MKUSDA CHURCH
Unity in Worship

12. MWOKOZI ALIYEPO DAIMA

MWOKOZI ALIYEPO DAIMA
Kijana mmoja wa Kiskoti, kwa jina Petro,alipopotea katika nyika yenye majani mengiusiku mmoja uliokuwa na giza jeusi kamawino, Mungu alimwita kwa jina lake:”Petro!” Sauti ile ya mbinguni ilipoita tena,Petro alisimama katika njia yake,akaangalia chini na kugundua kwambaalikuwa umbali wa hatua moja tukutumbukia katika shimo la machimbo yamawe lililokuwa limeachwa.
Je! isingekuwa ni ajabu kwetu sisi kamatungeweza kumsikia Mungu akituita kwamajina yetu? Je! yasingekuwa makubwakwetu endapo yeye angekuwa rafiki yetualiye karibu sana nasi-endapo tungewezakukaa pamoja naye kabisa na kuongeanaye kwa muda mrefu juu ya mapambanoyetu tuliyo nayo pamoja na zile ndoto zetu?


1.Kwenda Kwa Yesu Bila Kizuizi
Amini usiamini, sisi tunaweza kwenda karibu sana na Yesu sasa kuliko vileambavyo tungeweza endapo Yeye angeishi kabisa hapa pamoja nasi akiwani mtu anayeonekana kwa macho. Kuwa na Yesu kimwili katika mji wetukwa kweli lingekuwa ni jambo la ajabu, lakini hebu fikiria juu ya yalemakundi makubwa sana yatakayomsonga ili yapate kumwona kwa karibuzaidi. Fikiria juu ya muda wake mwingi ambao ungetakiwa kutumika.Lingekuwa ni jambo jema kuweza kupata dakika chache za kuongea nayeana kwa ana katika kipindi chote cha maisha yetu.
Kristo anapenda kujenga uhusiano wake na kila mmoja wetu. Hii ndiyosababu moja iliyomfanya aondoke duniani humu ili kwenda mbingunikufanya huduma ya pekee ambayo ingemwezesha kuja karibu na kilammoja wetu kila siku. Kwa sababu Yesu hajafungwa mahali pamoja kamaalivyokuwa alipokuwa hapa duniani, yeye kwa njia ya Roho Mtakatifu sasayuko tayari kuweza kuyaongoza maisha ya kila mtu mmoja mmoja atakaye.
Je, ni ahadi gani ya kutia moyo aliyoitoa Yesu kabla hajapaa juu kwendambinguni?
“NAMI NIPO PAMOJA NANYI SIKU ZOTE naam, mpaka mwisho wanyakati.” – (Mathayo 28:20).
Je, Kristo anafanya kazi gani kule mbinguni ambayo inafanya uwezekanouwepo kwa yeye kuwa “pamoja nanyi siku zote?”
“Basi, tuzingatie kwa makini imani tunayoungama. Maana tunayeKuhani Mkuu aliyeingia mpaka mbinguni; Yesu, Mwana wa Mungu.Huyu Mkuu wetu anaelewa kabisa unyonge wetu; yeye mwenyewealijaribiwa kama sisi kwa kila namna lakini hakutenda dhambi. Basi, natukikaribie bila hofu kiti cha enzi cha Mungu mwenye neema, tupokeehuruma na neema ya kutusaidia wakati wa shida ” – (Waebrania 4:14-16).
Zingatia ahadi hizi zinazotolewa kwetu tunapokuwa na Yesu kamamwakilishi wetu kila mmoja binafsi kule mbinguni: “Alijaribiwa kama sisi kwa kila namna.” “Kutuhurumia sisi katikaudhaifu wetu.” “Kutusaidia wakati washida.” Tukiwa na Yesu kama Kuhani wetuMkuu hatuendelei tena kutanga mbali nambingu iliyo mbali sana. Kristo anawezakutukaribisha sisi kuingia kabisa mbelezake Mungu. Si ajabu, basi, kwambatunaombwa sana tu “kikaribie bila hofu kiticha enzi cha Mungu mwenye neema”
Je, Yesu anakaa mahali gani kulembinguni?
“Lakini Kristo alitoa dhabihu moja kwaajili ya dhambi milele dhabihu ifaayokisha akaketi UPANDE KULIA WA MUNGU” – (Waebrania 10:12).
