MKUSDA CHURCH
Unity in Worship

14. SIRI YA OMBI LINALOJIBIWA

SIRI YA OMBI LINALOJIBIWA
Anatoli Levitini, mwandishi na mwanahistoriawa Kirusi, alitumia miaka yake mingi katikaGulag ya Siberia, ambako dua zilizotolewa kwaMungu zilionekana kana kwamba zimegandaardhini. Lakini alirudi akiwa mzima kiroho.”Mwujiza mkuu kuliko yote ni maombi,”aliandika. “Yanipasa tu kumgeukia Mungukimawazo na mara moja naisikia nguvuinayoingia ndani yangu kutoka mahali fulani,inaingia katika roho yangu, na mwili wanguwote. Je! hicho ni kitu gani? Je, naweza kuipatawapi hiyo nguvu inifanyayo mimi kuwa mtumpya na kuniokoa mimi, niliye mzee duni sana,niliyechoka na maisha, ambayo itaniinua juu yadunia hii? Inatoka nje yangu – wala hakunanguvu yo yote ulimwenguni humu ambyoingeweza kuipinga.”
Katika mwongozo huu tunaona jinsi maombi yanavyotusaidia kujengauhusiano wenye nguvu zaidi pamoja na maisha ya Kikristo yenye nguvu.


1.Kuzungumza Na Mungu
Je, tunawezaje kuwa na uhakika kwamba Mungu anatusikia tunapoomba?
“Ndipo mtaniita mimi na kwenda KUNIOMBA, nami NITA SIKILIZA.Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.”-Yeremia 29:12,13.
Je, ni uthibitisho gani aliotoa Yesu kuonyesha kwamba atasikia na kujibumaombi yetu?
“Basi nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona;bisheni, na mlango utafunguliwa kwenu.” – Luka 11:9.
Maombi ni maongezi ya pande mbili. Hii ndiyo maana Yesu anaahidianasema:
“Tazama nasimama mlangoni,nabisha. Mtu ye yote akiisikia sautiyangu, na kuufungua malngo,nitaingia na kula pamoja naye, na yeyepamoja nami.” – Ufunuo 3:20.
Kwa jinsi gani inawezekana kwetu kuketina kuwa na maongezi mazuri wakati wachakula cha jioni pamoja na Kristo?Kwanza, kwa kumwambia kila kitu tulichonacho moyoni mwetu kwa njia yamaombi. Pili, kwa kusikiliza kwa makini.Tunapotafakari wakati wa maombi,Mungu anaweza kuongea nasi moja kwamoja. Na tunapolisoma Neno la Mungukwa roho ya ibada, Mungu atawezakuongea nasi kupitia katika kurasa zake.
Maombi yanaweza kuwa njia ya maisha kwa Mkristo.
Kiswahili 14
2/6
“OMBENI BILA KUKOMA; shukuruni kwa kila jambo, maana hayondiyo mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.” – 1 Wathesalonike5:16-18.
Je! sisi tunawezaje “kuomba bila kukoma?” Je, yatupasa kupiga magotiwakati wote au kurudia-rudia kusema maneno ya kumsifu au kutoa dua?La, hasha. Lakini tunapaswa kuishi karibu sana na Yesu kiasi cha kujisikiahuru kusema naye wakati wo wote, na mahali po pote.
“Tukiwa katika makundi ya watu mitaani, katika shughuli ya kibiashara,tunaweza kutoa dua yetu kwa Mungu na kumsihi atupe uongozi wake…Daima tungeacha wazi mlango wa moyo wetu na kuuacha mwaliko wetuukipanda juu ili Yesu aweze kuja moyoni mwetu na kukaa humo kamamgeni wetu wa mbinguni.” – Steps to Christ, uk. 99.
Mojawapo ya njia bora sana ili kujenga uhusiano huo wa karibu sana nikujifunza kutafakari wakati tunapoomba.
“Kutafakari kwangu na kumpendeze yeye, mimi ninapomfurahiaBWANA.” -Zaburi 104:34.
Unapoomba usiharakishe tu kupitia orodha ya mambo unayotaka. Ngojea.Sikiliza. Kutafakari kidogo ukiwa katika maombi kunaweza kuuboreshasana uhusiano wako na Mungu.
“Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi.” – Yakobo 4:8.
Kadri sisi tunavyozidi kumkaribia sana Yesu ndivyo kadri tunavyowezakuonja kuwako kwake. Basi wewe unapaswa kuwa katika umbali wakuweza kuongea na Yesu, wala usiwe na wasi wasi juu ya kusema manenoyaliyo sahihi. Ongea tu naye kwa unyofu wa moyo na bila kuficha kitu.Ongea juu ya kila kitu. Yeye amepitia maumivu makali sana ya kifo kilechenyewe ili apate kuwa Msiri wako.


