SIRI YA FURAHA
Mwaka 1943, majeshi ya Uvamizi ya Kijapani yaliwaamuru wale “WananchiMaadui” wa Kimarekani na Ulaya kwenda katika kambi la waliotekwa vitanikatika lile Jimbo la china la Shantung.
Walilazimika kustahimili miezi mingi ya kuchosha sana, ya kukata tamaa, yakusongamana pamoja na ya hofu. Watu wenye tabia tofauti waligongana,hasira zililipuka. Magomvi madogo madogo yaliongezeka sana.
Lakini mtu mmoja alielezwa na mfungwa mmoja wa kivita kwamba “bilashaka lolote alikuwa ni mtu aliyehitajika sana na kuheshimiwa sana, tenaaliyependwa sana katika kambi lile. “-Eric Liddell, Mmishonari kutoka katikanchi ya Waskoti (Scotland).
Malaya mmoja wa Kirusi katikakambi lile baadaye aliwezakukumbuka ya kwamba yule Liddellni mwanaume peke yake aliyewezakumtendea yule mwanamke jambololote bila kutaka kulipwa kimwili.Mwanamke yule alipokuja mlekambini kwa mara yake ya kwanza,akiwa peke yake, na mwenyekudharauliwa, ndiyealiyemtengenezea yeye baadhi ya rafu za kuwekea vitu vyake.
Mfungwa wa vita mwingine alikumbuka kwamba, “yeye alikuwa na mbinuya upole, na ya kuchekesha iliyozilainisha hasira zao zilizovurugika vibaya”.
Katika mkutano mmoja uliojaa hasira wa wafungwa wale wa kivita, kilammoja alikuwa akitoa madai yake kwamba mtu fulani mwingine ndiyeangefanya kitu fulani kwa wale vijana watukutu wenye umri wa kuanziamiaka kumi na mitatu hadi kumi na tisa (matineja) ambao walikuwawanajitia katika matatizo. Liddell akatoa suluhisho lake. Aliandaa michezoya kujiburudisha, ufundi wa kutengeneza vitu kwa mikono, na madarasakwa ajili ya watoto wale, na kuanza kutumia wakati wake wa jioni pamojanao.
Liddell alijipatia sifa na utukufu katika Michezo ya Olimpiki ya mwaka wa192, alijinyakulia nishani ya dhahabu katika mbio za mita 400. Lakini katikauwanja ule mdogo sana wa kambi lile alijionyesha pia ya kuwa ni mshindikatika zile mbio za Kikristo, akajipatia sifa kutoka kwa wafungwa wa vitawale walioipenda sana dunia hii.
Je! Ni kitu gani kilichomfanya kuwa mtu wa aina yake? Ungeweza kuwaumeigundua siri yake saa 12 kila asubuhi. Ule ndio wakati alipotoka kimyakimya kwa kunyatia akiwapita wenzake waliolala usingizi, na kutulia kimyamezani, na kuiwasha taa ndogo ili itoe mwanga wa kumwezesha kulionadaftari lake ndogo na Biblia yake. Eric Liddell alitafuta neema na nguvu kilasiku kutoka katika utajiri wa Neno la Mungu.
1.Kitabu Cha Mwongozo Wa Kuishi Mtindo Wa Maisha Ya Kikristo
Biblia iliandikwa kama kitabu cha Mwongozo kwa Mkristo. Kimejaa visavingi vya watu halisi walio kama sisi waliokabiliwa na changamoto zile ziletunazokutana nazo kila siku. Kuwafahamu wahusika hao wa Biblia – furaha
na huzuni zao, matatizo yao na nafasizao nzuri walizopata hutusaidia sisikukomaa kama Wakristo.
Mtunga Zaburi, Daudi aonyeshamfano wa kulitegemea Neno la Mungukila siku kwa kulilinganisha namwanga wa tochi (kurunzi);
“Neno lako ni taa ya miguu yanguna mwanga wa njia yangu.” Zaburi119:105.
(Isipokuwa pale ilipoelezwavinginevyo, mafungu yote ya Maandiko katika GUNDUA Miongozoyanatoka katika Toleo Jipya la Kimataifa la Biblia – New InternationalVersion (NIV).
