jambo hilo kuwa zaidi ya jambo lakawaida la kuwazia tu. Sasa likawa ni jambo la kweli lililomshinda nguvu.


1.Yesu Anatupa Changamoto Ya Kukua Kwa Njia Ya Kushuhudia
Wanafunzi walikuwa wametumia miaka mitatu na nusu wakiyazingatiamaneno na matendo yake Kristo, na hatimaye kifo na ufufuo wake. Yesualipokuwa karibu kurudi mbinguni, aliwateua wanafunzi wake kuwawawakilishi wake.
“MTAPOKEA NGUVU akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu,NANYI MTAKUWA MASHAHIDI WANGU… hata mwisho wa nchi.”Matendo 1:8.
(Isipokuwa pale ilipoelezwa vinginevyo, mafungu yote yamaandiko katika GUNDUA Miongozo yanatoka katika Toleo jimpya la Bibliala Habari Njema.)
Wafuasi wake Kristo waliitoa mioyo yao kwake bila kuacha kitu katika ilesiku ya pentekoste, Kristo,yule aliyefufuliwa alikuwa ameyabadilisha maishayao kwa uwezo wa Roho. Wakawa mashahidi, sio tu wa kufufuka kwakekimwii na kupaa kwake, bali pia wa uweza wake wa ufufuo uliokuwaumeyabadilisha maisha yao.
Sisi kama Wakristo tu mashahidi pia wa ufufuo wake Yesu katika maishayetu wenyewe kwa kuwa tumeupokea uwezo wake utufanyao sisi kuwawapya.
“Kuna mwili mmoja na Roho mmoja, kama vile tumaini mliloitiwa naMungu ni moja. Kuna Bwana mmoja, imani moja na ubatizo mmoja;kuna Mungu mmoja na Baba wa wote, ambaye yuko juu ya wote,afanya kazi katika yote na yuko katika yote. Kila mmoja wetu amepewaneema kadri ya kipimo alichojaliwa na Kristo” – (Waefeso 2:4-7).
Tumehuishwa pamoja na Kristo, kwahiyo, tunaweza ku”udhihirish(a) wingiwa neema yake.” Naye anatutaka sisituzipeleke habari hizo njema kwaulimwengu mzima kuhusu kileawezacho kufanya ndani ya maisha yamwanadamu, kisha anatuahidi kwambaatakwenda pamoja nasi tukifanya hivyo(Mathayo 28:19-20).
H.M.S. Richards, muasisi wa hudumaya Redio ya Sauti ya Unabii, siku moja alitoa ushuhuda huu. “Miminimekwisha kuona badiliko ndani ya mioyo ya watu walioisikia hiyo injili yaKristo. Nimesafiri kwenda katika nchi ambako jina la Mungu na la Kristolililokuwa halijulikani kabisa mpaka kanisa lake lilipoipeleka injili kule.Nimewaona watu hao wakibadilika kutoka katika uchafu kwenda katikausafi, kutoka katika magonjwa kwenda katika afya, kutoka katika hofu yadaima ya mapepo na kuingia katika furaha ile itokanayo na kuishi maishaya Kikristo. Nimekwisha kuona badiliko katika hadhi waliyonayo wanawake.Nimeziona nyumba za kweli za Kikristo zikijitokeza kutoka katika giza lakipagani. Katika kila nchi niliyotembelea nimeona maisha ya watuyakibadilika. Mimi najua kwamba injili yake Kristo… ni uweza wa Munguuletao wokovu (Warumi 1:16). Najua kwamba kanisa linapoutangazaujumbe huo wa injili, mabadiliko hutokea ndani ya mioyo ya wanadamu,nayo yanaonekana kwa macho katika maisha ya wale wanaoitikia mwitowake.”
Mungu ametupa sisi wanadamu tulio dhaifu sehemu yetu maalum yakufanya katika kazi hiyo inayosisimua sana kwa sababu kule kutoaushuhuda wetu ni sehemu muhimu sana ya kukua kwetu. Ili imani yetuiendelee kuwa na afya, ni lazima itangazwe. Kama yule Larry alivyogunduakwa njia ya kuvutia sana, kugawa imani yetu kunatusaidia sisi kuwa nayokwa utimilifu zaidi, na kutufanya sisi tukue.