2.Jinsi Ya Kuomba
Tunapoingia katika maombi,tunaweza kupenda kufuatamuhtasari wa sala ya Bwana,sala ya mfano ambayo Yesualiwafundisha wanafunzi wakekuitikia ombi lao hili:
Tufundishe sisi kuomba.
“Baba yetu uliye mbinguni,jina lako litukuzwe, ufalmewako uje, mapenzi yakoyatimizwe hapa dunianikama huko mbinguni. Utupe leo riziki yetu. Utusamehe deni zetu,kama sisi nasi tulivyowasamehe wadeni wetu. Wala usitutiemajaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu, kwa kuwa ufalme ni wako,na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina” – (Mathayo 6:9-13).
Kulingana na mfano huo ambao Yesu aliutoa katika sala yake, sisitunatakiwa kumwendea Mungu kama Baba yetu aliye mbinguni.Tumwombe kwamba mapenzi yake yatawale mioyo yetu kama vile mapenziyake yanavyotawala katika mbingu yote. Tunamtafuta ili atupatie mahitajiyetu ya kimwili, msamaha wake, kwa ajili ya kuwa na roho ya kuwasamehewengine.
Kumbukeni ya kwamba uwezo wetu wa kuipinga dhambi unatoka kwaMungu. Sala ya Kristo inahitimisha kwa maneno ya sifa kwake.
Safari nyingine Yesu aliwafundisha wanafunzi wake kumwomba Baba “kwajina langu” (Yohana 16:23) – yaani, kuomba kulingana na kanuni zake Yesu.Hii ndiyo maana Wakristo kwa kawaida hufunga sala zao kwa manenohaya: “Katika jina la Yesu, Amina.” Amen (amina) ni neno la Kiebranialimaanishalo “Na iwe hivyo”.

Japokuwa sala ya Bwana inatoa mwongozo juu ya mambo tunayotakiwakuyaomba na jinsi ya kutunga sala, mawasiliano yetu na Mungu yanakuwabora sana kama yanatoka moyoni mwetu kwa hiari.
Tunaweza kuomba juu ya kila kitu. Mungu anataka tumwombe msamahakwa dhambi zetu (1Yohana 1:9), tumwombe atuongezee imani (Marko9:24), tumwombe uponyaji wa maumivu na magonjwa yetu (Yakobo 5:15),na kumwagiwa kwa Roho (Zakaria 10:1). Yesu anatuthibitishia kwambatunaweza kumpelekea yeye mahitaji yetu yote, pamoja na mashaka yetu;mno kuweza kumwomba.
(“Mwekeeni matatizo yenu yote, maana yeye anawatunzeni”) – 1 Petro5:7.
Mwokozi wetu anapendezwa na mambo yo yote madogo yahusuyo maishayetu. Moyo wake huchangamka wakati inapomwendea mioyo yetu kwaupendo na imani.


