MKUSDA CHURCH
Unity in Worship

11. UWEZO WA AJABU KATIKA MAISHA YANGU

UWEZO WA AJABU KATIKA MAISHA YANGU
Katika mwaka ule wa 1929 (Frank Morris) alipanda meli iliyokuwa ikiendaUswisi. Alikuwa ametazamia kufanya safari ile kwa muda fulani. Lakiniikageuka na kuwa safari ya kumdhalilisha. Mtumishi aliyewekwa kumtunzaalimfungia Frank katika chumba chake kila siku. Baada ya kupata kifunguakinywa, kwa haraka-haraka Frank aliweza kufanya mazoezi ya viungokidogo, lakini yeye alijisikia kana kwamba alikuwa mpumbavu kuwezakuongozwa vile huku na huku juu ya sitaha ya meli ile, kama vile yeyealikuwa mnyama anayeongozwa kwa kamba. Wakati wo wote alipokutanana abiria aliyeonyesha urafiki kwake na kumwalika kwenda kutembea naye,yule mtumishi alikataa, akawaambia kwamba alipaswa kumwangalia kilawakati.
Frank alikuwa mtu mzima, mwenye hisia zakawaida za udadisi na tamaa anazopaswakuwa nazo mtu mzima. Lakini yeye alikuwakipofu pia. Yule mtumishi alidhani kwambaasingeweza kujitunza mwenyewe. Frankalitendewa kana kwamba alikuwa kifurushivile, kilichopaswa kuburutwa huku na huku.
Lakini katika nchi ile ya Uswisi maisha yaFrank yalibadilika kwa namna ya kuvutiasana. Alipokuwa kule alijifunza habari zambwa waliokuwa wamepewa mafunzo yakuwaongoza vipofu. Aliporudi kuleMarekani pamoja na kiongozi [mbwa] wakewa safari wa Kijerumani aliyeitwa Buddy,Frank alianzisha Jicho Lionalo, sasa ni shirika lililoenea ulimwenguni kote.
Sasa Frank, akiwa na Buddy kando yake, aliweza kwenda ko kote, wakatiwo wote, na mtu ye yote. Hatimaye alijisikia huru. Katika maonyesho yakeya kwanza kwa waandishi wa habari penye njia panda yenye magari mengikatika lile Jiji la New York, yule Buddy alimwongoza bwana wake kwa ustadikutoka katika njia moja na kuingia katika njia nyingine wakati yale magariyalipokuwa yakiunguruma na kupita. Kwa kuwa yeye alimtumainia yuleBuddy, Frank alivuka kwa urahisi mpaka upande ule wa pili. Waandishi wahabari walioonekana pale walikuwa na wakati mgumu zaidi kuvuka pale;mmoja wao alichukua kabisa teksi ili kwenda upande ule wa pili.
Katika kurasa chache zifuatazo tunakwenda kujifunza juu ya RohoMtakatifu, kiongozi anayetaka sisi tuyakabidhi maisha yetu mikononimwake. Sisi sote tumelemaa kutokana na asili yetu moja ya kibinadamu,tunao upofu ule ule katika mambo yale yaliyo ya maana sana kwetu.Maisha yetu hupita kasi kwa namna ambayo tunajikuta wenyewetunayavumilia tu badala ya kwenda mahali fulani. Hata hivyo, sisi tunasita-sita kuyakabidhi maisha yetu kikamilifu kwa Kiongozi huyo. Lakini ugunduziunaomngojea kila mmoja wetu ni huu: sisi tutapata uhuru wa kweli nauwezo kwa kumtegemea Roho Mtakatifu kutuongoza katika maisha yetuyote.