2.Tunamshuhdua Kristo Kwa Namna Tuishivyo
Kijana mmoja mwanaume, aliyekulia katika nyumba iliyojaa matusi, sikumoja alitoa maoni yake haya. “Niliwaangalia wazazi wangu ambao kwakielelezo chao walinipa picha mbaya ya Mungu; sikuona kamwe kielelezocha mtu yeyote mwenye ngozi juu ya mwili wake anayenipenda mimi.”Watu wale wanaotuzunguka. Wanamhitaji sana mtu fulani atakayewapapicha nzuri ya Mungu. Wanamhitaji mtu fulani “mwenye ngozi juu ya mwiliwake” ambaye atawaonyesha tabia nzuri ya dini. Kwa kawaida hubiri letulenye nguvu nyingi kuliko yote mara nyingi ni namna sisi tunavyoishi. Kablawatu hawajayazingatia yale unayoyajua, ni lazima wajue kwamba weweunawajali kwa kiasi gani. Petro anatusihi, anasema.

“MWE NA MWENENDO WENU katiya watu wasiomjua Munguunapaswa kuwa mwema kabisa,ilihata watakapowasingizienikwamba mnatenda mabaya,waweze kutambua matendo yenumema na hiyo wamtukuze Mungukila siku ya kuja kwake. HAYONDIYO mliyoitiwa; maana Kristomwenyewe aliteseka kwa ajiliyenu, akawaachieni mfano, ilimfuate mwenendo wake” 1Petro 2:12,21.
Kwa kuwa “Kristo aliteswa” kwa ajili yetu pale Kalvari, basi, tunachokielelezo cha upendo wake wa kujitoa mhanga ambacho ki karibu sananasi. Upendo ule, ukijitokeza ndani yetu kama matendo ya upendo ambayosisi tunawatendea wengine, unaweza kuwa uwezo wenye nguvu nyingikiasi cha kuwavuta wasioamini kuja mikononi mwake Kristo.


3.Tunamshuhudia Kristo Kwa Njia Ile Tunayofikiri
Ibilisi alipomshambulia Yesu kule nyikani kwa vishawishi vyake vyakuamsha tamaa ya kula chakula, majivuno, na kiburi cha makusudi, Yesualipigana naye na kushinda kwa kunukuu Maandiko (Mathayo 4:4,7,10).Kristo alikuwa amejiandaa kwa sababu alikuwa ameujaza moyo wake nazile kweli za Biblia. Humo ndimo vita hii inamoupata ushindi wake aukushindwa kwake-yaani, ndani ya mioyo yetu.
“Maana kama vile mtu afikirivyo moyoni mwake, ndivyo alivyo”(Mithali 23:7).
Wakristo wanaokua hufikiri mambo yale ya mbinugni. Wanaweka nguvu zaozote katika kujenga tabia zile nzuri wanazojitahidi kuwa nazo.
“Furahini katika Bwana siku zote,… katika kila neno kwa KUOMBA nakutoa dua zenu, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane naMungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, ITAWAHIFADHI MIOYOYENU NA NIA ZENU katika Kristo Yesu. Hatimaye, ndugu zangu,mambo yoyote yaliyo ya KWELI, yoyote yaliyo ya STAHA, yoyoteyaliyo ya HAKI, yoyote yaliyo SAFI, yoyote yenye KUPENDEZA, yoyoteyenye SIFA NJEMA – iwapo kitu chochote ni KIZURI SANA ua KINASIFA NZURI- yatafakarini mambo kama hayo…. Na Mungu wa amaniatakuwa pamoja nanyi. “- (Wafilipi 4:4-9).
Kile tunachoilisha mioyo yetu kinaleta tofauti kubwa sana. Ukiweka uchafundani yako, utatoa nje uchafu. Ukiweka Neno la Mungu ndani yako, utatoanje maisha yake Mungu.


