TOKA MDHAMBI MWENYE HATIA HADIMTAKATIFU ALIYESAMEHEWA
Hapakuwa na alama zo zote za vidole. Hakuna silaha yo yoteiliyogunduliwa. Hakuna mtu ye yote aliyemwona mwuaji yule alipoingiakatika ofisi ya yule daktari. Hakuna ye yote aliyesikia hata zilipofyatuliwazile risasi. Lakini yule daktari alikuwa na risasi tano zimepenya shati yake.
Ilionekana kana kwamba ni uhalifuuliofanywa kwa ustadi sana. MwanzoniPolisi hawakuweza kupata vidokezo vyovyote. Lakini halafu waliona wayamwembamba sana uliofungwa kwenyechombo cha kuwekea kalamu ya risasijuu ya meza ya daktari yule. Waya uleulikwenda kwenye kinasa sauti(tepurekoda) kilichokuwa ndani ya mtotowa meza. Chombo kile cha kuwekeakalamu ya risasi, wakang’amua, kilifichahasa ile maikrofoni aliyoitumia yule daktari kuweka kumbukumbu yamazungumzo yake na wagonjwa aliokuwa akiwapa ushauri.
Wapelelezi waliirudisha nyuma ile tepu ya kurekodia sauti, na kwamshangao wao, wakaanza kuisikiliza ile tepu ilipofunguliwa tena kuhusianana uhalifu ule wenyewe. Mtu aliyeitwa Antoni alikuwa ameingia katika ofisiile na kuanza mabishano makali na yule daktari. Risasi zikafyatuliwa. Tepuile iliishia na sauti ya maumivu makali ya daktari yule, aliyekuwa akifa juuya lile zulia.
Kila habari ndogo ndogo ya kuogofya ilikuwa imerekodiwa. Yule mwuajialidhani kwamba uhalifu wake ule ungebaki kuwa siri milele. Alikuwamwangalifu sana kutokuacha kidokezo cho chote. Lakini ile tepu ilisimuliakisa chote.
Katika mwongozo huu tutajifunza habari za hukumu ya mwisho ya Munguwakati wanadamu wanaendelea “kuhukumiwa sawa sawa na matendo yaokama yalivyorekodiwa katika vitabu vile” (Ufunuo 20:12). Kwa wale ambaohawajampokea Kristo kama Mwokozi wao, itakuwa ni habari mbaya kwao.Lakini hukumu hiyo ni habari njema za ajabu kwa wale walioupata usalamawao ndani yake Kristo.
1.Unaweza Kuikabili Hukumu Hiyo Bila Kuogopa
“Tena Baba hamhukumu mtu ye yote, bali amempa Mwana hukumuyote.” – Yohana 5:22.
Ni kwa jinsi gani ule msalaba ulimwandaa Kristo kuwa Hakimu wetu?
“Mungu alimtoa [Yesu] kuwa kafara ya upatanisho kwa njia ya imanikatika damu yake. Alifanya hivyo ili kuonyesha wazi haki yake,… iliapate kuwa MWENYE HAKI NA MWENYE KUWAHESABIA HAKI walewamwaminio Yesu” – (Warumi 3:25,26).
Kifo cha Kristo kama badala yetu kinamwezesha kufanya kazi yake kamaJaji mwenye haki, na Mwenye kuhesabia Haki aliye na rehema awezayekumsamehe mwenye dhambi yule atubuye. Malimwengu yaleyanayochungulia yanapouliza swali hili, “Je! yawezekanaje kwa Jaji yuleasiyependelea kumtangaza mtu mwenye hatia kuwa hana hatia?” Kristo
anaweza kutoa jibu lake kwakuonyesha makovu katika viganjavyake. Amepata adhabu ya haki kwaajili ya dhambi zetu katika mwili wakemwenywe.
Vitabu vile vya mbinguni hutunzakumbukumbu za maisha ya kila mtummoja mmoja, na kumbukumbu hizozinatumika katika hukumu hiyo (Ufunuo20:12). Hizo ndizo habari mbaya kwawale wanofikiri kwamba dhambi zao zasiri pamoja na uhalifu wao wanaoutenda havitarudi tena kamwekuwasumbua. Lakini kuna habari njema za ajabu kwa wale wotewaliompokea Kristo kwa moyo mnyofu kama mtetezi wao kule mbinguni.”Damu yake Yesu…. Yatusafisha dhambi yote” (1 Yohana 1:7).
Je, Yesu anatupa nini ili kubadilishana na maisha yetu ya dhambi?