1.Mwakilishi Wa Kristo Ulimwenguni
Kristo alipokuwa tayari kupaa kwenda mbinguni, aliwaahidi wanafunzi wakekwamba atawapa zawadi ya thamani kuu isiyokadirika:
“Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke kwa maana nisipoondoka huyo MSAIDIZI hatakuja kwenu; bali miminikienda zangu, nitampeleka kwenu. Lakini atakapokuja, HUYO ROHOWA KWELI, ATAWAONGOZA awatie kwenye kweli yote…. YEYEATANITUKUZA MIMI kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu nakuwapasha habari”. – (Yohana 16:7,13,14).
Katika mpango wa Mungu, Yesu alihitaji kurudimbinguni kuwa Mwakilishi wetu mbele ya kile kiti chaenzi cha Mungu ili “aonekane sasa usoni pa Mungu”(Waebrania 9:24). Wakati Bwana wetu aliyesulubiwaanapotuwakilisha sisi kule mbinguni, tunaye pia RohoMtakatifu kama MSHAURI wetu na KIONGOZI wetuhapa hapa duniani. Yeye moja kwa moja ndiyeMwakilishi wa Yesu hapa.
Yesu alipokuwa hapa alifanya kazi zake akiwa amefungwa na mwili huu wakibinadamu, tena yeye asingeweza kuwa kila mahali. Lakini huyo RohoMtakatifu hana mipaka kama hiyo inayomzuia; ana weza kuhudumu kamaMshauri na Kiongozi kwa watu wasiohesabika walio mahali pengi kwawakati mmoja. Kristo anakidhi mahitaji yetu kwa njia ya huyo RohoMtakatifu.


2.Roho Mtakatifu Ni Nani?
Wengi wetu tunaweza kuwa na uhusiano wetu na Mungu Baba kama sisitunatafakari habari za mzazi wetu tuliyepata kumjua ambaye alitutunza nakutulea vizuri sana. Tena mawazoni mwetu tunaweza kuona picha ya YesuMwanawe, kwa sababu yeye aliishi kati yetu kama mwanadamu. LakiniRoho Mtakatifu ni vigumu zaidi kuiona picha yake na kujenga uhusianonaye. Hatuna mifano rahisi ya kibinadamu ya kumlinganisha nayo.Walakini, Biblia inatoa habari za pekee zinazomhusu huyo Roho Mtakatifu:
Ni nafsi Mashuhuri. Yesu alimtaja huyo Roho Mtakatifu kama nafsi,mmojawapo katika ule Uungu, akiwa pamoja na Mungu Baba na MunguMwana:
“Basi enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi,mkiwabatiza kwa jina la BABA, na MWANA, na ROHO MTAKATIFU” -(Mathayo 28:19).
Roho huyo anazo tabia za kibinafsi: yeye anayo NIA (Warumi 8:27);HEKIMA (1Wakorintho 2:10); anazo HISIA ZA UPENDO kwetu sisi (Warumi15:30); anajisikia HUZUNI tunapotenda dhambi (Waefeso 4:30); anaouwezo wa KUTUFUNDISHA sisi (Nehemia 9:20); na uwezo waKUTUONGOZA sisi.
Alihusika katika uumbaji. Huyo Roho Mtakatifu alishirikiana pamoja naBaba na Mwana katika kuiumba dunia yetu hii.
“Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na dunia… Roho wa Mungualitembea juu ya uso wa maji” – (Mwanzo 1:1,2,KJV).