4.Tunamshuhudia Kristo Kwa Namna Sisi Tunavyoonekana

Akiwa mwakilishi wa Kristo, Mkristo atakuwana adabu hata kwa namna anavyoonekanakwa nje, akiepuka kuzidi kiasi kwa njia yoyoteile.
“Inanyi wake, jiwekeni chini ya mamlaka yawaume zenu, ili kama wako waume wowote wasioamini neno la Mungu, wapatekuamini kwa kuuona mwenendo wenu.Haitakuwa lazima kwenu kusema neno,kwani wataona jinsi mwenendo wenuulivyo safi na wa kumcha Mungu. Katikakujipamba kwenu msitegemee mambo yanje nje, kama vile mitindo ya kusukanywele, kujivalia vitu vya dhahabu na nguomaridadi. Bali uzuri wenu unapaswakutokana na hali ya ndani ya utu wa kweli, uzuri usioharibika wa wemana utulivu wa roho, ambao ni wa thamani kubwaa mbele za Mungu.

Ndivyo walivyojipamba hapo kale wanawake waadilifu waliomtumainiaMungu; walijiweka chini ya mamlaka ya waume zao”- (1Petro 3:1-5).
Kuvaa mavazi na mapambo ya kawaida kumedhihirisha daima uzuri ule wakufanana naKristo. Kwa mfano ulio mkamilifu, wengine wangewezakuvutwa kuja kwetu kwa kuwa sisi tu Wakristo, sio kwa sababu ya manenoyetu tunayosema juu ya mitindo ya kisasa, bali kwa maneno ambayomaisha yetu yanamtangaza Yesu.


5.Tunamshuhudia Kristo Kwa Namna Tutendavyo
Mwanahistoria Edward Gibbon anatuambia sisi kwamba Galerio (Galerius)alipoliteka kambi la Waajemi, mfuko wa ngozi unaong’aa uliojazwa luluuliangukia mikononi mwa askari mmoja aliyekuwa akiteka nyara. Mtu yulealiutunza kwa uangalifu sana mfuko ule wenye manufaa, lakini lulu zile zathamani akazitupilia mbali.
Watu wale wanaozing’ang’ania furaha za juu juu tu ambazo ulimwengu huuunaweza kuwapa – huku wakimtupa Yesu mbali, Lulu ya Thamani kuu -wako katika hali mbaya sana kuliko yule askari aliyeteka nyara zile. Si malitu iwezayo kuteleza mikononi mwetu, bali na uzima wa milele. Kwa hiyoMaandiko yanatuonya, yanasema:
“Msiipende ulimwengu, wala cho chote kilicho cha ulimwengu. Mtuanayeupenda ulimwengu, upendo wa Baba hauwezi kuwa ndani yake.Vitu vyote vya ulimwengu – tamaa mbya za mwili, vitu wanavyovionawatu na kuvitamani, majivuno yasababishwayo na mali – vyote hivyohavitoki kwa Baba, bali vyatoka kwa ulimwengu. Ulimwengu pamojana vitu vyake vyote vyenye kutamanika unapita; lakini mtu atendayeatakalo Mungu, anaishi milele” – (1 Yohana 2:15-17).
Shetani anafanya kazi yake kwa bidii nyingisana kupaka dhahabu nje ya dhambi zilezinazoangamiza watu sana na yale mazoeamabaya kabisa. Matangazo ya vileohuwaonyesha tu watu wale ambao ni vijana,wazuri, wachapa kazi, na wenye furahanyingi sana. Hatumwoni mtu ye yoteanayetoka katika duka la vileo akichechemeakama kinyago na kuwa na kisalfeti (gunia)mkononi mwake.
Tunapaswa kuwa waangalifu kuhusu marafikiwale tunaoshirikiana nao ili tusije tukaziacha kanuni zile za Kikrsito (2Wakorintho 6:14). Kwa kweli, Kristo anatutaka sisi kuendeleakuwatembelea marafiki zetu hao wasiokuwa Wakristo. Uhusiano wetu namtu mmoja mmoja ndizo njia za msingi ambazo kwanza imani yetuinagawanywa kwa wengine hakikisha tu kwamba rafiki zako haohawakuvuti kukurudisha katika mwenendo wako ule wa zamani.
Kile tunachokiingiza katika maisha yetu, hata burudani tunayoichagua,vinalo shinikizo lake juu ya maisha yetu ya Kikristo. Tunahitaji kukitambuakile tunachoilisha mioyo yetu.
“Sitaweka mbele yangu neno la uovu” – (Zaburi 101:3).
Tukiilisha mioyo yetu kile kilicho bora kabisa, basi, kile kilicho kiovu kabisahakitaweza kutuvutia chini ili tupate kufanana nacho. Kule kuzishikilia sanazile kanuni za juu zaidi katika vitu vile tuviletavyo nyumbani na mioyonimwetu hakutayafanya maisha yetu kubanwa sana. Mkristo anayo mengi yakumfanya awe na furaha kuliko mtu mwingine awaye yote.
(“Wanionyesha njia ya kufikia uhai; kuwako kwako kunijaza furaha kamili,katika mkono wako wa nguvu mna mema ya milele”) ( Zaburi 16:11).