“Mungu alimfanya [Kristo] aliyekuwa hana dhambi kuwa dhambi kwaajili yetu ili ndani yake sisi tupate kuwa haki ya Mungu.”- 2 Wakorintho5:21.
Maisha yetu haya ya dhambi yanabadilishana na maisha yale makamilifuya haki aliyokuwa nayo Kristo. Kwa ajili ya maisha yale yasiyo na dhambina kifo chake Yesu, Mungu anaweza kutusamehe sisi na kututendea kanakwamba tulikuwa hatujapata kutenda dhambi kamwe.
Je, ni sifa gani alizo nazo Yesu ambazo zinamfanya kuwa Mtetezi na Jajiwetu?
2.Kristo Alikuja Wakati Ulipotimia
Wakati ule wa ubatizo wake, Yesu alipakwa mafuta na Roho Mtakatifu;
“Mara tu alipokwisha kubatizwa Yesu,alipanda kutoka ndani ya maji; dakika ile ilembingu ikafunuka, akamwona Roho waMungu akishuka kama hua na kutua juu yake. Na sauti kutoka mbinguni ikasema,”Huyu ni Mwanangu, ninayempenda; ninayependezwa sana” – (Mathayo 3:16,17).
Baada ya kupakwa mafuta kwa Kristo naRoho Mtakatifu wakati ule wa ubatizo wake,wanafunzi wake walitangaza, wakisema:
“Tumemwona Masihi’ [Kristo].’ – Yohana1:41.
Wanafunzi wale walijua kwamba neno lile laKiebrania “Masihi” lilimaanisha “MpakwaMafuta.”
Luka, mwanafunzi wa Yesu, aliweka katikakumbukumbu zake mwaka wa Yesu aliopakwa mafuta kama Masihi kuwaulikuwa ni mwaka ule wa kumi na tano wa Kaisari Tiberio (Luka 3:1). Kwetusisi mwaka ule ungekuwa sawa na mwaka wa 27 B.K.
Zaidi ya miaka 500 kabla ya Kristo kuja hapa, nabii Danieli alitabiri kwambaYesu angepakwa mafuta kama Masihi katika mwaka ule wa 27 B.K.
“Tangu kutolewa amri ile ya kuutengeneza na kuujenga upya Yerusalemuhata zamani zake Mpakwa Mafuta (Masihi)…. Kutakuwa na majuma ‘saba’na sitini na mawili jumla yake ni majuma sitini na tisa au siku 483 (7×69=siku 483). Katika mifano ya unabii wa Biblia kila siku ni sawa na mwakammoja (Ezekieli 4:6; Hesabu 14:34), hivyo siku hizo 483 ni sawa na miaka483.
Danieli alitabiri kwamba amri ile ya kuutengeneza na kuujenga upyaYerusalemu ingetolewa katika mwaka ule wa 457 K.K. (Ezra 7:7-26). Kwahiyo, ile miaka 483 ilikoma katika mwaka ule wa 457 na Kristo alipakwa mafuta mwaka wa 27 B.K., (yote hiyo miwili ikiwa ni sehemu tu ya miakayenyewe, kwa hiyo, kipindi sahihi kingekuwa miaka 483).
Kwa wakati ule ule hasa uliowekwa katika mwaka ule wa 27 B.K. Yesualijitokeza akiwa na ujumbe huu:
“Wakati umetimia” (Marko 1:15). Kutimizwa kikamilifu kwa unabii huo waBiblia ni uthibitisho unaovutia sana unaoonyesha kwamba Yesu waNazareti ni Masihi kweli, Mungu katika mwili wa kibinadamu.
Je, ni kwa muda gani Yesu alipaswa kuthibitisha ahadi ile?
“Naye alithibitisha agano [ahadi] thabiti na watu wengi kwa muda wa’saba’ moja [juma, Kiebrania].’ – Danieli 9:27
, sehemu ya kwanza.
Tunapoitumia kanuni ile ya mwaka mmoja siku moja, basi, “juma” hilolingekuwa sawa na miaka saba – kuanzia 27 B.K. mpaka 34 B.K – Yesuangeweza ku”lithibitisha agano,” au ile ahadi aliyokuwa ameitoa kwaAdamu na Hawa muda mfupi tu baada ya wao kutenda dhambi. Mungualifanya agano, yaani, ahadi, kwamba angeiokoa jamii ile ya kibinadmukutoka katika dhambi kwa njia ya yule mmoja ambaye angempeleka ili afekwa ajili ya dhambi zetu (Mwanzo 3:5).