3.Maombi Ya Faragha
Wengi wetu tunayo mambo fulani ambayotunasita kuwaambia hata marafiki zetu wa karibusana. Kwa hiyo, Mungu anatualika sisi kuutuamzigo huo katika maombi yetu ya faragha: tukiwakila mmoja peke yake na yeye. Si kwamba yeyeanahitaji maelezo yote. Mwenyezi anajua vizurisana kuliko sisi tunavyojua, makusudi yetuyaliyojificha moyoni mwetu, na chuki zetuzilizojificha ndani. Lakini tunahitaji kuifunua mioyoyetu kwake yeye atujuaye mpaka ndani kabisa,na atupendaye milele. Uponyaji unaweza kuanzaYesu anapoweza kuyagusa majeraha yetu.


Tuombapo, Yesu, Kuhani wetu Mkuu, yu karibu nasi kutusaidia:
“Tunaye mmoja ALIYEJARIBIWA KWA KILA NJIA, KAMA SISITUNAVYOJARIBIWA -lakini alikuwa hana dhambi. Basi na tukikaribiekiti cha neema kwa ujasiri, ili tupate kupokea rehema na kupata neemaya kutusaidia wakati wa mahitaji” – (Waebrania 4:15,16).
Je, una wasi wasi, mfadhaiko, hatia? Weka hayo mbele zake Bwana. Ndipoyeye anaweza kukidhi kila hitaji tulilo nalo.
Je, ni lazima tuwe na mahali maalumu pa maombi hayo ya faragha?
“wewe unaposali, ingia katika chumba chako, funga mlango nakumwomba Baba yako, ambaye.. atakujazi.” – Mathayo 6:6.
Zaidi ya kuomba wakati wa kutembea mitaani, kufanya kazi, au kufurahiamkutano fulani, kila Mkristo angekuwa na muda fulani uliotengwa kila sikukwa maombi yake yeye peke yake pamoja na kujifunza Biblia. Tunza miadiyako ya kila siku na Mungu wako wakati unapokuwa mchangamfu sana nawakati unapokuwa makini sana.


4.Maombi Ya Hadhara
Kujiunga pamoja na wengine katikamaombi huwaunganisha watu kwakifungo maalum na kukaribisha uwezawa Mungu kwa njia ya pekee.
“Kwa kuwa wawili au watatuwanapokusanyika pamoja katika jinalangu, nipo pamoja nao pale.” -Mathayo 18:20.
Mojawapo ya mambo makuu kulikoyote tuwezayo kufanya sisi kamafamilia ni kukuza maisha ya maombi ya pamoja. Waonyesheni watotokwamba tunaweza kupeleka mahitaji yetu kwake moja kwa moja.

Watakuwa na msisimko juu ya Mungu watakapoona anajibu maombiyanayohusu mambo halisi ya maisha yao. Ifanyeni ibada ya familia kuwawakati wa furaha na kubadilishana uzoefu wa maisha katika hali ya uhuru.