3.Kazi Za Roho Mtakatifu
(1)Huugeuza Moyo wa Mwanadamu.Katika kukutana kwake na Nikodemo,Yesu aliikazia sana kazi ya RohoMtakatifu ya kuubadilisha moyo wamwanadamu.
“Yesu akajibu, Amini, Amininakuambia, mtu asipozaliwa kwa majina kwa roho hawezi kuingia ufalmewa Mungu” – (Yohana 3:5).
Kuzaliwa kwa Roho” maana yake ni kwamba huyo Roho anatupatia sisimwanzo mpya. Ni zaidi ya kuibadilisha kidogo hapa na pale tabia yetu.Huyo Roho anatubadilisha sisi kuanzia ndani kwenda nje, akitimiza ahadihii, “Nami nitawapa ninyi moyo mpya” (Ezekieli 36:26).
(2)Hutuwezesha sisi kuyatambua matendo yetu mabaya na kutupatiashauku ya kuwa na utakatifu:
“Naye [Roho Mtakatifu] akiisha kuja, huyo ATAUHAKIKISHIAULIMWENGU kwa habari ya DHAMBI na HAKI na HUKUMU” – (Yohana16:8).
Unaposikia kisa cha kusisimua juu ya mtu fulani anayeachana na maishaya uasherati na kumgeukia Mungu na kuwa mwaminifu kwa mke au mumewake na kuwa mzazi anayejua kulea watoto, kumbuka kwamba kila hatuaaliyochukua kuelekea kwenye uzima ilikuja kutokana na msukumo wa RohoMtakatifu.
(3)Hutuongoza sisi katika maisha ya Kikristo. Yesu anazungumza nasimoja kwa moja kupitia kwa ile “sauti ndogo” ya huyo Roho.
“Na masikio yako yatasikia neno nyuma yako, likisema, Njia ni hiiifuateni; mgeukapo kwenda mkono wa kulia, na mgeukapo kwendamkono wa kushoto” – (Isaya 30:21).
Kwa njia ya matangazo ya Satelaiti, televisheni zetu zinatuletea daimakatika sebule yetu picha na sura mbali mbali kutoka katika bara lililo mbalinasi. Roho Mtakatifu kwa kiasi kidogo anafanya kazi yake kama Satelaiti yaMungu, akituletea kuwako kwake Kristo kutoka mbinguni kuja hapa duniani,na kumfanya awe karibu sana nasi wakati ule tunapomhitaji sana (Yohana14:15-20).
(4)Hutusaidia sisi katika maisha yetu ya sala.
“Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu kwa maana hatujuikuomba jinsi itupasavyo; lakini Roho mwenyewe hutuombea kwakuugua kusikoweza kutamkwa. Na yeye aichunguzaye mioyo aijua niaya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyoMungu ” – (Warumi 8:26,27).
Tunapojitahidi sana kutafuta maneno yanayofaa, Roho anatuombea sisi.Tunapokuwa tumekata tamaa kiasi cha kuweza kupiga kite [kuguna] tu kwaMungu, Roho anakikuza kilio chetu hicho kinyonge tunachotoa ili kuombamsaada kwake na kukifanya kiwe sala yenye nguvu mbele kabisa ya kilekiti cha enzi cha Mungu pale mahali anapoendelea kuhudumu Yesu sasa.
(5)Kukuza Sifa na Tabiaya Kikristo. Rohoanawafanya watu walewalio kama jangwa kirohokuwa kama mti ulio narutuba, uzaao aina zote zamatunda:
“LAKINI TUNDALA ROHO ni upendo,furaha, amani,uvumilivu, utu wema,fadhili, uaminifu, upolena kujitawala” -(Wagalatia 5:22,23).
Kuwa na tunda la Roho huonyesha kwamba sisi tunapandikizwa katika uleMzabibu wa kweli, yaani, Yesu (Yohana 15:5). Yesu anaweza kuishi kabisamaisha yake tele kupitia kwetu kwa njia ya uweza wa huyo Roho.
(6)Hututayarisha sisi kuwa mashahidi wake. Yesu anatoa ahadi hii:
“LAKINI MTAPOKEA NGUVU akiisha kuwajilia juu yenu RohoMatakatifu; nanyi mtakuwa MASHAHIDI WANGU…. Hata mwisho wanchi” – (Matendo 1:8).
Wale wote wanaotaka wanaweza kufanywa mashahidi wake kwa njia yahuyo Roho. Huenda sisi tusiweze kupata majibu yote, lakini huyo Rohoanaweza kutupa sisi kisa fulani cha kusimulia kinachoigusa mioyo na akiliza watu. Mitume wale walipata shida ya kuwasiliana na watu wale kabla yaPentekoste, lakini baada ya yule Roho kuwajia, walimtangaza Kristo kwauwezo uliowafanya wa “upindue ulimwengu” (Matendo 17:6, KJV).