Je, kungetokea nini katikati ya juma hilo la sabini?
“Katikati ya hiyo “saba” [juma, Kiebrania] atakomesha sadaka nadhabihu.” – Danieli 9:27
, sehemu ya mwisho.
Yesu alisulibiwa katika mwaka ule wa 31 B.K.”katikati ya juma.” Wakati ule wa kifo chakeKristo, Mungu akalipasua “pazia lile lahekalu… likapasuka vipande viwili toka juumpaka chini” Mathayo 27:51. Mnyama yulewa dhabihu alikuwa karibu kuchinjwa (mfanowa Yesu “Mwana-Kondoo wa Mungu”),akaponyoka mikononi mwa Kuhani. Hiiilikuwa ni ishara iliyoonyesha kwambaMungu hakutaka wanadamu waendelee tenakutoa dhabihu za wanyama. Unabii uleukatimizwa neno kwa neno, Yesu”akakomesha na kufanya pasiwe na hajatena ya kutoa dhabihu za wanyama. Tangukufa kwake Kristo, watu wanamwendeaMungu si kwa njia ya dhabihu za wanyamana makuhani wa kibinadamu, bali kwa njia ya Masihi, Mwana-Kondoo waMungu na Kuhani wetu Mkuu.
3.Uhakika Wa Dhambi Zilizosamehewa
Kulingana na unabii wa Danieli, je, kwa nini Yesu alikufa?
“Mpakwa mafuta huyo atakatiliwa mbali, lakini si kwa ajili yakemwenyewe.” Danieli 9:26, pambizo.
Alipokufa pale msalabani, Yesu “a[li]katiliwa mbali.” Alikufa, “lakini si kwaajili yake mwenyewe,” yaani, si kwa ajili ya kulipa fidia ya dhambi zakemwenyewe, bali kulipa fidia kwa dhambi za ulimwengu mzima.
Sisi twawezaje kujua kwamba Mungu amezisamehe dhambi zetu zote?
“Haki itokayo kwa Mungu huja kwa njia ya imani katika Yesu Kristokwa wote waaminio… WOTE WAMEFANYA DHAMBI…, naoWANAHESABIWA HAKI bure KWA NEEMA YAKE, kwa njia yaukombozi uliokuja kwa njia ya Yesu Kristo… KWA NJIA YA IMANIKATIKA DAMU YAKE” – (Warumi 3:22-25).
Pointi kuu katika mafungu hayo ni hizi: sisi “[s]ote [tu]mefanyadhambi,’lakini kwa sababu ya “neema,” ya Mungu, wote “wanahesabiwahaki” walio na “imani” katika uwezo wa kutakasa wa “damu” yake Kristo.Tunapohesabiwa haki, Mungu anatutangaza sisi kuwa hatuna hatia,anaondoa hatia inayotokana na dhambi zetu zilizopita. Na Mungu kwa njiaya imani katika Yesu Kristo.
Sisi sote tuliochakazwa na jitihadayetu ya kutaka kuwa wema kiasicha kutosha, ili kukifikia kiwangokile kinachotakiwa kwa kutegemeauwezo wetu wenyewe, tunawezakupata pumziko la kweli kwakukubaliwa na Kristo kwa neemayake. Yeye anatuahidi sisi,anasema, “Njoni kwangu ninyinyote msumbukao na wenyekulemewa na mizigo, naminitawapumzisha” (Mathayo 11:28).Sisi sote tuliolemewa na mizigo ya makovu tuliyopata zamani, kujiona kuwahatufai, tena tuna aibu, tunaweza kupata amani na utimilifu ndani ya Kristo.
4.Wakati Wa Hukumu Kuanza
Katika sura ya nane ya Danieli malaika alimwonyesha yule nabii pichakubwa ya matukio ya siku za baadaye. Danieli alimwona (1) Kondoo mume,(2)beberu, na (3) kutoka katika mojawapo ya pembe za yule beberu,”pembe nyingine iliyokuwa ndogo mwanzoni na kukua nguvu zake” (Danieli8:8,9); mifano hiyo inawakilisha (1)Umedi-Uajemi, (2) Uyunani (Ugiriki), na(3)Roma (Danieli 8:1-12,20-26).
Je, sehemu ya nne ya unabii huo ni ipi?
“Je, itachukua muda gani kwa maono haya kuweza kutimizwa-maonoyahusuyo sadaka ya kuteketezwa ya kila siku….? Akaniambia,’Itachukua jioni na asubuhi 2,300 [au siku, Kiebrania]; ndipo patakatifupatakapowekwa wakfu tena [patakapotakaswa].” – Danieli 8:13,14.