6.Tunamshuhudia Kristo Kwa Utoaji Wetu
Alipokuwa karibu kumbatiza muumini mmoja mpya, hayati MchungajiH.M.S. Richards aligundua kwamba yule mtu alikuwa na pochi ya fedhailiyokuwa imjeaa vizuri katika mfuko wake. Richards akamwuliza endapoalikuwa amesahau kuiacha fedha yake ile katika chumba cha kubadilishia nguo. “Mfuko wangu huu na mimi tutabatizwapamoja,” alieleza yule mtu. Alikuwa ameipataroho halisi ya Ukristo – yaani, kutoa ilikuwasaidia wengine. Wakristo hukua kwakutoa na ndiyo maana “Yesu mwenyewealisema. “Ni heri kutoa kuliko kupokea”.(Matendo 20:35). Kile tutoacho ili kuendelezaufalme wa Mungu kinaendelea kuwa nathamani ya milele.
“Msijiwekee hazina zenu duniani, nondona kutu viharibupo, na wezi huvunja nakuiba. Bali JIWEKEENI HAZINA ZENUMBINGUNI. Kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo namoyo wako”- (Mathayo 6:19-21).
Unapotoa kumbuka” Dunia ni mali ya BWANA, na vyote viijazavyo” (Zaburi24:1), hii ni pamoja na fedha na dhahabu (Hagai 2:8). Sisi wenyewe tu maliya Mungu,. Kwa sababu alituumba na kwa sababu yeye alituokoa kutokakatika dhambi zetu kwa kulipa fidia ya dhambi zetu kwa damu yake(1Wakorintho 6:19-20). Kila kitu tulicho nacho ni mali ya Mungu, kwasababu yeye ndiye “a(tu)paye nguvu za kupata utajri” (Kumbukumbu laTorati 8:18).
Ni kiasi gani anachotaka tutoe, huyo Bwana wetu aliyesulibiwa na kufufuka,ili tupate kushirikiana naye katika kuipeleka injili kwa wengine?
“Je! mwanadamu atampora Mungu? Lakini ninyi mnanipora mimi.Lakini ninyi mwasema, “Tumekupora kwa namna gani?
“Mmenipora ZAKA NA SADAKA…
Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu.Mnijaribu kwa njia hiyo,’ asema BWANA wa majeshi; Mwone kamaSITAWAFUNGULIA MADIRISHA YA MBINGUNI na kuwamwagienibaraka hata hamtaweza kuwa na nafasi ya kutosha kuiweka hiyobaraka” – Malaki 3:8-10.
Zaka ni “Sehemu ya kumi” ya mazidio” yote(Kumbukumbu la Torati 14:22, KJV; Mwanzo28:22). Kwa mkulima au mfanyabiasharamazidio hayo ni mapato baada ya kutoagharama za biashara (mtaji). Kwamfanyakazi, ni mshahara wake kamili.Kanuni ya kutoa zaka ni kanuni ya kimaadilikwa sababu inahusu tabia ya mtu.Tunaposhindwa kutoa zaka huwa tuna”mwibia” Mungu. Zaka ni ya Mungu, nayoinatakiwa kutumika kwa ajili ya kuwapa rizikiyao wachungaji wake Kristo peke yao(1Wkorintho 9:14), na kuimaliza kazi yakeduniani ili yeye apate kurudi (Mathayo24:14).
Yesu alipokuja hapa kuishi kati yetu, alitoa idhini yake ya kulipa zaka katikanyakati za Agano Jipya (Mathayo 23:23).
Je! hivi tutoe kiasi gani kama sadaka? Sadaka ni mtu mwenyeweanavyoamua kutoa. Kila mtu anatakiwa “atoe kama alivyokusudia kutoamoyoni mwake” (2Wakorintho 9:5-7). Wewehuwezi kumpita Mungu katikautoaji.
“Toeni, nanyi mtapewa. Kipimo cha kujaa, na kushindiliwa, nakusukwa-sukwa hata kumwagika, ndivyo mtapewa mapajani mwenu” -(Luka 6:38).
H.M.S. Richards siku moja alisimulia kisa hiki.
“Mpiga kamari mmoja aliyebobea katika maisha yake yote alihudhuriamikutano yangu kule Los Angeles, wala sitasahu kamwe wakati ulenilipozungumza naye tukiwa peke yetu nyuma ya ukumbi wa mikutano.Alitoa bunda la noti mfukoni mwake, Dola za Kimarekani 500, na kunipamimi zote, huku akisema, “Hii ndiyo zaka yangu ya kwanza.!