4.Karama Za Roho
Maandiko yanaweka tofauti iliyo dhahiri kati ya kipawa cha Mungu chaRoho Mtakatifu ambacho anakitoa kwa KILA MUUMINI ili kumwezeshakuwa na maisha ya Kikristo yenye ushindi, na zile karama mbali mbali zaRoho zinazotolewa kwa waumini ili wapate kutoa huduma yao kwa watuiletayo matokeo mazuri kwa kutumia njia mbalimbali.
“Hivyo husema [Kristo] alipopaa juu, aliteka mateka akawapawanadamu vipawa. Naye alitoa WENGINE kuwa MITUME, na wenginekuwa MANABII, na wengine kuwa WAINJILISTI, na wengine kuwaWACHUNGAJI na WAALIMU,kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu,hata kazi ya huduma itendeke hata mwili wa Kristo ujengwe” -(Waefeso 4:8, 11-12).
Si kila Mkristo anayepokea karama hizozote, wengine wanaweza kupokeakarama nyingi kuliko wengine; Rohondiye “humpa kila mtu, kipaji tofautikama apendavyo mwenyewe” (1Wakorintho 12:11). Roho ndiyeanayemtayarisha kila muumini ili apatekufanya sehemu yake maalumu katikampango wa Mungu. Mungu anajua ni linina ni wapi aweze kutoa karamazitakazowaletea mibaraka mingi sanawatu wake na kanisa lake.
Orodha ya karama za Roho inayopatikana katika 1 Wakorintho 12:8-10naijumuisha hekima, maarifa, imani, karama za kuponya, unabii, kunenakwa lugha mbali mbali, na kutafsiri lugha (fungu la 8-10).
Paulo anatusisitizia kutaka sana karama zilizo kuu,” halafu anaongezakusema, “Hata hivyo nawaonesha njia iliyo bora.” (1 Wakorintho 12:31).Sura ile ya upendo (1 Wakorintho 13) ambayo inakuja baada ya fungu hiloinatilia mkazo kwamba “lililo kuu kupita yote” ni upendo. Na huo upendo nitunda la Roho (Wagalatia 5:22).
Tungejishughulisha sana kulitafuta hilo tunda la Roho, halafu kumwachaRoho atugawie karama zake kama “anavyopenda mwenyewe”(1Wakorintho 12:11).
5.Utimilifu Wa Roho Wakati Wa Pentekoste
Siku ile ya Pentekoste, Rohoalimwagwa kwa kipimo kisicho nampaka, ili kutimiza ahadi ya Yesu:
“Lakini mtapokea nguvu, akiishakuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu;nanyi mtakuwa mashahidi wangu…hata mwisho wa nchi.” – Matendo 1:8.
Wakati wa Pentekoste Rohoaliwawezesha wale mitume kuhubiri injiliwazi wazi katika lugha za watu “wa kilataifa chini ya mbingu” (Matendo 2:3-6).
Baadhi ya wanafunzi wa Biblia hulinganisha kuja kwake Roho na mvuazinazonyesha mapema katika majira ya kupukutisha (autumn) na mvua zileza mwisho katika majira ya kuchipua (spring) katika nchi ya Palestina (Yoeli2:23). Roho yule aliyemwagwa siku ile ya Pentekoste alifanana na”mvua yakwanza” ya majira ya kupukutisha ambayo ilizifanya mbegu kuota na kulipalishe muhimu kanisa la Kikristo katika uchanga wake.


6.Mvua Ya Masika Ya Roho
Unabii wa Biblia unatuambia habari za siku inayokuja ambayo katika hiyoRoho wa Mungu atamwagwa kama manyunyu ya mvua juu ya kanisa lake, akiwatia nguvu washiriki wa kanisa na kuwafanya mashahidi (Yoeli2:28,29). Karne nyingi mpaka sasa zimekwisha kupita na habari ya wokovuimeenea katika sehemu kubwa ya ulimwengu huu. Sasa wakati umefikakwa “mvua ya masika” kunyesha ili kuzikomaza mbegu zilizoota, nakufanya nafaka iwe tayari kuvunwa.
Historia inapokwenda kufikia mwisho wake muda mfupi tu kabla ya Kristokuja mara ya pili, Mungu atamfanya kila muumini aliye mwaminifu awetayari kwenda mbinguni kwa njia ya kumwagwa kwa wingi sana kwa Rohowake. Je! wewe unaionja sasa ile “mvua ya kwanza” katika maisha yako,ambayo inaliandaa kanisa kupokea ile “mvua ya masika” ya Roho? Je!unaishi maisha yaliyojazwa Roho? Ukipewa uwezo huo na Roho, je!utamruhusu Mungu akutumie kupeleka habari ya upendo wake mwingi mnousiosadikika na habari ya kurudi kwake upesi?


