MKUSDA CHURCH
Unity in Worship

16. SIRI YA PUMZIKO LA MBINGUNI

SIRI YA PUMZIKO LA MBINGUNI
Miaka michache tu iliyopita wengine walikuwa wakibashiri kwamba muda simrefu tungekuwa na muda mwingi sana wa mapumziko ambaotungeshindwa kujua tufanye nini nao. Hizi zilikuwa ndizo sababu nzuri kwaubashiri ule wenye matumaini. Katika miji mikuu ya ulimwengumakompyuta yalikuwa yakizisaga-saga kazi ambazo zingechukua mwezimzima kuzifanya kwa sehemu tu ya nukta moja. Na yale maroboti yalikuwayameanza kuzifanya kazi ngumu sana za kuchosha katika viwanda vyakutengeneza mashine nzito.
Lakini baada ya makompyutahayo kutoa mfumo wao namaroboti kufanya kazi zao, badotunakosa hata pumzi kuzifanyakazi hizo muda wa siku hizi. Zaidiya yote, familia zinakosa mudawa kukaa pamoja. Waume nawake zao huona vigumu kupanga”muda unaofaa” wa kuwa pamojana watoto wao, licha ya waowenyewe kuwa na mudamchache wa kuwa pamoja.
Utafiti mmoja uliofanywa katika jumuia moja ndogo ulionyesha kwambawastani wa muda kila siku ambao mababa wanatumia wakiwa peke yao nawatoto wao wadogo sana ulikuwa nukta 37! Familia hazina muda, walahazina mawasiliano.
Je! Tunawezaje kupunguza hiyo kasi tuliyonayo kwa kiasi cha kutoshakuweza kuwa na uhusiano wetu tena?


1.Dawa Ya Maisha Yaliyojaa Mahangaiko
Yesu anayajua matatizo ya familia zilizo chini ya shinikizo hilo, nayeanataka sisi tujue kwamba pumiziko la kiroho ni sehemu ya maisha bora;
“NJONI KWANGU, ninyi nyote mliochoka na maisha na kulemewa namizigo, NITAWAPUMZISHA… MJIFUNZE KWANGU, kwa kuwa mimi nimpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata RAHA NAFSINIMWENU.” Mathayo 11:28, 29.
Biblia inatushauri kuionja hiyo raha kwa njia mbili: Kumwendea Kristo kwakutegemea msingi huu wa aina mbili, KILA SIKU na KILA JUMA.


2.Kuungana Na Yesu Kila Siku
Makundi ya watu wakati wote yalikuwa yakidai Kristo awasikilize wao tu.Naye Kristo bado aliweza kuonyesha moyo wa amani, mtulivu, kwa kilammoja aliyemzunguka. Hivi ilikuwaje? Alitumia muda wake kila sikukuongea na Baba yake aliye mbinguni. Alimtegemea Baba yake daima ilikupata nguvu za kumwezesha kukabiliana na changamoto za maisha(Yohana 6:57).
Endapo sisi tunataka kuishi maisha matulivu, na manyofu kama yeyealivyoishi, basi yatupasa kumtegemea Yesu daima – turuhusu Neno lake naRoho wake kutujaza na kututengeneza. Njia bora kuliko zote ya kuzipinganguvu zile zinazotuunguza sisi kama mtu mmoja mmoja na kututenganisha