Nuru tunayoipata kila siku kutoka katika Biblia inafunua wazi sifa ziletunazozihitaji katika maisha yetu na kanuni za kukua kiroho. Zaidi ya hayoyote, Biblia inatuonyesha Yesu, Nuru ya Ulimwengu. Maisha yetu yanamaana tu anapoyaangazia Yesu kwa Nuru yake.
2.Urafiki Unaotubadilisha Kabisa
Kristo anataka Biblia kwako iwe kama baruauliyoandikiwa mwenyewe itokayo kwa rafikiyako wa karibu sana.
“Ninyi nimewaita rafiki, kwa sababu kilakitu nilichokisikia kwa Babanimewajulisheni.” – Yohana 15:15.
Yesu anatutakia mema matupu. Neno lakelinatuingiza sisi katika familia ile ya ndani yaMungu; Yaani, ya wale anaowaambia sirizake na kuwafundisha yeye mwenyewe.
“Nimewaambieni ninyi mambo hayo, ilindani yangu ninyi mweze kuwa naamani.” – Yohana 16:33.
Ili kuweza kuionja amani hiyo, na uhusiano huo thabiti pamoja na Kristo, nilazima tuzisome barua zake anazotutumia. Hivyo ndivyo Biblia ilivyo: nibarua zitokazo mbinguni. Usiziache barua hizo bila kuzifungua. Ujumbeuwezao kuyabadilisha kabisa maisha yako ambao unauhitaji umo ndani yaNeno hilo.
Hapa upo ushuhuda mmoja kamili uhusuo matokeo ya kuisoma Biblia.”Mimi nilihitaji msaada, nao niliupata ndani ya Yesu. Kila haja yanguilitimizwa, njaa ya nafsi yangu ilishibishwa; kwangu Biblia ni ufunuo wakeKristo. Namwamini Yesu kwa sababu yeye kwangu ni Mwokozi waKimbingu. Naiamini Biblia kwa sababu nimeiona kuwa ni sauti ya Mungurohoni mwangu. ” – The Ministry of Healing, uk. 461.
3.Miongozo Ya Kuishi Kwa Kufuata Biblia Na Zile Amri Kumi
Kuziangalia kwa kifupi tu hizo Amri Kumi kutatusaidia kuelewa kwa nini hizopamoja na Biblia hujenga msingi muhimu sana wa maisha yaliyo manyofu.
Amri hizo kwa kawaidahuangukia katika sehemu kuumbili. Zile nne za kwanzahufafanua uhusiano wetu naMungu, na zile sita za mwishohufafanua uhusiano wetu nawatu wengine. Zinapatikanakatika Kutoka 20:3-17.
Amri mbili za kwanza zinaelezeauhusiano wetu na Mungu pamoja na ibada yake.
I.”Usiwe na Miungu mingine ila Mimi”.
II.”Usijifanyie sanamu ya kuchonga. Usizisujudie wala kuzitumikia…”
Amri ile ya 3 na ya 4 hueleza kwa juu juu tu uhusiano wetu na jina la Munguna siku yake takatifu.
III.”Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako…”
IV.”Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mamboyako yote, lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako…”
Amri ya 5 na ya 7 inaimarisha vifungo vya familia.
V. “Waheshimu baba yako na mama yako….”
VI.”Usizini.”
Amri ya 6, 8, 9 na 10 hutulinda sisi katika uhusiano wetu kijamii.
VII.Usiue.”
VIII.”Usiibe.”
IX.”Usimshuhudie jirani yako uongo.”
X. “Usiitamani nyumba ya jirani yako. Usimtamani mke wa jirani yako…..wala chochote alicho nacho jirani yako.”
Amri hizo kumi zinaweka mipaka ya uhusiano wetu kwa Mungu na kwawatu wengine. Hizo ni nguzo za kutuongoza katika mtindo wa maisha yetuya Kikristo.