Kristo aliye hai-mmoja anayetuelewa sisi-ni mwakilishi wetu kila mmojabinafsi katika kiti kile cha enzi “mkono wa kuume wa Mungu.”
Ni kwa jinsi gani maisha ya Yesu yalimwandaa kuwa Kuhani wetu?
“Ndiyo maana ilimbidi awe kama ndugu zake wa kila namna, ili aweKuhani Mkuu wao aliye mwaminifu na mwenye huruma katikakumtumikia Mungu, ili dhambi za watu ziondolewe. Na, anaweza sasakuwasaidia wale wanaojaribiwa na kuteswa” – (Waebrania 2:17,18).
“Ndugu” yetu aliyeshiriki katika ubinadamu wetu, na ambaye “alijaribiwa”kama sisi tunavyojaribiwa, hivi sasa yeye ni Kuhani wetu Mkuu ameketiupande wa kulia wa Mungu, “Alifanywa kama” sisi, anajua yaletunayoyapitia. Amepata kuwa na njaa, kiu, majaribu, na kuchoka sana kiasicha kuishiwa nguvu. Alijisikia kwamba alikuwa na haja ya kuhurumiwa nakueweleka.
Lakini zaidi ya hayo yote, Yesu anazo sifa za kuwa Kuhani wetu Mkuu kwasababu yeye alikufa ili “kufanya upatanisho” kwa ajili ya dhambi zetu. Alilipagharama yote ya dhambi zetu kwa kufa badala yetu sisi. Hii ndiyo Injili,yaani, Habari Njema kwa wanadamu wote kila mahali na kwa wakati wote.
Mmojawapo wa Wakurugenzi wa Shule yetu ya Biblia anatusimulia kisa hikikilichompata akisema “Binti yetu mdogo kabisa alipokuwa na umri wamiaka mitatu, alijibana kidole chake katika kiti cha kukunjwa, nakuuvunjavunja mfupa wake. Tulipomkimbiza kumpeleka kwa daktari, kiliochake kikali kutokana na maumivu yake kiliturarua kweli mioyo yetu. Tenakikamgusa mtoto wetu wa miaka mitano kwa njia ya pekee. Sitawezakusahau maneno yake aliyosema baada ya daktari kumshughulikia dadayake aliyejeruhiwa. Binti yule akalia kwa kwikwi, na kusema, ‘Baba,natamani kingekuwa ni kidole changu mimi!”
Wanadamu wote waliposetwa na dhambi na kuhukumiwa kufa milele, Yesualisema, “Baba, natamani ningekuwa mimi.” Naye baba akampa Yesu kilealichotamani pale msalabani. Mwokozi wetu amepitia kila aina ya maumivumakali ambayo kwayo sisi tuliteseka – na zaidi ya hayo!


2.Injili Katika Agano La Kale
Wana wa Israeli walipopiga kambiyao chini ya Mlima Sinai, Mungualimwagiza Musa kujenga patakatifuambapo paliweza kusafirishwa tokamahali hata mahali kwa ajili ya ibada”kama mfano wake, ulioonyeshwa[kwako Musa] mlimani “(Kutoka25:40). Karibu miaka 500 baadaye,Hekalu kuu la mawe la mfalmeSulemani lilijengwa ili kuchukuamahali pa hema takatifu lililokuwalikichukuliwa huku na huku. Nahekalu lile lililjengwa kwa mfano ule ule kabisa kama lilivyojengwa hematakatifu lililokuwa linachukuliwa huku na huku.

3.Huduma Ya Yesu Kwetu Imefunuliwa Katika Patakatifu
Patakatifu na huduma zake hufunua kile anachofanya Yesu sasa katikahekalu la mbinguni, na anachofanya sasa hapa duniani ili kututayarisha nakutuongoza kila mmoja wetu katika maisha yetu ya kila siku.
