JEHANAMU NI NINI NA IKO WAPI?
Kufyatua risasi kipumbavukulitokea wakati mwanafunzimmoja alipoingia katika shuleyake na kuwaua wanafunziwenzake kadhaa. Mwanaumemmoja mwenye chuki, ambayealikuwa amefukuzwa kazi, aliingiamahali pale alipokuwa akifanyakazi zamani na kumpiga risasimkuu wake wa kazi. Mama mmojaalisukuma gari lake dogo nakulitumbukiza ziwani likiwa nawatoto wake wawili ndani yake na kuwazamisha.
Kwa uchache katika mabara mawili maelfu wamechinjwa katika mauaji yasafisha-safisha ya kikabila. Uhasama wa muda mrefu uliochukua karnenyingi kati ya makundi mawili au zaidi ya makabila hayo ndicho chanzochake. Wanaume, wanawake, watoto, na hata watoto wachangawamepigwa risasi, wamekatwa-katwa, wamepigwa, na kubakwa.
Kutoa adhabu ya kifo kwa uhalifu huo wa kishenzi, hata kwa wauaji walewalio wakatili sana, kunashutumiwa na wengi. Makundi yaliyo kinyume nahukumu ya kifo yanapinga kwa makelele mengi, wakiita hukumu hiyo kuwasio ya kibinadamu ati ni “mfumo wa ibada ya kipagani.” Wanauliza hivi, je!wauaji hao hawarekebishiki?
Je! njia sahihi ya kibinadamu ya kuwaua wahalifu waliohukumiwa kuuawani ipi? Je! ni kile kiti cha umeme? Wengine wanadhani kudungwa sindanoyenye sumu ya kufisha ingekuwa ni njia isiyo na maumivu kabisa. Wenginewanatetea kwamba uhai wa mtu ungekoma kwa upesi zaidi kwakumnyonga.
Lakini katika majadiliano hayo yote yaliyojaa harara juu ya adhabu ya kifo,upo uchaguzi mmoja ambao hakuna mtu anayeufikiria. Hakunaanayependekeza kwamba wale wauaji wakatili, ambao kwa ukatili
wamekomesha maisha ya mtu mwingine, wapatilizwe kwa kuteswa vibayasana kimwili mpaka wafe. Kwa mfano, hakuna aliyependekeza kwambawauaji hao wachomwe moto polepole mpaka wafe.
Lakini, basi Wakristo wengi waaminifu wanadhani kwamba Baba yetu aliyembinguni atatenda vibaya kuliko hivyo. Wao wanasema, waovu ni lazimawateswe vibaya ili kubatilizwa kwa ajili ya dhambi zao. Tena, zaidi sana yahayo, wanafikiria kwamba maeneo ya Mungu anayoyatumia kuwauliawahalifu ni mahali pa mateso yasiyo na mwisho.
Ni kitu gani hasa kinachowapata waovu? Je! maangamizi yao yanapatanajena upendo na haki ya Mungu? Hebu na tuangalie Biblia itupe jibu.
1.Huzuni Kubwa Ya Mwisho Ya Yesu
Kwa miaka 6,000 Mungu amekuwa akiwasihi sana wanaume nawanawake:
“Kama mimi niishivyo, mimi Bwana Mwenyezi-Mungu…mimisikufurahii kifo cha mtu mwovu, bali napenda mtu mwovu aachane namwenendo wake mbaya, apate kuishi” – (Ezekieli 33:11).
Msalaba ulidhihirisha ni kwa kiwango ganiMungu anataka kuwaokoa wanadamuwalioanguka [dhambini]. Yesu alipopaza sautipale msalabani, akisema, “Baba uwasamehe,kwa kuwa hawajui watendalo,” aliufunua wazimoyo wake uliokuwa ukimwuma (Luka 23:34).Muda mfupi baada ya hapo Yesu akakata roho,na kama wengine waaminivyo, akafa kwakupasuka moyo wake (Yohana 19:30,34).
Lakini hata pamoja na udhihirisho huo wenyenguvu ya upendo wa Mungu, watu wengi badohawamgeukii Yesu. Na kadiri dhambiinavyoendelea kutawala katika dunia hii, ndivyoitakavyozidi kuongeza misiba ya wanadamu.Kwa hiyo ni lazima dhambi iteketezwe kabisa. Je! hivi Mungu anapangakufanya nini ili kuikomesha hiyo dhambi?