4.Aliyosema Yesu Juu Ya Hizo Amri Kumi
Siku moja Yesu alipokuwa akifundisha, kijana mmoja mwanaume mwenyeari kubwa aliharakisha kwenda kwake na kumwuliza, “Mwalimu, nitendejambo gani jema ili nipate uzima wa mielel?” (Mathayo 19:16). Yesu aliwezakuona yule kijana alikuwa akipambana na tatizo la fedha, ndipo akamshaurikuachana na mali yake na ku”zishik(a) amri” (fungu la 17).
Yule kijana mwanaume alijaribu kuukwepautambuzi wa tatizo lake alioufanya Kristo kwakuuliza ni amri zipi alizokuwa akiziongelea.Yesu akaorodhesha amri kadhaa katika zileAmri kumi (fungu la 18, 19).
Mwishowe, yule “mtawala kijana tajiri”aligeuka na kwenda zake kwa huzuni(mafungu ya 20-22). Kiakili yeye alizikubalizile Amri kumi, ila hakuweza kuitii roho ya ileSheria kwa kuachana na njia yake ya maishaya uchoyo.
Amri kumi zinatuonyesha sisi mipaka ambayo ndani yake unaweza kukuauhusiano wenye afya pamoja na Mungu na kila mmoja wetu. Yesu alisondakidole chake kwenye utii kuwa huo ndiyo njia ya kuipata furaha ya kweli.
“MKIZISHIKA AMRI ZANGU, mtakaa katika pendo langu, kama vilemimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake.Mimi NIMEWAAMBIA NINYI ILI furaha yangu iwe ndani yenu, naFURAHA YENU IWE KAMILI.” Yohana 15:10,11.
5.Mwongozo Kwa Maisha Yenye Furaha
Kitabu cha Mhubiri ni taarifa ya utafiti wa Sulemani juu ya furaha.Anaandika kumbukumbu ya safari zake za kutafuta furaha katika utajiri waulimwengu huu, nyumba za kifahari, mashamba ya mizabibu izaayo sana, bustani nzuri sana, na mashamba ya miti ya matunda matamu sana yenyeharufu nzuri. Aliongeza idadi ya watumishi wake. Alijikuta amezungukwa nakila kitu ambacho mtu angeweza kukitamani. Lakini furaha ikateleza nakwenda mbali naye, ndipo akaandika, akasema.
“Nilipozichunguza kazizote zilizokuwa zimefanywa na mikono yangu, na kusumbuka kwangukote katika kuzitenda, kila kitu kilikuwa hakina maana kabisa, ilikuwani sawa na kujilisha upepo” – (Mhubiri 2:11).
Ndipo Sulemani alipogeuka ili kuzitafuta anasa za ulimwengu huu kwatumaini la kuipata furaha. Akatawaliwa na mvinyo, wanawake, na nyimbo.Hitimisho lake ni hili:
“Bure kabisa, bure kabisa, nakuambia mimi, Mhubiri! Kila kitu ni burekabisa” (Mhubiri 12:8.
Zamani Sulemani alikuwa amepata kuonja na kuona ya kuwa Bwana yumwema. Alipoyalinganisha maisha yake yale ya kwanza ya utii wake kwaMungu na maisha yake ya kutafuta furaha katika mambo ya dhambi bilakujali kitu, wosia wake ukawa ni huu:
“Hili ndilo hitimisho la jambo hilo: Mche Mungu, na kuzishika amrizake, kwa maana huo ndio wajibu wote umpasao mtu.” – Mhubiri12:13.
Sulemani aliona angeweza kutafuta njia ya mkato ya kupata furaha kwakuishi maisha mapotovu. Karibu na mwisho wa maisha yake, alikuwamwanaume tosha kuweza kukiri kosa lake. Ili kuwaokoa wengine wasitendekosa lile lile, aliandika maneno haya,
“Yule aitunzaye Sheria, ana furaha.”Mithali 29:18, KJV.
6.Amri Kumi Ni Mwongozo Muhimu Sana Wa Agano Jipya
Katika Agano jipya, Yakobo alitoaushuhuda wake huu:
“Maana yeyote anayeishika sheriayote, lakini anajikwaa katika nenomoja tu ana hatia ya kuivunja yote.Kwa maana yeye aliyesema;”Usizini, pia alisema, “Usiue”,Usipozini, lakini ukiua, umekuwamvunja sheria. Semeni ninyi, nakutenda kama watu walewatakaohukumiwa kwa sheriainayowapa uhuru. “Yakobo 2:10-12.