Kwa kuwa patakatifu pale pa duniani palijengwa kwa mfano wa hekalu lambinguni, basi, panaakisi patakatifu pa mbinguni ambako Kristoanahudumu sasa. Kutoka 25-40 huelezea habari za huduma ile na taratibuzake za kafara ya patakatifu pale pa jangwani kwa kinagaubaga sana.Muhtasari mfupi wa vyombo vya patakatifu huonekana katika Agano Jipya:
“Agano la kwanza lilikuwa nakawaida taratibu zake za ibada namaskani takatifu ya duniani.Palitengenezwa hema ambayosehemu yake ya nje ilitwa MahaliPatakatifu. Humo mlikuwa na kinaracha taa, meza na mikate iliyotolewakwa Mungu. Nyuma ya pazia la pili,kulikuwa hema iliyoitwa MahaliPatakatifu sana. Humo mlikuwa namadhabahu ya dhambi kwa ajili yakufukizia ubani, na sanduku laagano, ambalo lilikuwa limepakwadhahabu pande zote, na ndani yake mlikuwa na chungu cha dhahabukilichokuwa na mana, fimbo ya Aroni ilikuwa imechanua majani, navile vibao viwili vilivyoandikwa agano. Juu ya hilo sanduku kulikuwana viumbe wenye mabawa, na mabawa yao yalitanda juu ya mahaliambapo dhambi huondolewa. Lakini sasa hatuwezi kusemakinaganaga juu ya mambo hayo ” – (Waebrania 9:1-5).
Hema hilo takatifu lilikuwa na vyumba viwili, yaani, Patakatifu, na Patakatifupa Patakatifu. Ua uliwekwa mbele ya pataktifu. Katika ua ule ilisimamamadhabahu ya shaba nyeupe ambayo juu yake makuhani walitoa dhabihuzao, na birika la maji walimonawa.
Dhabihu zilizotolewa juu ya madhabahu ile ya shaba nyeupe zilikuwamfano wa Yesu, ambaye, kwa njia ya kifo chake msalabani alikuwa ndiyeyule “Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!(Yohana 1:29). Mwenye dhambi aliyetubu alipokuja na dhabihu yakekwenye madhabahu ile na kuziungama dhambi zake, alipokea msamaha nautakaso. Vile vile mwenye dhambi leo anapata msamaha na utakaso kwanjia ya damu yake Yesu (1 Yohana 1:9).
Katika chumba kile cha kwanza, au Patakatifu,kile kinara cha taa saba kiliwaka daima,kikimwakilisha Yesu ambaye ni “Nuru yaulimwengu” inayowaka daima (Yohana 8:12).Meza ya mikate iliyowekwa wakfu ilimwakilishayeye ambaye ni “Mkate wa Uzima” ambayedaima yupo kukidhi njaa yetu ya kimwili na kiroho(Yohana 6:35). Ile madhabahu ya dhahabu ya kufukizia uvumba iliwakilishahuduma ya Yesu ya uombezi anayofanya kwa ajili yetu mbele za Mungu(Ufunuo 8:3,4).
Chumba cha pili, au Patakatifu pa Patakatifu, palikuwa na sanduku laagano lililofunikwa na dhahabu pande zote. Liliwakilisha kiti cha enzi chaMungu. Kifuniko chake cha upatanisho, au kiti cha Rehema, kiliwakilishauombezi wa Kristo, Kuhani wetu Mkuu, akiwaombea wanadamu wenyedhambi ambao wameivunja sheria ya Mungu ya Maadili [Amri Kuu]. zilembao mbili za mawe ambazo juu yake Mungu aliandika Amri Kumizilihifadhiwa chini ya kile kiti cha rehema. Makerubi wale wawili wa dhahabuwenye utukufu waliinamia kile kiti cha rehema kutoka katika kila mwisho walile sanduku. Nuru tukufu iliangaza katikati ya wale makerubi wawili, hiyoikiwa ni ishara ya kuwako kwake Mungu mwenyewe.
Pazia lilipaficha pale Patakatifu ili pasionekane na watu wakati makuhaniwalipokuwa wakiwahudumia katika ule ua. Pazia la pili mbele ya Patakatifu pa Patakatifu lilikikinga kile chumba cha ndani kisionekane na makuhaniwalioingia katika chumba kile cha kwanza cha Patakatifu.
Yesu alipokufa pale msalabani, je, ni kitu gani kilitokea kwa pazia lile?
“Hapo pazia la hekalu likapasukavipande viwili toka juu mpaka chini” -(Mathayo 27:51).