“Yule mtu hakuwa mzima, naye alikuwa hajafanya kazi nyingine yoyoteisipokuwa kupiga kamari kwa miaka 30 au 40 hivi, basi mimi nikamwuliza,utaishije kuanzia sasa?
“Alijibu, Nimebakiwa na dola tano au sita hivi, lakini hizo nyingine ni mali yaBwana. “Kisha nikamwuliza, utafanya kazi gani, basi?
“Sijui, alijibu, ila najua kwamba ni lazima nitoe zaka yangu kwa Mungu,yeye atanitunza.!
“Na kwa hakika Mungu alimtunza. Toba ya mtu yule ilikuwa ya kweli.Alikwenda njia yote katika kujitoa wakfu kwake, naye alikuwa na furahakatika maisha yake ya Kikristo. Na Mungu hatoi ahadi kwamba wauminiwote waaminifu watakuwa matajiri. Lakini tunayo ahadi kwamba Muumabajiwetu atatupatia mahitaji yetu ya maisha.
Kristo alitoa kila kitu kwa ajili yetu. Hebu sasa na tumpe kabisa mioyo yetu.Hebu na tuwaambie wengine habari zake Kristo kwa namna sisi tuishivyo,tufikirivyo, tuonekanavyo kwa nje, tutendavyo, na tutoavyo. Kwa nini sisitusiigundue furaha hii ya kuwaambia wengine habari za Kristo nakuendelea kukua katika neema yake ya ajabu?

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top
MKUSDA CHURCH