“Siku ya Bwana itakuja…. mbingu zitatoweka kwa kishindo kikuu; navitu vyake vya asili vitateketezwa kwa moto, nayo dunia itatoweka…” -(2Petro 3:10).
Hatimaye ni lazima Mungu aitakase dunia hii kutokana na uovu wake nakuikomesha dhambi kabisa. Wale wanaoendelea kung’ang’ania dhambihatimaye watateketezwa kwa moto huo ulioandaliwa kwa ajili yakumteketeza Iblisi, malaika zake, na dhambi katika dunia yetu hii. Ni wakatiwa kuhuzunisha jinsi gani kwa Yesu anapouangalia moto ukiwateketezawale aliokuja kuwafia ili kuwaokoa.
2.Wapi Na Lini Utakapowaka Moto Wa Jehanamu?
Kinyume na dhana zinazopendwa sana nawatu wengi, Mungu hana moto unaowakasasa mahali paitwapo “jehanamu” ambapowafu huenda wanapokufa. Jehanamuhutokea wakati ule dunia hii itakapogeukana kuwa ziwa la moto. Mungu anangojeakutekeleza hukumu hiyo dhidi ya waovumpaka hapo hukumu ya mwishoitakapotolewa mwisho wa ile miaka 1,000(Ufunuo 20:9-15).
“Bwana anajua jinsi ya kuwaokoa katikamajaribu watu wanaomcha Mungu, najinsi ya kuwaweka waovu katika adhabu hadi siku ile ya hukumu” – (2Petro 2:9).
Pia anaitakasa dunia yetu kwa moto huo utakasao.
“Lakini Mbingu na nchi za sasa zimehifadhiwa kwa neno la Mungu kwaajili ya kuharibiwa kwa moto. Zimewekwa kwa ajili ya siku ile ambapowatu wasiomcha Mungu watahukumiwa na kuangamizwa.” – (2 Petro3:7).
Kamwe Mungu hakupanga kwamba mwanadamu awaye yote amaliziemaisha yake katika mioto ile ya jehanamu. Lakini watu wanapokataakatakata kuachana na Shetani, halafu wanaendelea kuzing’ang’aniadhambi zao, basi, ni lazima wapokee hatimaye matokeo ya uchaguzi wao.
“Kisha atawaambia wale walio upande wake wa kushoto, ‘Ondokenimbele yangu enyi mliolaaniwa! nedeni katika moto wa milelealiotayarishiwa Ibilisi na malaika wake” Mathayo 25:41.
Kulingana na maneno hayo ya Kristo, je! ni lini jehanamu itakapowakamoto?
“Kama vile magugu yanavyokusanywa na kuchomwa moto, ndivyoitakavyokuwa mwisho mwa nyakati; Mwana wa Mtu atawatuma
malaika wake wawakusanye kutoka katika ufalme wake wale wotewenye kusababisha dhambi, na wote wenye kutenda maovu, nakuwatupa katika tanuru ya moto, na watalia na kusaga meno. Kisha,wale wema watang’ara kama jua katika ufalme wa Baba yao. mwenyemasikio na asikie!” – (Mathayo 13:40-42).
Magugu, yaani, wale watendao maovu, hawachomwi moto mpakautakapofika ule mwisho wa dunia. Kabla haijatekelezwa hiyo hukumu,malimwengu yote hayana budi kuthibitisha kwamba Mungu ni mwenye hakikatika kumshughulikia kila mwanadamu. Kama ilivyoelezwa kwakinaganaga katika Mwongozo 22, katika pambano kuu linaloendelea kati yaKristo na Shetani, Shetani amekuwa akijaribu kuyathibitishia hayomalimwengu kwamba njia ya dhambi ndiyo njia bora; Yesu amekuwaakionyesha wazi kwamba njia ya utii ndiyo ufunguo wa maishayanayoridhisha zaidi.
Mwisho wa miaka ile 1,000, udhihirisho huoutaishia katika hukumu ya Shetani, malaikazake, na waovu. Baada ya kufunguliwa vitabuvya kumbukumbu ambavyo vinafichua sehemualiyofanya kila mtu katika mfululizo wa matukiohayo ya kusisimua, ndipo Munguatakapomtupa Shetani, mauti na kaburi[kuzimu], pamoja na kila mmoja ambaye jinalake “halikuonekana limeandikwa katika kitabucha uzima…. Katika ziwa la moto” (Ufunuo20:15). Kulingana na fungu hili lifuatalo, yaani,Ufunuo 21:1, baada ya Mungu kuitakasa nchihii kwa moto kutokana na dhambi, anaumba,”mbingu mpya na nchi mpya.”