kifamilia na ile ya kutumia muda ulio bora pamoja na Kristo. Yeyeanatuambia hivi:
“KAENI NDANI YANGU, nami ndani yenu…. PASIPO MIMI HAMWEZIKUFANYA NENO LOLOTE” -(Yohana 15:4,5).
Mojawapo la mahitaji yetu makuukuliko yote kwa kipindi chetu hikini lile la kutega nguvu za Kirohozipatikanazo kwa njia ya kujengauhusiano wa siku – kwa siku naYesu. Jambo moja la maana sanalinalotakiwa kusisitizwa juu yauhusiano wetu na Kristo ni kaziyake iliyokamilika pale msalabanipumziko la kweli, usalama halisi,mambo hayo yanaweza kuwapotu kwa sababu ya lile jambo mojakuu alilolifanya Yesu ambalo linatajwa wakati ule alipolia kwa sauti kuualipokuwa akifa, alisema. “Imekwisha” (Yohana 19:30). Kwa manenomengine, ile kazi yake ya kutukomboa sisi ilikuwa imekamilika.
Maana ingalikuwa hivyo, Kristo angalipaswa kuteswa mara nyingi tangukuumbwa ulimwengu. Lakini sasa, nyakati hizi zinapokaribia mwisho wake,yeye ametokea mara moja tu kuondoa dhambi kwa kujitoa yeye mwenyewedhabihu. – (Waebrania 9:26).
Yesu alipokufa, aliziondoa dhambi”. Ndiyo maana yasemekana kwambaMuumini aliyeziungama dhambi zake anaweza “Kupumzika” katika kazi ileiliyokamilika ya Kristo. Sisi tunakubalika.
Hatia imejificha katika nyumba ya haraka ya kiwendawazimu tuliyo nayokatika maisha yetu siku hizi. Lakini Yesu alilisuluhisha tatizo hilo la hatiamara moja tu pale msalabani. Kilio cha Yesu, alichosema, “Imekwisha”kilitia muhuri ahadi yake aliyosema “Nitawapumzisha” na kuifanya iwe nijambo la kweli kabisa. Kristo aliikamilisha kazi yake ya kutukomboa sisipale Kalvari (Tito 2:14), halafu akapumzika kaburini siku nzima ya Sabato,na kufufuka kaburini siku ya Jumapili asubuhi kama mshindi dhidi yadhambi na mauti. Mkristo hawezi kuwa na ahadi kubwa kuliko hiyo yakupumzika katika kazi ya Kristo ile iliyokwisha.
“Kwa hiyo tumkaribie Mungu kwa mioyo iliyotakaswa kutokana nadhamiri mbaya, na kwa miili iliyosafishwa kwa maji safi. Tuzingatiekabisa tumaini letu tunalokiri, maana Mungu aliyefanya ahadi zake nimwaminifu.” – Waebrania 10:22,23
kwa kuwa yeye “aliyeahidi nimwaminifu,” basi, sisi tunaweza kuingia katika pumziko la wokovu ambaloYesu ametuahidi. Uthabiti, amani, na pumziko tunaloliona ndani ya Yesukila siku ni matokeo, sio ya neno lolote tulifanyalo, bali ya kile alichokifanyapale msalabani.
Tunaweza kupumzika ndani ya Kristo kwa sababu wokovu wetu ni wahakika. Uhakika huo hututia moyo kutumia wakati wetu pamoja na Kristokila siku, tukijilisha Neno lake na kuvuta hewa ya mbinguni kwa njia yamaombi yetu. Mahali pale pa kukutana na Yesu hutusaidia sisi kuyageuzamaisha yetu yaliyojaa mahangaiko na kuyafanya yawe ya amani na yenyelengo maalum.