Charles Spurgeon, Mhubiri Mkuu waKibaptisti wa karne iliyopita alitangazaakisema.” Sheria ya Mungu ni Sheriaya Mbinguni – takatifu, ya Mungu, nakamilifu—- Hakuna amri yake hatamoja iliyozidi kiasi; hakuna amri yakehata moja iliyopungua mno, lakiniyenyewe haina kifani kiasi kwambaukamilifu wake ni uthibitisho wa Uungu wake.” John Wesley, mmojawapowa Waasisi wa Kanisa la Methodisti, aliandika maneno haya juu ya tabia yakudumu ya sheria hiyo. “Sheria hiyo ya Maadili iliyo katika hizo amri kumi….Yeye (Kristo) hakuiondoa…. Kila kipengele cha Sheria hiyo ni lazimakiendelee kuwa na nguvu juu ya wanadamu wote na katika vizazi vyote….Sermons, gombo la 1, kurasa 221,222.
Billy Graham, Mwinjilisti wa Kiinjili wa Ulimwengu mzima aliyeheshimiwasana, anaziheshimu sana Amri kumi kiasi kwamba ameandika kitabu kizimajuu ya umuhimu wa amri hizo kwa Mkristo.
7.Uwezo Wa Kutii
Biblia pamoja na zile Amri Kumi ni mwongozo usiobadilika, wa muhimusana, na mkamilifu uletao maisha yenye furaha. Lakini, basi, mioyo ya watubado inayo mapambano ndani yake. Mwanamke mmoja alijieleza kamaifuatavyo: “Mimi naamini kwamba hizo Amri kumi zinawafunga watu wote,nina hakika kwamba kuzishika huleta furaha. Nimejitahidi kwa nguvu zangu zote kuzishika, lakini siwezi kuzishika.
Ninaanza kuamini kwamba hakunamtu mwingine awaye yote anayeweza kuzishika.”
Mwelekeo wa asili wa mtu ni kujaribukuishi maisha hayo ya utii kwa hizoamri za Mungu. Lakini kujitahidi kamahuko, tena na tena, kunakotoka katikamoyo wenye dhambi wa mtuhuleta jibuhili la kukatisha tamaa, “Mimi siwezikutii!” kwa nini? Kwa sababu.
“Nia yenye dhambi ina uadui naMungu. Haitii sheria ya Mungu, walahaiwezi kuitii.” Warumi 8:7.
Je! Kusudi la sheria hiyo ya Amri kumi ni nini?
“Kwa njia ya sheria (Amri kumi) sisi tunaitambua dhambi.” Warumi3:20.
Kazi ya sheria (Amri Kumi) ni kutufanya tutambue kabisa kwamba sisi” tuwenye dhambi tuliopotea na kuwa bila tumaini, ambao tunamhitaji Mwokozi.
“Sheria (Amri kumi na Sheria ya Kafara) ilipewa madaraka juu yetukutuongoza kwa Kristo ili tupate kuhesabiwa haki kwa imani.” -Wagalatia 3:24.
Yesu ndiye jibu! Mara tu sisi tunapokuwa miguuuni pake Yesu, tukiwahatuna uwezo wowote kabisa, tunaweza kupokea msamaha kwa ajili yadhambi zetu, pamoja na uwezo toka kwake utakaotuwezesha kuzitii amrizake kwa njia ya imani.
8.Utii Kwa Amri Kumi Utokanao Na Upendo
Yesu anatuambia kwamba utii ni matokeo ya upendo.
“Mkinipenda, mtazishika amri zangu” – Yohana 14:15.
Tukimpenda Mungu, tutazitii amri zile nne za kwanza zinazofafanuauhusiano wetu na Mungu; na kama tukiwapenda watu, basi, tutazitii zile sitaza mwisho ambazo hufafanua uhusiano wetu na wengine.
Mtu awaye yote anayezikanyaga Amri Kumichini ya miguu yake anatenda dhambi.