5.Siri Saba Za Maombi Yanayojibiwa
Musa alipoomba, Bahari ya Shamu iligawanyika. Eliya alipoomba, motoulishuka kutoka mbinguni. Danieli alipoomba, malaika aliyafumba makanwaya simba wale wenye njaa kali. Biblia inatueleza visa vingi vya kusisimuavya maombi yaliyojibiwa. Tena inapendekeza kwetu maombi kama njia yakupata ule uweza kwetu maombi kama njia ya kupata ule uweza mkuu waMungu. Yesu anaahidi hivi:
“Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nami nitalifanya” – (Yohana14:14).
Lakini maombi mengine bado yanaonekana kana kwamba hayasikilizwi.Kwa nini? Hapa chini zipo kanuni saba zitakazokusaidia wewe kuomba kwaufanisi zaidi:
(1)Uwe karibu sana na Kristo.
“NINYI MKIKAA NDANI YANGU, na maneno yangu yakikaa ndani yenu,ombeni mtakalo lote nanyi mtapewa.” – Yohana 15:7.
Tunapoupa kipaumbele uhusiano wetu na Mungu na kuwa karibu naye,tutakuwa tunasikiliza na kutazamia kupata majibu kwa maombi yetuambayo, vinginevyo, tusingeyatambua.
(2)Endelea Kumtumaini Mungu.
“MKIAMINI, mtapokea yote myaombayo katika sala zenu” – (Mathayo21:22).
Kuamini au kuwa na imani, maana yake ni kwamba tunamtazamia Babayetu aliye mbinguni kwamba kweli atatupa hayo mahitaji yetu. Kama weweuna wasiwasi kwamba huna imani, basi, kumbuka kwamba Mwokozialitenda mwujiza kwa mtu yule aliyemsihi sana akiwa amekata tamaa,aliyesema:”
“Naamini, nisaidie kutokuamini kwangu!” – (Marko 9:24).
Wewe kazana tu kuitumia imani ULIYO nayo; usiwe na waiswasi juu yaimani ile usiyo nayo.
(3)Jisalimishe kimya kimya chini ya mapenzi ya Mungu.
“Huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu cho choteSAWA SAWA NA MAPENZI YAKE, anatusikia” – (1 Yohana 5:14).
Kumbuka kwamba Munguanataka kutufundisha sisi, pamojana kutupa sisi vitu, kwa njia yamaombi. Kwa hiyo, wakatimwingine anatuelekeza upandemwingine. Maombi ni njia yakutusogeza sisi zaidi na zaidikaribu na mapenzi ya Mungu.Hisia zetu zinatakiwa ziwe kalikutambua majibu ya Mungu nakujifunza kitu kutokana nayo.Kuyafuatilia kwa karibu maombiyetu fulani fulani ya pekee pamoja na kile kinachotokea kuhusiana nayo nimsaada mkubwa kwetu.
Roho Mtakatifu atakusaidia kulenga shabaha yenyewe: “Rohoanawaombea watakatifu kulingana na mapenzi ya Mungu” (Warumi 8:27.Kumbuka kwamba mapenzi yetu yangeweza kulandana siku zote namapenzi ya Mungu endapo sisi tungeweza kuona kama yeye anavyoona.
(4)Mngojee Mungu kwa Saburi.
“NALIMNGOJA BWANA KWA SABURI, akaniinamia akakisikia kiliochangu” – (Zaburi 40:1).

Jambo kubwa hapo ni kukaza mawazo yako yote kwa Mungu, kukazamawazo yako yote juu ya suluhisho lake. Wala usithubutu kumwombaMungu akusaidie kwa dakika moja, na halafu kujaribu kuzizamisha shidazako kwa kujifurahisha katika anasa dakika inayofuata. Umngoje Bwanakwa saburi; tunahitaji kuwa na nidhamu hiyo vibaya sana.
(5)Usiing’ang’anie Dhambi iwayo yote.
(“Kama ningalinuia maovu moyoni, Mwenyezi-Munguhangalinisikiliza”)- Zaburi 66:18.
Dhambi ijulikanayo hukata mara moja uweza wa Mungu katika maisha yetu;inatutenga mbali na Mungu (Isaya 59:1-2). Huwezi kuishika nakuing’ang’ania dhambi kwa mkono mmoja na kunyosha mkono mwinginekupokea msaada wa Mungu. Ungamo la dhambi litokalo moyoni hasapamoja na toba ya kweli ndilo suluhisho la tatizo hilo.
Kama sisi hatutaki kumruhusu Mungu kutuweka huru mbali na mawazo,maneno na matendo yetu mabaya, basi, maombi yetu hayawezi kutuleteajibu lo lote.
“Hata mwaomba, wala hampati, kwa sababu mwaomba vibaya, ilimvitumie kwa tamaa zenu” – (Yakobo 4:3).
Mungu hatajibu “ndiyo” kwa maombi ya uchoyo. Acha wazi masikio yakoyapate kuisikia sheria ya Mungu [Amri Kumi], yaani, mapenzi yake, nayeataacha masikio yake wazi kuzisikia dua zako.
“Yeye aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria [Amri Kumi], hata sala yakeni chukizo” – (Mithali 28:9).
(6)Tambua Kwamba Unamhitaji Mungu.
Mungu huwajibu wale wanaoomba kuwako kwake na uweza wake katikamaisha yao.
“Heri wenye njaa na kiu ya haki, maana hao watashibishwa.” -Mathayo 5:6.
(7)Kuendelea Kuomba Tu.
Yesu alitoa kielelezo cha kuwapo kwa haja ya kuendelea tu kutoa dua zetukwa kusimulia kisa kile cha mjane aliyekuwa anaendelea tu kuomba nakuendelea kuja kwa hakimu akiwa na ombi lake lile, lile. Mwishowe yulehakimu alisema, huku akiwa ameudhika vibaya sana, “Kwa kuwa mjanehuyu ananiudhi, nitahakikisha kwamba nampatia haki yake.” Kisha Yesualitoa hitimisho lake hili: “Je! Mungu hatawapatia haki wateule wakewanaomlilia mchana na usiku? Je! atazidi kuahirisha kuwapatia haki yao?”(Luka 18:5-7).
Zungumza na Mungu juu ya mahitaji yako yote, matumaini yako yote, nandoto zako zote. Omba mibaraka ya pekee, omba msaada unapokuwa nashida. Endelea kutafuta, tena endelea tu kusikiliza, mpaka ujifunze kitufulani kutokana na jibu lake Mungu.