3.Kuungana Na Yesu Kila Juma
Baada ya Kristo kuiumba dunia hii kwasiku sita (Wakolosai 1:16-17), alitoapumziko la Sabato. Ni nafasi ya kila jumatuliyopewa ili kuuendeleza mwunganowetu huo pamoja naye.
“Mungu akaona kila kitu alichofanyakuwa ni chema kabisa. Ikawa jioniikawa asubuhi; siku ya sita. Hivyondivyo mbingu na duniazilivyokamilika pamoja na vitu vyote vilivyomo. Siku ya saba Mungu
akawa amemaliza kazi yake yote aliyofanya; siku hiyo ya saba Munguakapumzika baada ya kazi yake yote aliyofanya. Mungu akaibariki sikuya saba na kuitakasa, kwa kuwa siku hiyo Mungu alipumzika baada yakazi yake yote ya kuumba” – (Mwanzo 1:31-2:3).
Kama Muumbaji wao, Yesu “akapumzika” Sabato ile ya kwanza pamoja naAdamu na Hawa, naye “akaibariki” siku ya Sabato na “kuifanya takatifu”.Mungu ndiye aliyeuanzisha mzunguko wa juma – la – siku – saba, si kwafaida yake mwenyewe, bali kwa faida ya Adamu na Hawa na kwa faida yetusisi leo. Kwa kuwa aliwapenda sana watu wale aliokuwa amewaumba,alipanga kwamba kila siku ya saba katika maisha yao yote ingewekwawakfu kwa ajili ya kutafuta kuwako kwake yeye. Kila Sabato, kama yeyealivyoiita, ilipaswa kuwa siku ya pumziko la kimwili na burudiko la Kiroho.Kuingia kwa dhambi katika ulimwengu wetu kulifanya haja ya pumziko laSabato iwe kubwa zaidi.
Mwokozi yule aliyemwahidi Adamu na Hawa “pumziko” lile, alimpa Musa,mnamo miaka elfu mbili baadaye, sheria juu ya ule Mlima Sinai(1Wakorintho 10:14) Yesu alichagua kuiweka amri ile ya pumziko-la-Sabatokatikati kabisa ya zile amri Kumi. Amri ya nne inasomeka hivi:
“IKUMBUKE SIKU YA SABATO KWA KUITAKASA. Siku sita utafanayakazi, na tenda mambo yako yote, Lakini siku ya saba ni Sabato yaMwenyezi-Mungu, Mungu wako. Siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe,wala mwanao, wala binti yako, wala mtumwa wako wala mtumishiwako wa kike, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliyenyumbani mwako. Maana, kwa siku sita mimi Mwenyezi-Munguniliziumba mbingu na duniai, bahari, na vyote vilivyomo, kishaNIKAPUMZIKA siku ya saba. Kwa hiyo, MIMI MWENYEZI-MUNGUNILIIBARIKI siku ya Sabato na NIKAITAKASA” – (Kutoka 20:8-11).
Mungu aliianzisha Sabato kama siku inayopaswa kum”kumbuk(a)” Bwanaaliye “zifanya mbingu na nchi.” Pumziko – la-Sabato la kila jumalinatuunganisha sisi na Muumbaji wetu aliyeibariki siku hiyo na kuitenga.
Yesu alipoishi hapa duniani, aliitumia vizuri kila nafasi nzuri kwa kudumishamwungano huo na Baba yake. Alinufaika na pumziko-la-Sabato kwakuabudu siku ya Sabato, kama Luka anavyotusimulia:
“Akaenda Nazareti, mahali alipolelewa, na SIKU YA SABATO akaingiakatika singagogi, KAMA ILIVYOKUWA DESTURI YAKE.” – (Luka 4:16).
Ikiwa Yesu aliyekuwa Mungu – Mwanadamu alihitaji kupumzika mbele zaBaba yake siku ya Sabato, basi, sisi tulio wanadamu kwa hakika tunalihitajizaidi hilo pumziko. Yesu alipozifagilia mbali sheria zile zilizoweka vizuizivingi walivyokuwa wameviweka Wayahudi katika ile Sabato (Mathayo 12:1-12), yeye aliwaonyesha kwamba Mungu alikuwa ameiweka Sabato kwa ajiliya kuwaletea watu manufaa.
“Akawaambia, Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, simwanadamu kwa ajili ya Sabato. Basi Mwana wa Adamu ndiye Bwanawa Sabato pia” – (Marko 2:27,28).
Yesu alisisitiza sana umuhimu wa Sabato hata wakati wa kifo chake. AlikufaIjumaa, “Siku ya Maandalio, na Sabato ikaanza kuingia “(Luka 23:54).Wakati ule alitangaza. Akasema, “Imekwisha,” yaani, kazi yake ya kujahapa duniani na kufa kama badala ya taifa zima la Kibinadamu ilikuwaimekamilika (Yohana 19:30; 4:34; 5:30). Kisha ili kusherehekea utume wakeuliokwisha, Yesu alipumzika kaburini Sabato ile nzima.
Kama Kristo alivyomaliza kazi yake ya uumbaji katika siku ile ya sita, kishaakapumzika siku ya Sabato, ndivyo kwa kufa kwake msalabani alivyomalizakazi yake ya ukombozi katika siku ile ya sita, na halafu akapumzika siku ileya saba.
Jumapili alfajiri Yesu alitoka kaburini kama Mwokozi Mshindi (Luka 24:1-7),Tayari alikuwa amewataka wanafunzi wake kuendelea kukutana naye sikuya Sabato baada ya ufufuo wake. Akizungumza juu ya kuangamizwa kwaYerusalemu, ambako kulitokea karibu miaka arobaini hivi baada ya kifochake, aliwaagiza, alisema.

“Ombeni, ili kukimbia kwenukusiwe wakati wa baridi, walasiku ya Sabato.” Mathayo 24:20.
Mwokozi wetu alitaka wanafunziwake pamoja na waongofu waowaendelee na desturi alizokuwaamewafundisha (Yohana 15:15,6).Aliwataka wayaonje yote mawili,yaani, pumziko – la – Wokovu napumziko – la -Sabato.Hawakumwangusha. Wanafunzi wake waliendelea kuitunza Sabato baadaya kifo chake Kristo (angalia Luka 23:54-56; Matendo 13:14; 16:13;17:2:18:1-4).