Patakatifu pa Patakatifu paliachwa waziYesu alipokufa. Baada ya kifo cha Yesu,hakuna pazia liwalo lote lote liwezalokuwepo kati ya Mungu Mtakatifu namuumini aliye mnyofu wa moyo; Yesu,Kuhani wetu Mkuu, anatukaribisha nakutuingiza kabisa mbele za Mungu(Waebrania 10:19-22). Tunayo njia yakukifikia chumba kile ambamo kimo kiticha enzi cha Mungu kwa kuwa Yesu niKuhani wetu Mkuu aliye mkono wa kuliawa Mungu. Yesu ndiye anayetuwezesha sisi kuja mbele za Mungu – yaani,hadi ndani ya ule moyo wa upendo wa Baba. Basi “na tukaribie.”


4.Ufunuo Wa Kristo Akifa Kutuokoa
Kama palivyotumika pale patakatifu pa kidunia kama mfano mdogo kabisawa hekalu lile la mbinguni ambako Yesu anahudumu sasa kwa ajili yetu,huduma zile zilizoendeshwa katika patakatifu pale pa kidunia zilikuwa”mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni” (Waebrani 8:5). Lakini ipo tofautidhahiri ambayo inajitokeza: mkuhani wale waliohudumu katika hekalu laduniani wenyewe walikuwa hawana uwezo wa kusamehe walikuwa hawanauwezo wa kusamehe dhambi, lakini pale msalabani Yesu “alitokea maramoja tu katika utimilifu wa nyakati zile ili aziondolee mbali dhambi kwakujitoa dhabihu yeye mwenyewe” (Waebrania 9:26).
Kitabu kile cha Mambo ya Walawi cha Agano la Kale kinaeleza kwa undanisana huduma zile zilizoendelea kufanywa katika patakatifu pale. Taratibuzile za ibada ya dhabihu ziligawanywa katika sehemu mbili: huduma za kilasiku na huduma za kila mwaka. (Mwongozo 13 unazishughulikia hudumazile za kila mwaka).
Katika zile huduma za kila siku makuhani wale waliotoa dhabihu kwa ajili yamtu mmoja binafsi na kwa ajili ya mkutano mzima. Mtu ye yote alipotendadhambi, alitakiwa kuleta mnyama asiye na waa lolote kama sadaka yake yadhambi, ‘a[li]weka mkono wake juu ya kichwa cha hiyo sadaka ya dhambi,na kumchinja kuwa sadaka ya dhambi mahali hapo pa sadaka zakuteketezwa” (Mambo ya Walawi 4:29). Hatia ya mwenye dhambi yuleilipaswa kuhamishiwa kwa mnyama yule asiye na hatia kwa njia yamaungamo ya dhambi na kuweka mikono juu ya kichwa cha mnyama yule.Jambo hilo lilikuwa mfano wa Kristo akiwa amebeba hatia yetu pale Kalvari;yule mmoja asiye na dhambi alifanywa kuwa “dhambi kwa ajili yetu” (2Wakorintho 5:21). yule mnyama wa dhabihu alipaswa kuuawa na damuyake kumwagwa kwa sababu ilisonda kidole chake mbele kwenye ileadhabu kuu kuliko zote ambayo kwayo Kristo aliteswa vibaya palemsalabani.


5.Kwa Nini Damu?
“Pasipo kumwaga damu hakunamsamaha” (Waebrania 9:22). Kilekilichotokea katika patakatifu pale paAgano la Kale kilisonda kidole chakembele kwenye tendo lile moja kuu lawokovu alilolitenda Kristo. Baada yayeye kufa kwa ajili ya dhambi zetu,”aliiingia patakatifu pale pawili maramoja tu kwa damu yake mwenyewe,baada ya kupata ule ukombozi wamilele” kwa ajili yetu (fungu la 12). Damu ya Yesu ilipomwagika palemsalabani kwa ajili ya dhambi zetu, “pazia lile la hekalu [kule Yerusalemu] ililipasuka vipande viwili toka juu mpaka chini” (Mathayo 27:51). Kwasababu ya ile kafara aliyoitoa Yesu pale msalabani, hapakuwa na haja tenaya kutoa dhabihu zile za wanyama.