3.Jehanamu Itawaka Kwa Muda Gani?
Waumini wengi wanalikubali wazo hili lisemalo kwamba mioto ile yajehanamu inawaka milele na milele. Hebu na tuangalie kwa makini mafunguyale yanayoeleza jinsi Mungu anavyoishughulikia dhambi pamoja na wenyedhambi.
“Na miale ya moto huwaadhibu wale wanaomkataa Mungu na walewasiotii Habari njema ya Bwana ya Yesu. Adhabu yao itakuwakuangamizwa milele na kutengwa mbali na utukufu wake mkuu” – (2Wathesalonike 1:8,9).
Tafadhali zingatia kwamba hayo “maangamizi ya milele” sio sawa na”mateso makali ya milele.” Maana yake tu ni kwamba hayo ni maangamiziyanayoendelea milele. Matokeo yake ni mauti ya milele. Petro alizungumzajuu ya siku ya hukumu na ya “kuangamizwa kwao wanadamu wasiomchaMungu” (2Petro 3:7).
Kulingana na Yesu, maneno yote mawili, yaani, “roho na mwili”huangamizwa katika Jehanamu (Mathayo 10:28). Katika hotuba yake ya
mlimani, Yesu alizungumza juu ya mlango ulio mwembamba “uendaouzimani,” na njia ile pana “iendayo kwenye maangamizi” (Mathayo 7:13,14).Katika Yohana 3:16, Yesu anaeleza kwamba Mungu “akamtoa Mwanawepekee,” bali wawe na uzima wa milele.” Yesu anailinganisha miisho miwili:uzima wa milele au kuangamia sio kuchomwa moto milele na milele.
Tunapaswa kuhitimisha kwa kusema kwamba ni dhahiri ya kuwa jehanamuina mwisho wake; mwisho wake ni mauti na maangamizi ya waovu.
Semi zinazoeleweka wazi katika maandiko yote zinatuambia kwambawaovu wataangamizwa. “Waovu wataharibiwa” (Zaburi 37:28),”wataangamizwa” (2Petro 2:12), “watatoweka kama moshi” (Zaburi 37:20).Moto ule utawateketeza kabisa hadi watakuwa majivu (Malaki 4:1-3).
“Mshahara wa dhambi ni mauti, “sio uzima wa milele katika jehanamu;(Warumi 6:23).
Kusudi la adhabu ya mwisho katika moto ule wa jehanum ni kuiondoadhambi kabisa ulimwenguni humu, sio kuiendeleza dhambi milele na milele.
Ni vigumu kabisa kumwazia Kristo aliyeulilia mji ule mkaidi kutokana naajali yake, na ambaye aliwasamehe wale waliomwua, kwamba atumieumilele wake wote kuyaangalia maumivu yale makali ya waliolaaniwa.
Ni dhahiri kwamba jehanamu ina mwishowake. Mwisho wa miaka 1,000, Munguananyesha moto chini kutoka mawinguni nakumwangamiza kabisa Ibilisi, malaika zake,pamoja na waovu wanaoendeleakuzing’ang’ania dhambi zao. “Moto” huouna”shuka kutoka mbinguni” nakuwateketeza kabisa (Ufunuo 20:9).
Kulingana na maneno yake Kristo, motohuo ni “moto usiozimika” (Mathayo 3:12).Hakuna zima moto iwayo yote iwezayokuuzima mpaka umalize kazi yake yakuteketeza kabisa.
Mungu anaahidi kwamba, kutokana na moto huo utakasao, yeye ataiumba”nchi mpya,” ambayo ndani yake “taabu zote zilizopita zitakuwazimesahaulika,” na “sauti ya kuomboleza na kulia haitasikika tena ndaniyake” (Isaya 65:16-19).
Ile ni siku ilioje! Kila chanzo kiletacho huzuni kubwa kitakuwa kimetowekakabisa. Mungu atayafutilia mbali kabisa majeraha ya dhambi kutoka katikakila moyo, ndipo furaha yetu itakuwa imetimilika.