Yohana yule aliyependwa sana alidumisha mwungano wake wa kila jumana Kristo katika siku ya Sabato. Katika miaka yake ya baadaye aliandika,akisema, “Siku ya Bwana nilikuwa katika roho” (Ufunuo 1:10). Kulingana namsimamo wa Yesu, “Siku ya Bwana” ni Sabato, “Kwa maana Mwana waAdamu ndiye Bwana wa Sabato “(Mathayo 12:8).
Siku ya Sabato tunaadhimisha mambo makuu kuliko yote mawilialiyoyakamiisha kwa ajili yetu. Yaani, kutuumba sisi na kutuokoa. Uzoefuhuo wa kuitunza Sabato utaendelea kule mbinguni:
“Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazofanya, zitakavyokaambele zangu, anatangaza BWANA,… ‘toka Sabato hata Sabato,wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema BWANA” -(Isaya 66:22,23).


4.Manufaa Ya Pumziko-la-sabato
Siku hizi watu wanakanyagana ovyo katika maisha yao ya kiwendawazimu.Watu wanateketea mmoja mmoja. Famili zinasambaratika chini yashinikizo. Lakini Mungu anawapa Sabato yake kama njia bora zaidi yakuishi yale maisha mema.
Hebu na tuyaangalie baadhi ya manufaa ya pekee ya hilo pumziko-la-Sabato:
1)Sabato ni kumbukumbu ya uumbaji, na kwa kuitakasa, tunamjengeakumbukumbu Muumbaji wetu. Saa zake takatifu zinatupa nafasi nzuri ajabuza kushughulikia na maisha yetu mapya tuliyoyaanza katika dunia hiiiliyoumbwa na Mungu. Je! ni lini kwa mara ya mwisho wewe au familia yakomlitumia muda wenu kwa kuzama kabisa katika kutafakari ule uzuri mtulivuwa njia ile ya msituni au kijito kile kinachotiririka kupitia katika miamba ile?Sabato inatupa muda wa kutumia pamoja na Yesu na kuona kidogo tumaajabu yake aliyoyafanya kwa ajili yetu.
2)Siku ya Sabato tunaionja furaha yakumwabudu na kushirikiana naWakristo wengine. Kuna faida katikakumsifu Mungu tukiwa pamoja nawengine kama kundi la watu waabuduopamoja. Sabato inatupa sisi muda wapekee wa kukusanyika pamoja kamakundi la kanisa na kuzichaji upya betrizetu za kiroho.
3)Sabato inatupa sisi fursa ya kutendamatendo ya wema kwa kuwafikiriawengine. Je! jirani yako amekuwa mgonjwa katika juma hili ulipokuwa hunanafasi ya kumtembelea? Rafiki yako alipotaka umsikilize kwa kusikitikapamoja naye kwa kufiwa na mumewe, je! shinikizo la maisha yako ya kilasiku lilimnyima mama huyo upendo wako wa kwenda kumtazama? Yesualitoa shauri hili: “Ni vyema kutenda mema siku ya Sabato” (Mathayo12:12).
4)Sabato ni Siku ya kuviimarisha vifungo vya Familia. Yesu alipoamuruhivi, “Siku hiyo (ya Sabato) usifanye kazi yoyote” (Kutoka 20:10).
Asingekuwa ametoa dawa nzuri zaidi kwa mababu walio walevi wa kazi nakwa akina mama wanaosumbuka sana. Sabato ni ishara kubwa sanaisemayo SIMAMA kwa familia nyingi. Simama na kuacha kuyaruhusumambo yale ya muhimu zaidi kwako mambo yale yaliyo ya maana sana.Sabato ni siku moja ambayo katika hiyo tunaweza kuondoa shinikizo namahali pake kuweka maombi, kuondoa kazi ngumu na kuweka kichekobadala yake, kuziondoa ratiba zenye shughuli nyingi na mahali pakekuweka tafakuri ya kimya kimya. Pumziko -la-Sabato huipa familia nzimamuda wa kuungana na Kristo na kuchota nguvu za Kiroho kutoka kwake(kwa matumizi yetu).