Yesu alipomwaga damu yake kutoka katika msalaba ule, alikuwa anatoasadaka ya maisha yake makamilifu ya utii kuwa badala ya kushindwa kwetukwingi. Baba na Mwana walipotenganishwa kwa nguvu pale Kalvari, Babaaligeuka na kuangalia kwingine kwa utungu na Mwanawe alikufa kutokanana moyo wake uliopasuka. Mungu Mwana aliingia katika historia yetu nakuchukua mwilini mwake athari kamili za dhambi zetu na kuonyesha wazijinsi utendaji wa mabaya unavyoleta maafa ya kusikitisha kweli kweli. Hapondipo angeweza kuwasamehe wenye dhambi bila ya kuihafifisha dhambi.Kristo alifanya “amani kwa damu yake iliyomwagika pale msalabani”(Wakolosai 1:20).


6.Ufunuo Wa Yesu Akiishi Kutuokoa
Je! ni kazi gani anayofanya Yesu siku-kwa-siku katika hekalu lile lambinguni?
“Naye kwa sababu hii aweza kuwaokoa kabisa wale wanaokuja kwaMungu kupitia kwake, kwa sababu YU HAI SIKU ZOTE ILIAWAOMBEE” – (Waebrania 7:25).
Yesu sasa “yu hai’ ili kutoa damu yake, yaani, kafara yake, kwa ajili yetu.Sasa yeye anafanya kazi kwa bidii nyingi ili kumwokoa kila mwanadamukutoka katika dhambi iletayo mauti. Wengine kwa kuelewa vibayawanadhani kwamba Yesu, akiwa kama Mwombezi wetu, yuko kulembinguni kwa madhumuni ya kumsihi sana Mungu ambaye hataki iliatusamehe sisi. Kwa kweli ni Mungu anayeikubali kwa furaha kubwa kafaraile aliyoitoa Mwanawe kwa ajili yetu.
Kama Kuhani wetu Mkuu, Kristo piaanawasihi sana wanadamu. Yeyeanafanya kazi yake ili kuwasaidia waleambao hawajali kitu ili waiangalie kwamara ya pili ile neema yake,anawasaidia wenye dhambi ambaowanakata tamaa ili walishikilie sanatumaini lao linalopatikana katika injili, nakuwasaidia katika waumini kupata utajirimwingi zaidi katika maombi yao. Yesuanayatengeneza maisha yetu iliyapatane na amri [Kumi] za Mungu nakutusaidia kuzikuza tabia zetu ambazozitaweza kustahimili lile jaribio la wakati.
Mungu aliyatoa maisha yake na kufa kwa ajili ya kila mwanadamu aliyepatakuishi katika dunia hii. Na sasa, yeye akiwa Kuhani Mkuu au Mpatanishi,”yu hai siku zote” ili kuwaongoza watu wakikubali kifo chake kwa ajili yadhambi zao. Wanadamu hawatapotea kwa kuwa wao ni wenye dhambi, balikwa sababu wanakataa kupokea msamaha ambao Yesu anawapa.
Dhambi iliharibu uhusiano wa karibu sana ambao Adamu na Hawawalifurahia kuwa nao pamoja na Mungu. Lakini Yesu, kama Mwana-Kondoowa Mungu, alikufa ili kuwaweka huru wanadamu wote mbali na dhambi nakuwarudishia tena urafiki ule uliopotea. Je! hivi wewe umemgundua yeyekuwa ni Kuhani wako Mkuu, Mmoja aliye hai siku zote ili apate kuudumishauhusiano huo uwe wa karibu na wa kusisimua sana?
Kifo chake Kristo kilichotolewa kama sadaka ya dhambi ni cha pekeekabisa. Huduma yake Kristo kule mbinguni haina kifani. Ni Kristo peke yakeanayemleta Mungu karibu sana kando yetu. Ni Kristo peke yakeanayefanya uwezekano uwepo kwa Roho wa Mungu kuweza kukaa kabisandani ya mioyo yetu. Alijitoa kabisa yeye mwenyewe ili kutufanya sisitutimike. Anastahili vile vile tujitoe wakfu kwake kama yeye alivyojitoa. Hebuna tumpokee kabisa kama Mwokozi na Bwana wa maisha yetu.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top
MKUSDA CHURCH