Danieli alizimia kabla yule malaika hajaweza kumweleza sehemu ya siku2,300 ya unabii ule na sura ya nane inafunga bila kutoa tafsiri yake yote.Lakini baadaye yule malaika alitokea tena na kumwambia hivi:
“Yafahamu maono haya:’ Saba’ sabini [majuma, Kiebrania]yameamriwa [yamekatwa, Kiebrania] juu ya watu wako na mji wakomtakatifu, ili kumaliza makosa, kukomesha dhambi, na kufanyaupatanisho kwa ajili ya uovu.” – Danieli 9:22-24.
Kwa kweli, hizo siku 2,300 ni miaka 2,300, kila siku moja ikiwakilishamwaka mmoja (Ezekieli 4:6). Majuma sabini, au miaka 490, ilikuwa ndiyosehemu ya kwanza ya kile kipindi kirefu zaidi cha miaka 2,300. Vipindivyote viwili vilianza katika mwaka ule wa 457 K.K. wakati Uajemi ilipotoaamri ya “kuutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu.” Miaka ile 490ikitolewa kutoka katika miaka 2,300, inabaki miaka 12,810. Ikiongezwamiaka hiyo 1,810 kwa mwaka 34 B.K; mwaka ambao miaka ile 490 ilifikiamwisho wake, inatufikisha kwenye mwaka ule wa 1844 B.K.
5.Patakatifu Pa Mbinguni Patakaswa – Hukumu
Malaika yule alimwambia Danieli ya kwamba katika ule mwaka wa 1844,yaani mwisho wa ile miaka 2,300, “patakatifu patatakaswa” (Danieli 8:14,KJV). Lakini hilo maana yake nini? Tangu mwaka wa 70 B.K. Waromawalipoliteketeza hekalu kule Yerusalemu, watu wa Mungu hawana hekalu lolote hapa duniani. Kwa hiyo patakatifu patakapotakaswa kuanzia ule
mwaka wa 1844 ni lazima pawe ni pale patakatifu pa mbinguni ambapohekalu lile la duniani lilikuwa nakala yake halisi.
Haya! Kutakaswa kwa patakatifu palepa mbinguni maana yake ni nini?Israeli ya zamani iliita siku ile yakupatakasa patakatifu pa kidunia YomKippur, yaani, Siku ya Upatanisho. Kwakweli ile ilikuwa ni Siku ya HUKUMU.
Kama tulivyogundua katika Mwongozo12, kazi ile anayofanya Kristo kwa ajiliyetu katika patakatifu pale ina awamumbili: (1) Dhabihu za kila siku ambazohulenga ile huduma ya Kuhani katika chumba kile cha kwanza cha Patakatifu. (2) Dhabihu ya kila mwakaambayo inaitilia nguvu huduma ya Kuhani Mkuu katika chumba kile cha pili,yaani, Patakatifu pa Patakatifu ( Walawi 16).
Katika lile hekalu la kidunia, watu walipoziungama dhambi zao siku kwasiku, damu ya wanyama wale waliochinjwa ilimwagwa kwenye pembe yamadhabahu ile, kisha ilihamishiwa katika Patakatifu (Mambo ya Walawi 4na 6). Hivyo, kwa mfano, siku baada ya siku dhambi zilizoungamwaziliingizwa ndani ya Patakatifu na kuwekwa pale.
Halafu, kila mwaka, katika ile Siku yaUpatanisho, patakatifu pale palitakaswakutokana na dhambi zotezilizoungamwa katika kipindi cha mwakauliopita (Mambo ya Walawi 16). Ilikufanya utakaso huo, Kuhani Mkuualitoa sadaka maalum ya mbuzialiyewekwa wakfu. Kisha aliichukuadamu yake na kuingia nayo mpakaPatakatifu pa Patakatifu na kuinyunyizadamu ile ya utakaso mbele ya kilekifuniko cha upatanisho [kiti charehema] ili kuonyesha kwamba damu yaYesu, Mkombozi aliyekuwa anakuja,ingeweza kulipa fidia ya dhambi ile.Kisha kwa mfano yule Kuhani Mkuu aliziondoa dhambi zile zilizoungamwakutoka patakatifu pale na kuziweka juu ya kichwa cha mbuzi yule mwingine,ambaye alipelekwa mbali katika jangwa na kuachwa afe kule (Mambo yaWalawi 16:20-22).