5)Sabato ndio wakati ambapo Yesu anakuja karibu nasi zaidi kwa njia yapekee. Kila uhusiano uliopo unahitaji muda unaofaa uwepo, na uhusianowetu na Kristo hauna tofauti. Kuitumia siku nzima kwa ajili yake Kristo kilajuma ndiyo njia kuu ya kuufanya urafiki wetu naye uwe safi na wakufurahisha sana. Sabato inatupa muda wa ziada kwa ajili ya kujifunzaBiblia na maombi, muda wa ziada wa kuwa peke yetu pamoja na Kristomahali pa kimya na kusikiliza.
Yesu “akaibariki siku ya saba na kuifanya takatifu” kwa ahadi ya kuwakokwake (Mwanzo 2:3). Unaweza kuelewa kwa nini ni jambo la maanakuitunza Jumamosi, siku ya saba ya juma, kama Kristo aliitenga wakati ulewa uumbaji ili apate kuitumia kwa kuwasiliana nasi kwa njia ya pekee.
Yesu alipoifanya Sabato yaonekana kabisa kwamba alikuwa anakifikiriakizazi chetu mawazoni mwake. Ndiyo tunayoihitaji hasa katika mazingirayetu ya maisha yaliyojaa shinikizo. Ni siku ambayo inatutenga kweli mbalikabisa na mambo mengine yote. Ni siku ya kumwabudu Mungu,kuwasiliana tena na uumbaji wake, na kuuimarisha uhusiano wetu badalaya kuvishuhulikia vitu.


5.Ni Kilionja Mapema Pumziko La Mbinguni
Tunaweza kufanya muhtasari wa manufaa tunayoweza kupata kwakujiunganisha na Kristo kwa njia ya kukutana naye KILA SIKU na KILAJUMA kwa kutumia neno moja tu – pumziko. Neno hili “Sabato” linatokakatika neno la Kiebrania limaanishalo pumziko, basi, si jambo laajabu yakwamba Maandiko yanaiita hiyo siku ya saba kuwa ni “Sabato yakupumzika kabisa” (Mambo ya Walawi 23:3).
“(Mungu) amesema juu ya siku ya saba kwa maneno haya: Siku yasaba Mungu alipumzika na kuacha kufanya kazi yake yotealiyoifanya…. BASI LIMESALIA PUMZIKO-LA-SABATO KWA WATU WAMUNGU…. Basi, na tufanye bidii kuingia katika pumziko lile”- (Waebrania 4:4-11).
Kulionja hili “Pumziko-la-Sabato” kila jumahutuwezesha sisi kuionja mapema ilefuraha tutakayoipata katika lile pumzikokamilifu kule mbinguni. Pumziko lile sikukaatu kivivu, linamaanisha kujisikia u salamamoyoni, una hali ya amani na hali njema yamaisha iliyo katika shina lile la maisha teleya kweli. Aina hiyo ya pumziko la kirohoinaweza kuthaminiwa tu kwa kulionja.Ushuhuda wa wale walioonja pumziko-la-wokovu pamoja na hilo pumziko-la-Sabatounajulikana kote. “Kama wewe umeingiakatika pumziko la Yesu kwa njia yakuungana naye kila siku na kila juma, basi,utaigundua furaha kuu kuliko zote katikamaisha yako.”
Je! ungependa kumshukuru Yesu kwazawadi yake hiyo ya pumziko? Je,ungependa kumshukuru kwa ahadi yake ya pumziko-la-wokovu analokupakila siku ili kukabiliana na changamoto za maisha, na kwa ahadi yake yakukupa pumziko-la-Sabato kila juma ili kuufanya imara uhusiano wakopamoja naye? Endapo wewe hujapata kamwe kufanya hivyo, Je!
ungependa kuupokea wokovu anaokupa? Je, ungependa kumwambiakwamba unatamani kuitunza Sabato yake kila juma? Je! ungependakumwambia, “Ndiyo, Bwana! Natamani kuipata furaha yangu katika siku ileuliyoiweka? Kwa nini usitoe ahadi yako kwake sasa?
(Huenda wewe unashangaa: Ni nani aliyeibadili Sabato kutoka Jumamosikwenda Jumapili, siku ya kwanza ya juma? Badiliko hilo lilifanyika lini? Je!hivi Mungu alitoa idhini yake kwa badiliko hilo? Maswali haya yatajibiwakatika Mwongozo 21.)

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top
MKUSDA CHURCH