4.”Milele” Katika Maandiko
Katika Mathayo 25:41 Yesu anazungumza juu ya “moto wa milele,aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake.” Je, neno hili “milele” linadokezakwamba jehanamu hiyo ni ya milele? Yuda 7, anaeleza habari za Sodomana Gomora kuwa “imewekwa kuwa mfano wa wale watakaopata adhabuyao katika ule moto wa milele.” Ni dhahiri kwamba miji ile haiendelei
kuteketezwa kwa moto ule. Lakini moto wenyewe ULIKUWA wa milele kwamaana kwamba ulisababisha maangamizi ya kudumu.
Katika 2Petro 2:6 tunasoma mara moja tena habari za moto wa milele.Lakini maandiko hayo pia huonyesha wazi kwamba Mungu “akaihukumumiji ya Sodoma na Gomora, akiiteketeza kabisa kwa moto na kuifanyamajivu, akaifanya iwe mfano wa kile kitakachowapata wale wasiomchaMungu.” Wale wasiomcha Mungu waliokuwa Sodoma na Gomorahawaendelei kupata maumivu makali; waliteketezwa kabisa kuwa majivuzamani sana. Na, hata hivyo, moto ule uliowateketeza ni “wa milele’ kwakuangalia matokeo ya kazi yake – yaani, maangamizi yale ya kudumu.Milele maana yake ni adhabu ya kudumu, sio kuendelea tu kuadhibiwa.
Kwa kuwa kile kitabu cha Ufunuokinatumia lugha ya mifano dhahirikama ile, baadhi ya vifungu vyakevya maneno vimeeleweka vibaya.Kwa mfano,
Ufunuo 14:11 husemamaneno haya juu ya walewaliopotea, “moshi wa maumivu yaohupanda juu hata milele na milele.”Maneno haya yanasikika kanakwamba ni mateso yasiyo na mwisho. Lakini, tena, hebu na tuliache Andikokulitafsiri Andiko.
Kutoka 21:6 katika toleo la KJV huzungumzia habari za mtumishikutobolewa sikio lake kama ishara ionyeshayo kwamba yeye angeendeleakumtumikia bwana wake “milele.” Katika mfano huu neno hili “milele”lingemaanisha kadiri uhai wa mtumishi yule ambavyo ungeendeleakuwapo. Yona, aliyekaa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la yulenyangumi (Mathayo 12:40), anatoa taarifa yake kwamba alikuwa ndani mle”milele” (Yona 2:6). Bila shaka zile siku tatu na lile giza lisilokuwa namatumaini kwake vilionekana kana kwamba ni milele.
Basi hatuna budi kuwa waangalifu kuelewa ni jinsi gani na lini maandikoyanapotumia lugha ya mafumbo, ya mashairi. Moshi ukipanda juu milelekutoka katika ziwa lile la moto ni njia dhahiri ya kuonyesha maangamizi yamilele. Ufunuo 21:8 hutuambia waziwazi kwamba ziwa lile linalowaka motona kiberiti “ni mauti ya pili.” Jehanum ina mwisho wake. Waovuwanateketezwa kwa moto; yaani, wanaangamizwa kabisa.
5.Kwa Nini, Iweko Hiyo Jehanamu?
Hapo mwanzo Mungu aliiumba dunia hiiikiwa kamilifu. Lakini dhambi ikaja na kuletamisiba, uharibifu, na mauti. Kama jioni mojaungerudi nyumbani kwako na kuikutanyumba yako imepekuliwa na kuharibiwa,je! ungeiacha katika hali ile milele? Hasha.Ungefagia takataka na uchafu,ungepasafisha mahali pale kabisa, nakuitupilia mbali samani [fanicha]iliyoharibiwa kiasi cha kutowezakutengenezeka tena. Mungu atafanya vivyohivyo. Ataushughulikia uharibifu na uchafuziwa dhambi kwa mara moja tu, na kuiumbadunia mpya mahali pake. Kusudi la Mungu kuitakasa dunia hii kwa moto nikutayarisha njia ya kupatikana dunia kamilifu kwa ajili ya kuishi ndani yakewale waliookolewa.