7.Masharti Ya Kumpokea Roho Mtaktatifu
Siku ile ya Pentekoste Roho Mtakatifu aliwagusa mioyo wale walioisikia injilihata wakapiga kelele, wakisema, “tutendeje ndugu zetu, tufanye nini sisi?”(Matendo 2:37).
“Petro akawaambia, ‘TUBUNIMKABATIZWE, kila mmoja kwa jinalake Yesu Kristo mpate ondoleo ladhambi zenu, NANYI MTAPOKEAKIPAWA CHA ROHO MTAKATIFU” -(Matendo 2:38).
Toba-yaani, kugeuka na kuiacha ilenjia ya maisha ya dhambi nakumgeukia Kristo – ndilo sharti lakukipokea kipawa hicho cha Roho[wala sio kwa kunena kwa lugha]. IliRoho apate kumwagwa juu yetu, nilazima kwanza tutubu na kumkabidhiKristo maisha yetu yote. Yesu alikazia pia ule utayari wa kumfuata yeye nakumtii kama sharti jingine la kupokea hicho kipawa cha Roho Mtakatifu(Yohana 14:15-17).


8.Maisha Yaliyojazwa Na Roho
Kabla hajaondoka duniani, Yesu aliwaagiza wafuasi wake, akisema:
“Wasitoke Yerusalemu, bali kingojeeni KIPAWA alichoahidi Babayangu kuwapa… Kwa kuwa Yohana ALIBATIZA KWA MAJI, bali, ninyiMTABATIZWA KATIKA ROHO MTAKATIFU baada ya siku chache” -Matendo 1:4,5.
Tena na tena Maandiko Matakatifu yanaonyesha kwamba Mkristo hanabudi “kujazwa Roho Mtakatifu” (Matendo 2:4; 4:8; 4:31; 6:3; 6:5; 7:55; 9:17;13:9; 13: 52; 19:6). Roho Mtakatifu anayafanya maisha ya Mkristo kuwayenye utiifu na mazuri kwa sababu maisha yale yaliyojazwa na Roho hufikiakiwango kile kikamilifu cha maadili ambacho Kristo alikiweka kwa ajili yetu.
Akiwa anaeleza habari za maisha ya Kikristo yaliyojazwa na Roho Pauloalitoa ombi hili kwa niaba ya kila muumini:
“Naomba kwamba kutoka katika utajiri wa utukufu wake AWAFANYEIMARA KWA UWEZA WAKE KWA NJIA YA ROHO WAKE KATIKAUTUKUFU WENU WA NDANI, ili Kristo apate kukaa mioyoni mwenukwa imani….. Basi, kwake yeye awezaye kufanya mambo ya ajabumno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, KWA KADIRI YA UWEZAWAKE UTENDAO KAZI NDANI YETU.”
Kama Frank Moris, aliyekuwa na mbwa wake mwaminifu wa kumwongoza,Basi, sisi tukiwa na kiogozi wetu Roho Mtakatifu ndani yetu, tunawezakufanya mambo ya ajabu mno kuliko vile tulivyoweza kufanya zamani.Tukiwa na tamaa mpya na uwezo mpya tunawezeshwa naye kusongambele kwa imani badala ya kujaribu kuyastahimili tu matatizo ya maishayetu.

Uzoefu wa kuwa na maisha haya yaliyojazwana Roho unafanywa kuwa mpya kila siku kwanjia ya maombi na kujivunza Biblia. Maombiyanatusogeza karibu sana na Kristo, na kulekujifunza Neno la Mungu kunatufanya tukazemacho yetu kuelekea kwenye nguvu zake.Mambo hayo yanakivunjilia mbali kizuizi chaaina yote kilichopo kati yetu na Kristo, ambachokingeweza kumzuia asitumwagie kipawa chakecha Roho, ambacho thamani yake haikadiriki.Hivyo ndivyo tukuavyo na kuziondoa tabia zetuzile mbaya na mielekeo yetu mibaya, na mahalipake kuwekwa tabia nzuri.
Warumi 8 hutoa maelezo ya kusisimua juu yamaisha yaliyojazwa na Roho. Uisome sura hiyokila uwazapo, na kuzingatia ni mara ngapi Paulo anasonda kidole chakekwa “Roho” wa maisha ya Kikristo.
Je! wewe umefanya ugunduzi wako wa ajabu kuhusu maisha yaleyaliyojazwa na Roho? Je! unatambua kuwako kwa huyo Roho katikamaisha yako? Je! unauonja ule uweza wake utiao uzima katika maishayako? Fungua maisha yako ili ule uweza mkuu kuliko wote katikaulimwengu upate kuingia.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top
MKUSDA CHURCH