“Kila mmoja atendaye dhambi anaivunjasheria (Amri Kumi); ukweli ni kwamba,dhambi ni uvunjaji wa sheria (Amrikumi),” 1Yohana 3:4.
Lakini Mungu na ashukuriwe, tunayeMwokozi aliyekuja katika dunia hii na kufa,alifufuliwa, na sasa yu hai kwa ajili ya kusudi moja tu:
“Lakini ninyi mnajua ya kwamba alikuja ILI AZIONDOE DHAMBIZETU.”- Fungu la 5.
Ndani yetu hatuna uwezo wowote kutuwezesha kuishika hiyo sheria yaMungu (amri kumi). Upendo wa Mungu “uliomwagwa…. Ndani ya mioyoyetu” ndilo tumaini letu la pekee.
9.Neema Ya Mungu Na Utii Wetu Kwa Sheria Yake
Wokovu ni zawadi. Hatuwezi kuufanyia kazi ili tuweze kustahili kuupata.Tunaweza tu kuupokea kwa imani. Tunakupokea huko kuhesabiwa haki(kuwa katika msimamo sahihi na Mungu) kama zawadi; kwa njia ya imanipeke yake kwa sababu ya neema yake Mungu.
“Kwa maana MMEOKOLEWA KWA NEEMA, kwa njia ya IMANI-na hiyohaitokani na nafsi zenu wenyewe, ni ZAWADI TOKA KWA MUNGU – Si kwa matendo, mtu yeyote asije akajisifu” Waefeso 2:8.
Hatuwezi kuzishika amri hizo kwamatendo yetu wenyewe – yaani, kwakujitahidi kwetu. Hatuwezi kuzishikaamri hizo ili tupate kuokolewa. Lakinitunapomwendea Yesu kwa imani naunyenyekevu na kuokolewa naye, hapondipo upendo wake unaijaza mioyoyetu. Kama matokeo ya neema hiyo yaMungu na kukubaliwa naye, sisitunaingiwa na shauku ya kumfuatayeye na kumtii kwa njia ya uwezo waupendo wake ulio ndani ya mioyo yetu(Warumi 5:5).
Paulo anatilia mkazo wake juu yakutokufaa kabisa kwa juhudi zakibinadamu, naye anadokeza kwambasisi hatuko chini ya sheria kama njia ya kujipatia wokovu wetu, bali tuko”Chini ya neema.”
“Je! Tutende dhambi (tuzivunje Amri kumi) kwa sababu hatuko chiniya sheria (amri kumi) bali chini ya neema? Hasha!” – (Warumi 6:15).
Kwa nini? Kwa sababu moyo ule unaosukumwa na upendo unazaa maishaya utii utokanao na upendo huo! (Warumi 13:10). Kumpenda Kristo ni kumtiiyeye.
“Yeye aliye na amri (kumi) zangu na kuzitii, ndiye anipendaye mimi.”Yohana 14:21.
Eric Liddel alidhihirisha kwamba, hata katika mazingira mabaya sana,muumini aliyepewa uweza wa Mungu unaweza kuishi maisha ya kuridhika,maisha ya utii. Liddell alionyesha wazi tabia yake iliyowavutia watu katikakipindi kile cha dhiki na hofu. Uhusiano wake wa upendo kwa Kristo ulimtianguvu kwa njia ya Roho Mtakatifu, na kumwezesha kuyatimiza “matakwaya haki yanayodaiwa na sheria” (Warumi 8:1-4). Uhusiano wa upendo nayule Mwokozi aliyesubiliwa na kufufuka unaweza kuzaa aina hiyo yamaisha.
Je! Hivi wewe umeigundua mwenyewe siri hii? Upendo wa Kristo kwa ajiliyako ulimfanya atoe maisha yake kwa ajili ya dhambi yako. Yeye anajitoleakuutia nguvu uhusiano wako wote kwa kukupa upendo wake na kuku”fan(ya) (wewe) kuwa (m) kamilifu katika kila tendo jema ili upate kutendamapenzi yake” (Waebrania 13:12). Jibu lako ni lipi?