Lakini Mungu anakabiliwa na tatizo zito kwa sababu dhambi hiyohaikuharibu tu dunia hii, bali pia imewaambukiza watu. Dhambi iliharibuuhusiano wetu naye na kati yetu sisi kwa sisi. Wanadamu wanaedeleakusumbuliwa na watoto wanaoteswa, ugaidi, picha za wanawake walio uchizinazoamsha ashiki, na maelfu ya kansa nyingine za kiroho. Siku mojaMungu atalazimika kuiangamiza dhambi kabisa, kwa sababu dhambi ndiyoinayowaangamiza watu. Tatizo la Mungu ambalo ni gumu kulitatua ni hili;jinsi gani akiteketeze kile kirusi cha dhambi kiletacho mauti kutoka katikadunia hii na wakati huo huo asiweze kuwaangamiza watu wotewalioambukizwa nacho? Suluhisho lake lilikuwa ni lile lakukichukua kirusihicho cha dhambi ndani ya mwili wake mwenyewe; akairuhusu ile kansa yadhambi kumwangamiza yeye kabisa pale msalabani. Matokeo yake nihaya:
“Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki, nayeatatusamehe dhambi zetu na KUTUSAFISHA UDHALIMU WOTE.” – (1Yohana 1:9).
Mungu anampa bure kila mmoja suluhisho lake kwa hilo tatizo la dhambi.Lakini ukweli wa kusikitisha ni kwamba wengine wanaung’ang’ania ugonjwahuo wa dhambi kwa nguvu zao zote. Na Mungu hatatumia nguvukuwalazimisha watu hao ili wapate kuichagua njia yake ya uzima wa milele.Wale wanaolikataa suluhisho lake hatimaye wataangamizwa kabisa pamojana ugonjwa huo. Sababu ya kweli ya kuwako hiyo jehanamu ni hii:
“Kwa sababu mimi nilipoita ninyi hamkuitika, niliponena hamkusikia.Mlitenda yaliyo mabaya machoni pangu, mlichagua mambonisiyoyafurahia mimi” – (Isaya 65:12).
Wakiwa wametengwa mbali na Yesu kwa uchaguzi wao wenyewe, waovuwatagundua kwamba kumbe njia pekee iliyobaki kwao ni kukabiliwa na ilemauti ya milele.
6.Nini Gharama Ya Kupotea?
Ijapokuwa maandiko hayafundishi kwamba moto ule wa jehanamuunasababisha maumivu yasiyo na mwisho, yanatupa picha ya harakakuonyesha ni jambo la kutisha jinsi gani kupotea. Waovu wataukosa uzimawa milele. Litakuwa ni jambo la kuogofya jinsi gani kutambua kwambafuraha ile ya kuishi milele pamoja na Mungu imeteleza mikononi mwao, yakwamba hawatauonja kamwe uhusiano ule wenye furaha kamilifu naupendo milele hata milele.
Kristo alipoangikwa pale msalabani, dhambi za ulimwengu mzimazikimtenga na Baba yake, bila shaka alipata wale watakaopotea milele.
Waovu wanapoliangalia lile giza jeusi,lenye ukiwa, mbele yao, wanaona tu
maangamizi yao ya milele. Hawanabudi kufa bila kuwa na tumaini lakufufuliwa mara ya pili. Wakati huo huowanaona jinsi walivyomsukumia mbalihuyo Kristo mara kwa mara alipokujakaribu nao akiwa na maneno ya upendoya kutaka kufanya amani nao. Mwishowatapiga magoti yao na kukiri kwambaMungu ni mwenye haki na upendo(Wafilipi 2:10,11).
Si ajabu, basi, kwamba waandishi wa Biblia wanasisitiza sana juu yetukuhusu uzito wa uchaguzi wetu tunaofanya pamoja na madai ya Kristokwetu.
“Basi, tukiwa wafanyakazi pamoja na Mungu, tunawasihi msikubali ileneema mliyopokea kutoka kwa Mungu ipotee bure, Mungu asema hivi:”Wakati wa kufaa nimekusikiliza, wakati wa wokovu nikakusaidia”.Basi, sasa ndio wakati wa kufaa, sasa ndiyo siku ya wokovu” – 2Wakorintho 6:1,2.
Siwezi kufikiria juu ya msiba mkubwa kuliko ule wa mtu fulani anayeitumiavibaya kafara ya Yesu kwa kuchagua kupotea. Njia zilizobaki mbele yetuziko dhahiri kabisa: yaani, yale maangamizi ya milele – kutengwa milelembali na Mungu, au urafiki wa milele pamoja na Kristo ambao unakidhishauku yetu ya ndani kabisa ya moyo wetu. Je! wewe unachagua ipi? Kwanini wewe usiugundue mwisho wako kwa kukaa ndani ya Kristo leo?