6.Malaika Wanayahudumia Mahitaji Ya Waombao
Mtunga Zaburi alishangilia kwamba kwa njia ya huduma ya malaika waBwana maombi yake yalijibiwa:
“Nalimtafuta BWANA akanijibu; akaniponya na hofu zangu zote…malaika wa BWANA hufanya kituo kuwazunguka wale wamchao nakuwaokoa” (Zaburi 34:4-7).
Tunapoomba, Mungu anawatuma malaika zake kujibu maombi yetu(Waebrania 1:14). Kila Mkristo anaye malaika wake mlinzi anayetembeapamoja naye:
“Angalieni msimdharau mmojawapo wa wadogo hawa. Kwa maananawaambia ya kwamba MALAIKA WAO mbinguni siku zote huutazamauso wa Baba yangu aliye mbinguni.” – Mathayo 18:10.
Kwa sababu ya maombi yetu tunayotoa:
“Bwana yu karibu. Msiwe na wasiwasina jambo lo lote, lakini katika kila jambokwa maombi na dua zetu pamoja nakushukuru, wekeni mambo yenumyatakayo mbele zake Mungu. Ndipoamani ya Mungu, ipitayo ufahamu wote,itawahifadhi mioyo yenu na nia zenukatika Kristo Yesu.” – Wafilipi 4:5-7.


7.Mtindo Wa Maisha Ya Kikristo
Biblia inaeleza wazi juu ya mtindo wamaisha ya Kikristo. Kulingana na Waefeso4: 22-24, Mkristo anatakiwa ku”vua” mtindowake wa maisha ya zamani uliotokana na”tamaa zenye kudanganya”, na ku”vaa” mtindo mpya wa maisha ambaoume”umbwa kwa mfano wa Mungu.” Katika maandiko hayo na mwongozotuligundua kwamba wakati ule wa kuzaliwa upya sisi tuna”umbwa upya”kuwa watu tofauti ndani ya Kristo.
Mwongozo huu na miongozo sita inayofuata hutangaza upya mtindo wamaisha ya Mkristo; huifunua siri ya maisha ya Kikristo yenye furaha.Itakusaidia wewe kujenga uhusiano wenye nguvu zaidi na Kristo, ambaomatokeo yake yatakuwa mtindo wa maisha ya Kikristo ulio tofauti. Kwa hiyokaza macho yako kwa Yesu leo hii, nawe unaweza kuwa na sehemu katikasherehe ile ya mwisho ya ushindi wakati amani yake Kristo itakapotawalabila kupingwa.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top
MKUSDA CHURCH