Taratibu hiyo ya ibada iliyofanywa kila mwaka katika siku ya upatanishoilipatakasa pale patakatifu kutokana na dhambi. Watu waliiona kuwa ilikuwani siku ya hukumu kwa kwa sababu wale waliokataa kuziungama dhambizao walifikiriwa kuwa ni waovu, nao “walikatiliwa mbali na watu wake[Mungu]” (Mambo ya Walawi 23:29).
Alichofanya kwa mfano, yule Kuhani Mkuu, mara moja kwa mwaka, Yesuanafanya mara moja kwa wakati wote akiwa Kuhani wetu Mkuu (Waebrania9:6-12). Katika siku hii kuu ya hukumu yeye anaziondoa kutoka katikapatakatifu dhambi zile zilizoungamwa za wale wote waliompokea kamaMwokozi wao. Kama sisi tumeziungama dhambi zetu, basi, yeye ataifutakumbukumbu ya dhambi zetu wakati ule (Matendo 3:19). Huduma hiyo nikazi ya hukumu ambayo Yesu aliianza katika mwaka ule wa 1844.
Katika mwaka wa 1844 saa ya hukumu ilipoanza kule mbinguni ujumbe wasaa ya hukumu imekuja ulianza kuhubiriwa ulimwenguni kote (Ufunuo 14:6-7). GUNDUA Mwongozo baadaye litaushughulikia ujumbe huo.
6.Kukabiliana Na Kumbukumbu Ya Maisha Yako Hukumuni
Tangu mwaka wa 1844 Kristo, kama Jaji, amekuwa akiichunguzakumbukumbu ya kila mmoja aliyepata kuishi ili kuthibitisha ni akina naniwatakaokuwamo miongoni mwa wale watakaookolewa Yesu atakapokuja.Kama Jaji wetu, Yesu “anazifuta” dhambi zote za wenye haki kutoka katikakumbukumbu zao za maisha zilizoko kule mbinguni (Matendo 3:19).
Jina lako linapoitwa katika hukumuhiyo, itakuwa rahisi kwako kukabilianana kumbukumbu ya maisha yako -ENDAPO wewe utakuwa umempokeaKristo kama mbadala wako. Nahukumu ya wenye haki itakapokwisha,Yesu atarudi duniani kuwalipa ujirawao (Ufunuo 22:12,14).
Je! hivi wewe u tayari Yesu akija? Au,je! kuna kitu fulani ambacho umekuwaukimficha? Je! unao uhusiano huru nawa kweli na yule Mmoja anayetoa ahadi hii:
“Tukiziungama dhambi zetu yeye ni mwaminifu na wa haki, hataatuondolee dhambi zetu na kutusafisha udhalimu wote.” – 1 Yohana1:9.
Ungamo maana yake rahisi ni kukubali kukabiliana na dhambi zetu,kupokea msamaha wa Mungu, na kukiri kwamba tunahitaji uweza wake naneema yake.
Alipokuwa akilitembelea gereza moja katika mji wa Potsdam, mfalmeFrederick William alisikiliza maombi kadhaa ya msamaha. Wafungwa wotewaliapa kwamba Majaji wale walipendelea, mashahidi walikuwa wa uongo,au wanasheria walikuwa si wanyofu ambao walihusika na kifungo chao.Toka seli hata seli kisa kile kile cha kutendewa vibaya, wao wakiwa hawanahatia, kiliendelea kusimuliwa.
Lakini katika seli moja mfungwa mmoja hakuwa na la kusema. Akiwaameshangaa, Frederick akamtania, “Nadhani na wewe pia huna hatia yoyote.”
“Hasha, mfalme,” yule mtu alijibu, “Mimi nina hatia, tena nastahili kabisayote ninayopata.”
Mfalme akamgeukia mlinzi na kumwita kwa sauti kuu, “Njoo umwachilieupesi mhuni huyu kabla hajaliharibu kundi hili zuri la watu wasio na hatia yoyote.”
Je! tunajiandaaje kwa hukumu hiyo? Tunajiwekaje tayari kwa ajili ya kujakwake Kristo? Kwa kuikiri kweli peke yake kwa moyo mnyofu: Mimi nastahilikabisa adhabu ya kifo kwa dhambi zangu, lakini yule mwingine amechukuamahali pangu na kunipa msamaha wake wa ajabu.
Amua sasa hivi kwamba chochote kile kinachotokea, wewe utadumishauhusiano wako na Kristo ukiwa unatazamana naye jicho-kwa-jicho kwaunyofu wa moyo-kwa-moyo kwa uaminifu.